Kukusanya Michango ya Sadaka kwa As...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kukusanya Michango ya Sadaka kwa Asilimia Kutoka Katika Michango Hiyo.

Question

Kuna hukumu gani ya kisheria kwa yanayofanywa na baadhi ya jumuia za kutoa misaada kutokana na kaukli yao: "Kusanya michango ya sadaka na una fungu lako ndani yake?" na hata kama jambo hili linajuzu, basi ni mipaka gani ya fungu ambalo linajuzu kwa mkusanyaji wa michango kulichukua?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Inajuzu kuchukua ujira wa fedha kwa mkusanyaji wa michango ya sadaka kama ile ya misikitini, na jambo hili lina dalili kadhaa, na miongoni mwake ni kauli ya Mwwenyezi Mungu Mtukufu: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia} [AT TAWABAH: 60], Basi hiyo ni dalili ya kuchukua mali kama ujira wa kukusanya Zaka ya wajibu. Hakuna shaka yoyote kuwa kutoa sadaka kunajuzu zaidi kutokana na kuwa kwake sunna.
Ibn Al Arabiy alisema: kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na wanao zitumikia; na wanaoifanyia kazi} nao ni wale wanaokuja kwa ajili ya kuikusanya zaka, na wanapewa jukumu hilo la kuikusanya; na hii ni dalili ya kwamba jambo hili ni ufanisi wa hali ya juu, nayo ni kwamba vinavyokuwa katika fardhi za kutoshelezeana basi inajuzu kwavyo kuvichukulia ujira. Na hii ndio asili ya mlango huu. Na Mtume S.A.W. akaashiria katika hadithi yake sahihi: "Nilichokiacha baada ya kutoa matumizi ya familia yangu na chakula cha wafanyakazi wangu ni sadaka)), na dalili ya kuwa huo ni ujira ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amemmilikisha yeye hata kama ni tajiri". [Ahkaam Al Quraani 524/2, Dar Al Kutub Al Elmiya]
Wanazuoni wamekubaliana juu ya mfanyakazi wa Taasisi ya Kukusanya Zaka kwamba anastahiki kulipwa ujira wa kazi yake. Na ingawa wanachuoni hao wametofautiana kuhusu kiasi cha ujira huo anaoustahiki kwa kazi yake. Na kilicho sahihi ni kwamba mtumishi huyu ana malipo sawa na watumishi wenzake katika milango mbali mbali ya Fiqhi, kama hapatakuwapo sharti yoyote kinyume cha hivyo. Kwani waislamu hufuata masharti yao waliojiwekea.
Ibn Qudamah Al Hanbaliy alisema: "Akichukua jukumu la kutoa mgao ataanza na msambazaji na atampa kiasi chake kwani yeye huchukua kwa kulipia haki yake kwa uhakika kuliko yule anaechukua kwa ajili ya liwazo tu. Na Imamu anapaswa kumteua Msambazaji kabla ya kumtuma na anatakiwa amtume bila ya sharti lolote kwani Mtume S.A.W, alimtuma Omar R.A, kama msambazaji na wala hakumlipa ujira wowote, na aliporejea akampa ujira huo. Na iwapo Imamu ataainisha kiwango cha ujira basi atamlipa, au laa si hivyo atamlipa ujira unaofanana na wa watumishi wengine". [Al Kafiy 332/1, Ch. Al Maktab Al Islamiy]
Na Sheikh Eleesh Al Malikiy alisema: "Kwa hiyo kazi ya ukusanyaji wa Zaka inaswihi kwa mtumwa, mtu wa kabila la Hashimiy na hata kwa kafiri. Na watapewa ujira wao unaolingana na kazi zao kutoka katika Hazina ya Mali ya Waislamu (Baitul Mali). Na katika masharti ya mtumishi pia awe mwanaume aliyebaleghe, na mtumishi huyo atapewa sehemu ya fedha ya zaka iwapo atakuwa fakiri au masikini bali hata akiwa tajiri; kwani ujira huo ni kwa ajili ya kazi alioifanya. Na pameanzwa kwa kupewa mtumishi sehemu ya ujira unaolingana nae, na atapewa ujira wote iwapo utakuwa ni kiwango cha ujira unaolingana na kazi yake." [Manhi Al Jalel 87/2, Ch. Dar Al Fikr]
Na katika dalili pia ni Kipimo cha yaliyopokelewa kwenye Mlango wa Wakfu; ambapo ni sheria kumpa Mwangalizi ujira wake kwa kazi yake ya kuhifadhi Wakfu na kuiboresha, kwani sharti ni ujira kwa kuwa jambo hili limekubaliwa na wanazuoni, laa si hivyo atapewa ujira unaolingana na kazi yake. [Tazama: Al Bahr Araaiq Sharh Kanz Adqaiq 254/5, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy, Hashiyat Adsuqiy Ala Asharhu Al kabeer 88/4, Ch. Dar Al fikr, Mughniy Al Muhtaaj Sharhu Menhaju Atwalebeen 394/2, Ch. Dar Al Fikr, Sharhu Muntaha Al Iradat 395/2,Ch. Dar Al fikr]
Al Bukhariy alipokea kutoka kwa Abi Hurairah R.A. kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Warithi wangu wasigawane Dinari au Dirhamu kwa kile nilichokiacha baada ya matumizi ya wake zangu. Na malipo ya wafanyakazi wangu ni sadaka." Al Hafedh Bin Hajar katika sharhi yake: "Na jambo hili lina maana kuwa ni sheria kumpa ujira Mtumishi wa Wakfu, na maana ya mtumishi katika Hadithi hii ya Mtumeni ni mfanyakazi na mtumishi au Kiongozi baada ya Mtume S.A.W." [Fateh Al Bariy 406/5, Ch. Dar Al Maarifah]
Na Ibn Nujaim akasema: "Kinachopatikana katika yale aliyoyataja Khaswafu ni kwamba kile anachokifanya mtoa wakfu kwa mtawala hakina kiwango maalumu bali ni kwa mujibu wa ilivyozoeleka kwa watu katika kitoelewacho wakati pale mtoa wakfu anapopitisha uamuzi ili aweze kufanya kwa masilahi yake kama nyumba na matumizi yake au kuuza nafaka na kutoa kile kilichokusanyika kwake kwa namna ambayo mtoaji wa wakfu ameshurutisha, na wala habebeshwi jukumu la kazi hiyo yeye mwenyewe isipokuwa atafanya kama wafanyavyo watu wengine kama yeye. Na wala haifai kwake kupuuzia. Ama kwa upande wa kile kinachofanywa na walipaji na wawakilishi hivyo sio wajibu juu yake hata kama ataufanya utawala kuwa chini ya mwanamke na akamwandalia ujira maalumu basi hatabebeshwa jukumu mwanamke huyo isipokuwa kwa kiasi wafanyacho wanawake kama ilivyotambulika. Lau watu wa Wakfu watagombana na watumishi na wakamwambia mtawala hakika Mtoa Wakfu amefanyiwa hivi kwa malipo ya kazi yake naye hafanyi kazi yoyote, Mtawala hambebeshi jukumu la kazi ambayo haifanywi na watawala. Na iwapo utasema: mweka wakfu anaposhurutisha kuwapo kwa msimamizi, mletaji na mfanya mahesabu, sasa kila mmoja kati ya hao ana kazi gani? nitasema: Kuamrisha na kukataza, kuendesha na kuweka mikataba pamoja na kushika fedha ni kazi ya Msimamizi, na ukusanyaji wa mali kwa wenye kukodisha kila mwezi na kutoa mali hiyo ni kazi ya mkusanyaji, na kuzipanga mali na kuzipima ni kazi ya mfanya mahesabu. [Al Bahr Araaiq Sharh Kanz Adqaiq 264/5, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy].
Sheikh Taqiy Edeen Ibn Taimiah akasema: "Na mtu atakaetoa wakfu kwa ajili ya mwalimu au wanachuoni, kwa hiyo msimamizi kisha Kiongozi watakadiria cha kuwapa…kwani kimetangulizwa chenye thamani na kinachofanana nacho kwa kuwa anachokichukua ni ujira na kwa ajili hiyo ni haramu kuchukua zaidi ya ujira unaomfaa bila ya kuwapo sharti lolote." [Sharhu Muntaha Al Iradat 503/2, Ch. Dar Al fikr]. Na hatukunukulu kutoka katika vitabu vyake, kutokea usahihishaji ndani yake kuhusu maudhui hii.
Na katika mlango wa Mlezi kukuza mali ya Yatima, ni ruhusa kwa mlezi au kwa alieusiwa, kuifanyia biashara mali ya yatima, huku pakiwepo tofauti kati ya wanazuoni kati ya uwajibu na uzuri wa kufanya hivyo. Pamoja na tofauti kati ya wanazuoni, juu ya kwamba je inajuzu kwa mtu alieusiwa Yatima kufanya hivyo au hapana budi ampe mtu mwingine aiwekeze mali hiyo. Na tofauti hii kati ya wanazuoni sisi hatuizungumzii kwa kirefu ukiongezea kuihakiki tofauti hiyo. Kilicho muhimu kwetu hapa ni kukubalika kimsingi kuifanyia biashara mali ya yatima, na asili yake ni kuzuia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima.} [AL ANAAM 152]
Asarkhasiy akasema: "Na mtu aliyeachiwa mayatima, anapaswa kuchukua hatua kwa namna ambayo ndani yake yatima anakuwa na mtazamo wake binafsi wa kufanya biashara yeye mwenyewe au kwa nusu ya mali kama alivyofanya Aisha R.A. katika mali ya mtoto wa ndugu yake au aitumie mali yake kwa kuwekeza au aitoe kwa mtu mwingine ili awekeze, kama Omar R.A alivyokuwa akitoa mali ya yatima kwa ajili ya kuiwekeza. [Al Mbswot 99/21, Ch. Dar Al Maairifa]
Malik akapokea kutoka kwa Yahya kwamba alisema: "Aliwanunulia watoto wa ndugu yake waliokuwa mayatima chini ya ulezi wake biashara na akaiuza kwa faida kubwa baadae. Amesema Malik: ((hakuna ubaya wowote wa kuifanyia biashara mali ya mayatima kwa ajili yao, ikiwa mlezi anaaminika. Sioni kuwepo kwa aina yoyote ya dhamana." [Al Mwatwa Uk. 251, Ch. Dar Ihyaa Aturaath Al Arabiy].
Na Al Mawardiy akasema: "Inajuzu kwa Mlezi wa yatima kuifanyia biashara mali ya yatima huyo kwa masharti yanayozingatiwa ndani yake, na hili ni tamko la wanachuoni wote. Na Omar Bin Shuaib akapokelea kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake kwamba Mtume S.A.W. akasema: "Zifanyieni biashara mali za yatima haziliwi kwa zaka. Na imepokelewa (zifanyieni biashara katika mali za mayatima haziliwi kwa zaka)". Na ilipokelewa kwamba Omar Bin Al Khatwab R.A. alifanya biashara kwa mali ya yatima aliyekuwa akimlezi, na ilipokelewa kwamba Aisha R.A. alifanya biashara baharini katika mali za watoto wa ndugu yake Mohamad Bin Abi Bakr, walipokuwa mayatima na yeye alikuwa akiwalea, na haukuwa kwa maswahaba hao wawili pingamizi yeyote bali ilikuwa na ijmai ya wanachuoni.
Na kwa kuwa (Mlezi) katika mali ya mtoto yatima, anachukua nafasi ya mtu mzima aliye na akili katika mali yake mwenyewe, kwa kuwa vitendo vya mtu mwenye akili ni kuitumia mali yake kibiashara, kwa hiyo Mlezi wa yatima ni mwakilishi mwenye uwezo wa kuitumia kibiashara kwa kuwekeza mali hiyo kwa yule anayeaminika. Na biashara ni katika sababu zenye nguvu mno kwa kuzalisha mali hiyo na Mlezi ni bora zaidi kufanya hivyo kuliko mtu mwingine yeyote. [Al Haawe 361/5, Ch, Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Al Bahutiy akasema: "Inapendeza kuifanyia biashara mali ya yatima kwa kauli ya Omar na wengine ((zifanyieni biashara mali za mayatima ili msizile kama sadaka)) na Walii (mlezi) wa yatima au mwendawazimu anaweza kuitumia mali ya yatima au mwendawazimu katika kuwekeza kwa mtu mwaminifu ambaye ataifanyia biashara kwa kuchukua sehemu ya faida kwani Aisha R.A, aliitumia mali ya Muhammad bin Abuu Bakari R.A, na kwa kuwa Walii (Mtunza) ni mwakilishi wa mtu aliyezuilika kuitumia fedha yake katika kila jambo ambalo lina masilahi na mtu huyo." [Kashaaf Al Qinaai 449/3, Ch. Dar Al Fikr]
Jambo hili haliishii tu katika uchukuaji wa fedha kwa matokeo ya kufanya kazi ya fedha, bali jambo hili ni pana zaidi kuliko hivyo, kwa hiyo inajuzu kuchukua mali kwa kumuajiri mtu wa kufanya baadhi ya ibada kama vile kufundisha na kumsomea mtu dua kwa namna ambayo inakuwa ni kwa njia ya Fardhi za kutoshelezeana, kama vile Ibnul Arabiy alivyotangulia kusema. Na hili ndilo sahihi na lenye nguvu katika maneno ya wanazuoni.
Ibn Qudamah akasema: "Na kumkodi mtu kwa ajili ya kufanya ibada ya hija, kuadhini, kufundisha Qurani na Fiqhi, na elimu nyingine, kwa kila chenye kuleta manufaa, na mfanyaji wake anatakiwa awe mtu wa karibu, kuna mapokezi mawili: mapokezi ya kwanza, haijuzu, na hiyo ni madhehebu ya Hanafiyah na Ishaqa. Na mapokezi ya pili: inajuzu, na hayo ni madhehebu ya Malik, Ashafiy na Ibn Al Munzer, kwani Mtume S.A.W. amesema: "Kitabu cha Mwenyezi Mungu kina haki zaidi kulipiwa kwa kile mlichokifanya", imepokelewa na Al Bukhariy, na maswahaba wa Mtume S.A.W. walichukua ujira kwa kuomba dua kwa Quraani na wakamwambia Mtume S.A.W. kwa tendo hilo basi akafikiana nao.
Na kwa sababu inajuzu kuchukua malipo juu yake, kwa hiyo inajuzu pia kumpa ajira kwa malipo kama vile kujenga msikiti na majumba… na iwapo tutasema: inajuzu kumkodishia mtu anaehiji. Inajuzu kutulipia kwa mwenye jukumu bila ya kukodisha, kwa hiyo hukumu yake inakuwa kama ilivyotangulia. Na iwapo mtu anamkodisha mtu ili amfanyie mtu ibada ya hija au amfanyie ibada hiyo mtu aliyekufa, masharti ya ukodishaji yatazingatiwa; kama vile kujua ujira utakaotolewa, mkataba wake na kile atakachokichukua kama ujira atakimili. Na ni halali kwake kukitumia atakavyo. [Al Mughniy 224/3, Ch. Aktabat Al Qahira]
Sheikh Taqiy Adeen Ibn Taimia anasema: "Inajuzu kwake achukue ujira kwa kufundisha Fiqhi, Hadithi na Elimu nyinginezo iwapo atakuwa anahitaji. Na huu ni mtazamo wa Madhehebu haya." [Al Ekhtyarat Al Fiqhia 491/1, Ch. Dar Al Maarifah]
Kutokana na hayo yaliyotangulia: Inajuzu kukusanya misaada ya fedha na kuchukua kiasi kidogo cha misaada hiyo kwa mujibu wa makubaliano. Na ujira wa mfanyakazi ukawa kwa malipo yanayolingana na kazi yake, kwa sharti tu asivunje taratibu na sheria za uendeshaji wa kazi zilizowekwa na Taasisi za Nchi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukfu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas