Kutoweka kwa Wasifu Unaozingatiwa Katika Uchukuaji wa Zaka na Yanayojitokeza Juu Yake
Question
Ni ipi hukumu kwa anayepewa mali ya zaka kwa ajili ya kukidhi haja zake -kama vile mtu mwenye madeni au msafiri- kisha baada ya kuchukua mali haja yake ikatoweka? Je, analazimika kuirudisha mali hiyo au inakuwa miliki yake?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Na asili ya suala hili ni tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu ulio faradhishwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.} [AT-TAWBAH 60]
Zaka zimewekewa watu hawa wenye idadi maalumu bila ya kuwapo wengine. Na Fakiri: Ni yule asiyekuwa na mali na wala hana chumo lolote, kwa hiyo huyu atakuwa katika nafasi ya mafukara kutokana na haja yake aliyonayo. Na asili ya neno hili "Fakiri" katika lugha ya Kiarabu ni kama vile mtu aliyejeruhiwa katika uti wake wa mgongo. Na Masikini: Ni yule mwenye mali au chumo lisilomtosheleza kukidhi mahitaji yake. Na asili ya neno hili "Masikini" kwa lugha ya kiarabu ni kama vile kushindwa kwake kumemweka chini.
Na wafanyakazi wake: Ni wale wenye kuhangaikia makusanyo ya Zaka. Na wale walio wageni katika Imani: Ni watu waliosilimu na nia yao bado ina unyonge ndani yake, kwa hivyo wanaliwazwa nyoyo zao kwa Zaka, au mabwana ambao kuwapa wao Zaka na kuwalea kunaweza kukawafanya wenzi wao wakasilimu.
Na watumwa: Na kuna kuitumia Zaka kwa ajili ya kuwakomboa watumwa, kwa kumsaidia mtumwa (aliyekuwa na mkataba na bwana wake) kwa sehemu ya Mali ya Zaka ili aweze kujikomboa. Na imesemwa pia ni kumnunua mtumwa na kumwacha huru au kuwakomboa mateka.Kuachana na herufi 'lam' kwa herufi 'Fii' katika Aya ya Qurani, kumetokea ili kuashiria kwamba kustahiki kwa upande mmoja sio kwa ajili ya Mtumwa. Na ikasemwa pia kuwa ni kwa ajili ya kutoa idhini kwamba wao wana haki zaidi kupewa hiyo Zaka.
Na Wenye Madeni: Ni wale wanaodaiwa bila ya kuhusika na maasi au matumizi mabaya kama watakuwa bado hawawezi kuyalipa Madeni hayo, au kwa ajili ya kuwasuluhisha watu hata kama ni matajiri, kwa kauli ya Mtume S.A.W.: "Sadaka haiwi halali kwa kumpa tajiri isipokuwa kwa mambo matano: Kwa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye deni, au kwa mtu aliyelinunua deni kwa mali yake, au kwa mtu mwenye jirani masikini akatoa sadaka yake kwa masikini huyo na masikini akaitoa mali hiyo kumpa tajiri kama zawadi au mfanyakazi katika Zaka".
Na katika Njia ya Mwenyezi Mungu: Na katika kuitumia kwenye Jihadi kwa kuwapa watu waliojitolea na kwa kununulia vifaa kama vile farasi na silaha. Na imesemwa pia katika ujenzi wa madaraja na viwanda. Na Mpita Njia wa Mwenyezi Mungu: Yaani Msafiri aliyeishiwa fedha. [Tafseer Al Baidhawiy 85-86/3, Ch. Dar Ihiyaa At Turaath Al Arabiy]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja aina nane na kuzigawa kwa mafungu mawili: Ya Kwanza. Ina maana ya kuwa na haki ya mali ya Zaka kwa kutaja herufi ya (Lam) katika Aya ya Qurani, herufi ambayo inafidisha umiliki: {Wa kupewa sadaka ni Mafakiri, na Masikini, na Wanao zitumikia, na wa kuzipa nguvu nyoyo zao}, na hili ndilo lisemwalo na wanachuoni kwa uchukuaji endelevu.
Na kundi jingine lina maana ya kuwa na haki ya kupewa zaka kwa herufi ya (Fii) iliyopo katika Aya ya Qurani, herufi ambayo inafidisha kiambishi elezi, na hili ndilo lisemwalo na wanachuoni wa Fiqhi kwa uchukuaji angalifu.
Na Inajengeka juu ya hayo kwamba aina yoyote miongoni mwa zile zilizomo kwenye kundi la kwanza, kama sifa yake inayozingatiwa ilitoweka kukosekana katika uchukuaji wa Zaka –kama ufakiri kwa mfano - basi Zaka hairudishwa.
Na kwamba aina yoyote miongoni mwa kundi la pili, kama aina hiyo ilitoweka kwa kutokuwa na wasifu unaozingatiwa katika uchukuaji wa Zaka -kama deni kwa mfano- basi Zaka itarudishwa.
Al Fakhru Rraziy alisema: "Wenzetu wakasema: Na udhibiti wa fungu (sehemu ya) mtumwa ni kumpa bwana wake anaemmiliki kwa idhini ya Mtumwa aliyeandikishiana naye. Na dalili juu ya hili ni kuwa Mola Mtukufu amethibitisha kuwa Zaka zitolewe kwa watu wa aina nne waliotangulia kutajwa hapo kabla kwa kutumia herufi ya (Lam ya Umiliki ndani ya Aya ya Qurani) na hayo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wa kupewa sadaka ni Mafakiri, na Masikini, na Wanaozitumikia, na wale wa Kuzipa nguvu nyoyo zao}, Na alipomtaja mtumwa, badala ya kutumia herufi ya "Lamu" katika Aya ya Qurani, akatumia herufi ya Fii, badala yake, na akasema: {katika kukomboa Watumwa}. Kwa hiyo tofauti hii lazima iwe na faida, na faida yenyewe ni kuwa aina hizo nne za wapokeaji wa Sadaka zilizotangulia kuelezwa hapo kabla, hupewa mafungu yake ya Sadaka ili wayatumie watakavyona. Ama kwa upande wa Watumwa, wao fungu lao huwekwa kwa ajili ya kuwakomboa utumwani, na wala hawapewi wao binafsi na hawawezi kulitumia fungu hilo watakavyo, bali huwekwa kwa ajili ya Mtumwa na hulipwa kwa ajili yao tu. Na hivyo hivyo ndivyo ilivyo kauli kwa wale wenye madeni, nao mali hutolewa kwa ajili ya kuyalipa madeni yao, na kwa wapiganaji pia mali hutolewa kwa ajili ya kuwaandalia mahitaji yao ya kivita, na kwa msafiri vivyo hivyo.
Na ifanywayo katika Zaka: Kwamba katika aina nne za mwanzo: Wao hupewa mali ili waitumie watakavyo, na katika aina nne za mwisho: Wao hawapewi mali, bali mali hiyo hupelekwa kwa pande za mahitajio yanayozingatiwa katika sifa ambazo kwa ajili yake wao wanastahiki kupewa mafungu ya Zaka." [Mafateeh Al Ghaibu 86/16, Ch. Dar Ihyaa Al Turaath Al Arabiy]
Al Bahutiy alisema: "(Na atakapolipwa) yaani mdaiwa (mwenye deni) (mali atakayoitumia kulipia deni lake, haitajuzu) kwake (kuitumia mali hiyo katika kitu kingine hata kama mtu huyo ni fakiri); kwani yeye huchukua mali hiyo uchukuaji wa mchunga (na iwapo mdaiwa atapewa mali) kutoka katika Zaka (kwa sababu ya ufakiri wake, inajuzu kwake kulipia deni lake) kwa kuimiliki mali hiyo miliki kamili. Ataitumia Mali hiyo jinsi atakavyo kama ikiamuliwa hivyo, basi msingi wa madhehebu ni kama alivyoutaja Almajdu na kufuatwa, na pia akamfuata katika matawi na mengine: (Ni kwamba atakayechukua kwa sababu inayopelekea hivyo bila tatizo –kama vile Ufakiri, Umasikini, au Ufanyiaji kazi au Ugeni katika Dini– basi ataitumia kama afanyavyo kwa mali yake nyingine aliyonayo. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaongezea wao Zaka, kwa hivyo herufi ya Lamu katika Aya ni kwa ajili ya kumiliki.
Na hata kama haitakubalika kuichukulia hivyo kwa sababu ya kuitumia kwake mali hiyo aliyoichukua yeye kama fungu maalumu, kwa kutothibitika umiliki wake juu ya mali hiyo kwa upande unaostahiki kuichukua, kama sio hivyo, basi atairejesha, kama vile wachukuavyo: Mtumwa mwenye kuandikishiana na bwana wake, Mdaiwa, Mpiganaji, na Msafiri. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaongezea Zaka kwa neno "Fii" (lililopo katika Aya), na neno hili ni kiambishi kielezi. Na kwa kuwa wanne wa mwanzo wanachukua kwa maana kuwa inapatikana Milki kwa kuchukua kwao, nayo ni kuwatajirisha Mafakiri na Masikini, na kuwapendezesha dini wageni katika Uislamu, na kulipia ujira wa watumishi wa Zaka, na wengine huchukua maana ambayo haikupatikana kwa kuchukua Zaka, basi wakatawanyika. Na kwa ajili hii, hurejeshwa kilichochukuliwa katika Zaka kutoka kwa Mtumwa mwenye mkataba na bwana wake, Mdaiwa, Mpiganaji na Msafiri iwapo Mtumwa huyo au Mdaiwa wataondoshewa dhima, au aliyechukua deni akawa hadaiwi au akabaki nalo, au pamoja na kubaki na msafiri." [Kashaafu Al Qenai 282/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Hii inahusika na kundi la kwanza, ama kundi la pili, huondoshwa ndani yake Mtumwa mwenye mkataba na Mpiganaji; ama kwa upande wa wakwanza ni kwa kumpoteza anaye husika, na ama kwa upande wa pili ni kwa mfungamano wake na nchi baada ya kubadilika hali katika maandalizi ya Jihadi tofauti na ile iliyotangulia, hawakubakia isipokuwa Mdaiwa na Msafiri.
Kwa upande wa mdaiwa, Jamhuri ya wanachuoni imesema kuwa iwapo hatakuwa na haja ya mali baada ya kuchukua Zaka kabla ya kuitoa katika deni lake basi atapokonywa zaka hiyo, na pia iwapo atasamehewa deni lake, au akalilipa bila ya kuitumia zaka, au akalipiwa na mtu mwingine. Na Albahutiy amelizungumzia jambo hili katika kitabu chake cha Kashfu Al-Qanai juu ya mdaiwa.
Na Sheikh Adarder alisema: "Na akikaa kwa maana akaishi ugenini baada ya kupewa zaka, basi atapokonywa isipokuwa awe fakiri katika nchi yake kama vile Mpiganaji aliyeamua kukaa bila ya kwenda vitani nae atapokonywa na hufuatiwa hali hii na mtu aliyeitoa mali na alikuwa tajiri na katika upokonyaji wake kutoka kwa mdaiwa hutosheka baada ya kuichukua na kabla ya kuilipia deni, na kutopokonywa hutokea (kwa kusitasita) ni kwa Al Lakhmiypeke yakeAmesema: Na kama ingelisemekana kuwa atapokonywa naye, basi ingelikuwa ni mwelekeo basi amechagua ya kwanza na basi ni bora zaidi kwa mwandishi kwamba anasema na akachagua kupokonya kutoka kwa mdaiwa aliyekuwa ni mtoshekaji. [Asharhu aL Kabeer 898/1, Ch. Dar Al Fikr].
Imamu Nawawiy alisema: "Wamesema jamaa zetu kuwa Mdaiwa hupewa Zaka iwapo atakuwa na deni, na akililipa deni hilo au dhima ya deni ikamwondoka hatapewa Zaka kwa sababu hiyo isipokuwa atapewa kiasi cha mahitaji yake, na iwapo atapewa kitu na hakulipia deni lake kwa kitu hicho bali akaondoshewa dhima ya deni hilo au akalipiwa au yeye akalilipa sio kwa mali ya Zaka bali kwa mali ya mtu mwignie, basi kuna njia mbili moja wapo na ambao mwandishi ameikubali na wengine ni kwamba hurejeshwa kutoka kwake kwa kutoihitaji mali hiyo. Na njia ya pili ameisimulia Araafiiy na wengine kwamba kinyume na ile iliyotangulia, kwa Mtumwa Mwenye Mkataba na bwana wake iwapo atalipiwa deni basi hata kuwa na dhima ya kulilipa, na iwapo atapewa kitu katika mali ya Zaka na akalipia deni kwa kutumia baadhi ya mali hiyo kwa hiyo kilichobaki kina njia mbili na Mwenyezi Mungu anajua.
Amesema Ibnu Kajji katika kitabu cha: [Atajriid], "Lau mtu alibeba jukumu la kuchukua Fidia ya aliyeuawa, tukampatia, ikaja kujulikana kuwa yeye ni muuaji na akalinda Fidia hiyo, basi itarejeshwa kwa Mdai aliyepokea kwa kile kilichochukuliwa na kutumiwa kwa Mdai mwingine. Na ikiwa alikikabidhi kwawenye kustahiki deni hakitarejeshwa kwake na wala muuaji hatatakiwa kulipa Fidia, kwani Fidia hiyo imeondoka kwa kulipa. Amesema iwapo atajitolea kuilipa itachukuliwa na kuingizwa katika Baitul Maali.Na lau tulimpatia ili ailipe kwa ndugu wa Marehemu aliyeuawa na watu wakamwondoshea dhima ya kulipa kabla hajawalipa basi mali hiyo itarejeshwa." [Al Mjmou' Sharh Al Muhadhab 209/6, Ch. Dar Al Fikr]
Ama Msafiri, Jamhuri ya wanazuoni imeona kwamba pesa alizozichukua zirejeshwe kama hatatoka katika mji aliko pita na sio fakiri katika mji wake, na wakahitilafiana je?atarejesha alichokichukua hata kama atasafiri kisha akarejea na akawa hajazitumia fedha hizo alizozichukua au alizitumia kiasi na nyingine zikabaki?Na maneno ya Al Bahutiy katika kitabu cha [Kashfu Al Qanai] yalitangulia kumwelezeaMsafiri.
Na Al Kharashiy alisema: "Mgeni akidai kuwa yeye ni Msafiri basi ataaminika iwapo atakuwa katika hali ya ufakiri, kwani hana amjuaye hapo alipo. Amesema Malik: Atampatia wapi amjuaye?Na hali yake iko wazi bila ya kuapa.Na iwapo atakaa basi atapokonywa pesa aliyopewa kamavile mpiganaji alivyopokonywa. Kwa maana kwamba wote wawili, Msafiri na Mpiganaji.Mpiganaji anapochukua Zaka kwa ajili ya vita au Msafiri anapochukua mali kwa ajili ya safari yake alikotoka na akawa hajafanya hivyo, bali akaamua kukaa, basi hupokonywa Zaka hiyo na kurejeshwa sehemu yake, isipokuwa kuchukua kwake kuambatane na ufukara wake au kitu kingine chochote, basi mali hiyo haitachukuliwa." [Sharhu Mukhtaswar Khalili 219/2, Ch. Dar Al Fikr].
Na Al Khatweb Asherbiniy alisema: "(Na mpiganaji hupewa) imekuja wakati wa kutoka kwake kama ilivyozungumzwa kwenye kitabu cha [Raudhwa], na asili yake ni (Msafiri) vile vile kwa kumpimia juu yake... (na iwapo hawatatoka) pamoja na wenzao hata kama wanajiandaa kwa vita na safari (atarejesha) kutoka kwao mali walioichukua, kwa kuwa sifa ya kustahiki kupewa mali hiyo haijapatikana.Na Jamhuri ya wanazuoni haijazungumzia kiwango ambacho inawezekana kukichelewesha.Na Sarkhasiy amekikadiria kiwango hicho kuwa ni siku tatu.
Angalizo: Muktadha wa maelezo ya mwandishi ni kwamba Mpiganaji na Msafiri wakitoka na wakarejea na wakabakisha kitu basi hakirejeshwi kutoka kwao. Ama Mpiganaji iwapo atapigana vita na akarejea na akabaki kuwa na kitu katika mali aliyoichukua na wala hajaitumia yeye mwenyewe basi itarejeshwa hiyo iliyobakitu. Ni kwamba imebainika kuwa mtoaji yuko juu zaidi ya haja yake. Na iwapo ataitumia yeye mwenyewe au hajaitumia na kilichobaki ni kidogo basi hakirejeshwi kitu chochote katika hicho. [Mughniy Al Muhtaaj 184/4, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Ibn Abideen alisema: "Na akasema katika kitabu cha [Al Fathu] pia: Sio halali kwa Msafiri kuchukua zaidi ya hitajio lake la safari na ni bora kwake akope kama atakuwa na uwezo na halazimiki kufanya hivyo kwa kujuzu kushindwa kwake kulipa, na wala halazimiki kutoa sadaka kile kilichobakia mkononi mwake pale anapokuwa na uwezo kwa mali yake aliyonayo, kama fakiri anapotosheka na mtumwa mwenye mkataba anaposhindwa kutekeleza mkataba wake. Na wote hao wana mali ya Zaka na hawalazimiki kutoa sadaka. [Hashiyat Ibn Abdeen 343-344/2, Ch. Dar Al Fikr]
Na yatokanayo na yaliyotangulia ni kwamba: Atakaekuwa katika kundi la kwanza ambalo linakusanya Fakiri, Masikini, na Mtumishi wa Zaka, harejeshi kilichobakia katika kile alichokichukua kutoka katika Zaka, lakini alie katika kundi la pili ambalo linahusika na Mwenye deni na Msafiri, kwa yule atakayeondokewa na tatizo lake atalazimikia kurejesha mali ya Zaka iliyobakia mikoni mwake.Na huu ndio usawa.Lakini mtoaji hakalifishwi kuifuatilia Zaka yake aliyoitoa; kwani kufanya hivyo kunaleta ugumu wa kumbebesha jukumu lisilokuwa lake.Kwani zingatio hapo ni katika haki yake kwa jinsi ilivyokuwa wakati wa kutoa Zaka hiyo, bali mpokeaji ndiye anaekalifishwa kwa jambo hilo la kurejesha mali ya Zaka iliyosaza, au serikali itabeba jukumu hilo kama itakuwa inakusanya Zaka.
Na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi wa kila kitu.