Swala ya Maiti Asiyekuwapo.

Egypt's Dar Al-Ifta

Swala ya Maiti Asiyekuwapo.

Question

Je, inajuzu kumswalia maiti asiyekuwapo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Swala ya jeneza ni faradhi ya kutoshelezeana. Hadithi kadhaa zimezungumzia fadhila yake, na miongoni mwa Hadithi hizo ni ile ilizopokelewa na Ahmad pamoja na wanazuoni wengine kutoka kwa Malik Bin Hubaira alisema: Mtume (S.A.W) amesema: "Hakuna muumini yeyote anayekufa akaswaliwa na umma wa waislamu wanaokaribia kuwa safu tatu, isipokuwa husamehewa madhambi yake yote". Na Imamu Muslim amepokea kutoka kwa Aisha (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: "Hakuna maiti yeyote inayoswaliwa na umma wa kiislamu unaofikia watu mia moja na wote wakamuombea msamaha isipokuwa mja huyu husamehewa". Na kutoka kwa Ibn Abaas Radhi za Allwah ziwafikie wote wawili alisema: nimemsikia Mtume (S.A.W) akisema: "Hakuna mwislamu yeyote anayekufa na wanaume arubaini wakamswalia, wanaume hao hawamshirishi Mwenyezi Mungu kwa chochote, isipokuwa huwakubalia maombi yao kwa maiti huyo". Imepokelewa na Imamu Muslim.
Na asili katika swala ya jeneza ni kuwapo kwa maiti mbele ya imamu na watu wengine wanaomswalia, anawekwa akielekezwa upande wa Kibla kwa ajili ya kuswaliwa, na pamoja na hivyo, inajuzu kumswalia hata kama hayupo mbele ya imamu pamoja na wanaomswalia lakini kwa masharti mawili;
Sharti la kwanza: Mji wa maiti uwe mbali na mji wa swala ya Maiti hata kama masafa baina yake ni kisai kisichofikia umbali wa safari ya kufupisha swala. Na ikiwa wanaomswalia maiti pamoja na maiti huyo wako katika mji mmoja basi swala ya maiti haijuzu isipokuwa kwa kuwapo aliyekufa, hata kama mji huo utakuwa mkubwa kiasi gani! Na huwenda kilicho chepesi zaidi ni kuuzingatia ukaribu na umbali wa mji katika zama zetu hizi kwa kuizingatia mipaka baina ya mikoa, na wala haishurutishwi kujuzu kwa swala ya maiti asiyekuwapo kwamba awe ameelekea Kibla.
Na sharti la pili: ni zingatio la wakati, kwani wanazuoni wa Madhehebu ya Shafiy wanafungamanisha kusihi kwa swala hiyo kwa yule aliyekuwa katika wale waliofaradhishiwa wakati wa kutokea mauti hayo, kama vile awe ni mtu mzima, mwislamu na mwenye twahara, kwani yeye anatekeleza faradhi aliyoambiwa, kinyume na yule ambaye hana sifa hizo. Na wanazuoni wa madhehebu ya Hanmbaliy wao wameufungamanisha wakati kwa mwezi mmoja tangu kutokea kwa msiba na wakatoa sababu ya kufanya hivyo kwamba haijulikani kama mwili wa marehemu unaweza kuendelea kuwepo bila ya kuharibika kwa zaidi ya muda huo. [Rejea Nehayat Al Muhtaaj 485/2, Ch. Dar Al Fikr, Na Sharhu Al Muntaha 363/1, Ch. Aalam Al Kutub].
Hivyo ndivyo tunavyotoa fatwa ya jambo hili. Na huu ndio ukweli wa madhehebu Shafiy na Hanmbaliy, na matini zao zinayatamka hayo. Imamu Ibn Hajar anasema: "Na maiti isiyokuwapo ndani ya mji au nchi huswaliwa swala ya kutokuwapo" iwe ni sehemu iliyo mbali na mji kwa namna ambayo kwa kawaida hainasibishwi na mji huo kwa kuchukua tamko la Zarkashiy kutoka kwa Mwandishi wa Alwaafiy, na akaipitisha kuwa nje ya uzio ulio karibu naye ni kama kuwa ndani yake, (Yaani hukumu ya nje ya uzio ni kama hukumu ya ndani ya uzio) na kinachochukuliwa katika hukumu kutokana na maneno ya Al Asnaawiy ni kwamba udhibiti wa ukaribu hapa, ni kwa namna ambayo inakuwa wajibu kutayamamu, naye anaelekea kuwa iwapo patakusudiwa umbali wa shamba na wala sio ukaribu, na wala hapashurutishwi kuwa kwake katika mwelekeo wa Kibla; na hayo ni kuwa Mtume (S.A.W) aliambiwa kuhusu mauti ya Nagashiy siku ya kifo chake, basi Mtume (S.A.W) akamswalia yeye na maswahaba wake. imepokelewa na Maimamu wawili Imamu Bukhari na Imamu Muslim, na matukio hayo yalikuwa katika mwaka wa tisa, na ikaja: Kwamba kitanda chake kilinyanyuliwa kwa ajili ya Mtume (S.A.W) hadi akakiona, na hali hii ni kwa kukisia kusihi kwake na wala hapakanushwi utafutaji wa dalili yake; kwani hali hii hata kama swala ya aliyekuwapo karibu na maiti kwa upande wa Mtume (S.A.W) ni swala ya ghaibu kwa upande wa Maswahaba wake". [Tuhfat Al Muhtaaj 149/3, Ch. Dar Ihiyaa Aturath Al Arabiy]
Ashams Aramliy amesema: "Na huswaliwa swala ya ghaib kwa yule aliye nje ya nchi) hata kama ni kwa umbali mdogo chini ya mwendo wa kupunguza swala, na katika upande usio wa kibla na anayeswali akiwa ameuelekea upande huo, kwani Mtume (S.A.W) alimswalia Nagashiy akiwa Madina siku ya mauti yake huko Uhabeshi, imepokelewa na Maimamu wawili, Bukhari na Muslim, na haya yametokea mwezi wa Rajabu mwaka wa tisa ….
Na wamekubaliana wanazuoni wote waliojuzisha kumswalia maiti swala ya ghaibu kwa kuwa swala hiyo inaondosha faradhi ya kutoshelezeana isipokuwa kwa yale yaliyosimuliwa kutoka kwa Ibnu Alkatwaaniy. Na lililo wazi ni kwamba ni sehemu ya kuondosha faradhi ya kutoshelezeana kwa namna ambayo wale waliokaribu wameijua.
Kwa upande wa yule aliyekuwapo mjini na hata kama mji huo utakuwa mkubwa hatamswalia maiti swala ya ghaibu kwa kuwapo wepesi wa kuwa karibu yake, na wamefananisha na swala ya kadhaa kwa yule aliye ndani ya mji pamoja na uwezekano wa kuhudhuria au kuwapo kwake, na lau maiti alikuwa nje ya uzio ulio karibu na yeye basi ni kama yuko ndani yake, kwani mara nyingi makaburi huwa nje ya uzio na kama kuna ugumu kwa aliyopo mjini kuhudhuria kwa kufungiwa sehemu au kwa ugonjwa, haukuwekwa mbali uwezekano wa kujuzu hilo kama alivyo tafiti Al-adhraiiyu, na akalipitisha Ibnu Abii Dam katika kitabu chake cha Almahbuus; kwani wao wametoa sababu ya kuzuia kuwepo urahisi wa kumfikia maiti… (Na sahihi zaidi ni umaalumu wa kusihi kwake) kwa maana kuwa ni sahihi kumswalia maiti asiyekuwapo na kuliswalia kaburi lake (kwa yule aliye miongoni mwa ndugu wa karibu) (ni faradhi kwake wakati wa umauti wa ndugu yake) bila ya mwingine; kwa kuwa mwingine ni Sunna na hii haiwi Sunna kwake kwa kuwapo sehemu ya mazishi.
Azarkashiy akasema: Maana yake haufanywi mara moja baada ya nyingine. Na akasema katika kitabu cha Majmuui: maana yake ni kwamba haijuzu kwa jinsi ilivyo, kuanza kuiswali bila ya kuwapo jeneza, kinyume na swala ya Adhuhuri huswaliwa kwa jinsi ilivyo, huanza kuswaliwa bila sababu". [Nahayat Al Muhtaaj 485-486 /2, Ch. Dar Al Fikr]
Na katika kitabu cha [Kashaaf Al Qinai] kwa Al Bahutiy; "(Na imamu ataswalisha) ni bora zaidi (na mwingine kuswalia jeneza lisilokuwapo hata kama litakauwa umbali wa masafa mafupi, au) liwe (upande usio kuwa Kibla) kwa maana kuwa mwelekeo wa Kibla cha Msikiti (kwa nia ya mwezi) kama vile swala juu ya kaburi, lakini inakuwa mwezi hapa tangu kufa kwa mtu, kama ilivyo katika kitabu cha: [Sharhi ya Al Muntahaa]. Kwani Mtume (S.A.W) alimswalia Nagashi na alisimamisha watu katika safu na akasema Allahu Akbaru mara nne." (wanazuoni wamekubaliana juu yake).
Wala haisemwi kwamba wanaomswalia hawapo katika ardhi ya Wahabeshi. Kwa sababu hiyo si katika madhehebu yanayopingana nayo, kwani huzuiwa swala kwa aliyekufa kifo cha kuzama majini na aliyetekwa na hata kama hakuwa ameswaliwa pamoja na kuwa yeye yuko mbali nao, kwani Mfalme Najashiy ni Mfalme wa Uhabeshi aliyetangaza Uislamu wake inakuwa mbali kwa kuwa hakuna yeyote aliyemuafiki kumswalia, na kauli kuwa ardhi ilisogezwa kwake (Mtume S.A.W) na akafichuliwa mwili wa Najashiy hadi akamuona wakati wa kumswalia, kama ingelikuwa ina asili basi Mtume angeliisema kwa Maswahaba wake, na tuseme kwa yale yaliyo ndani yake miongoni mwa miujiza mikubwa kama ilivyonukuliwa kuwaambia umauti wake na siku aliyokufa, na pia kama ingelikuwa hivyo basi isingekuwa hivyo kwa Maswahaba wake na (wala) wasingemswalia yule ambaye (yuko katika moja ya pande mbili za Mji hata kama) mji huo (ni mkubwa na hata kwa tabu ya mvua au ugonjwa;) kwani hiyo inawezekana kuhudhuria kwake na inafanana na lau kama ingelikuwa wote wawili wako katika upande mmoja, na kujitenga kwake na Mji kunazingatiwa kuwa ni katika kile kinachozingatiwa kuwa kuelekea huko ni aina ya safari". [Kashaaf Al Qinai 143/2, Ch. Dar Al Fikr]
Na dalili kuu kwa madhehebu ya Shafiy na Hanmbaliy ni hadithi ya swala ya Mtume (S.A.W) juu ya Anajashiy Mfalme wa Uhabeshi, lakini madhehebu ya Malikiy wamechukizwa na swala ya ghaibu kwa maiti, na madhehebu ya Hanafiy wamesema swala hiyo siyo sahihi.
Al Kharashiy anasema: "(Na hakuna swala ya ghaibu) ina maana kuwa inachukiza kumswalia maiti asiyekuwapo kwa kuzama majini au kwa kuliwa na mnyama mkali au aliyekufa katika sehemu au kitongoji fulani, na Mtume (S.A.W) kumswalia Mfalme Najashiy ni katika jambo linalomuhusu yeye peke yake, ni jambo maalumu kwake na hiyo ni kwa kuwa ardhi ilisogezwa kwake na akajua siku ya kufa kwake na akawaambia Maswahaba wake siku ya kifo hicho, na akawatokea na kuwaongoza katika swala ya ghaibu kabla hajazikwa, na hakuna yoyote aliyefanya hivyo baada yake, na wala hakuna yeyote aliyemswalia Mtume (S.A.W) baada ya kuzikwa. Na katika kumswalia kuna utashi mkuu, kwa hiyo ina maana ya kumuhusu yeye, yaani maalumu kwake tu". [Sharh Mukhtasar Khalil 143/2, Ch. Dar Al Fikr]
Na katika kitabu cha [Hashiyat Adsuqiy ala Sharh Al Kabeer]: "(Na kauli yake isemayo, na wala haliswaliwi jeneza lisilokuwapo) kwa maana kuwa inachukiza kuliswalia, na ama kwa upande wa swala ya Mtume (S.A.W) alipokuwa Madina, akimswalia Najaashiy baada ya kupokea taarifa ya kifo chake katika nchi ya Uhabeshi, hiyo ni maalumu kwa Mtume peke yake, au kwamba swala yake haikuwa kwa maiti asiyekuwapo kwa kupelekwa au kunyanyuliwa kwa Mtume (S.A.W) mpaka akamuona na ikawa swala yake kama vile swala ya imamu anapomswalia maiti akiwa mbele yake, na hakuna ikhtilafu yoyote katika kujuzu kwake. Na amejibu Ibnul Arabiy kwa majibu mawili kwa pamoja kwani kila moja lina umaalumu wake na kuwa kulirejesha kwa Mtume kiasili kunakosa dalili, na wala halipo". [247/1, Ch. Dar Al Fikr]
Na imekuja katika kitabu cha: [Aduru Al Mukhtaar cha Al Haskafiy: "Haisihi kwa asiyekuwapo na aliyebebwa juu ya kipando na aliyewekwa nyuma ya kipando hicho, kwani yeye ni kama imamu kwa upande mmoja kinyume na upande mwingine, kwa kusihi kwake kwa mtoto mdogo, na swala ya Mtume (S.A.W) kwa Mfalme Najashiy ni maana ya kilugha na ni maalumu kwake yeye".
Ibn Abdeen amesema katika maelezo yake: "(Tamko: la kilugha) ina maana ya dua tu, na hiyo ni mbali, (kauli yake: au kiumaalumu) au kwa sababu kitanda chake kiliinuliwa kwa Mtume (S.A.W) ili akione mbele yake. Basi swala ya jeneza ya wale walio nyuma ya imamu inakuwa kwa namna ambayo imamu analiona jeneza lake kinyume na maamuma, na hali hii sio kizuizi cha kumfuata imamu. Amefunguka. Na akatoa dalili ya uwezekano wa hali hizi mbili kwa namna ambayo haina nyongeza juu yake na kwa hivyo basi, akairejesha kwake, na kwa ujumla wa hayo ni kwamba iwapo maswahaba wengi wa Mtume (S.A.W) walikufa wakiwamo miongoni mwao waliohifadhi Quraani tukufu na wasomaji wazuri wa Quraani tukufu na haikupokelewa kutoka kwake kuwa aliwaswalia wasomaji hao wa Quraani tukufu pamoja na kwamba Mtume (S.A.W) alikuwa analipa umuhimu jambo hilo hadi akasema: (Hafi yoyote kati yenu isipokuwa mniombe mimi idhini nimswalie, kwani swala yangu kwa maiti huyo ni rehema kwake)". [Rad Al Mehtaar 209/2, Ch. Dar Al Fikr]
Na katika yale yaliyonukuliwa na wanazuoni wa madhehebu ya Hanafiy na Malikiy katika vitabu vyao, tunakuta kwamba wao hawajatoa dalili kwa yale waliyoyasema, dalili kutoka katika Quraani au Hadithi, bali walijibu kwa kutohoa dalili za wanazuoni wa madhehebu ya Shafiy kwa Hadithi ya swala ya Mtume alipomswalia mfalme Najashiy kwa dua maalumu, lakini yale aliyoyasema Ibnul Arabiy ni kuwa umaalumu huo na kunyanyuliwa huko kunakosa dalili na hakuna jibu lenye nguvu. Ama kwa upande wa madai ya kutofanya hivyo kwenye kaburi la Mtume (S.A.W) baada ya kufa kwake, kwa uhakika hii sio dalili, kwani hakuna maelezo yoyote.
Na kauli ya mwisho ni: kwamba hakuna tatizo katika swala ya jeneza juu ya maiti asiyekuwepo kwa sharti zilizotajwa hapo juu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya yote.

Share this:

Related Fatwas