Swala ya Jeneza kwa Maiti Waliokusa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Swala ya Jeneza kwa Maiti Waliokusanywa kwa Pamoja.

Question

Huswaliwa vipi swala ya jeneza kwa maiti zaidi ya mmoja waliokusanywa pamoja? Je tutamswalia kila maiti peke yake? Na kama tutawaswalia wote kwa pamoja na mara moja, ni upi utaratibu wa kuyapanga majeneza yao? Na haswa pakiwepo wanaume na wanawake?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya utangulizi huu:
Wakati mwingine hutokea mkusanyiko wa zaidi ya jeneza moja kwa ajili ya kuyaswalia majeneza hayo kwa wakati mmoja, kama ilivyotokea mara nyingi na baadhi ya vitabu vya fiqhi na pia vitabu vingi vya historia vimeitaja hali hiyo. Na hali hii huwa katika mazingira ya vita, magonjwa na matetemeko ya ardhi n.k. Kama ilivyotolewa na Ibn Abi Shaibah kutoka kwa Abdu Rabuh Ibn Abi Rashed alisema: Watu walikuwa katika janga la ugonjwa wa Tauni uangamizao wakawa wanawaswalia wanaume na wanawake kwa kuwatenganisha, Basi Jaber Bin Zaid akaja – kwa jinsi Abdu Rabuh anavyofikiria- basi akaweka wanawake mbele ya wanaume na akaswalia majeneza yote kwa pamoja.
Hukumu sahihi katika jambo hili ni kuwa yaswaliwe majeneza yote kwa pamoja, na yawekwe majeneza ya jinsia tofauti kama safu za swala zinavyokuwa, na patangulizwe upande wa imamu wanaume kisha watoto na baadaye wanawake.
Ama dalili ya kujuzu kwa swala ya majeneza yote kwa pamoja imepokewa kutoka kwa Masahaba (R.A) na waliokuja baada yao, kama Sunan Anisaaiy kwamba Ibn Omar aliyaswalia majeneza tisa kwa pamoja, na akawaweka wanaume wakimfuatia imamu, na wanawake wakikielekea kibla, na akawapanga safu moja, na jeneza la Umm Kulthum Bint Ali mke wa Omar Bin Al Khatwab na mwanawe aliyeitwa Zaid wote wakawekwa pamoja, na Imamu siku hiyo alikuwa ni Said Bin Al Aas, na miongoni mwa watu waliokuwepo; Ibn Omar, Abu Hurairah, Abu Saiyed na Abu Qatadah. Kwa hiyo basi, kijana aliwekwa mbele ya Imamu, na mtu mmoja akasema: Basi ninalikana jambo hilo, na mimi nikamtazama Ibn Abaas, Abi Hurairah, Abi Said na Abi Qatadah na nikasema: Hivyo walivyofanya kuna hukumu gani? wakasema: Hiyo ni Sunna.
Na tamko la wazi la maswahaba wote kwa pamoja kuwa namna ya utekelezaji huu ni Sunna unaipa hukumu ya kurejea kwake kwa Mtume (S.A.W) jambo ambalo linamaanisha kupendeza kwake. Kisha utaratibu wa kuwapanga maiti mbele ya imamu umewekwa kwa mujibu wa ubora wao kwa mapokezi yanayoelezea ubora kwa mujibu wa sharia ya kiislamu, na hii ni kwa njia ya kupendeza. Kama ambavyo kukusanya ni bora zaidi kwa ajili ya kuharakisha mazishi na hili ndilo jambo linalotakiwa na sharia ya kiislamu, na pia linawapunguzia waislamu uzito, ambapo pia ni jambo linalotakiwa na sharia ya kiislamu.
Na kwa mfano wa tuliyoyataja watu wa elimu wamesema:
Al Bahutiy amesema: "(Na iwapo watakusanyika maiti wote wakiwa wanaume) kwa maana kuwa hakuna mwanamke kati yao au khuntha, (au) walikusanyika maiti (makhuntha) (peke yao) hakuna wanaume wala wanawake waliyo pamoja nao (watasawazishwa baina ya vichwa vyao) kwani msimamo wao ni mmoja. Na iwapo watakusanyika maiti wa jinsia tofauti basi vichwa vyao vitasawazishwa kati ya kichwa cha kila jinsia (na mmoja mmoja kama Imamu) atasimama mbele ya kifua cha mwanaume na katikati kwa mwanamke, na atasimama kati ya wawili hao iwapo maiti ni ya khuntha. (Na itatangulizwa kwa Imamu miongoni mwa maiti katika kila jinsi ile ya aliyo mbora wao), yaani: Mbora zaidi kuliko wote miongoni mwa jinsia hizo; kwani anayestahiki kutangulizwa kwa uimamu kwa sababu ya ubora wake, basi anastahiki kutangulizwa wakati wa kuswaliwa kwa jeneza lake, na hayo yanaungwa mkono kwa kuwa: (Mtume (S.A.W) alikuwa akimtanguliza katika kaburi mtu ambaye amehifadhia Quraani zaidi), atatangulizwa mbele ya Imamu yule aliye huru aliyebaleghe kisha mtumwa aliyebaleghe, kisha mtoto, khuntha na mwanamke, haya yamenukuliwa na kundi la wanazuoni kama ilivyoandikwa (Na iwapo watakuwa sawa) kwa ubora basi atatangulizwa mwenye umri zaidi, kwa ujumla wa kauli ya Mtume (S.A.W) (Ukubwa ukubwa) basi (Na iwapo watakuwa sawa) katika umri, basi aliyeingia Uislamu kabla yao, basi (Na iwapo watakuwa sawa) katika hayo basi kupiga kura, basi atatangulizwa aliyechaguliwa kwa kura kama ulivyo uimamu, na atatangulizwa mbora zaidi miongoni mwa maiti mbele, kwani haki ni bora ifuatwe na sio yenyewe ifuate, (na sehemu ya kati ya mwanamke inawekwa ikielekea kifua cha mwanaume) iwapo watakutana basi Imamu asimame na mmoja kwa kila mmoja miongoni mwa maiti hao katika kisimamo chake, (Na kuwajumaisha maiti na kuwaswalia ni bora zaidi kwao kuliko kumswalia kila mmoja peke yake), ili kuhifadhi uharaka na uwepesi" [Kashaaf Al Qinaiy 112/2, Ch. Dar Al Fikr.].
Na AShiraaziy amesema: "Na iwapo majeneza yatakusanyika basi atakaetangulizwa kumfuatia Imamu atakuwa ni mbora wao, na ikiwa ni mtoto au mwanamke au khuntha kisha mwanamke, kwa yaliyopokelewa kutoka kwa Ibn Omar (R.A) kwamba aliswalia jeneza tisa wanaume na wanawake basi akaweka wanaume wamfuatie Imamu na wanawake welekee kibla", na Amaar Bin Abi Amaar amepokea kwamba Zaid Bin Omar Bin Al Khatwab na mama yake Ummu Kulthum Bint Ali Ibn Abi Twalib (R.A) walikufa basi Said Bin Al Aas aliwaswalia swala ya jeneza basi akamuweka Zaid mbele yake na mama yake akaelekea kibla, miongoni mwa watu waliokuwepo Al Hassan, Al Husein, Abu Huraira, Ibn Omar na kiasi cha thamanini miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (S.A.W) na (R.A) wote. Na ni bora kila mmoja aswaliwe peke yake, na iwapo wote wataswaliwa swala moja basi inajuzu; Kwani kusudio la kuwaswalia maiti hao ni kuwaombea Dua, na jambo hili linatuka kwa pamoja. [Al Muhadhab 246/1, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Al Kassaniy amesema: "Kisha, namna gani majeneza hupangwa pale yanapokusanywa kwa pamoja? Tunasema kuwa: Hali haiepukani na kuwa majeneza hayo ni ya jinsia moja au jinsia tofauti tofauti, na iwapo watakuwa na jinsia moja tu basi wakitaka watawaweka safu moja, kama wanavyopanga safu katika hali ya uhai wao wakati wa swala, na wakitaka watawaweka mmoja mmoja kuelekea kibla; Ili Imamu awaelekee wote, na hili ni jibu la wazi la mapokezi.
Na imepokewa kutoka kwa Abu Hanifa kwa mapokezi yasiyo ya asili, kwamba wa pili ni bora zaidi kuliko wa kwanza, Kwa kuwa Sunna ni kuwa Imamu asimame kwa kumuelekea maiti, na hii hutokea kwa wa pili kinyume na wa kwanza na iwapo watawaweka mmoja baada ya mwingine inapaswa kuwa mbora wao amfuatie imamu, na mkubwa wao kwa umri. Na Abu Yusuf alisema kuwa: Na lililo zuri zaidi kwangu watu bora huwa wanamfuatia Imamu kwa kauli ya Mtume (S.A.W): "(Wanifuatie miongoni mwenu wale waliobaleghe) kisha akiweka kichwa cha kila mmoja miongoni mwao kuelekea kichwa cha mwingine ni vizuri, na ikiwa ataweka mfano wa lundo kama alivyosema Ibnu Abii Lailaa; nako ni kichwa cha pili kuwa katika bega la mtu wa kwanza basi ni bora zaidi. Na kadhalika ilipokelewa kutoka kwa Abii Hanifa kwamba wakiwekwa hivyo ndivyo basi ni bora pia, kwani Mtume (S.A.W) na Masahaba wake wawili wamezikwa hivyo, na inapendeza kisimamo cha swala kiwe juu ya utaratibu huo pia.
Na iwapo jinsia za wafu zitakuwa tofauti, kwa kuwapo wanaume na wanawake, basi wanaume watafuatia baada ya Imamu na wanawake watakuwa nyuma ya wanaume kuelekea kibla, kwani hivi ndivyo wanavyopangwa safu nyuma ya Imamu katika hali ya uhai wao, kisha wanaume wanakuwa karibu na Imamu kuliko wanawake, na hivyo ndivyo inavyokuwa katika hali ya kuwa kwao maiti. [Badaei' Al Swanae' 316/1, Ch. Al Maktabah Al Elmiyah]
Na Badr Adeen Al Ainiy alisema: "Wanazuoni wamesema: Na iwapo majeneza ya wanaume na wanawake yatakusanyika mwanamume atawekwa kumfuatia Imamu mweleko wa kibla, kisha mwanamke amfuatie kibla, na yakikusanyika majeneza ya mwanamume, mtoto, mwanamke na khunsa basi mwanamume atawekwa kumfuatia Imamu, kisha mtoto katika upande wa kibla na khuntha kisha mwanamke amfuatie kibla, basi mwanamke atakuwa wa mwisho mwelekeo kibla". [Sharh Sunan Abii Dauwd 123/6, Ch. Maktabat Arushd]
Na kuna wanazuoni waliosema kuwa ni bora kumswalia kila maiti peke yake. Al Khatweeb Asherbiniy alisema: "Na tamko lake: (Inajuzu) linafahamika kuwa ni bora kumswalia kila maiti peke yake, na hivyo ndivyo ilivyo; kwani hivyo ndivyo itendwavyo zaidi na kukubalika zaidi na wala sio kuchelewesha sana. Na japo kuwa Al Mutwaliy amesema: Hakika ni bora zaidi kukusanya kwa ajili ya kuharakisha mazishi yaliyoamrishwa. Ndio, iwapo atachelea mabadiliko au mlipuko kwa kuchelewa basi ni bora kukusanya". [Mughniy Al Muhtaaj Fi Sharh Minhaaj Atwalibin 31/3, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na jibu kwa hawa ni kuwa yale waliyoyataja yanakwenda kinyume cha Sunna, kwani yeye kutangulizwa mbele yake, ni kanuni isemayo: (jambo lenye utendaji mwingi ndilo lenye ubora mwingi) sio kwa uwazi wake, kuna sura nyingi zilizotokana nayo, miongoni mwazo ni ile iliyokuwa kwa ajili ya kuendana na utendaji wake Mtume (S.A.W) kama vile katika tawi lililotengana na ambao Asuyutiy kaeleza na kutoa sababu: Swala ya Adhuha ubora wake ni rakaa nane, na zaidi yake ni rakaa kumi na mbili. Na za kwanza ni bora zaidi kwa sababu ya kuendana na jinsi Mtume (S.A.W) alivyofanya.
Halafu sisi na wao tunaafikiana katika kujuzu kwa swala ya jeneza ya mkusanyiko wa maiti kwa ujumla au kwa kila mmoja peke yake, lakini hitilafu katika ipi swala iliyo bora zaidi.
Ibn Al Munzer alisema: "tumehadithiwa na Is-Haaq, kutoka kwa Abdul-Razaq, kutoka kwa Athauriy, kutoka kwa Abi Huswain, kutoka kwa Musa Bin Twalha, kutoka kwa Othman Bin Afaan, "Yeye aliweka mwanaume amfuatie Imamu na mwanamke afuatie kibla". Na tumehadithiwa na Ismail akasema: Abu Bakr aliswalia jeneza la maiti mawili, Ibn Numair aliswalia jeneza la maiti mawili, kutoka kwa Al Hajaaj, kutoka kwa Othman Bin Abdullah Bin Mawheb, kwamba Zaid Bin Thabit na Abu Hurairah hivyo ndivyo walikuwa wakifanya, na kwa hayo Said Bin Al Musayib akasema, na kadhalika Al Shabiy, Al Nakhaiy, Atwaa, Azuahariy, Yahiya Al Nswariy, Malik, Sufiyaan Athauriy, Ashafiy, Ahmad, Ishaaq na wenye rai.
Na kundi moja la wanazuoni lilisema: wanawake wanawekwa wakimfuatia Imamu na wanaume wanawekwa wakifuatia kibla: hilo ni tamko la Al Hassan, Al Qasem na Salem, na kauli hiyo imepokelewa kutoka na Musalamah Bin Mahklad, na ipo kauli ya tatu: Nayo ni kuwa aswaliwe mwanamke peke yake na mwanamume peke yake, Ibn Maghfal alifanya hayo, na akasema jambo hilo halina shaka, Abu Bakr akasema: " Na kwa tamko la kwanza ninasema: Kwa ajili ya Sunna ambayo ameitaja yule ambaye tumeyataja hayo kutoka kwake miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (S.A.W)" [Al Ausat Fi Asunan na Ijmai na hitikafu 421/5, Ch. Dar Twebah]
Inafaa kutanabahisha kuwa Imamu mteule ndiye anayewaswalia maiti kwa pamoja, na iwapo hatakuwapo na wakahitilafiana ndugu, mawalii wa maiti basi atatangulizwa yule anayetangulizwa na sharia, kwa ajili ya uimamu kwa utaratibu wa yule anayezingatiwa kuwa ni mbora wao kisheria.
Ibn Qudamah alisema: "Na iwapo majeneza yatakusanywa, basi ndugu zao watashauriwa kuhusu nani wa kutangulizwa kuswalia kwa kuangalia wa mwanzo wao kwa uimamu katika swala za faradhi. Na Kadhi amesema: Anatangulizwa wa zamani kwa maana kwamba aliyemtangulia maiti wake. Na sisi tunaona kuwa wao wako sawa na wanafananishwa na ndugu mawalii wao iwapo watakuwa sawa kwa daraja, pamoja na kauli ya Mtume (.A.W) "Anawaswalisha watu yule aliyembora wao wa kuisoma Qur-ani" na iwapo atataka walii wa kila maiti kumswalia maiti wake peke yake basi inajuzu. [Al Mughniy 362/2, Ch. Maktabat Al Qaherah]
Na kutokana na yaliyotangulia na yanayohusiana na swali: Basi hakika ni bora kuyaswalia majeneza haya kwa pamoja badala ya kuyatenganisha kati ya kila kundi la maiti na kumswalia kila mmoja peke yake, kama tulivyokwishasema katika fatuwa, mpangilio wa majeneza unakuwa kama zilivyo safu za swala za faradhi, wanaume wanatangulizwa upande wa Imamu kisha watoto na baada yao wanawake, kuelekea kibla.

Share this:

Related Fatwas