Taazira (Uadabishaji) kwa Mali kati...

Egypt's Dar Al-Ifta

Taazira (Uadabishaji) kwa Mali katika Mabaraza ya Kimila.

Question

Imeenea katika nchi yetu ya Misri – na hasa vijijini- kitu kinachoitwa (Mabaraza ya kimila/Jadi), nayo ni mabaraza ambayo watu wamezowea kutatua baadhi ya matatizo mbali mbali na viunga vya mahakama, na baadhi ya waliogombana wanaweza kuhukumiwa kwa kutoa sehemu ya mali kama adhabu kwao kwa ajili ya kutoa fidia kwa mgomvi wao.Je ni halali kuchukua fidia hii kwa mtu aliyehukumiwa kuchukua fidia hiyo au hapana?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Taazira (Uadabishaji) ni adhabu isiyokadiriwa kisheria iliyoyawajibu katika haki ya Allah au haki ya mwanaadamu, katika kila maasi ambayo mara nyingi hayana adhabu maalumu wala kafara.Ni adhabu ambayo inahusu kumzuia muhalifu asiufanye uhalifu au kuurejea uhalifu huo.
Na asili ya (Uadabishaji) Taazira ni kuwa umeruhusiwa kisheria; Kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu….} [AN-NISAA: 34] akahalalisha au kuruhusu kupiga wakati wa kwenda kinyume au kuasi.Hayo yakaujulisha usheria wa taazira kwa mwenye haki.Na katika Sunna ni yale yaliyopokelewa na An-Nasaiy na Al-Haakim: "Kuwa Mtume S.A.W. alimuadabisha mtu mmoja kwa tuhuma, akamfunga usiku na mchana kisha akamuachia huru" [Ameipokea Abu Daud na An-Nasaiy na Ibn Majah na Al- Hakim] na akapokea Abu Daudi na An-Nasaiy na Al-Hakim kwamapokezi yao kutoka kwa Abdillahi bin Amru, Kutoka kwa Mtume S.A.W. "aliulizwa kuhusu matunda yenye kuning’inia? Akasema: Atakaye yaweka mdomoni mwake kwa shida bila kuyabeba kwapani hakuna ubaya wowote juu yake.Na atakayetoka na kitu ni juu yake kulipa gharama yenye thamani ya kilekitu alichotoka nacho na adhabu".
Na neno Al-khbuna: Ni vazi la pamba ambalo huvaliwa juu ya nguo.Na ncha ya nguo, ni sehemu anayoichukua mtu katika nguo yake na kuipandisha juu, na maana yake ni kwamba atakayekula matunda kwa kuzidiwa bila ya kuchukua kitu katika matunda hayo basi hana adhabu mtu huyo, na akichukua kitu basi ni juu yake kutoa gharama na ataadhibiwa na hivyo ni kwamba ikiwa hicho kitu alichokichukua hakikuwa chombokilichofikia kiwango cha kukatwa mkono. Na maana yake katika Hadithi ya Abdillahi bin Amru: "Hakuna kukata mkono katika mnyama, isipokuwa katika kile kilicho hifadhiwa na zizi au sehemu ya kulala wanyama kikafikia thamani ya ngao, katika hilo kuna kukata mkono.Na ambacho hakijafikia thamani ya ngao, ndani yake kuna gharama sawa na alichokichukua na kuna kupigwa mijeledi ya adhabu". Na maana yake ni kwamba kitu ambacho hakijafikia kiwango cha kukatwa mkono basi malipo yake ni kutozwa gharama pamoja na kuadhabiwa.
Na ushahidi katika Hadithi hizo mbili ni kupitishwa kwa adhabu iliyoko chini ya mipaka.Na adhabu hii ya karipio ni ibara ya adhabu kadhaa zinazoanzia na adhabu nyepesi nyepesi ambazo ni ushauri,muongozo au kutelekezwa na kumsusia.Na inaweza kufikia adhabu kali kabisa kama vile kifungo au kupigwa bakora.Na huenda ikaishia kwenye kuuwawa muda mwingine kwa baadhi ya rai za wanachuoni.Na mtazamo wa hilo anaachiwa Kadhi kwa mujibu wa kile anachokiona.Akichunga katika hilo aina ya uhalifu, muda na eneo ulipofanyika uhalifu huo pamoja na hali ya muhalifu, kwa sharti la kufikia kiwango cha adhabu ambayo ni kuzuia makosa yasitendeke na kukemea.Na aina ya adhabu za karipio (Ni kumuadabisha/kumkaripia kwa kutoa mali). Na wametofautiana wanachuoni juu ya kujuzu kwake katika kauli tatu:
Kauli ya kwanza: Inajuzu bila ya masharti.Nayo ni kauli ya Abuu Yussuf, na moja ya kauli mbili za wafuasi wa madhehebu ya Al-Hanafiyah, nayo ni kauli ya Al-Shaafiy katika madhehebu ya zamani, na kauli ya Maalik na Ahmad katika maeneo maalumu kwenye madhehebu yao. Na akaitetea kauli hiyo Taqiyu El-Din Ibn Taymiyah, na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim, na Al-Khataabiy akahusisha na Hassan Al-Basary na Ouzai na Is-haak [Rejea: Rad al Mukhtar 4/285, Ch. Dar al Fikr, wa Magmaa al Anhar 1/609, Ch. Dar Al Ihyai Aturath Al Arabiy, na Haashiyat Al-Adawiy A’laa Al-Khurashiy 8/110, Ch. Dar Al Ffikri, wa Faslu Al Maqaal fil Jawaab an Haadithat Suaal wa Nafyu al Oukuuba Bil Maal lil Ikhmimiy uk 3, Ch. Mustafa Al-Halaby, na Magmou 5/304, Ch. Maktabat Al Irshaad, na Al-Insaaf 3/189, Ch. Dar al Ihyai Aturath Al Arabiy, na Maalim Al-Sunan lil Khatabiy 2/260, Ch. Al-Matbaa Al Elmiyah. Na Magmou Fatawa li Ibn Taymiyah 28/110, Ch. Magmaa Al-Malik Fahd bil Madinat Munawarah).
Watu wa kauli hii wametoa dalili kwa kutumia Aya ya (Kafara ya kiapo) na kwa Hadithi nyingi. Ama aya za kafara,ni kauli yake Mola Mtukufu: {Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu} [AL MAIDA: 89]. Aya hii ni asili inayojulisha uhalili wa kutoza faini ya fedha kiuhalali; kwani kusema uwongo ni maasi yasiokuwa na adhabu iliyokadiriwa na inayolingana nayo katika sura.
Na katika Hadithi iliyopita ya matunda yalioning’inia, ndani yake kuna kauli: "Na atakayetoka na kitu miongoni mwayo ni juu yake kulipa gharamana adhabu", na ushahidi uko wazi.
Kati ya hizo: Hadithi ya Abuu Hurairah R.A.inasema: "Alisema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu S.A.W.: “Swala nzito kwa wanafiki ni Swala ya Isha na Swala ya Alfajiri, na laiti watu wangelitambua thawabu zinazopatikana ndani ya swala hizo basi wangeliziendea walau kwa kutambaa. Nilifikiria ni amrishe ikimiwe swala, kisha ni muamuru mtu awaswalishe watu kisha niondoke na watu wakiwa wamebeba mzigo wa kuni twende kwa watu wasio swali ni unguze nyumba zao kwa moto”. [Wamekubalina Maimamu wawili Bukharin na Muslim (Muttafak A’alaih)].
Hii iko wazi kwamba Mtume S.A.W. alikusudia kuunguza nyumba za watu ambao hawahudhurii Swala ya Jamaa, na hakuna kitu kilichomzuwia Mtume S.A.W. kufanya hivyo isipokuwa ni kutokana na kuwa ndani ya majumba hayo kuna wanawake na watoto, na katika uchomaji moto ni adhabu ya uharibifu wa mali.
Na katika hizo pia: Ni Hadithi ya Bhazi Bin Hakiim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kuwa Mtume S.A.W. alisema: “Katika kila ngamia wanaopelekwa kuchunga wakifikia arobaini basi atatolewa zaka mtoto wa ngamia aliyekamilisha miaka miwili na inaingia mwaka wa tatu, Na ngamia hatofautishwi na hesabu zake, na atakayeziwilia hakika sisi tutamchukua na nusu ya mali yake ni haki katika haki za Mola wetu Mtukufu.Si halali kwa watu wa Muhammad kuchukua chochote”. [Ameipokea Ahmad na Abu Daud na Al-Nassaaiy na wengineo].
Na Hadithi hii nidalili ya wazi kabisa kwa wenye kujuzisha.Na kwa ajili hiyo, maneno yamekuwa mengi juu yake, hadi wakadai wenyekuzuia Hadithi hii isitumike..
Na miongoni mwa Hadithi hizo: ni Hadithi ya Suwaid Bin Muqran R.A. alisema: “Aliniona mimi nikiwa mmoja kati ya watoto saba wa Muqran hatuna kijakazi isipokuwa mmoja, mdogo wetu alimpiga, akatuamrisha Mtume S.A.W. tumuache huru”.
Na katika riwaya nyingine: “Aliniona na mimi nikiwa ni wa saba kwa ndugu zangu tukiwa pamoja na Mtume S.A.W. na hatuna kijakazi isipokuwa mmoja, akaamua mmoja wetu na akampiga, akatuamrisha Mtume S.A.W. tumuachie huru”. [Imepokewa na Muslim].
Amri ya Mtume S.A.W. kumuachia huru kijakazini adhabu ya fedha, ikiwa yeye kama atamuacha huru kwa ajili ya kumuadhibu basi inakuwa ni adhabu kwake, hakunufaika naye kwa upande wa kumfanyisha kazi wala hata kwa kumuuza. Na mfano wa hayo ni Hadithi ya Abi Masoud Al Badriy R.A. alisema: “Nilikuwa nampiga kijana kwa mjeledi, nikasikia sauti nyuma yangu: Tambua ewe Abuu Masoud, sikuifahamu sauti kutokana na hasira. Akasema: Aliponikurubia, kutahamaki ni Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. mara akawa anasema: "Tambua ewe Aba Masoud. Tambua ewe Aba Masoud. Akasema: Nikautupa mjeledi mkononi mwangu, akasema: Tambua ewe Aba Masoud hakika Mwenyezi Mungu anafahamu zaidi juu yako kuhusu kijana huyu. Akasema: nikasema: kamwe sitampiga mtumwa baada ya huyu. Na katika riwaya nyingine: nikasema: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, akasema: ama laiti kama usingefanya hivyo basi ungelikugusa moto”. Imepokewa na Muslim.
Na hii inamaanisha kwamba Abuu Masoud aliadhibiwa kwa mali yake ili aokoke na adhabu ya akhera.
Na katika maana yake ni Hadithi ya kijakazi aliyepigwa kofi na bwana wake wakati mbwa mwitu alipokula mbuzi mmoja katika mbuzi wake, Mtume s.a.w. akasema kumwambia: “Yuko wapi Allah? akasema: Mbinguni. Akasema: Mimi ni nani? Akasema: Wewe ni Mtume wa Allah. Akasema: Muache huru hakika yeye ni muumini”. [Imepokelewa na Muslim].
Na katika Hadithi pia: Ni Hadithi ya Al-Baraa Bin A’zib alisema: “Alinituma Mtume s.a.w.kwa mwanaume aliyemuowa mwanamke wa baba yake baada yake ya kwamba nimkate shingo na nichukue mali yake”. [Imepokelewa na Imam Aham na As-hab Sunan].
Watu wa rai hii wametolea ushahidi pia kwa matendo ya baadhi ya maswahaba kwa kutoa adhabu ya fedha au mali.Katika hao ni Sayyidina Umar kuichoma moto sehemu iliyokuwa ikitumika kuuzia pombe, na kulichoma motoJumba la Saad Bib Abi Waqaas alipojifungia ndani yake na kuwa mbali na anaewachunga na akawa anahukumu akiwa ndani ya Jumba hilo, na kuwatuma wafanyakazi wake kuchukua nusu ya mali zao, na kumwaga kwake maziwa yaliyochakachuliwa. [Tabsirat Al Hukaam 2/293, Ch. Maktabatul Kulliyaat Al Azhariyah], Inaongezwa juu ya hayo kwa anaejuzisha kuadhibu kwa kuuwa, kwa rai basi kujuzu kuadhibu kwa fedha au mali ni bora.
Kauli ya pili: Ni kuzuia moja kwa moja, na ndiyo kauli ya Jamhuri ya wanazuoni wa Madhehebu manne [Rejea: Fat-hi Al Qadiir 5/345, Ch. Dar Al Fikri, na Hashiyat Ibn A’abidin 4/61, na Hashiyat Al-Sawiy A’alaa Shareh Al Kabiir 4/355, Ch. Dar Al-Fikri, na Faslu Al- Maqaal uk. 40, na Anaa al Matalib ya Sheikh Zakariya Al Ansariy 1/360, Ch. Dar Al Kitab al Islamiy, na Al Magmou 5/334-335, na Al Mughny ya Ibn Qudaamah 9/149, Ch Dar Al Fikri, na Sharhe al Bahutiy 6/124, Ch. A’Alami Alkutub).
Wakatoa ushahidi wa kuzuwia kwa Aya na Hadithi ambazo zinakataza kula mali za watu kwa batili, kama vile kauli yake Mola Mtukufu: {Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili] [AL- BAQARA:188], na kauli yake Mtume S.A.W. “Hakika damu zenu na mali zenu na heshima zenu ni haramu juu yenu”, na kauli ya S.A.W. “Si halali kwa Muislamu kuchukua fimbo ya nduguye bila ridhaa ya nafsi yake”. [Ameipokea Ahmad na Abu Daud na Al Tirmidhiy]. Kama walivyotoa ushahidi kwa kauli yake S.A.W. “Hakuna katika mali haki ya kuchukuliwa isipokuwa Zaka”. [Imepokewa na Ibn Maajah na Al-Tabaraaniy]. Haikutengwa haki isipokuwa zaka, na yanabakia yasiokuwa hayo katika katazo au kemeo; kwakuwa (Haki) imekuja kama Jina lisiloainika katika njia ya kukanusha nayo ina maanisha kuenea.
Lakini dalili hizi zilizotajwa na jopo kwa ujumla, na dalili za kauli ya kwanza… hukasanywa kwa mujibu wa ujumla na umaalumu.Zinachukuliwa dalili za jumla katika hali isiyokuwa ya mfanya maasi ambaye anapaswa kuadhibiwa, kama ambavyo Hadithi ya Ibn Maajah ni dhaifu. Anasema Ibn Hajar katika (Al Talkhis) baada ya kuitoa Hadithi hii: “Ibn Maajah na Al-Tabaraniy katika Hadithi ya Fatma bint Qays kwa hili, na ndani yake yupo Abu Hamzah Maymun Al- Au’ar mpokezi wake kutoka kwa Al- Shaabiy, naye ni dhaifu” [2/356, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Na akasema Al-Nawawiy: “Hadithi hii ni dhaifu sana haitambuliki” (5/335]
Wakataofautisha baadhi ya wafuasi waMadhehebu ya Maalik kati ya kuadabisha kwa mali na kuadabisha katika mali, wakajuzisha katika ya pili bila ya kujuzisha ya kwanza. [Faslu El Maqal uk 44, 45]. Na maana ya adhabu katika mali, ni hakimu kumuadhibu mkosaji kwa kuchukua mali aliyofanyia maasi au ikiwa ni sababu ya yale maasi, na anaweza kuzipeleka zile fedha katika maslahi anayoyaona kwa kutumia njia ya kujitahidi kwake.Ama adhabu kwa pesa: Ni hakimu kuchukua kutoka kwa mhalifu kiwango cha mali kwa njia ya kumtoza gharama kama kumkemea na kumuadabisha kwa maasi yake.Ya kwanza lengo lake ni kuharibu killichosababisha maasi.Na ya pili ni kuadabisha. Na wakatoa sababu ya mgawanyo huu kwa dharura ambayo inamili kwa kutokuwepo utekelezaji wa sheria na baadhi ya watu kutoizingatia katika adhabu za kimwili.
Na tunaloliona kuwa lina nguvu ni kujuzu adhabu kwa fedha, na ndiyo iliyochukuliwa na sheria ya Misri kama ilivyoelezwa katika kipengelea cha (22 cha adhabu), ambapo imeeleza kuwa adhabu ya gharama ni kumuwajibisha mtuhumiwa kutoa fedha na kuingizwa kwenye hazina yaserikali kiwango cha pesa kilicho kadiriwa kwenye hukumu, na sheria imebainisha kiwango cha gharama kwa kila kosa.
Na ipasavyo na katika uhalisia wa swali: Inajuzu kwa baraza la kijadi kumlazimisha mmoja wawenye kugombana kulipa sehemu ya mali kwa mgomvi wake.Na ni halali kwa mgomvi au hasimu kuchukua mali hiyo.Lakini ichungwe katika kukadiria adhabu iwe inaendana na kosa, isivuke kiwango ikaziidishwa, na wala isipuuziwe ikapotezwa haki, na mengine yasiyokuwa hayo ambayo yanaathari katika hukumu, na kuchukua tahadhari kwamba adhabu ya mali isije kuwa kisingizio cha kula riba, pamoja na kuweka mazingatio ya kupatikana maslahi yanayotarajiwa katika adhabu hiyo, nayo ni kumfanya muhalifu auache uhalifu wake.Na maslahi hayo yanaweza kuwa naathari hasi itakapothibitisha hukumu ya kisheria juu mtu aliyetakiwa kuadhibiwa kwa kutoa fedha kuwa anastahiki kukatwa mkono. Ni wajibu wa kila baraza la jadi kufuata inavyotakiwa, na kwa aina ambayo italeta maslahi na kwa vidhibiti ambavyo vinaafikiana na misingi ya sheria.
Na Mwneyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote

Share this:

Related Fatwas