Kutoa Dalili Kupitia Misingi ya Kif...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoa Dalili Kupitia Misingi ya Kifiqhi

Question

Kuna baadhi ya matini za kisheria ambazo zimetajwa kwa ujumla na zimeainishwa na matini nyingine, na zipo matini za kisheria ambazo zimetajwa pasipo na masharti na zimewekewa masharti kwa matini nyingine, wanavyuoni wamezungumza kuhusu kuziainisha matini za kiujumla na kuziwekea masharti, wamezungumza kuhusu jambo hilo katika sehemu za Usuulu Al-Fiqhi na katika sehemu nyingine pia, na wamezungumza kuhusu mambo yanayoziainisha matini na yanayoziwekea masharti; kama vile Qur'ani, Sunnah, makubaliano ya wanavyuoni na vipimo, kuhusu maelezo ya hayo, je, baadhi ya wanavyuoni walisema kuwa misingi ya kifiqhi inaainisha matini na kuziwekea masharti? na kama hawakusema hivyo, basi ni vipi kuhusu msimamo wa Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Wanavyuoni wametofautiana kuhusu ufafanuzi wa Usuulu Al-Fiqhi kutokana na tofauti yao katika dhana yake; Je, ni suala la kiujumla au ni suala la wingi tu? Tunachagua kwa kila kundi na ufafanuzi wake, miongoni mwa ufafanuzi wa kundi la kwanza: Ni jambo la kiujumla ambalo linatumika katika chembe/sehemu nyingi, kutokana na mambo hayo hukumu zake zinaeleweka. [Rejea: Al-Ashbah wa Al-Nadhair kwa Al-Subki 11/1, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.].
Miongoni mwa ufafanuzi wa kundi la pili ni: hukumu ya watu wengi siyo ya kiujumla, na hukumu hii haitumiki katika chembe/sehemu nyingi, kwa ajili ya kujua hukumu zake kutokana nayo. [Rejea: Ghamz Uyun Al-Basaair Sharhu Al-Ashbah wa Al-Nadhair kwa Al-Hamudi 15/1, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah.].
Inaonekana kwamba sababu ya wale wanaofafanua suala hilo ni la wengi ni kwamba: misingi mingi ya kifiqhi ina mifano inayotengwa nayo, na hazitekelezwi hukumu zake, na anayesoma vitabu vya Usuulu Al-Fiqhi ndiye anayezingatia jambo hilo. [Utangulizi wa kitabu cha Qawaid Al-hisni kwa Dkt. Al-Shaalan 1/23, Maktabat Al- Rushd].
Lakini jambo hili la pekee haliibatilishi kabisa misingi hii kwa ujumla; hasa kwa sababu jambo ambalo wanavyuoni wengi wameafikiana juu yake ndilo jambo linalozingatiwa katika sheria, vile vile masuala yanayofuatiwa ni sahihi ingawa baadhi ya sehemu hazikuzingatiwa. [Rejea: Mausuatul Qwaid Al-Fiqhia kwa Dkt./ Mohammad Sidqi Al-Ghazi 1/32, Muasasat Al-Risalah, na Al-Muwafaqat kwa Al-Shatby 2/53, Dar Ibn Affan].
Na kwa kuwa misimgi hii ni mingi haipunguzi chochote kutoka thamani yake ya kielimu na hadhi yake iliyo kubwa katika Fiqhi, hasa kudhibiti kwake kwa matawi ya hukumu za kielimu kwa udhibiti hupatikana katika kila kundi la matawi yale yale, na marudio ya kiungo kwa kiungo kinachokusanya inagawa tofauti ya masomo yao na sehemu zao, ili kutengeneza njia ya upimaji na ufananizi. [Rejea: Utangulizi wa Sharhu Al-Qawaid Al-Fiqhiya kwa Zarqa uk. 35].
Kwa hivyo, ilikuwa miongoni mwa faida za misingi ya kifiqhi ambayo ni muhimu zaidi ni: kudhibiti mambo mbalimbali kuyapanga katika njia moja ili kuweza kutambua uhusiano kati ya chembe/sehemu zinazotawanywa, na mwenye kuangalia atazidishiwa kwa mtizamo sahihi ambao unamsadia kutambua sifa zinazokusanya chembe. [Al-Qawaid Al-Fiqhiya kwa Dkt. / Yaqub Al-Bahussein uk. 114].
Na inawezekana kugawanywa kwa misingi ya kifiqhi kwa mujibu wa vyanzo vyake katika sehemu mbili:
Sehemu ya kwanza: Misingi iliyotokana na matini ya kisheria: Huenda kwa lafudhi yake, kama vile: "matunda yanahitaji dhamana kutoka kwa mwuzaji", hii ni matini ya Hadithi tukufu imepokelewa na Maimamu wanne wa Sunan. Pia inawezekana misingi hii imeanzishwa kutokana na matini yenyewe, bila ya haja ya kufuata chembe na kupata hukumu, kama vile: jambo ambalo ni rahisi halibatilishwi kwa jambo ambalo ni gumu, na huu ni msingi unaochukuliwa kutoka Hadith Tukufu isemayo: "kama nikiwaamrisheni kwa chochote, basi tekelezeni mnavyoweza". (Hadithi hii inakubaliwa).
Sehemu ya pili: misingi ambayo wanavyuoni wameipata kutokana na kufuata hukumu hizi: na ndio ambao wanavyuoni wanafuata katika sehemu mbalimbali, na wengi wao waliunda katika sentensi fupi, kama vile: kuridhika kwa kitu ni kuridhika kwa yatakayotokana nacho, mwenye shughuli nyingi hashughulishwi na kazi nyingine. [Al-Ashbahu wa Al-Nadhair kwa Al-Suyuti uk. 28.16].
Ama mgawanyiko wake kwa mujibu wa kukusanya na kuenea, misingi imegawanyika katika sehemu nne:
Sehemu ya kwanza: misingi mikuu ambayo inakusanya masuala mengi, na milango mbalimbali ambayo inakaribia kuwa nayo. Nayo ni misingi mitano ambayo inasemekana kwamba Fiqhi imejengwa nayo, nayo ni: mambo yanategemea makusudio yake, uhakika haufutwi kwa wasiwasi, na ugumu huleta urahisi, na uharibifu hufutwa, na mila huzingatiwa.
Sehemu ya pili: misingi ambayo ni karibu na iliyotangulia, lakini ipo chini zaidi kuliko hiyo, Al-Suyuti ametaja miongoni mwao katika kitabu cha “Al-Ashbahu wa Al-Nadhair” misingi arobaini, miongoni mwao ni: jitihada haibatilishwi kwa jitihada nyingine, na yakikusanyika mambo ya haramu na ya halali, mambo ya haramu yanashinda, na misingi mingi kama hii Al-Suyuti amezitaja dalili zake kama vile msingi wa kwanza usemao: jitihada haibatilishwi kwa jitihada nyingine.
Al-Suyuti alisema: “Asili ya msingi huu ni makubaliano ya masahaba R.A., Ibn Al-Sabbagh amesema hivyo. Na katika msingi wa tatu: kuwapendelea watu katika vitendo vya kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu kunachukizwa, lakini katika vitendo vingine kunapendezwa, Mwenyezi Mungu anasema: {bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji}. Msingi wa thelathini na nane, usemao: jambo ambalo ni rahisi halibatilishwi kwa jambo ambalo ni gumu, Ibn Al-Sobki alisema: msingi huu ni miongoni mwa misingi ambayo ni mashuhuri sana yaliyotokana na Hadithi ya Mtume S.A.W. isemayo: "kama nikiwaamrisheni kwa chochote, basi tekelezeni mnavyoweza".
Sehemu ya tatu: misingi ambayo wanavyuoni wametofautiana, kama vile, misingi ya ishirini iliyotajwa na Al-Suyuti katika kitabu cha tatu cha “Al-Ashbahu wa Al-Nadhair”, naye mara nyingi anaitaja kwa mtindo wa swali, kama vile: Je mifumo ya mikataba inazingatiwa au maana zake tu?
Sehemu ya nne: misingi ambayo ina masuala mbalimbali katika sehemu maalum miongoni mwa sehemu za Fiqhi, na mengi yao inazingatiwa hukumu ya kijumla, nayo ni: iliyoainishwa kwa sehemu moja na inakusudiwa kwayo masuala yanayofanana, mara nyingi inahusu madhehebu fulani.
Ama Mgawanyiko wake kwa mujibu wa kuwa misingi ya kimsingi au isiyo ya kimsingi, misingi hii imegawanywa katika sehemu mbili:
Sehemu ya kwanza: misingi ya kimsingi, nayo ni misingi ambayo haitafuti msingi mwingine, kama vile misingi mikuu mitano na aidha misingi arobaini iliyotajwa na Al-Suyuti, nayo ni ile iliyotajwa hapu juu.
Sehemu ya pili: misingi isiyo ya kimsingi, nayo ni misingi ambayo inafuta msingi mwingine, na kufuata kwake ni kwa mujibu wa njia mbili:
A) kuwa matawi kutoka misingi mikubwa zaidi kama vile: asili ni kuwa mtu yeyote hana dhambi, msingi huu uko chini ya msingi usemao: Ukweli haufutwi kwa wasiwasi.
B) kuwa msingi una sharti kwa msingi mwingine, kama vile: uharibifu haufutwi kwa uharibifu mwengine, msingi huu una sharti kwa msingi mwengine usemao: uharibifu hufutwa. [Rejea: Utangulizi wa kitabu cha Tahqiq qawaid Al-Hisni 30/1, na Mausuatul Qwaid Al-Fiqhia kwa Al-Ghazi 1/32, Muasasatu Al-Resalah, na Al-Qwaid Al-Fiqhiah kwa Yaqob Al-Bahussein uk. 118.].
Kuhusu suala hilo hukumu ni kwamba matini zinaruhusiwa kuainishwa na kuainishwa kwa misingi ya kifiqhi kwa ujumla, lakini tumeweka sharti kwa hukumu hii kwa sababu hali halisi inaonesha kwamba misingi ya kifiqhi haiendi kwa njia moja, baadhi yao asili yake ni matini ya kisheria, baadhi yao imechukuliwa kutoka maana ya matini moja au zaidi, baadhi yake haina matawi isipokuwa michache tu, baadhi yake wanavyuoni wametofautiana kama ilivyotangulia hapo juu, baadhi yake haina chini yake isipokuwa matawi machache kama vile msingi huu: anayeharakisha kitu fulani kabla ya kufika wakati wake, huadhibiwa kwa kunyimwa kwake, Al-Suyuti alisema baada ya kuutaja msingi huu: “Zingatio: Kama ukifikiri kuhusu tuliyoyataja utajua kwamba maana zinazojitokeza mbali na msingi ni zaidi kuliko zinazo karibu nao. Bali, kwa kweli, msingi huu hauna isipokuwa kunyimwa kwa muuaji kutoka urithi.” [Al-Ashabah wa Al-Nadhair uk. 153].
Pia matini inayotakiwa kuainishwa ni jambo la lazima iwe na uwezo wa kuainishwa, lakini kama haina uwezo wa kuainishwa, basi haiwezekani kuainishwa kwa misingi ya kifiqhi, wala kwa misingi mwingine.
Miongoni mwa dalili zinazothibitisha hivyo ni iliyopokelewa kutoka kwa Al-Bukhari katika Sahihi yake kwa kusema: Adam alituambia kwamba Shu’bah alituambia kwamba Al-Azraq bin Qais alisema: Tulikuwa katika eneo la Al-Ahwaz tukipigana na kundi la Mashia linaloitwa Al-Hururiah, na wakati nilipokuwa kando ya mto huko, mtu mmoja alikuwa akisali, na kamba ya farasi wake iko mkononi mwake, farasi wake alianza kukimbia mbali yake na mtu huyu anamfuata -Shubah alisema: mtu huyu ni Abu Barzah Al-Aslami- mmoja wa Khawarij alimwombea mtu huyu dua mbaya. Mtu huyu alipoondoka, alisema: Nilisikia kauli yenu, “Na nilipigana vita pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. vita sita -au saba– na ya nane niliona urahisi wake”, na hali ya kumfuatilia farasi wangu ninaipenda zaidi kuliko kumwacha kwenda zake na hali hii itakuwa ngumu kwangu.
Kisha imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka Hadithi ya Al-Azraq bin Qais kwamba alisema: Tulikuwa kwenye mto katika eneo la Al-Ahwaz, ambao maji yake yamekauka, Abu Barza Al-Aslamiy alikuja akiwa amepanda farasi, alisali na akamwacha farasi wake, farasi aliondoka, Abu Barza akaacha sala yake na kumfuatilia farasi wake mpaka akamkuta akamchukua na akakamilisha sala yake, mtu mmoja akasema: Tazameni Sheikh huyu, kaacha sala yake kwa ajili ya farasi, Abu Barza akasema: hakuna yeyote amenikaripia tangu Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alipofariki, na akasema: nyumbani kwangu ni mbali na hapa, kama nikisali na nikamwacha, sitaweza kurudi kwa familia yangu mpata usiku, na akataja kuwa aliambatana na Mtume, S.A.W., basi aliona urahisishaji wake.
Hadithi hii ina dalili ya kwamba Abu Barza R.A. alipokaripiwa na mmoja wa Khawarij na alipoombewa dua mbaya kwa sababu ya kugeukageuka katika sala, naye ameamuriwa kwa utulivu katika sala, basi yeye amekabili hali hii kwa msingi wa kifiqhi, ameufahamu msingi huu kutokana na kutazama matawi mengi ya urahisishaji wa Mtume S.A.W., naye hakutoa dalili kutoka Hadithi fulani ya Mtume S.A.W. ambayo inabainisha kwamba Mtume, S.A.W., amefanya kwa farasi wake kama alivyofanya Abu Barza, lakini alieleza hivyo kutokana na kufuatilia hali zake S.A.W. kwa hivyo Abu Barza amefahamu msingi usemao: Urahisishaji ni mahitaji ya kisheria, ambapo aliutangulia msingi huu au aliuhusisha na suala la utulivu, inagawa ameacha sala yake kama ilivyo wazi kutoka hadithi hii ya pili, lakini ameuhusisha msingi wake na aya hii: {wala msiviharibu vitendo vyenu} [MUHAMMAD: 33], wala haisemekani kwamba labda ameuhusisha msingi wake kama wanavyuoni wa madhehebu ya Shafii walivyouhusisha na aya hii: {Hapana njia ya kuwalaumu wanaofanya wema} [AT TAWBAH: 91], kwa sababu alisema dalili yake na hakunyamaza mpaka tunabahatisha uwezekano huu.
Imetajwa kuainishwa kwa matini na msingi wa kifiqhi katika maneno ya wanavyuoni, na hali hii inaonesha usahihi wa yale tuliyoyataja.
Katika Hadithi sahihi imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume, S.A.W. alisema: “Kama mmoja wenu akiamka kutoka katika usingizi wake, basi asizamishe mkono wake katika chombo mpaka anawe mara tatu, kwa sababu hajui mkono wake ulikuwa wapi (alipokuwa amelala)”.
Ibn Qudaamah amesema: “Imepokelewa kutoka kwa Abu Hafs kutoka kwa Omar Ibn Al-‘Ukbari katika Hadithi hii ina ongezeko kutoka kwa Mtume, S.A.W. nalo ni: basi kama akiingiza mkono wake katika chombo kabla ya kuuosha amwage maji. Na pengine utwahara wa maji haukubatilika wala si lazima kumwaga maji haya; kwa sababu utwahara wa maji ulikuwepo kwa uhakika, na hali ya kukataza kuuzamisha mkono haihukumu kubatilisha utwahara wa maji; kwa sababu maji bado ni twahara, hivyo pia utwahara wake haubatiliki, basi hatuhukumu kwa unajisi wa mkono wala unajisi wa maji, na sababu ni kwamba uhakika haufutwi kwa wasiwasi, basi kwa kuwa wasiwasi haufuti uhakika wa utwahara basi pia utwahara hauondoki. Na kwa hakika sisi hatukuhukumu unajisi wa mkono wala wa maji, na kwakuwa uhakika hauondoki kwa shaka, basi ni bora (Kutumia shaka hapa ni bora) [Al-Mughni 1/71, Maktaba ya Kairo].
Katika Hadithi ya Abu Dawood iliyopokelewa kutoka kwa Al-Baraa Ibn ‘Azib, alisema: alikuwa na ngamia mkali akaingia katika bustani akaiharibu, Al-Baraa Ibn ‘Azib akamwambia Mtume S.A.W. hivyo, Mtume S.A.W. “akahukumu kwamba kuhifadhi bustani katika mchana ni jukumu la wenye bustani, na kuhifadhi mifugo katika usiku ni jukumu la wenye mifugo, na kwamba kudhamini kwa vilivyoharibiwa na mifugo katika usiku ni jukumu la wenye mifugo”.
Al-Suyuti amesema: “msingi wa sita usemao: mila inazingatiwa ... Katika kuwapeleka mifugo wakati wa mchana na kuwahifadhi usiku, lakini kama mila ya jamii fulani ni kinyume cha hivyo, basi kuzingatiwa kwake ni sahihi zaidi”. [Al-Ashbah wa Al-Nadhair kwa Al-Suyuti uk. 89].
Katika Hadithi ya Abu Hurayrah R.A., kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisema: “Jirani hamzui jirani yake kutia mbao katika ukuta wake”, basi Abu Huraira alisema: “Kwa nini ninawaoneni mnapuuza Hadithi hii, naapa kwa Mwenyezi Mungu nitaifanya Hadithi hii kama amana juu ya mabega yenu”.
Sheikh Abdul Rahman Al-Bassam alisema katika maelezo yake: “Kama mwenye mbao ana haja, na mwenye ukuta hana madhara kutokana na kutia mbao, basi mwenye ukuta analazimishwa ampe ruhusa katika faida hii, ambayo haina madhara licha ya kwamba jirani yake anahitaji hivyo. Na kama hatampa ruhusa mtawala anaweza kumlazimisha kufanya hivyo. Lakini kama kuna madhara, au hakuna haja, basi uharibifu haufutwi kwa uharibifu mwengine.” [Taisiir Al-Allamh Sharhu ‘Omdatul Al-Ahkaam uk. 521, maktaba ya Al-Sahabah].
Madhehebu zimetofautiana katika suala hilo, na hizi ni baadhi ya matumizi wa wanavyuoni katika vitabu vya fiqhi na maelezo ya Hadithi kwa misingi ya kifiqhi kuhusu kuainishwa kwa matini za kiujumla, nazo ni bora zaidi katika kutoa dalili ambapo labda yanatajwa maneno ambayo hayafiki isipokuwa ya kinadharia tu wala hayafikii kuyatekeleza.
Na tunaweza kujadili hayo kuwa dalili za kisheria zina matini za kisheria na matini zingine, matini za kisheria kutoka Qur'an na Sunna zinazochukuliwa kwa mujibu wa kutoa dalili: matini hizi zimepangwa kwa utukufu, lakini siyo kwa nguvu, kwa sababu matini hizi labda zinakuwa dhaifu katika suala la uthabiti kama vile kusoma kwa njia isiyo ya kawaida, na Hadithi mapokezi yake ni dhaifu, au katika suala la umuhimu kama vile matini zinazofutwa, kinyume cha makubaliano. Misingi ya kifiqhi ina misingi ya kiujumla inayotegemea matini za kisheria, nazo ni karibu zaidi kwa makubaliano, na misingi hii pasipo na shaka inaainishwa kwa matini. Pia kuna misingi chini ya iliyotangulia lakini mingi kati yake ina dalili mbalimbali kutoka Qur’ani au Sunna au makubaliano.
Al-Tofiy alisema: “hebu tuzungumze kuhusu Usuulu Al-Fiqhi msingi moja baada ya mwingine, katika kupanga kwa mujibu wa utukufu wake siyo nguvu yake. Nayo katika utukufu: Quraani kisha Sunna, halafu makubaliano ya wanachuoni, kwa sababu Quraani ni maneno ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni matukufu na makubwa zaidi kuliko Mtume ambaye maneno yake ni Sunna, na Mtume S.A.W. ni mtukufu zaidi kuliko wenye jitihada wanaoafikiana juu ya makubaliano. Ama kupanga kwa mujibu wa nguvu, basi makubaliano, kisha Quraani, halafu Sunna, kwa sababu makubaliano hayafutwi, kinyume cha Quraani na Sunna, zinazofutwa, basi inawezekana kuwa aya au hadithi inayopinga makubaliano ikawa imefutwa”. [Sharhu Mukhtasar Al-Raudha 1/111, Muasasatul Resalah].
Kama ilivyo kwamba asili ya matini za kiujumla zinahusishwa/zinaainishwa, na inawezekana kuzitoa/kuzitenga matini nyingi miongoni mwao kwa kuzihusisha, basi vile vile kama misingi ambayo ina matini nyingi sana imelinganishwa kwa matini moja ya kiujumla, basi matimi hii inaainishwa kwa misingi hii.
Ibn Al-Najjar alisema: “Hakuna matini ya kiujumla ila imeainishwa isipokuwa chache tu, na inaruhusiwa kuainishwa “hata kwa matini ya kiujumla iliyosisitizwa” kwa sababu usisitizo wake hauzuii kuainishwa kwake kwa mujibu wa kauli ya wanavyuoni iliyo ni sahihi, na kwa mujibu wa dalili ya kauli ya Mwenyezi Mungu katika aya hii: {Basi Malaika wote pamoja walimsujudia (30) Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu} [Al-Hijr: 30-31] na katika Hadithi isemayo: "wahurumie wote isipokuwa Abu Qatada". Na inawezekana kuainishwa kamwe (Matini isiyo na mpaka) mpaka “ibakie matini moja tu” miongoni mwa matini za kiujumla kwa mujibu wa mtazamo wa wanavyuoni wengi... na iliyokuwa katika matini ndiyo sahihi kwa mujibu wa madhehebu ya Imam Ahmad na wenzake. Ibn Mufleh alisema: inawezekana kuainishwa matini ya kiujumla mpaka inabakia mmoja tu kwa mujibu wa wanavyuoni wetu. Al-Halawaniy alisema, huu ni mtazamo wa kundi la wanavyuoni. Pia Ibn Qadhi Al-Jabal alisema kwamba: Ibn Burhan alisema: madhehebu hii inazingatiwa zaidi kuliko nyingine. Al-Qadhi Abdul Wahab alisema: mtazamo huu ni mtazamo wa Imam Malik na wanavyuoni wengi. Vile vile Al-Juaini alisema kwamba wanavyuoni wa Sunna wote wameafikiana juu ya hivyo. [Sharhul Kawkab Al-Muniir 3/273, maktaba ya Al-‘Obeikan].
Ama kwa nini wanavyuoni hawakutaja “Misingi ya Kifiqhi” kuhusu matini inayoainishwa kwa misingi katika vitabu vya misingi ya kifiqhi, jibu ni kwamba misingi yote ya kifiqhi haiendi kwa njia moja, kama ilivyotajwa hapo juu, basi haiwezekani kuhukumiwa kwa ujumla. Halafu kama msingi unategemea matini ya sheria, basi tutoe dalili kutoka matini tu ili iwe wazi katika kukubalika na kujibu, kama vile kuainishwa kwa kitabu kwa habari ya mtu mmoja, nayo ni wazi kwa sababu ya maneno ya wanavyuoni kuhusu hilo, kinyume cha msingi wa kifiqhi ambao haijulikana chanzo chake isipokuwa baada ya utafiti mkubwa. Pia sehemu za vitabu vyote vya zamani vinazungumza juu ya orodha fulani ya kielimu, kwa hivyo mjadala unaendelea katika uwanja wake. Vile vile mwenye jitihada hahitaji kujua matawi ya kifiqhi; kwa sababu ni mwenye jitihada tu, kwa hivyo misingi ya kifiqhi haiangaliwi kwa ajili ya kuainishwa kwa matini za kiujumla, lakini jambo hilo halitokei kwa mujibu wa upande wa kielimu, na wao wanaoanzisha misingi ya kifiqhi ni wale wafuasi wa madhehebu hiyo baada ya kufariki mweye madhehebu hiyo kwa muda mrefu.
Ama kuhusu kuainishwa kwa matini ambazo hazina sharti kwa misingi ya kifiqhi, asili yake iliyotajwa hapo juu inatajwa hapa; kama walivyotaja wanavyuoni wengi katika vitabu vyao.
Al-Amdi alisema: “Kama ikijulikana maana ya matini ya kiujumla, na ile iliyo na sharti, basi yote tuliyoyataja kuhusu kuainishwa kwa matini za kiujumla yaliyoafikiwa, yaliyotofautiwa, yaliyochaguliwa, ndiyo yaliyotumika katika kuweka masharti kwa matini za kiujumla, basi wewe uzingatie mtazamo huu na utumike katika hali hii.” [Al-Ihkam fii Usuul Al-Ahkam 3/4, Al-Maktab Al-Islami, na vile vile katika kitabu cha Irshadu Al-Fuhuul 10/2, Dar Al-kitabu Al-Arabi].
Kutokana na yaliyotangulia, inaruhusiwa kuainishwa matini na kuziwekea masharti kwa mujibu wa misingi mitano ya Kifiqhi ambayo masuala yote ya kifiqhi yanatokana nayo, vili vile misingi ya kifiqhi ya kijumla ambayo chembe/sehemu nyingi sana zinatokana nayo, na asili yake ni msingi arobaini; mingi kati yake inadalili za kisheria ambazo ni wazi na zimezingatiwa, tumetaja mifano miongoni mwao. Lakini misingi hii arobaini haiendi kwa kiwango kimoja cha nguvu, lakini baadhi yake ina tawi moja tu kama ilivyotajwa, kwa hivyo, kuhusu misingi arobaini inaainishwa kwa nguvu tu, nayo ndiyo inayotegemea matini za kisheria au makubaliano ya wanavyuoni. Kisha matini ya kijumla inayokubali kuainishwa iainshwe. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.

Share this:

Related Fatwas