Ukweli wa Kuchinja kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu na Tofauti Kati ya Kutoa kwa Ajili ya Thawabu na Ushirikina
Question
Kuna uvumi zamani na sasa katika vijiji vya Misri kuhusu kuchinja kitu kwa ajili ya walii fulani yakifanikiwa maombi ya muombaji nadhiri katika kaburi la walii huyo kutaka Baraka zake ili Mwenyezi Mungu akubali dua hiyo, je, tendo hili ni miongoni mwa mambo ya ushirikina au la?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba zake na wanaomfuata, baada ya hayo:
Al-Dhabhu (yaani kuchinja) ni: kukata koo kutoka ndani, ambapo ni pahala pa kuchinjwa sehemu ya koo. Na (Al-Dhabihu) ni: jina la wanyama wanaochinjwa na wanyama wengine, Mwenyezi Mungu anasema: {Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu} [AL-SAAFFAT: 107]. [Rejea: Lisan Al-Arab 2/436, kidahizo cha: Dha bi hu, Dar Sader.].
Kama Mnyama akiwa si mwitu basi anachinjwa katika koo chini ya shingo, ni bora kuwa kuchinja ngamia kutoka chini ya shingo na pia kila mnyama ambaye ana shingo refu miongoni mwa wanyama wanaoliwa, wakati ambapo wanyama wenye shingo fupi wanachinjwa katika koo, mnyama kama akiwindwa, basi huuawa – na hali hiyo inaitwa kuchinjwa kwa dharura, yaani anajeruhiwa kwa jeraha katika sehemu yoyote mwilini kinachosababisha kumwua, kama mnyama yule akiuawa bila ya kufuata njia moja miongoni mwa njia zilizotangulia, basi ni nyamafu ambayo haiwezekani kuliwa nyama yake.
kuchinjwa kunaweza kuwa ibada kama mwislamu akitaka kukaribia kwa Mwenyezi Mungu, kama katika hali ya kuchinja mnyama wa sadaka katika sikukuu za kuchinja, Hakika (yaani kuchinja kondoo au mbuzi wawili kwa mtoto wa kiume na kondoo au mbuzi mmoja kwa mtoto wa kike katika siku ya saba baada ya kuzaliwa), na nadhiri, kwa hiyo Uislamu ulizingatia upande wa Ikhlasi (Kufanya kwa ajili ya Allah tu,) na umeupa umuhimu mkubwa, Mwenyezi Mungu anasema: {Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi} [AL KAWTHAR: 2].
Al-Tahir Ibn Ashour alisema katika kitabu cha [Al-Tahrir wa Al-Tanwir» (30/574, Al-Dar Al-Tunisia.]: “Neno la (kwa) katika kauli yake (kwa Mola wako Mlezi) lina maana ya kuainisha sala kwa Mwenyezi Mungu pekee yake tu, siyo kwa yeyote mwingine. Na aya hii inadokeza kwa washirikina wanaoyasalia masanamu kwa kuyasujudia na kuyatufu. Mwenyezi Mungu anasema: {Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.} (AL-ANAAM: 162)
Al-Tabariy alisema katika tafsiri ya aya hii: “Tumeambiwa na Ibn Hamiid alisema, Tumeambiwa na Hikaam, imepokelewa na Anbasah, imepokelewa na Muhammad Ibn Abd Al-Rahman, imepokelewa na Qasim ibn Abi Bizah, imepokelewa na Mujahid: {Hakika Sala yangu, na ibada zangu}, alisema: ibada ni, kuchinja katika Hija na Omrah”. [Jamii Al-Byaan kwa Al-Tabariy 12/284, Muasasat Al-Resalah].
Uislamu ulisimama msimamo muhimu katika suala hili, ulitangaza adhabu kwa matendo ya wajinga ambao walikuwa wakiabudu masanamu na kuchinja kwao badala ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo, Mwenyezi Mungu amekataza kula nyama za wanyama waliochinjwa siyo kwa ajili yake, Mwenyezi Mungu alisema: {Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.} [AL-BAQARAH: 173].
Al-Tabariy alisema katika kueleza aya hii: {Na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu}, ina maana ya kwamba: Wanaochinjwa kwa ajili ya Miungu na masanamu na wanatajwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Ilisemwa: {Na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu}; kwa sababu walipotaka kuchinja kwa ajili ya kuwakaribu na Miungu yao, wakiita jina la Miungu ambao wametaka kuwakaribu nao kwa kuchinjwa huko, mpaka ilisemwa kwa kila mwenye kuchinja, kama akiita jina la Mwenyezi Mungu au hakuita, kwa sauti ya juu au pasipo na sauti ya juu… imepokelewa na Yunus alisema, tuliambiwa na ibn wahb alisema, Ibn Zaid alisema –nilipomwuliza kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu}, alisema: waliochinjwa kwa Miungu wao, masanamu yanayoabudiwa na yanayoitwa majina yao juu yao. Akasema: Wanasema: (kwa jina la mtu fulani), kama unavyosema: (kwa jina la Mwenyezi Mungu) akasema, hii ni kauli yake: {na kilichotajwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu}. [Jaami Al-Bayaan 3/319].
Imam Al-Nawawiy anasema katika maelezo ya hadithi hii: (Mwenyezi Mungu amemlaani anayechinja kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu), hadithi hii ilipokelewa na Imam Muslim katika sahihi yake kutoka Ali ibn Abi Talib, R.A. Kwamba: “kuchinja kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu; maana yake ni kuchinja kwa kuita jina lisilo la Mwenyezi Mungu, kama mtu aliyechinja kwa ajili ya sanamu au msalaba au kwa ajili ya Musa au kwa ajili ya Issa au kwa ajili ya Kaabah, na kadhalika, yote hayo ni haramu, mnyama aliyechinjwa haruhusiwi, kama anayechinja ni Mwislamu au Mkristo au Myahudi.. Kama akikusudia kumwadhimisha (kumtukuza) anayechinjwa kwake kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu na kumwabudu, basi hivyo, ni kukufuru”. [Sharhu Al-Nawawi ala Sahih Muslim 13/441, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi].
Baadhi ya watu wanaweza kuchanganya kati ya kuchinja kwa asiye Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumwabudu, kumheshimu na kukaribiana naye, na kati ya kuwasindikiza baadhi ya Waislamu wakati wa kutembelea makaburi ya mawalii na kuchinja wanyama ambao ni kama nadhiri kwao, kuwagawa katika makaburi ya wema na mawalii, wala hawakaribii kwa wanyama hawa waliochijwa kwa walii mwema, lakini wanataka malipo yafike kwa aliyekufa, yaani: anachinja badala yake ili malipo yafike kwake, wala hachinji kwa ajili yake na ili kukaribia kwake, kwa sababu hii nia yake na makusudi yake, pengine anaelezea matakwa yake ya kutoa malipo ya kuchinja kama zawadi au sadaka kwa mwema yule lakini kupitia maneno yasiyo sahihi, na aliyetamka maneno hayo hatambui kosa lake, kwa hivyo, hairuhusiwi baada ya kusikia maneno hayo tu kuwashutuma Waislamu kuwa wao ni makafiri na wanawaabudu wema hawa, hasa kwamba maneno kama hayo yamepokelewa na masahaba watakatifu R.A. Imepokelewa na Abu Daud Saad ibn Ibada R.A. Alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ummu Saad alikufa, sadaka ipi ni bora kwake? Akasema: “maji”, akachimba kisima, na akasema: Kisima hicho kwa ajili ya Ummu Saad. Yaani: Kisima hicho ni sadaka kwake.
Kwa mujibu wa hivyo, nadhiri na kuchinja kwa ajili ya mawalii na wema kwa maana hiyo iliyokusudiwa na watu ni sahihi na siyo ushirikina kama wanvyosema baadhi ya watu, siyo kinyume cha itikadi sahihi na kumwabudu mwenyezi Mungu pekee yake.
Imam Al-Nawawi anasema katika kitabu cha “Al-Majmu’u” akibainisha hali hii maalum: “Al-Rafii alisema: Ujue kwamba kuchinja kwa ajili ya anayeabudiwa na kwa jina lake ni kama kusujudu kwake, na hali hizo mbili miongoni mwao aina ya heshima na ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ambaye ndiye anastahiki ibada, basi anayechinja kwa asiye Mwenyezi Mungu kama mnyama au sanamu kwa nia ya kuheshimu na kuabudu, si halali kuchinjwa kwake, na tendo lake hilo ni kukufuru kama kwamba anayesujudu kwa asiye Mwenyezi Mungu na kumwabudu, vile vile, kama akichinja kwa asiye Mwenyezi Mungu kwa nia ile. Ama kama akichinja kwa asiye Mwenyezi Mungu, kama kwamba akichinja kwa ajili ya Kaabah, kwa nia ya kuiheshimu, au kwa sababu ni nyumba ya Mwenyezi Mungu au kwa ajili ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi inaruhusiwa kwa maana hii, kwa mujibu wa aliyesema: Nimetoa zawadi kwa Kaabah, vile vile, inaruhusiwa kuchinja wakati wa kumpokea Sultani, kwa sababu kumshangalia kwake ni kama kuchinja Hakika ya kuzaliwa kwa mtoto, na kwa mfano kama huu, haupelekei kukufuru, na pia kusujudu kwa wengine kwa nia ya unyenyekevu na utii, hali hii haipelekei kukufuru pia, ingawa inakatazwa, na kwa mujibu wa hali hii, kama anayechinja akisema: kwa jina la Mwenyezi Mungu na kwa jina la Muhammad na alitaka kusema nachinja kwa jina la Mwenyezi Mungu na naomba baraka kwa jina la Muhammad, basi kauli hii haihurumiwa, na kauli ya mwenye kusema kwamba hairuhusiwi, inawezekana kauli hii izingatiwe kuchukiwa; kwa sababu jambo linalochukiwa linaweza kukanwa kwa ruhusa yake” [Al-Majmu’u 8/385, Dar Al-Fikr].
Hatupaswi kuhukumu haraka kwa ushirikina juu ya anayechinja kwa mawalii kwa nia ya kufikisha malipo kwao. Kwa sababu ushirikina kunatokea kama mtu akiamini manufaa ya kibinafsi katika asiye Mwenyezi Mungu au uwezo wa kibinafsi kwa madhara, vile vile, akimwabudu asiye Mwenyezi Mungu, basi tunalazimisha tufuate dhana njema kwa watu hawa; kwa sababu wanavyuoni wa umma wameafikiana kuwa Muislamu akitenda tendo linaloweza kusifiwa kwa kukufuru kutoka mitazamo tisini na tisa, na linaweza kusifiwa kwa imani kutoka mtazamo mmoja tu, basi mtazamo mmoja huu unachukuliwa, na mitazamo yote mengine inaondolewa.
Ibn Abidin alisema katika “Al-Durr Al-Mukhtar” [4/229, Dar Al-Kutub Al-Alamiyah.]: “Hairuhusiwi kutoa fatwa kwa kukufuru Mwislamu kama ikiwezekana kufahamu maneno yake kwa dhana njema, au kuna kutoafikiana katika kufuru yake, hata kama ipo hadithi dhaifu tu”. Ukafiri ni miongoni mwa masuala ambayo yanapaswa kuangaliwa vizuri, kwa sababu matokeo yake ni hukumu za kidunia na kiakhera, maana ya kuthibitika uasi ni kumwaga damu na kupoteza fedha na kuharimisha kwa mke wake, na kushuhudia juu yake kwa kukaa milele katika moto kama akifa juu ya hali hii. Na kwa ajili ya hatari ya jambo hili, inapaswa kulidhihirisha na kulichunguza vizuri kabla ya kuhukumu kwa kufuru, hasa kwa watu ambao umethibiti Uislamu wao, basi wakati inapowezekana kufahamu matendo ya Mwislamu au kauli yake kwa kufuatana na dhana njema inalazimishwa hivyo, hasa kwamba Uislamu wake ni dalili ya nguvu inayomwondolea hukumu ya ukafiri.
Kwa mujibu wa hayo yaliyotangulia hapo juu, na kwa mujibu wa hayo yaliyotajwa katika swali, yaliyofanywa na baadhi ya Waislamu katika makaburi ya mawalii wema wa Mwenyezi Mungu kuhusu kugawa nyama zilizochinjwa kama sadaka katika makaburi yao kwa ajili ya kulisha wapendwa wa walii huyo au mwengine, na kwamba kauli ya mmoja wao kuwa nyama hizi kwa ajili ya Al-Hussein, (R.A) –kwa mfano- Lazima kufasiriwa kwa njia inayoruhusiwa kama kauli ya Bwana wetu Saad: “Kisima hiki kwa ajili ya Ummu Saad”, na mambo yote hayo siyo miongoni mwa kumwabudu asiye Mwenyezi Mungu na ambayo anayoyatenda ni kafiri, Mwislamu hakufuru kwa kutenda hivyo isipokuwa akikusudia kumwabudu na kumkaribia asiye Mwenyezi Mungu kwa kuchinja huku akiamini kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika athari na kuendesha mambo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.