Kulibusu Kaburi la Mtume S.A.W na M...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kulibusu Kaburi la Mtume S.A.W na Makaburi ya Watu Wema Katika Umma

Question

Je, vipi kuhusu hukumu ya kulibusu kaburi la Mtume S.A.W. na makaburi ya wanaotenda wema katika Umma?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kabla ya kujibu kuna mambo mawili ni lazima kuyasisitiza, nayo ni:
La kwanza: kwamba tofauti ziliopo katika suala hili na mifano yake inayofanana nayo haziwezi kusababisha kuchukua maoni fulani ya kufuru na imani, katika masuala kama hayo huenda yakachukua mtazamo mmoja sahihi na mwingine dhaifu, na hali hii ni ya kidhana, na kujisahau kutokana na hali hii kunapelekea makosa katika hukumu.
La pili; tukubali tu kwamba suala la kidhana ambalo wanavyuoni hawakusema juu ya kufuru na imani, pamoja na kutolichunguza suala hilo katika mfumo wake wa utata ambao tukilichunguza kati ya wasomi pia husababisha makosa katika hukumu.
Na kulibusu kaburi la Mtume, S.A.W. na makaburi ya watu wema katika Umma ni aina ya kutaka baraka kwao, na jambo hilo limepitishwa na zaidi ya mmoja miongoni mwa wanachuoni kama ikikusudiwa kutaka Baraka tu,na siyo kutukuza, na hukumu hii inachukuliwa na wanachuoni wa madhehebu ya Shafi'iy, wanachuoni wengi miongoni mwao wamesema hivyo, Al-Nawawiy anasema katika Al-Manhaj: “kugusa kaburi au sanduku, hata kaburi lake S.A.W. kwa mkono na kulibusu ni uzushi mbaya unaochukiza”.
Ibn Hajar alieleza katika kitabu cha Al-Tuhfa akisema: “kauli yake: (na kulibusu) yaani kulibusu kaburi na kuligusa na kuvibusu vizingiti wakati wa kuzuru mawalii, katika kitabu cha Al-Nihaya na Moghni. Kauli yake: (uzushi ... nk) Ndiyo, ikiwa nia ya kuyabusu makaburi yao ni kutaka baraka, basi hali hii haichukizi kama ilivyosemwa, wamesema kuwa ikiwa hakuweza kuligusa Al-Hajar Al-Aswad (jiwe jeusi) likiwepo katika Kaaba ni bora kuliashiria kwa fimbo na kuibusu fimbo hiyo, na wamesema kwamba: ni vizuri kubusu sehemu yoyote ya Kaaba. Alisema: inaruhusiwa kuyabusu makaburi na mifano yake kama vizingiti.
Na kauli yake: (wameruhusu ... nk), basi inapimwa kwa mujibu wa yaliyotajwa. Na kauli yake: (kama hakuweza ... nk), inachukuliwa kwamba pahala pa mawalii panapokusudiwa kupozuru kama vile, Bwana Ahmad Al-Badawi kama ilikuwa na msongamano unaozuia kulifikia kaburi au unaosababisha mchanganyiko wa wanaume na wanawake, basi haruhusiwi kalikaribia kaburi, lakini atasimama katika pahala anapoweza kusimama vizuri pasipo na mashaka na asome chochote, na aashirie kwa mkono wake au mfano wa ishara kwa walii anayemkusudia kumzuru.
Sheikh wetu ametegemea hivyo, Al-Basri alisema baada ya kutaja maneno yaliyotajwa katika Kitabu cha Al-Nihaya, na Al-Suyuti alisema katika kitabu cha Al-Tawshih ala Al-Jamii Al-Saghiir kwamba baadhi ya wanachuoni wenye ujuzi wamefahamu kutokana na kulibusu Al-Hajar Al-Aswad (jiwe jeusi) kwamba inaruhusiwa kuyabusu makaburi ya watu wema. Nasema kwamba: kuhusu maelezo yaliyotangulia pamoja na usahihi wa kukataza yale yanayohisiwa kuwa ni kutukuza makaburi kuna kuna msimamo dhahiri, hata kama ni sawa, ni lazima kwa anayeiga asiyabusu makaburi ya mawalii mbele ya wajinga ambao hawawezi kutofautisha kati ya kutukuza na kutaka Baraka, na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi." [3/175, Ch. Dar Ihyaa Al-Turaath Al-Arabiy.
Dalili ya kuruhusiwa kwa kulibusu kaburi la Mtume, S.A.W. na makaburi ya watu wema, ni dalili ile ile iliyopokelewa kuhusu kulibusu Al-Hajar Al-Aswad (jiwe jeusi) na kwa kupenda hivyo, Al-Bukhaariy ameainisha sehemu katika kitabu chake cha hadithi: sehemu hii inahusiana na kulibusu jiwe jeusi, na ametaja hadithi mbili, imepokelewa na Omar Ibn Al-Khattab na mwanawe, pia Abu Daud, Al-Tirmidhi, Al-Nasaai, Ibn Hiban, Al-Darami na wengine wameainisha sehemu ile ile, imepokelewa na Omar kwamba alikuja mbele ya Al-Hajar Al-Aswad (jiwe jeusi) akalibusu na akasema: hakika najua kwamba hili ni jiwe tu, halina manufa wala halina madhara na lau sikumwona Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. akilibusu nisingelibusu kamwe.
Baadhi ya wanavyuoni wametambua (Wametohoa) kwamba kuruhusiwa kwa kuzibusu nguzo ni kuruhusiwa kwa kila kitu kinachofanana nacho katika utakatifu na kuheshimiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa nia ya kupata baraka, kupata thawabu, na upendo wake, kama ikiwa ni kwa wanadamu au kitu kingine, na vimeingia katika hukumu hiyo vitabu vya maarifa, Quraani na makaburi ya watu wema yanaingia katika hukumu hii, wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi na ya Hanbali wamesema kuwa: Inaruhusiwa kuibusu Quraani kwa ajili ya heshima yake, kwa iliyopokelewa kutoka Omar R.A. kwamba yeye alikuwa akiichukua Quraani kila siku na kuibusu, akisema, ahadi ya Mola wangu na uchapishaji wa Mola wangu, na pia Othman R.A. alikuwa akiibusu Quraani na kuupangusa juu ya uso wake.
Al-Nawawiy alisema katika Al-Tibian: “Tumesimulia katika Musnad Al-Darami kwa mapokezi yaliyo sahihi kutoka kwa Ibn Abi Mulaikah kwamba Ekrima Ibn Abu Jahl alikuwa akiweka Quraani juu ya uso wake na akisema: Kitabu cha Mola wangu Kitabu cha Mola wangu”. [Rejea: Rad Al-Muhtaar 5/246, Ihyaa Al-Turath wa Kashf Al-Qinaa 1/137, Dar Al-Fikr].
Bader Al-Ini alisema: “Sheikh wetu Zainuddin alisema: ... Kuhusu kuyabusu maeneo yenye heshima kwa nia ya kupata baraka, vile vile ni vizuri kuibusu mikono ya watu wema na miguu yao kwa mujibu wa nia, Abu Huraira amemwomba Al-Hasan, R.A. amfunulie sehemu Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alipombusu kitovuni mwake ili aibusu yeye pia kama alivyofanya Mtume ili apate baraka kwa athari zake na wajukuu wake, Thabit Al-Banaani alikuwa mara kwa mara haiachi mikono ya Anas R.A. mpaka aibusu, na akisema: mkono huu uliugusa mkono wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. Pia amesema: Al-Hafidh Abu Said Ibn Al-Alai aliniambia kwa kusema: Niliona katika maneno ya Ahmad Ibn Hanbal na Ibn Nasser na wengine miongoni mwa wanavyuoni kwamba Imam Ahmad aliulizwa kuhusu kulibusu kaburi la Mtume, S.A.W. na kuibusu mimbari yake, akasema: hakuna shida hata kidogo, akasema: tumemwona Sheikh Taqi Al-Din Ibn Taymiyyah anafanya hivyo akawa akishangaa katika hilo, na akasema: tumeshangaa lakini vipi na tumesimulia kwamba Imamu Ahmad amefua shati kwa Al-Shafiy na akanywa maji hayo ya kufulia, basi ikiwa hali hii ni ya kuwatukuza wanavyuoni, basi vipi kuhusu masahaba? Na vipi kuhusu athari za manabii?
Al-Muhib Al-Tabari alisema: inawezekana kufahamu(Kutohoa) kutokana na kulibusu hili jiwe na kuashiria kuta za kaaba kwamba inaruhusiwa kukibusu chochote kwa ajili ya kumuadhimisha Mwenyezi Mungu, na kwamba kuhusu jambo hilo kama haijatajwa hukumu ya kuruhusiwa, basi pia haijatajwa hukumu ya kuchukiza, nimeona katika baadhi ya maneno ya babu yangu Muhammad Ibn Abi Bakr kutoka kwa Imamu Abu Abdullah Muhammad Ibn Abi Al-Saif kwamba baadhi yao walikuwa walipoiona misahafu wanaibusu, na kama akiona sehemu za hadithi, wanazibusu, na kama akiyaona makaburi ya watu wema wanayabusu. Na hali hii labda inaruhusiwa katika chochote kinachotakiwa kumuadhimisha Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi” [Umdatul Qarii 9/241, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi].
Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ahmad kuhusu kulibusu kaburi la Mtume, mwanawe ameitaja kauli hii kutoka kwake katika kitabu cha Al-Ilal, akisema: “Nikamuuliza –aulizaye ni Abdullah Ibn Ahmed Ibn Hanbal na aulizwaye ni babake- kuhusu mtu anayegusa mimbari ya Mtume, S.A.W. na kutaka baraka kwa kuigusa na kuibusu na anafanya hivyo hivyo kwa kaburi lake anataka kumkaribia zaidi Mwenyezi Mungu? Ahmed Ibn Hanbal alisema, hakuna tatizo lolote”. [2/492, Dar Al Khani katika Al-Riyadh].
Haiwezi kusemwa kwamba kuruhusiwa kwa kubusu vitu hivi ni jambo la lazima kunategemea dalili; kwa sababu kauli ya Omar R.A: “Na lau kuwa sikumwona Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. analibusu, basi nisingelibusu, anakusudia Al-Hajar Al-Aswad (jiwe jeusi)”, kauli hii inapingana na iliyopokelewa kwamba yeye alikuwa akibusu msahafu, na kwa ajili ya yaliyopokelewa na wengine pia, basi jambo hilo halihitaji dalili, pengine kauli ya Omar (R.A) ni maoni yake tu, na kwama haihitaji dalili, kwa sababu jambo hili lina wasaa, Imamu Al-Dhahabi aliwajibu wale waliosema, kwa nini haikupokelewa kutoka kwa masahaba wote kulibusu kaburi la Mtume, S.A.W.? Alisema, akieleza: “kwa sababu wao walikuwa pamoja naye alipokuwa hai na wakaibusu mikono yake na walikuwa karibu kugombana juu ya maji ambayo ameyatumia katika udhu wake, na wakagawana nywele zake siku ile ya Hija, na pia alikuwa kama akitema mate, basi mate yake hayaanguki isipokuwa katika mkono wa mtu yeyote na kuupaka uso wake, na kwa sababu bahati hii haijapatikana kwetu tumeelekea juu ya kaburi lake Mtume S.A.W. kwa kuliashiria, kuliheshimu, na kulibusu, je huoni Thabit Al-Banaani alifanyaje? Alikuwa akiubusu mkono wa Anas Ibn Malik na kuuweka juu ya uso wake akisema: mkono huu uliugusa mkono wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W.
Kisha alitoa upatanishi wa kushangaza kati ya wanaoruhusu jambo hilo na wanaolikataza akisema: “Mambo haya hayafanyi muislamu isipokuwa ni upendo zaidi kwa Mtume, S.A.W. kwa sababu muislamu ameamuriwa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake zaidi kuliko upendo wake mwenyewe, mtoto wake, watu wote, fedha zake, pepo na Wanawake wazuri waliokuwepo ndani yake, pia kuna watu miongoni mwa waumini wanawapenda Abubakar na Omar zaidi kuliko upendo wao wenyewe. Jandar alituambia kwamba yeye alikuwa katika mlima wa Al-Biqaa akasikia mtu akimtukana Abubakar akauchomoa upanga wake, akamkata shingo yake, na kama angemsikia anamkutana baba yake asingehalalisha kumwaga damu yake, hivi huoni masahaba katika hali ya upendo wao zaidi kwa Mtume, S.A.W. walisema, hatusujudu kwako? Akasema: la, kama wakiruhusiwa, basi wakasujudu kwake kwa nia ya kumheshimu na kumtukuza, siyo kusujudu kwa nia ya kumwabudu kama walivyofanya ndugu zake Yusufu A.S. kwake, na hivyo ndivyo ilivyosemwa kuhusu Muislamu anayesujudu kwa kaburi la Mtume, S.A.W. kwa nia ya kuliheshimu na kulitukuza, basi muislamu huyo hakukufuru kabisa, lakini ni muasi na ajue kwamba jambo hilo limekatazwa, na pia kusali kwenye kaburi”. [Mu’jam Al-Shuyukh 1/73, maktaba ya Al-Sadiq katika Taif]. Jambo hilo linatokana na kumpenda Mtume S.A.W. mno.
Ibn Hajar Al-Haytamiy katika kijitabu chake Tuhfatul Zuwar Ila Kabri Al-Nabii Al-Mukhtaar, alisema kama alivyosema Al-Muhib Al-Tabari, na baada ya kukumbuka maneno yake kuhusu kuruhusiwa kwa kulibusu kaburi la Mtume S.A.W. alisema: “jambo hilo linatokana na kumpenda Mtume mno, hali ambayo inamfanya mtu mwenye kuwa na shauku nyingi sana inamfanya kutenda baadhi ya mambo pasipo na lawama, kwa mujibu wa hali ya upendo wake”.
Kisha akasema: “Kauli yake Ibn Hajar na Al-Tabari-kuhusu kuruhusiwa kwa kutaka baraka ya kaburi la Mtume ruhusa haikanushi kuwepo machukizo(Karaha), inaruhusiwa kufanya kitu ambapo ni cha kuchukiza, au pengine wanafanya hivyo kwa nia ya kutafuta kupona, kama alivyosimulia Ibn Al-Munkadir R.A. kwamba alikuwa mgonjwa, akaweka shavu lake juu ya kaburi la Mtume, S.A.W. akakaripiwa kuhusu hilo, akasema: napata tabu kwa ugonjwa basi nikiona hivyo natafuta kupona kwa kaburi la Mtume, S.A.W. au inawezekana kwamba maana yake ni kutaka baraka, imepokelewa kutoka kwa Al-Munkadir kwamba alikuwa akija katika sehemu ya msikitini akilala, akaambiwa kuhusu jambo hilo, akasema: niliona Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. katika sehemu hii - alisema katika ndoto -. Nia yake ni heshima na kutukuza, watu hutofautiana katika vyeo vyao kama ilivyokuwa pale wanapomwona Mtume S.A.W. hawawezi kuzidhibiti nafsi zao, bali wanakwenda haraka kwake, wengine wanakwenda polepole, na wengine wanachelewa na wote ni kheri.” [S26- 28, Ch. Dar Al-Sahaba lel-Turath katika Tanta].
Kukatazwa kwa kulibusu kaburi la Mtume labda kunaelekezwa kuwa ni heshima tu, hakuna uhusiano wowote wa karibu au wa mbali na mambo ya imani na kutoamini, na imepokelewa na Ibn Hajar kutoka kwa Al-Hilimi kuhusu heshima ya kulizuru kaburi la Mtume akisema: “Inachukizwa kugusisha tumbo na mgongo katika kuta zake, na pia kulifuta kwa mkono wake au kulibusu na kusujudu juu yake, lakini kwa mujibu wa heshima awe mbali nalo kama alivyokuwa mbali na Mtume, S.A.W. kama lau angekuwa hai”[ Tuhfatul Zuwar, uk. 20] kukataza hilo ni kwa mujibu wa heshima, hakuna nafasi kwa ukafiri na ushirikina.
Ibn Hajar amepokea habari kuhusu kuruhusiwa kwa kulibusu kaburi la Mtume, S.A.W. akataja kutoka kwa Yahya bin Sad Sheikh wa Imam Malik (R.A) kwamba alipotaka kwenda Iraq alikuja kwenye mimbari na akaifuta na akaomba dua. Kisha akasema: “Ibn Al-Jamaa alisema: Hii inabatilisha iliyopokelewa na Al-Nawawiy kuhusu makubaliano ya kuacha hivyo. Al- Sobki akasema: kutofuta kwenye kaburi la mtukufu siyo miongoni mwa masuala yaliyoafikiwa na wanavyouni kuhusu kuachwa kwake, imetajwa katika hadithi moja kwamba Marwan Ibn Al-Hakam alimwona Abu Ayyub Al-Ansari amesimama karibu na kaburi akakamata shingo yake akaipindua na akamwambia: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. amesema: "Kama akipewa utawala mtu ambaye hafai kutawala, basi subirini siku ya kiyama", pia imetajwa kwamba Bilali alipofika kumtembelea Mtume, S.A.W. alikwenda kwenye kaburi lake tukukufu na akaanza kulia na kuelekeza uso kwake [Tuhfatul Zuwar, uk. 21.22].
Kwa mujibu wa hilo inaruhusiwa kulibusu kaburi lililotukufu na makaburi ya watu wema kwa nia ya kutaka baraka, na tunatoa wito kwa Waislamu wasitofautiane kwa kufuata maoni maalum juu ya masuala haya, basi kujitahidi kuwa na muungano ni jambo la lazima na ni wajibu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas