Haki za Binadamu Katika Uislamu na...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu Katika Uislamu na Mahusiano yake na Mtazamo wa Uislamu kwa Binadamu

Question

Ni yapi mahusiano kati ya mtazamo wa Uislamu kwa mwanadamu na mtazamo wake katika haki za binadamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1. Hakika mwanadamu katika Uislamu ananafasi ya juu, na umuhimu wa kipekee ambao haupatikani kwa viumbe wengine ukiwatoa malaika, mwanadamu ndio mbora wa viumbe juu ya ardhi, na mwenye heshima, na mwenye cheo cha juu na mtukufu wao, kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amemdhalilishia vilivyomo ndani ya ulimwengu ili anufaike navyo, na aimarishe ardhi {Na hakika tumewatukuza wanadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba} [AL ISRAA: 70].
2. Kadhia ya kwanza mbayo Uislamu unataka kuifanya kuwa kauli mbio ya ujumbe wake ni kumchukuwa mwanadamu katika kumuelekeza ili ahakikishe mambo yaliyopo katika uhalisia wake miongoni mwa sifa zinazomfanya kuwa bora kuliko viumbe vingine. Uislamu unahifadhi heshima ya mtu, kwa ajili hiyo umetoa wito wa kuhifadhi dini, nafsi, akili, utu na mali, ukaharamisha kufanya uadui juu ya haki hizi.
3. Kama ambavyo Uislamu unalinda pia heshima ya kundi, kwa maana hiyo ukahifadhi uhuru wake, na ukatupilia mbali kutumia nguvu zake za kiutu au vyanzo vyake vya kiuchumi, ukahifadhi utu wake usifanyiwe uadui kwa njia yeyote ile.
4. Na ustarabu wa sasa ni mkusanyiko wa maswali yote, haukuliacha swali kuhusu sehemu katika sehemu za mwanadamu ambapo halikutafuta jawabu lake, na maswali haya hayana majawabu kinyume na (Imani ya dini) inamkusanya mwanadamu aliyosafi mwenye kuifahamu dunia yake, na mwenye imani safi kwa mambo ya ghaibu yake yasiyojulikana, unamkusanyia msingi wa kuwa na imani na akili yake, na msingi wa kuwa na imani na maisha, na sio zaidi ya (Misingi na akida “Imani”) ambayo tunayoisikia katika ustarabu huu mpya.
5. Kama ambavyo majibu ya ustarabu wa sasa vyovyote utakavyokuwa, ni majibu tu ya zama ambayo yanatatua tatizo la muda, na hayavuki kwenda kwenye tatizo la milele: Tatizo la maswala yaliyopita, na yaliyokuja katika zama, na yanayokuja bila kuwa na mwisho, na hakuna majawabu ya haya yote isipokuwa itikadi ya kidini ambayo anaiamini mwanadamu au anatakiwa aiamini.
6. Itikadi hii ipo kama inavyotakiwa kuwepo, na ama upotevu ni kwa yule anaoutaka katika vitu vingine ambavyo unasimamia au kutegemea, na haisimamii juu ya kitu kingine, itikadi hii ya kidini haipo leo ili kesho itupiliwe mbali, itikadi hii ndiyo msingi wa maisha, nguzo zake ni zama na nyumati, maisha na matumaini.
7. Hakika ustaarabu wa kisasa tangu ujitokeze hadi utakapofikia mwisho wake, umekuwa ukimuonesha mwanadamu na ubinadamu, itikadi baada ya itikadi, na mpaka hivi sasa hatujawahi kuona, kwamba kilichooneshwa kiwe cha kale kinachokaririwa mara kwa mara au kipya kilichovumbuliwa katika itikadi kwamba ni bora kuliko ya Quraani tukufu. Na yaliyo bora zaidi ndani ya Itikad hii ni kwamba ina utajiri mkubwa na majaribu, na ni katika sharti la Akida ya Dini yenye ubainifu ulio hai, itikadi ambayo imewakusanya mamilioni ya viumbe, na imewaimarishia umoja wao yenyewe peke yake katika kila aina ya mapambano, siku ambapo nguvu za watu wanazozitegemea ziliwatupa
8. Muadilifu yeyote hawezi kushauri kuhusu utu na ubinadamu kwa itikadi ya utu na ubinadamu iliyosahihi na yenye kufaa kuliko itikadi ya Quraani. Iliusikiliza utu na ubinadamu kwa vitu vya kihistoria ikasema kuwaambia: Binadamu ni sarafu ya kiuchumi, na ubinadamu haupo pamoja na makundi yanayoutengenezea bei na malipo. Na ukasikiliza utu na ubinadamu kwenye ufashisti, ukasema kuwaambia: Hakika mwanadamu ni mmoja anayetokana na asili ya bwana, na hakika wana wote wa ubinadamu ni waja wa asili ya bwana, na kitu kilichopo kiukweli ni mtu mmoja, na dalili ya ukweli wa uwepo wake ni afanye anavyoweza katika manufaa au maudhi, kila anapoamini mwisho wa watu wengine na matukio, na rai nyinginezo tofauti na hizo na madhehebu.
9. Ama mwanadamu katika itikadi ya Quraani yeye ni kiumbe mwenye kuwajibika kati ya viumbe vyote alivyoviumba Mwenyezi Mungu, anaamini kwa akili yake vile alivyoviona au kusikia, na anaamini kwa dhamiri zake yale mambo ya siri, yasiyofikiwa na macho wala masikio.
10. Na ubinadamu katika itikadi ya Quraani ni familia moja tokea wale waliopita hadi wale wajao baadaye, wana nasabu moja, na Mungu Mmoja, mbora wao ni yule mwenye kufanya mema, na akajikinga na maovu, akawa na nia ya kweli katika mema aliyoyafanya.
11. Mwanadamu: Kiumbe mwenye Majukumu.
12. Quraani imeinyanyua dini kutoka katika itikadi za ukohani, ukati kati, na vitendawili na kuwa imani au itikadi yenye uongofu na kuongoza….. hakuna kosa ikiwa ( kiumbe mwenye kuwajibika)) ni katika sifa bora ambazo imezitaja Quraani kuhusu mwanadamu, ima kwa kuhusika na maagizo, au kwa ujumla katika kuonesha sifa na kashfa kuwa ni katika asili yake na vitendo vyake.
13. Mwanadamu ni muhusika wa matendo yake- mtu mmoja na kundi- mtu mmoja haadhibiwi kwa dhambi za mtu mwingine, wala umma haudhibiwi kwa dhambi za umma mwingine {Kila mtu lazima atapata alicho kichuma} [ATT'UR, 21], {Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao} [AL BAQARA, 132].
14. Na majukumu yamesimamia katika nguzo: Kufikisha, elimu, na kazi. Ama kufikisha, haifai kufuata kwa yeyote ambaye hajafikiwa na wito au mlingano {Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa} [YUNUS: 47]. Ama elimu, hakika aya ya kwanza katika kitabu aliyoipokea mwenye wito S.A.W. ilikuwa ni amri ya kusoma na kuisifia elimu {Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui} [AL-A'LAQ:1-5].
15. Ama kazi yenyewe imewekewa sharti ndani ya Quraani kwa kumkalifisha kazi ambayo nguvu ya mwanadamu inaweza kuifanya, na harakati anayoifanya kwa ajili ya Mola wake na nafsi yake; {Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo} [ AL- BAQARA, 286], {Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe} [ AN NAJM, 39].
16. Mwandau: Kiumbe mwenye akili aliyekalifishwa.
17. Nafasi ya mwanadamu katika Quraani ni nafasi yenye utukufu katika mizani ya imani, na katika mizani ya fikra, na katika mizani ya viumbe ambayo inapimiwa tabia za viumbe kati viumbe wote.
18. Ni kiumbe aliyekalifishwa, na hii ndio sahihi katika kumuelezea mwanadamu kuliko kauli ya wanaosema kuwa mwanadamu ni kiumbe mwenye kuongea, na ni kauli yenye heshima zaidi kwa mwanadamu, na Quraani imejaa maelezo yanayoilenga na kuzungumzia (akili) kwa yote inayoyamiliki, na kila kazi iliyojulikana kwa wenye akili na wenye busara, kabla ya kuwa (akili) ni somo wanalolizungumzia wasomaji. Akili katika Uislamu ni uelewa wa ufahamu alionao mtu na ambao humzuia na yale yanayokataliwa na utu uzima. Nayo ni ufahamu na fikra inayobadilika katika nyuso za vitu na ndani ya mambo, nayo ni muongozo unaopambanua kati ya uongofu na upotevu, nayo ni mtazamo na mazingatio, nayo ni ufahamu unaotekeleza nyuma ya macho, nayo ni kumbukumbu inayochukua kutoka muda uliopita kwa ajili ya muda wa sasa, na inakusanya mazingatio ya yaliyokuwa kwa yale yanayokuwa.
19. Akili katika Uislamu kwa maana zote hizi imeunganishwa kwa kila hoja miongoni mwa hoja za makalifisho, na kuamrisha mema, na kila katazo katika yaliyokatazwa, na zaidi yaliyomo ndani ya Quraani katika kuelezea hayo ni: {Je! Hamzingatii?} [AL ANBIYAA: 10], {ili mpate kufikiri} [AL BAQARAH, 266], {Basi hamfikiri?} [AL -AN-A'AM, 50], {Je! Hawaoni?} [ASSAJDAH, 27].
20. Hakika akili hii kwa kila kazi miongoni mwa kazi zake inayoamrishwa ni hoja kwa waliokalifishwa katika mambo yatakayowasaidia katika mambo ya ardhini na mbinguni, na katika mambo ya nafsi zao na mambo ya muumba wao, kwao wao kama alivyosema kuwahusu: {Na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto} [AL I'MRAN, 191].
21. Wakati ambao zilikuwa nyumati kabla ya Uislamu zikifahamu kuwa utume ni kujua mambo yaliyofichikana na kufichua siri, ambavyo hutumiwa katika kurejesha kitu kilichopotea, kurejesha kilichoibiwa, na kupata hapa katika mambo ya kheri na shari, na zipo nyumati zinazoufahamu utume kama ni upatanisho kati ya anayeabudiwa na waja wake kwa lengo la kuwaombea uongofu. Ukaja utume wa Uilamu na mambo ambayo hayajatokea katika wito wa dini, kwa kuwa unamzungumzia mwanadamu sifa zake zenye kubakia, na hasa zile zenye kuhusika naye nayo ni akili. Utume wa Uislamu ni utume wa kufahamu na muongozo, na wala sio Utume wa kupeleleza na kutabiri, nao ni utume wa uongofu kwa kuzingatia na kutazama na kufikiria, na wala sio Utume wa mambo yasiyokuwa ya kawaida na vitisho vyenye kutisha macho na ufahamu, na kutishia dhamira kwa kuhofisha na ugaidi ambao unaeleweka kukubali ushawishi.
22. Hakika ni Utume wenye kubashiri haumiliki manufaa wala madhara {Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu ninge jizidishia mema mengi, wala ovu lisinge nigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa watu wanao amini}[ AL- A'RAAF: 188]. Utume wa Uislamu ni Utume wa akili na makalifisho, na kwa ajili hii ulifaa kuwa Utume wa mwisho.
23. Kwa ajili hiyo hakika Uislamu kwa kusimama kwake katika kuikinaisha akili yenye majukumu kwa aya za ulimwengu umehitimisha hoja na dalili za mapadri na viongozi kama ilivyohitimisha hoja za Mitume kwa miujiza na mambo yaliyonje ya desturi, Uislamu haukubali udhuru wa mtu anayezorotesha akili yake kwa kutii hadithi za uongo, au kuwatii mabwana wenye kiburi, au kuwatii mapadri wenye kuvaa usultani wa dini kwa ajili ya mali.
24. Kunatofauti ya mbali kati ya imani inayoifuta akili, na imani inayoifanya akili kuwa lengo la matendo yake, kisha anajuwa wapi inaanzia, na wapi inaishia imani, hakika imani hapa ni matokeo ya kazi ya akili na lengo la juhudi zake, na sio matokeo ya uvivu na kubatilisha kuwepo kwake. Lakini akili yenye mipaka haiufikii uwepo wa moja kwa moja usiokuwa na mipaka, kwa hiyo akili iseme: Kuwa hakuna kuamini kwa uwepo huu wa moja kwa moja ambao siufikii. Akili haisemi haya, lakini akili inaposema kwa ulazima wa imani katika yale ya sahihi haiwezi kuyaona haitakuwa imefuta kazi zake, na kubatilisha uwepo wake, bali kwa hivyo inafikia lengo la matendo yake, ni akili inayozidi juu yake imani. Na akili inayozidi juu yake imani ndiyo akili ambayo Quraani imeizungumzia kwa kuipa majukuma au kuikalifisha, nayo ni akili ya Muumin ambaye anasaidiwa na utume kwa kumbashiria na kumkumbusha.
25. Mwanadamu: Roho na mwili.
26. Imani ya roho ni moja ya imani za ghaibu katika Quraani, na imani ya ghaibu ni msingi wa kina katika misingi ya uchamungu, inayosimamia juu yake kila dini inayoikubali dhamiri ya mwanadamu, lakini fadhila za kwanza katika imani za ghaibu ni kuwa haivurugi akili za waumini, wala kubatilisha makalifisho kwa kuihutubia akili yenye majukumu. Imani kwa roho haikuilazimisha akili ya mwanadamu kinyume miongoni mwa vinyume ambavyo huipasua akili kati ya vinyume viwili, na haikuifunga nafsi ya mwanadamu kwa fundo la kuchanganyikiwa kati ya maumbile mawili. Roho na mwili katika Uislamu ni milki binafsi ya ubinadamu, iliyokamilisha uhai, na moja yao haipingi au kukataa katika njia ya nyingine, haijuzu kwa muumini kuunyima mwili haki yake ili kutekeleza haki ya roho, na wala haifai kuinyima roho kwa ajili ya kutekeleza haki ya mwili, na wala hatosifiwa kwa kufanya israfu katika kutafuta radhi za huyu, wala radhi za yule, {Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia} [AN NAH'L, 9].
27. Hakuna utata katika Uislamu kati ya roho na mwili, na wala hakuna mzozo kati ya dunia na akhera: {Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia} [AL-QAS'AS, 77].
28. Kufanya jitihada katika dunia sio upotevu wa njia ya akhera, na hakuna katika Uislamu kati ya roho na mwili, au kutengana kati ya akili na mada, au kukatika kati ya mbingu na ardhi, bali ni imani katika muongozo mmoja, unaifanyia vizuri roho, kama inavyoufanyia mwaili bila israfu, wala kufanya ujeuri.
29. Mwandamu: kusimamia amana.
30. Amana/uaminifu katika Uislamu inamaanisha majukumu, ahadi/mkataba na uwajibikaji, {Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu na ardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanaadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhaalimu mjinga} [AL-AH'ZAB: 72]. Na amana inamaanisha kuvumilia tabu za makalifisho, na kusimamia, na ameielezea kwa neno amana ikiwa ni tanabahishi kuwa amana hiyo ni haki za kuangaliwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kaziweka kwa waliopewa jukumu hilo, na akawaaminisha juu yake, akawajibisha juu kuipokea kwa utiifu mzuri na unyenyekevu.
31. Mwanadamu: Majukumu na uhuru.
32. Katika masharti ya makalifisho: Utiifu na uhuru, katika Quraani tukufu kuna mazungumzo yenye kujirudia kuhusu akili, na ubainifu wenye kujirudia kwa ajili ya kumuhukumu mwanadamu mwenye akili kwa kheri na shari, ikiwa ni pamoja kumuegemezea matashi yeye mwenyewe katika kustahiki kwake malipo au adhabu, na katika Quraani pia kuna aya za wazi zinazoegemeza matashi kwa Allah Mtukufu, na inaeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye muumba mwenye kukadiria, ambaye anakadiria uongofu na upotevu, na anampa kila kitu mja wake, na kumuongoza, na yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mwenye kufanya atakalo ambaye anawaumba viumbe wake, na anaumba wayafanyayo, ili awe mwanadamu roho na mwili ni katika uumbaji wa Allah, na ili yawe makalifisho ya mwanadamu ni utashi kutoka kwa Allah.
33. Ama utashi wa mwanadamu akili haikubali kuwa ni utashi wa mtu mmoja pekee anayekwenda hivihivi bila masharti, na kama si hivyo yenyewe kwa yenyewe ingelikuwa na sharti kwa mwanadamu mwengine, na vipi mwanadamu huyu mmoja anakuja na matakwa yake moja kwa moja akiwa yeye pekee kati ya wanadamu wenzake wanaokwenda kwa masharti.
34. Na hapa yakawa matakwa ya mwanadamu na uhuru wake upo katika wigo wa makalifisho, na wala hakuna katika akili kitu kinachoitwa uhuru wa kuchapishwa, unaopita kwenye vikwazo vyote, kwa kuwa kupita katika vikwazo vyote ni jambo lisilokubalika, na lisilokuwepo.
35. Na pia ikiwa Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu ikiwa ni mwenye kukalifishwa, hakika makalifisho yanahitaji uhuru na matakwa katika kuchagua mpaka lipatikane hilo kalifisho, na kwa ajili hiyo katika Uislamu ni kwamba unapondoka uhuru na matakwa basi huanguka kalifisho. Mwanadamu haufahamu mtazamo ambao ni mtukufu na wenye heshima kwake kuliko mtazamo wa Uislamu, na akili ya mwanadamu haifahamu -mfano wa Uislamu- madhehebu yaliyompa anachostahiki, haukumpuuzia bila kumkadiria au kumuheshimu na kumsababishia hasara, na hakumpa nguvu yake ikamshindishwa. Na wala mwanadamu hafahamu mfano wa makalifisho haya matukufu ambayo yamempa utiifu na uhuru, wala hakuna mfano wa uhuru huu unaomnyanyua mwanadamu, na wala haumshushi.
36. Mwanadamu: Familia moja:
37. Uislamu umemuweka mwanadamu katika sehemu sahihi pale alipofanya mgawanyo wake sahihi kuwa ni mtoto wa mwanaume na mwanamke, na kuwa anajinasibisha kwa watu wake kabila lake na kwenye familia ya binadamu. Na familia ya binadamu haifadhilishi kati ya udugu bila ya matendo mema, na bila uchamungu {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari} [AL H'UJURAAT: 13].
38. Na wingi katika Uislamu umefanywa ili iwe ni sababu ya nguvu ya kuunganisha mahusiano ya kufahamiana, na kumfahamisha mwanadamu siri zote za kuumbwa kwake, na wingi unajuhudi na mbinu za kutoa hazina za ardhini, na kushindana kwenye mambo ya kheri {Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri} [AL MAIDAH: 48].
39. Hakika muungano huu katika mahusiano ya mwanadamu umefungwa kibwebwe na mshikamano kati ya watu wote katika mahusiano na Allah, Mola wao, na Mola wa viumbe vyote, ambaye anawafanya sawa kati yao, na kuwafanyia dini yao kwa rehema na uadilifu. {Na Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu, hapana Mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu} [ AL BAQARAH: 163].
40. Hakika ulimwengu wa mwanadamu ni neno lisilofahamika kwa wanaomuamini Mola mwingine asiyekuwa Mola wa viumbe vyote, na hakika misingi ya tabia njema inapokatika sababu kati ya mema na maovu, na kati ya malipo na adhabu, na hakika ubinadamu ni wenye kukusanya kitu kisichokuwepo kabla ya kuwepo mwanadamu mwenye majukumu muhusika.
41. Lakini yupo mwanadamu mmoja, mwanadamu analingana na mwanadamu wakati wa kumuamini Mola Mmoja Pekee, Mola wa watu na Mola wa viumbe vyote, mbora wao mbele yake ni mchamungu wao, na mbora wao ni mwenye kuwatangulia katika mambo ya kheri.
42. Hakika maadili ya matendo na tabia hayatakuwa na uadilifu pamoja na imani– kama imani ya Bani Israil- kwa Mola ambaye ndiye Mola wa aina hii au watu maalumu, kati ya Mwenyezi Mungu kuumba makabila asiyoyachagua, na watu au mataifa asiyoyatazama. Ni vipi utapatikana ubinadamu wa aina moja chini ya mfano wa imani kama hii.
43. Na hakika maadili au misingi hii ni upuuzi kwa watu wanaostahiki dhambi na yale waliyoyafanya, na msamaha unaondoka kwao, na waliyopanda kwake, na wanageuka geuka kati ya neema na mateso bila ya hatia ya dhambi, na bila uombezi wa toba, na bila nia ya kufanya uovu, wala nia ya kukufuru.
44. Na kwa ajili hiyo kama tulivyosema: Hakika ulimwengu wa kibinadamu ni neno lisilofahamika kwa watu wenye kumuamini mola asiyekuwa mola wa viumbe. Na hapa inakuwa haukupatikana ulimwengu wa kibinadamu, na haukupatikana ubinadamu chini ya staarabu zote hizi, isipokuwa chini ya kivuli cha ustaarabu unaomuamini Mungu Mmoja, na kuwa ubinadamu unatokana na asili moja, na kuwa marejeo yake ni mamoja, ama staarabu na madhehebu na falsafa zinamtoa mwanadamu goigoi/mzembe “mjinga”, na mwanadamu mbaya.
45. Na kufuatia mtazamo huu wa wazi na wa kina kuhusu mwanadamu katika Uislamu unakuja mtazamo wa Uislamu katika haki za binadamu, na ulipokuwa mtazamo kwa mwanadamu ni wa kina, yakawa yote yaliyojengewa juu yake katika mitazamo kikawaida yanakuwa ni ya kina zaidi.

Share this:

Related Fatwas