Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa Mta...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa Mtazamo wa Kiisilamu.

Question

Je, uhuru wa vyombo vya habari unamaanisha kuukwepa ukweli au unalazimu kusema ukweli?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ni wajibu wetu kuwa na fahari ya kuwa ni wananchi katika taifa hili, na tunalifurahia kila tulionapo linatangulia na kuwa na nguvu. Na huwa tunajawa na huzuni pindi tulionapo linazama, kudidimia na kupoteza mwelekeo. Tunakuwa na bishara njema pindi tulionapo taifa letu lipo huru na linatoa kitu kipya, na huwa tunajawa na simanzi pale tulionapo linadorora au pale tumuonapo mtu anayejaribu kuharibu jina lake. Siku zote huwa tunalitafutia mema pamoja na wananchi wake na tunamili upande wa kulisifia na wala hatumruhusu yeyote kuacha kulipenda taifa hili au kuwa na mawazo potofu ya kutaka kujitenga nalo, na hapa ndipo ninapokumbukia maneno ya mshairi Abu Ulaa:
Nikaliambia: ewe jua unaedhihiri kama dhahabu, ni nani basi apingae mfano wako
Na myayusho wa fedha unatamani, unapoona mawingu yako yanapofunika mchanga
Miongoni mwa vitu vyenye kuchanganya mwenendo wa marekebisho na ufahamu wa uhuru wa vyombo vya habari ni suala hili: Je? Uhuru wa vyombo vya habari unamaanisha kuukwepa ukweli? Au ni lazima vyombo vya habari vieleze ukweli? Kwa mfano magazeti, kuna baadhi ya habari zinahitaji maelezo, na maelezo haya inabidi yatolewe, hali hii ni hali ya upeo wa juu kabisa wa uhuru wa magazeti, na ikiwa kuna nafasi ya kutaja maelezo kwa sharti yawe ni ya uhakika na ya ukweli. Na mpaka kufikia kuandika habari kwa namna hii, itampasa mwandishi awe amefanya juhudi kubwa sana si kwa kutumia akili yake ila kwa msaada wa maelezo ya kina yaliyo na ukweli. Na hali hii ndio iliyomkuta Weiter Jet, hali ambayo imepelekea kujiuzulu kwa Nixon. Na kwa asomae habari zilizowafika waandsihi wawili wa habari Bob Woodward na Carl Bernstein katika kesi hiyo mnamo mwaka wa 1974 kutokana na juhudi na fursa walizopewa za kuenza habari kwa uhuru hali ya kuamini kuwa kazi ifanywayo kwa ukweli haina budi kutoa matunda yake, na mpaka majina yao yakawekwa katika kumbukumbu kutokana na kisa cha Weiter Jet na wakatunga kitabu wakakiita “Vijana wa raisi” ambacho baadae kikatengenezewa filamu kwa jina hilohilo na kufanikiwa kupata mauzo makubwa mnamo mwaka 1976 A.D.
Na aina hii ya uhuru wa kueneza maelezo kwa kutumia vyombo vya habari inahitaji akili zenye ufahamu zilizoandaliwa kupokea habari kama hizi na kuwepo kwa uamsho uliowekwa kabla wa kuweza kupambanua, zipi habari sahihi na zipi zenye kutaka kuleta utata, na wanahabari waliobobea ambao hawaandiki isipokuwa habari zenye uhakika, wamekwisha chaguliwa na ambao hawajali isipokuwa kueneza ukweli. Na chochote wakiandikacho basi huwa kimepitiwa kwa uhakika na wala hakihitaji tena kurudiwa. Pia kuna uhuru wa maoni na mawazo na uhuru wa kutoa huduma na kwa kupitia mambo haya matatu ndio uhuru wa vyombo vya habari hukamilika kama itakiwavyo kupitia katiba ya Misri kwa kuzingatia kuwa ni chombo cha nne kinachojitosheleza.
Na mpaka kufikia hali hii, hapo ndipo vyombo vya habari vitakuwa vinaathiri wananchi wote kwa kuwajengea akili iliyozinduka, na watafanya kazi kwa ajili ya taifa lao. Hivyo, inatupasa tuwe na subira kutokana na hali tuliyonayo kwa kipindi hiki ambacho neno la Mtume (Rehma na amani zimshukie) linathibitisha kwa kusema: “Watu watajiwa na miaka ya uongo (zama za uongo) muongo ataaminiwa na mkweli ataonekana ni muongo, mwaminifu ataonekana ni mtu wa khiyana na mtu wa khiyana ataaminiwa na wapuuzi ndio watakaokuwa wakiongea,” Pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani hao wapuuzi? Akasema: “Mtu mjinga azungumzae kuhusu mambo ya Umma.”
Na kuhutubia kwa Mjinga hakuna hukumu maalumu inayoruhusu au inayozuia, na hapa ninakusudia kwamba inaweza kuwa kuna ulazima wa kufanya hivyo pindi haja itapelekea kupatikana uwezo wa kumfahamu na kuweza kupambanua kati ya zuri na baya. Baadhi ya watu hudhani kuwa sio hao wajinga tu bali hata baadhi ya wasomi wenye kujitahidi hudhani kuwa – kila lenye kufanana na tukio hili (Kuzungumza mtu mjinga) kuwa ni katika mambo yasiyofaa kabisa. Imamu Nawawiy anaona kinyume na hivyo, kwani anaelezea Hadithi ya Jibrilu ambayo imepokewa kwa sharti la Imamu Muslim ambayo inazungumzia alama za kiama na ndani ya Hadithi hiyo kuna maneno haya: “Mjakazi kumzaa Bwana wake” anasema; “ Elewa kuwa Hadithi hii haina dalili ya kuruhusu kuuzwa wazazi (Mama) wa watoto, na wala haina dalili ya kuzuia wasiuzwe, na Maimamu wawili wakubwa wametoa dalili juu ya hili jambo, mmoja wao ametoa dalili ya kuruhusu na mwengine ya kukataa.Kweli inashangaza kwa hili jambo kutokea, kwani sio kila lililoelezwa kuwa ni dalili ya kiama linakuwa haramu au jambo lisilofaa, kwani hata kujenga majumba makubwa kwa wafugaji na kuenea kwa mali na wanawake hamsini kuwa chini ya himaya ya mwanamme mmoja, haya yote sio mambo ya haramu, bali hizi ni dalili tu na wala hakuna jengine ndani yake.Inaweza kuwa mbaya au nzuri na inaweza kuwa jambo la wajibu likaunganishwa na la kupendeza, na jambo la kupendeza likaunganishwa na jambo la wajibu. Mwenyezi Mungu anasema: {Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu,na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, nauovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka} (AN NAHL; 90). Tunaona kuwa kufanya uadilifu ni wajibu na kufanya hisani ni jambo linalopendeza, pamoja na kuwapa msaada jamaa wa karibu n.k. Mtume Rehma na amani zimfikie anasema: “Mambo matano ni katika maumbile: Tohara (Jando), kunyoa, kukata kucha, kunyoa nywele za kwapani na kupunguza masharubu.” Tohara ni lazima (Wajibu) kwa mwanamme lakini kunyoa nywele za kwapani ni katika mambo yanayopendeza. Na mfano wake.
3-Na kutokana na Hadithi ya Samar bin Jundab (Mwenyezi Mungu amwie radhi) nayo ni Hadithi ndefu ndani yake kuna maneno haya yafuatayo: “Na hayo hayatakuwa hivyo mpaka muone mambo makubwa yatakayowashinda nyoyoni mwenu, na mutaulizana kati yenu je? Mtume wenu alikutajieni haya.” [Imetolewa na Ahmad katika kitabu chake 16/5. Na Ibn Khuzayma 327/2.]
Basi hii ndio hali tuliyonayo ambayo bado haijatulizana.Na kuna mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka ambayo wajinga (Wasioelewa) ndio wanaoyaongelea kwa Umma, katika kutoa nasaha na hata katika matibabu, au hata kutoa fatwa tena bila ya elimu. Na pia hata Quraani huwa hawajahifadhi isipokuwa sura ndogo ndogo.Na watu hawa wakataka kuchukua jukumu la kuongoza watu kwa ujumla, na wakawa wanaongea kuhusu ukomonisti usiokuwepo au fani mpya.Na wapo wanaotaka tusijielewe na wala tusiielewe dini yetu na historia yetu, na wapo wanaotutaka tuwe magaidi wa kimawazo ima tuwafuate wao au sote tutakwenda motoni.Na moto kwake ndio sawa na pepo na pepo ni sawa moto, kwakuwa tayari wao ni Madajjal (Waovu). Mtume (Rehma na amani zimshukie) anasema kuhusu Dajjal “Dajjal atatoka akiwa na mto na moto, atakayeingia katika moto wake atapata malipo yake na kuondoshewa makosa yake, na atakayeingia katika mto wake atabeba makosa yake na kuondoshewa malipo yake.” Abu Daudi.
4- Na kujiepusha na haya yote ni kuwa na subira na kuhakikisha kuwa uhuru unapatikana na kuwaacha waropokaji (Wajinga) wajulikanembele za watu kutokana na upuuzi wao na fikira zao finyu, na kuendelea kujenga misingi imara ya uenezaji wa habari yenye kufuata haki na yenye kujiepusha na hali tete na porojo. Na yule ambaye atakaefanya upuuzi basi na ajifunze au aone haya au ajisitiri au aamue kufanya kweli au hata ajaribu kufanya juhudi hata kama hatofikia kiwango kinachostahiki. Namimi nina matumaini mazuri kuwa hali hii ya uvivu na uchovu huenda ikamalizika. Magazeti ya kuleta msisimko yameanza kuonekana Marekani tangu mwaka 1830 na kuendelea hadi leo, na imekuwa ni kama kitu cha kufanyia kejeli kwa jamii iliyosoma pindi wamuonapo mtu kashika gazeti la namna hii mkononi mwake na kusoma, ni kama kwamba huwa wanajiuliza moyoni mwao kwa mshangao mkubwa (Je, bado unajifundisha tu?) Utamaduni huu hautachukua muda mwingi kwa sababu ya maendeleo makubwa ya kimawasiliano na teknolojia.
Na mpaka kufikia katika hali hii ni lazima tusubiri.{Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayo yaeleza.} (YUSUUF; 18) Na pia itahitajika kujitolea heshima zetu kwa ajili ya watu. Imepokewa na Abuu Hurayra (Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) kuna kijana wa kiisilamu alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu mimi sina mali za kutoa sadaka na nimeifanya heshima yangu kuwa ni sadaka. Akasema, Mtume (Rehma na amani zimshukie) kuwa hakika amesamehewa.” [Imepokewa na Ibn Barri, 1694/4.]
Na ikibidi kuwa nao mbali basi na tuwe nao mbali kwa namna nzuri. {Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa uzuri} (AL MUZZAMIL; 10) Na tushikamane nasifa za waja wa Mwenyezi Mungu, kwani anasema Mola: {Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama! 64. Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama. 65. Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi } [AL FURQAAN; 63-65] Na hayo yote ni kwa ajili ya kufikia uhuru unaopasa ambao jamii nyengine huwa wanamwaga damu kwa kuukosa (Uhuru huu), na wala hatuwezi kufikia hapo isipokuwa kwa maadili mema!
Chanzo: kitabu Simaat Al- Asr, Mufti wa Misri Profesa Ali Juma.

Share this:

Related Fatwas