Kuoana Kati ya Binadamu na Majini.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuoana Kati ya Binadamu na Majini.

Question

Nini hukumu ya kuowana kati ya binadamu na majini?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Baada ya utangulizi, Jini ni kinyume cha binadamu, na mmoja anaitwa Jinni.Inasemwa kuwa Jini: liliitwa kwa jina hilo kwa sababu ya kufichikana na halionekani. [Mukhtar Al Sahah, Mada ya: J N N].
Amesema Ibn Mandhour: “Kila kilichojificha ni jini na kwa jina hilo limeitwa jini kwa kutoonekana kwake kwa macho, na kwa maana hiyo kiliitwa kitoto kwa kujificha kwake ndani ya tumbo la mama yake, kwa jina la Jini: Ni viwiliwili vya moto vyenye nguvu za kimaumbile”. [Lisaanu Al Arab, Madah ya: J N N].

Amesema Al Baydawiy: “Na majini ni viwiliwili vyenye akili vilivyofichikana na sehemu kubwa ya miili yao ni moto au hewa”.[Tafsir al Baydawiy, 4/224, chapa ya Al maktabat al tijaariya al kubra], na kuwepo kwa majini kumethibitika ndani ya Quraani na Sunna na Ijmaa. Na mwenye kupinga uwepo wao ni kafiri kwa kukanusha kwakemambo yanayo julikana katika dini kwa ulazima wake.

Na wamekubaliana wanachuoni kuwa wao wameamrishwa na wamezungumzishwa kama binadamu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi} [ADH-DHARIYAAT: 56]. Na kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka} [AR RAHMAAN: 33], na katika Hadithi iliyopokelewa na Al Baihaqiy kutoka kwa Ibn Abbas R.A. alisema: Alisema Mtume S.A.W. "Alikuwa hapo kabla Mtume akitumwa kwa watu wake maalumu, na mimi nikatumwa kwa watu na majini".

Jini kumuowa mwanadamu akili haizuwii kutokea kwake, na kauli ya kusema kuwa majini wameumbwa na moto na wanadamu wameumbwa na udongo, kwa maana hiyo sehemu ya moto inazuwia kutengeneza mbengu za binadamu katika mfuko wa uzazi wa Jini kwa sababu ya unyevunyevu na kudhoofika kwa sababu ya joto kali la moto, hilo amelijibu Al Imam Al Shabaliy akasema: “Hakika hao majini wakiwa wameumbwa kwa moto basi sio wenye kubakia katika umbile lao la moto, bali imekuwa kitu kisichowezekana kwao wao kula na kunywa na kuzaliana,kama vile haiwezekani kwa wanadamu kutokana na asili ya udongo kufanya hivyo, na kama tukikubali kutokuwa na uwezo wa kupandikiza mbegu, italazimu kutowezekana kupandikiza mbegu wakati huohuo kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa, na dalili ya kutowezekana huko ni Hadithi aliyoitoa Abu Daoud na Al-Nassaaiy na Ahmad katika Hadithi ya Abuu Said Al-Khudriy: (kuwa Mtume S.A.W. alisimama kuswali swala ya Alfajiri na yeye akiwa nyuma yake, kikamchanganya kisomo, alipomaliza kuswali akasemma: laiti mkiniona na Ibilisi nikamuashiria au kumnyooshea mkono wangu na nikaendelea kumkaba hadi nikapata ubaridi wa udenda wake kati ya vidole vyangu hivi – kidole gumba na kinachofuatia- na kama si dua ya kaka yangu Sulaiman angekuwa amefungwa kwenye nguzo katika nguzo za msikiti watoto wa Madinah wakimchezea), aliyoyafanya Mtume S.A.W. ni dalili ya kuhama kutoka kwenye hali yake ya umotomoto.Laiti angelikuwa amebakia katika hali yake ya moto, baridi hii imekuja kutoka wapi?” [Ahkaam Al Murjan fil Ahkaam Aljaan cha Al- Shabaly Al-Dimashkiy Al-Hanafiy uk. 106, ch.. Maktabat Al-Quraani].

Na Quraani tukufu imezungumzia uwezekano huu akasema Mola Mtukufu: {Hajawagusa mtu kabla yao wala Jinni} [AR-RAHMAAN: 56], Ikajulisha kuwa Jini lina jimai na linagusa, At-tabariy akataja na riwaya mbali mbali katika hayo akasema: Kutoka kwa Ibn Abbas R.A.: Hajawagusa mtu kabla yao wala Jini, akataja na kama hayo kutoka kwa Ali Ibn Abii Twaalib na Ekrimah na Mujaahid, na akataja riwaya kutoka kwa Asim kutoka kwa Abi Al-aaliyah, inayojulisha uwezekano wa kutokea kwa ndoa kati ya Jini na binadamu na ndani yake ikiwa kama atauliza muulizaji: Na je, wanajamiiwa majini wanawake? Itajibiwa kwa kusema: (Hajawagusa mtu kabla yao wala Jinni) [Jamii Al- Bayaan fii taawil Al-Quraani 23/65, Chapa ya Muasasat Ar-Risaalah].

Amesema Al-Alousiy: “Na kukanya kugusakwa mwanadamu, ama kwa Jini akasema Mujahid na Al-Hassan: Jini linaweza kuwajamii wanawake wa kibinadamu pamoja na waume zao ikiwa kama mume hakumtaja Allah Mtukufu.Kukataa hapa ni kwa wote wenye kujamii.Na ikasemwa: Hakuna haja ya kufanya hivyo, kwani inatosha katika kupinga kugusakwa majini uwezekano wao, na hakuna shaka katika uwezekano wa jini kumwingilia mwanadamu, bila ya kuwa na mume wake asiyemtaja Allah Mtukufu” [Ruoh Al-Maaniy ya Al-Alousiy 14/118, Chapa ya Dar al-Kutub al- Elmiyah].

Amesema Al Fakhru Ar- Raaziy: “Nini faida ya kutaja majini, pamoja na kwamba majini hayafanyi jimai? Tunasema: Si hivyo, bali majini yana watoto na wajukuu, lakini tofauti ni kuwa wao, je wanamuingilia mwanadamu au hapana? Na kauli mashuhuri ni kwamba wanamuingilia, na kama si hivyo peponi pasingekuwepo familia na ujamaa au ukaribu, likawa swala la kujamiina majini wao kwa wao ni kama suala la mwanadamu na majini kwa upande wa ishara ya kukanusha.” [Tafsir al-kabiir 29/376, Chapa ya Dar Ihyaa Al Turaath Al Arabi].

Na anasema Allah Mtukufu akimweleza Ibilisi: (Na shirikiana nao katika mali na wana) [BANI ISRAIL: 64], Amesema Imam Al Qurtubiy: “Imepokelewa kutoka kwa Mujahid alisema: Atakapo fanya jimai mtu na akakwa hakusema Bismilahi hujiviringisha Jini katika njia yake ya mkojo na anafanya jimai pamoja naye. Na hii ndiyo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hajawagusa mtu kabla yao wala Jini} [AR RAHMAAN: 56], na amepokea Abu Daud na akaifanya kuwa Hasan Ibn Hajar katika kitabu al-mushkaa katika Hadithi ya mama Aisha alisema: Alisema Mtume S.A.W.: "Hakika miongoni mwenu kuna waliotengwa. Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni wepi hao waliotengwa? Akasema: Ambao Jini anashiriki katikati yao". Imepokelewa na At-tirmidhiy Al Hakim katika nawaadir al Usuul. Amesema Al Harawiy: wameitwa kwa jina hilo kwa kuwa limeingia kati yao jasho geni. Amesema At-Tirmidhiy al hakim: Jini linajisifu kwa mwanadamu katika mambo na kuchanganyikana.Wapo baadhi yao wanaowaoa” [tasfiri Al- Qurtubiy 10/289, Chapa ya, Dar al-Kutub Al- Misriyah].

Na katika kitabu cha Ain Al-Maabud Sharhe ya Sunan Abi Daud: “Amesema katika Fat-hu al Wadud: Kwa kuiwekea kasra Ar-Rau yenye shaddah- amesema: Maana yake ni waliotengwa au waliowekwa mbali na kumtaja Mwenyezi Mungu wakawa hawaingilianimpaka akashirikiana nao shetani.Na makusudio ya mtunzi kuileta Hadithi hii katika mlango huu: ni kuwa duwa wakati wa kuingilia ina athari kubwa na kinga kwa majini na mashetani.Wallah A’alam” [Aun Al-Maabud Sharhe Sunan Abi Daud 14/9, Chapa ya .Dar Al Kutub Al-Ilmiyah].

Na ama ndoa ya Jini kwa mtu, kwa maana ya Jini kumuoa mtu haijuzu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu) [AN-NAHL: 72], na kauli yake Mtukufu: {Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbienu wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu} [AR-ROOM: 21].

Amesema Al-Zamakhshariy katika Al-Kashaaf: “(kutokana na nafsi zenu) maana yake kutokana na jinsi yenu” [Al- Kashaaf 2/620, Chapa ya Dar- Al Kitab Al Arabiy].

Amesema Imam Al- Raaziy: “Na maana yake: Kuwa yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaumba wanawake ili waolewe na wanaume” [Al-Tafsir Al-Kabiir ya Al-Raaziy 20/244, Chapa ya Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy].

Amesema Al-Qurtubiy: “(Wake zenu kutokana na nafsi zenu) maana yake kutokana na Adam ameumbwa Hawaa. Na ikasemwa pia: Maana yake amejaalia kutokana na nafsi zenu, yaani kutokana na jinsi zenu na aina zenu na maaumbile yenu” [Tafsir Al-Qurtubiy 10/142].

Na akasema Al-Baydawiy: “(Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu) yaani kutokana na maumbile yenu ili mliwazanena ili wawe watoto wenu mfano wenu” [Tafsir Al-Baydawiy 3/234]

Na Mtume S.A.W. amekataza ndoa ya majini, amesema Harb Al-Kurmaaniy katika mas-ala yake kutoka kwa Ahmad na Is-haak: Alitueleza Muhammad Bin Yahya Al-Qatiiy: Alitueleza Bishir Bin Umar: Alitueleza Ibn Luhay’-ah kutoka kwa Yunus Bin Yaziyd kutoka kwa Al-Zuhariy alisema: (Alikataza Mtume S.A.W. kuhusu ndoa ya majini). Na Hadithi kama ni mursal basi inapewa nguvu na kauli za wanachuoni, na inaharamisha kwa kuepusha mlango wa ufisadi/uharibifu ambao unaweza kuongezeka. Ameambiwa: Hakika hapa kuna mwanaume Jini anamchumbia kijakazi anadai kuwa yeye anataka halali, akaulizwa Maalik R.A. hukumu ya binadamu kuowana na majini? Akasema: Nina chukia nitakapomkuta mwanamke ni mjamzito akiulizwa: Nani mume wako? Akasema: Ni katika majini, ufisadi utaenea katika Uislamu kwa sababu hiyo”, anakusudia kuwa mzinifu anaweza kutoa sababu kuhusu mimba yake kuwa inatokana na kuolewa kwake na Jini, na kwa kuwa ufisadi utakaopatikana ni mkubwa, vipi yatakuwa matumizi, malezi na unyonyeshaji na ni nani atawalazimisha kutekeleza hukumu ya mahakama? Na tutahukumiana wapi? Katika mahakama zetu au mahakama zao? Madhara yanayopatikana ni makubwa kuliko maslahi yanayodhaniwa kupatikana. Imeharamishwa ndoa ya aina hii kwaajili ya kuondoa madhara. Hutangulizwa manufaa, na kwa kuwa Allah Mtukufu ameweka mapenzi huruma na utulivu katika ndoa, vipi itakuwa kwa ndoa hii ambayo haitokei ndani yake isipokuwa udanganyifu na wasiwasi katika moyo na akili!

Amesema Al-Haskafiy Al-Hanafiy: “Ndoa kwa wanachuoni wa sheria ni mkataba unaoelezea milki ya starehe maana yake uhalali wa mwanaume kustarehe na mwanamke wake ambapo hakikuzuwia kizuwizi chochote cha sheria kumuowa mwanamke huyo. Na hapo hahusikimwanaume, na huntha kwakujuzu uwanaume wake, na maharimu, na Jini, na zimwi la majini; kwa tofauti za kinjinsia” [Ad-Dur Al-Mukhtar 3/4, Chapa ya Dar Al-Kutub Al Elmiyah].

Ibn A’abidin ametoa maoni katika maneno yake akasema: “Na kauli yake: Na majini, na zimwi la majini, kwa dalili ya hoja ya tofauti ya maumbile; kwa kuwa kauli yake Allah Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu} [AN-NAHL:72], amebainisha muradi katika kauli yake: {basi oeni mnao wapenda katika wanawake} [AN-NISAA: 3], ni mwanamke katika wasichana wa binadamu kwa hiyo hauthibiti ufumbuzi mwingine bila ya dalili; na kwakuwa majini yanajiweka katika sura na maumbile mbali mbali, anaweza kuwa Jini mwanaume akajiweka katika umbile la kike, na yaliyosemwa ya kwamba atakayeuliza kuhuusu kujuzu kuyaowa majini inatokana na ujinga wake wa kutokuuwaza upande huo; kwa kuwa kuleta picha kuwa inawezekana kutokana na kuthibiti kwa Hadithi kujibadilisha kwao kimaumbile, athari na hikaya nyingi, na kwa ajili hiyo imethibiti makatazo ya kutowauwa baadhi ya wanyama kama ilivyoelezwa katika mambo ya karaha katika suala la kuwa kutofikiria hivyo haijulishi ujinga wa muulizaji kama ilivyosemwa katika Al-Ashbaah. (angalizo) katika Al-Ashbaah kutoka kwa As-sarajiyah: Haifai kuowana kati ya wanaadamu na majini, na zimwi maji; kwa tofauti ya kimaumbile. Faida ya ushirikiano ni kwamba haifai kwa jini kumuowa mwanadamu nayo ni faida ya hoja pia”.

Amesema Ibn Najym: “Na baadhi yao wametoa dalili ya kuharamisha ndoa ya majini kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat An-NAHL: {Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu} [AN-NAHL: 72], maana yake kutokana na jinsi mlivyo na aina zenu na katika maumbile yenu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe} [AT TAWBAH: 128], yaani katika binadamu, mwisho. Na baadhi yao wametoa dalili kutokana na yaliyopokelewa na Harb Al-Karmaniy katika masuala yake kutoka kwa Ahmad na Is-haq kutoka kwa Al-Zuhariy alisema: (alikataza Mtume S.A.W. kuwaowa majini), nayo ikiwa ni mursal basi inapewa nguvu na kauli za wanachuoni, akapokea zuwio hilo kutoka kwa Al-Hasan Al-Basary na Qatadah na Al-Hakm Ibn Uyainah na Is-Haak Ibn Rahawayhi na Uqbah Ibn Al asam R.A. itakapo amulika kuzuwia binadamu kumuowa Jini, basi zuwio la jini kumuowa mwanadamu ni bora zaidi, na kinachojulisha hilo ni kauli yake katika Al-Sarajiyah: haifai kuowana, nayo inawakusanya wote” [Al-Ashabah wa An-Nadhair ya Ibn Najym 31409, Chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elimiyah].

Amesema mshereheshaji wa Al-Ashabaah Ahamad Al-Hamuwiy: “Imenidhihirikia kutosihi binadamu kumuoa jini mwenye kuambatana na mtu, nako ni kusema kwamba: Asili katika tupu ni haramu isipokuwa sheria ilitoa idhini katika ndoa au kuwaowa wanawake katika wanaadamu kwa kauli yake Mtukufu: {Basi oeni mnao wapenda katika wanawake} [AN-NISAA: 3], na wanawake ni jina la kike la wana wanadamu kama ilivyo katika Aakam Al-Murjan, wakabakia wanawake wasiokuwa binaadamu katika asili ya uharamu” [Ghamz Uyuun Al-Basaair 3/408, Chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elimiyah].

Amesema As-Suyutiy “katika masuala ambayo sheikh Jamal Al-Din Al- Esnawiy aliyauliza kwa Kadhi wa makadhi Sharaf Al-Din Al-Baarziy: Ikiwa atahitaji kumuowa mwanake Jinni – kwenye dhana ya uwezekano- je hiyo inaruhusiwa au inazuwiliwa?hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu} [AR-ROOM: 21], akamsifia Al-Baarziy Allah Mtukufu kwa kufanya hivyo kuwa ni katika maumbile yanayozoeleka. Na ikiwa tutaruhusu hivyo je? Atalazimishwa kuhusu kubakia katika makazi au hapana? Na je? katika kuzuwia ni kutokana na kujiweka katika umbile lisilokuwa la binadamu wakati anapoweza, kwa kuwa inaweza tokea hali ya kukimbiana au hapana? Na ataaminiwa katika mambo yanayohusiana na masharti ya kusihi ndoa kama vile walii na kutokuwa na vizuizi au hapana? Na inaruhusiwa kukubali hayo kutoka kwa kadhi wao au hapana? Na je atakapomuona katika sura isiyokuwa ile aliyoizowea na akadai kuwa ndiye, ataaminiwa na kujuzu kwake kumuingilia au hapana? Na je wanalazimishwa kufanya mambo waliyoyazowea kutokana na nguvu zao, kama vile mifupa na mambo mengine itakapo wezekana kula vitu vingine au hapana? Akajibu: Haruhusiwi kumuowa mwanamke Jini, kwa dhana ya Aya mbili tukufu; kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat AN-NAHL: {Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu}[ AN-NAHL: 72], na kauli yake katika surat AR-ROOM: {Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu} [AR-ROOM:], wamesema wafasiri katika maana ya aya hizo: (Amekuumbieni wake katika jinsi yenu), maana yake kutokana na jinsi mlivyo, aina zenu na katika maumbile yenu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe} [AT TAWBAH: 128], yaani katika wanaadamu; kwa kuwa wale ambao ni halali kuwaowa ni: Wasichana wa baba wa dogo na wajomba, akaingia katika aya hiyo aliye mwisho kwa umbali wa undugu, kama inavyofahamika katika aya ya Surat Al-AHZAAB: {Na mabinti ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama yako} [AL-AHZAAB: 50], na waliyoharamishwa ni wasiokuwa hao, na wao ni asili na matawi, na tawi la asili ya kwanza na tawi la kwanza katika asili zilizobakia, kama ilivyo kwenye aya ya kuharamisha katika Surat AN NISAA, na haya yote ni katika nasaba, na hakuna nasabu kati ya majini na wanadamu. Hili ni jawabu la Al-Bariziy. Ukisema: unanini katika hayo? Nitasema: ninayo yaamini ni uharamu, kwa njia: miongoni mwa njia hizo: ni aya mbili zilizo tangulia. Na nyingine: ni kama alivyoyapokea Harb Al-Kurmaniy katika masuala yake kutoka kwa Ahmad na Is-haaq wamesema: Alitueleza Muhammad Bin Yahya Al-Qatiiyi, alitueleza Bishri Bin Umar, alitueleza Ibn Luhay’ah kutoka kwa Yunus Bin Yaziyd kutoka kwa Al-Zuhariy alisema: (Alikataza Mtume S.A.W. kuhusu ndoa ya majini). Na Hadithi hii kamani Mursal basi inapewa nguvu na kauli za wanachuoni.Akapokea zuwio hilo kutoka kwa Al-Hasan Al-Basary na Qatadah na Al-Hakam Ibn Uyainah na Is-Haak Ibn Rahawayhi na Uqbah Ibn Al asam. Amesema Al-Jamaal Al-sajastaaniy akiwa ni katika Al-hanafiyah katika kitabu cha “Minyat Al Muftiu An Al Fataawa al Sarajiyah”: hairuhusiwi kuowana kati ya majini na watu, na zimwi la majini kwa tofauti ya kijinsi au kimaumbile. Na miongoni mwake: ni kuwa ndoa imefanywa kuwa sheria kwa sababu ya kujenga ukaribu,utulivu,kuliwazana, na mapenzi, ambayo hayapo kwa majini, bali kilichopo kwao ni kinyume ya hayo, nao ni uadui usioisha. Pia katika dalili hizo: kuwa haikupokelewa idhini ya kisheria katika hilo, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {basi oeni mnao wapenda katika wanawake} [AN-NISAA: 3], na wanawake ni jina la wanawake wa wanaadamu tu, na waliobakia kinyume na hao wanaingia katika uharamu, kwa asili katika ndoa ni haramu hadi ipokelewe dalili ya kuhalalisha. Na pia katika dalili hizo:ni kwamba mtu huru asiyekuwa mtumwa amezuwiliwa kuoa kijakazi; kutokana na matatizo anayoyapata mtoto kutokana na utumwa.Na hakuna shaka kwamba kutokana na jini kusababisha madhara, hakuna wasiwasi wowote kimaumbile hata kitabia. Na kuwasiliana nao na kuchanganyikana kuna matatizo zaidi ya madhara ya utumwa ambao matumaini ya kuondoka kwake ni makubwa.Itakapozuiwa kumuowa kijakazi pamoja na kuwa ni jinsi moja kwa tofauti katika aina, kuzuwiliwa kuowa asiyekuwa katika jinsi au aina moja ni bora zaidi. Na ufumbuzi huu una nguvu zaidi.Sijaona aliyeutilia maanani. Unapewa nguvu pia kuwa imekatazwa punda kumrukia farasi, na sababu ya hilo: Kwa kutofautiana kijinsia na kitakachozalika kati yao kinakuwa katika umbile la nyumbu, kinalazimu kuuwawa.Na katika hadithi ya kukataza, kutoka kwa Ali Bin Abiy Twaalib: (Hakika wanafanya hivyo wale wasio jua), kuzuia hayo kutokana na haya tuliyataja ni bora zaidi. Na itakapokuwa imeamulika kuzuia, kuzuia ndoa ya jini na mtu ni bora na ni vizuri” [Al- Ashbaah Wa Al –Nadhaair lil- As-Yutiy uk. 257, Chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elimiyah].

Amaesema sheikh Al-Islam Sheikh Zakariya Al-ansaariy Al-Shaafiiy: “Amesema Ibn Yunus: katika vizuizi vya ndoa ni kutofautiana kinjisia.Haifai kwa mwanadamu kumuoa Jinni.Na kwa kauli hiyo alitoa fatwa Al-Baariziy kwa kauli yake Allah Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu} [AN-NAHL: 72], na akapokea Ibn Abi Ad-Dun-ya “alikataza kuwaowa majini" [Asnaa Al-Mataalib Sharhe Raud Al-Taalib 3/163, Chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy].

Amesema Al-Khatiib Al-Sharbiniy: “Haifai kwa mwanadamu kumuoa Jini kama alivyosema Al-Emaad Bin Yunus, na akaitolea fatwa Ibn Abd al- Salaam. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake} [AL- A'RAAF: 189], akasema tena Mola Mtukufu: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile} [AN-NISAA: 1], na akapokea Ibn Abi Ad-Dun-ya “Alikatakaza Mtume S.A.W. kuwaoa majini” [Mughniy Al-Muhtaj lil-Khatib As-Aharbiyniy 4/286, Chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elimiyah].

Na akasema Ibn Mufallah Al-Hanbaliy: “Katika Mughniy na katika vitabu vinginevyo kuwa wosia haufai kwa jini kwani yeye hawezi kumili kwa kumilikishwa kama vile zawadi, anakabiliwa na kuzuilika kujamiiana na binadamu kwa kukosa uwezowa kumiliki,kwa kuwa hali hiyo ipo katika mkabala wa mali, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu} [AN-NAHL: 72], na akasema Mola Mtukufu: {Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbienu wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu} [AR-ROOM: 21], na wametaja watu wetu maana hii katika sharti la usawa, na hapa inakuwa ni bora, na wamezuia hilo waliowengi miongoni mwa waliokuja baadae katika wafuasi wa Madhehebu ya Hanafiy, na baadhi ya Al-wafuasi wa Madhehebu ya Shaafiy. Na katika masuala ya Harb mlango wa kuowana na majini: kisha akapokea kutoka kwa Al-Hassan na Qatadah na Al-Hakam na Is-Haak kuchukizakwake, na akapokea katika riwaya ya Ibn Luhay’ah, na kutoka kwa Yunus, kutoka kwa Al-Zuhariy: “Alikataza Mtume S.A.W. kuwaowa majini” [Al-Furuui Li Ibn Mufallah Al-Hanbaliy 1/605. Chapa ya A’alam Al Kutub].

Kutokana na hayo yaliyotangulia, Jini kumuoa mwanadamu inawezekana kiakili lakini ni haramu kisheria. Na Allah ndiye ajuwaye zaidi.

Share this:

Related Fatwas