Kulilipa Deni la Maiti Kwa Mali ya ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kulilipa Deni la Maiti Kwa Mali ya Zaka

Question

Mtu akifana deni, na yeye na jamaa zake hawana pesa za kulipia deni hilo, na kuna mtu anaetaka kutoa sadaka kwa kumlipia deni maiti huyo. Je inajuzu kuchukua kiasi cha fedha za kulipia deni kutoka katika Zaka au hapana?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Miongoni mwa aina za watu wanaopewa Zaka ni wenye madeni (wadaiwa), kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, nawanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, nakatika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katikaNjia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibuulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu niMwenye kujua Mwenye hikima.} [AT-TAWBAH 60]
Na wenye madeni ni wingi wa mwenye deni, naye ni mtu anaedaiwa na hawezi kulilipa deni hilo. Na anaedai huitwa pia mdai, na neno hili la kiarabu Ghurmu linamaana ya ulazima au uwajibikaji, na ndio maana mdaiwa akaitwa ghaarim kwani deni linamwandama. Na mdai ambaye ni Ghariimu kwa Kiarabu ameitwa hivyo kwa kumuandama kwake mdaiwa.
Na kuna aina nyingine ya (Ghuramaau) wadaiwa ambao ni wanachuoni kwa ajili ya masilahi ya wengine; kama kwa mfano kuna makabila mawili au mitaa miwili yenye uchochezi, ndani yake kuna mauaji au uharibifu wa mali, basi yeye huyu mwanachuoni anabeba jukumu la kusuluhisha baina ya wagombanao. Kwa hivyo aina mbili za mwanzo hawastahiki zaka kwa ajili ya kulipia madeni yao ila itakapokosekana fedha ya kulipa deni hilo. Na aina ya pili ni yule anaestahiki Zaka hata kama atakuwa Tajiri.
Na ulipaji wa deni la Mdaiwa hata kama kwa mali isiyokuwa ya Zaka ni katika mambo makubwa ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na ni katika utiifu bora zaidi wa Mola. Ni sawa na kumwondoshea Mwislamu mazito na machungu yanayomkabili.Na katika hadithi ya AbuuHurairah alisema: Mtume S.A.W. amesema: "Mtu atakayemwondoshea muumini tatizo miongoni mwa matatizo ya duniani Mwenyezi Mungu atamwondoshea tatizo miongoni mwa matatizo ya siku ya Kiama. Na atakayemrahisishia mtu mwenye jambo gumu Mwenyezi Mungu atamrahisishia yeye duniani na akhera, na atakayemsitiri mwislamu, Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na akhera. Na Allah yukatika kumsaidia mja iwapo mja huyo ataendelea kumsaidia nduguye. [Imepokelewa na Muslim]
Na ikiwa mdaiwa yuhai na ameshindwa kulipa deni lake basi anastahiki kupewa mali ya Zaka kiasi cha kutosha kulipia deni lake.Ama akiwa ameiaga dunia na hakuacha fedha za kulipia deni lake, wanachuoni wamekhitilafiana juu ya kujuzu kutolewa zaka kwa ajili ya deni la maiti, na kuna rai mbili:
Rai ya Kwanza: Haijuzu kutumia Zaka kulipa deni la maiti, na hiyo ni rai ya wanazuoni wa kihanafiy, wa kihanbaliy na hiyo ni sahihi zaidi kwa wanazuoni wa Kishafiy.
Al Kassaaiy anasema katika kitabu cha [Bada'I Al Swana'I 9/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: "Kuitumia Zaka katika aina mbali mbali za wema kama vile kujenga misikiti,makazi ya askari, Manyweshelezeo, kukarabati madaraja, kukafini maiti na kuwazika haijuzu; kwani kimsingi hakuna umiliki wowote uliopatikana. Na vile vile lau alilipia deni la maiti aliyekuwa fakiri kwa kushindwa kwake kulilipa, kwa sababu umiliki haujatokea kwa fakiri huyo kwa kutoishika mali hiyo. Na lau fakiri aliye hai atalipiwa deni lake kwa mali ya Zaka bila ya yeye kuamrisha hivyo haitajuzu; kwa sababu hakuna umiliki uliojitokeza kwa kutokabidhiwa fedha hizo, na iwapo itakuwa kwa amri yake basi malipo hayo yatajuzu."
Na katika kitabu cha: [Adaaru Al Mukhtaar kwa Al Haswkafiy, alipowazungumzia watu wanaostahiki Zaka, haitumiki katika kujenga msikiti, na wala kununua sanda ya maiti au kumlipia deni, lakini inajuzu kulipa deni ya mtu fakiri anayeishi hata kwa amri yake.
Ibn Abdeen anasema katika [Al Hashiyah]: "(Kauli yake: na kulipa deni lake); Kwa sababu malipo ya deni la maiti hayahitaji umiliki wa mali kutokana na madeni, kwa dalili kuwa wao wawili lau wangeliamua kutoa sadaka kwa maana ya mdai na mdaiwa kwa maana ya kuwa mdaiwa hana deni basi kitarejeshwa kilichochukuliwa. Na mdaiwa hawezi kukichukua. Kwa maana kuwa kulipia deni la maiti ni bora zaidi. Ni kwamba mtoaji wa fedha atarejesha alichokitoa katika suala la sadaka kwani imemdhihirikia yeye kuwa hakuna deni kwa mdai, na amepokea kisicho haki yake kwa kuwa amekipokea kutoka katika dhima ya mdaiwa wake." [Hashiyat Ibn Abdeen 344/2, Ch. Dar Al Fikr]
Na Anawawiy alisema katika kitabu cha [Al Majmou' 211/6, Ch. Dar Al Fikr]: "Kama mtu atakufa akiwa na deni na hajaacha mali ya kurithiwa.Je, Atalipiwa deni lake kwa fungu la wadaiwa? Hapa kuna njia mbili alizozisema mwandishi wa kitabu cha Al Bayaan. Moja yao: Haijuzu, na hiyo ni kauli ya Aswaimariy, na madhehebu ya Anakhaiy, Abi Hanifah na Ahmad. Na ya pili: Inajuzu kwa maana yaujumla ya Aya, Na kwamba inasihi mtu kujitolea kwa ajili ya kulipa deni kama ilivyo kwa aliye hai, na hakuna hata njia moja kati ya mbili iliyopitishwa, na Darimiy amesema: iwapo mdaiwa ataiaga dunia na warithi wake hawajapewa deni hilo. Na akasema Ibnu Kaji: ikiwa mtu ataianga dunia huku ana deni, kwetu sisi ni kuwa deni lake halilipwi kwa mali ya Zaka na wala haitumiki mali hiyo kwa kumkafini, isipokuwa wanapewa mali hiyo warithi wake kama watakuwa mafukara, na kwa mfano huu wamesema wanachuoni wenye Rai na Imamu Malik. Amesema: na amesema Abuu Thauri: Deni la maiti na pia kukafiniwa kwake hulipwa kwa mali ya Zaka."
Lakini An Nawawiy alisahihisha kutojuzu katika kitabu cha [Ar Rawdhah] basi akasema: "Mwenye kitabu cha [Al Bayaan] akataja:Ni kwamba lau mtu amekufa akaacha deni na hakuna cha kulilipia deni hilo, kwa hiyo katika kulilipa kwake kutokana na fungu la Zaka, kuna hali mbili, na hakubainisha njia iliyo sahihi zaidi. Na njia iliyo sahihi zaidi na maarufu: ni kuwa deni halilipwi kwa mali ya Zaka, hata kama atakuwa maiti huyo ameacha deni." [182/2 Ch. Alam Al Kutub].
Na katika kitabu cha [Al Enswaf] kwa Al Mardawiy: "Inashurutishwa wakati wa kutoa Zaka mtoaji aimiliki mali hiyo ya zaka, na wala haijuzu kuwapa mafakiri chakula cha mchana na wala chakula cha jioni, na wala deni la maiti halilipwi kwa mali hiyo ya zaka, deni alilojitakia maiti kwa masilahi yake au ya mwingine, na Sheikh Taqiyu Diin amechagua kujuzu, na akataja moja ya Hadithi mbili kutoka kwa Imamu Ahmad; kwamba mwenye deni hashurutishwi kuimiliki mali aitoayo. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema {Na wenye deni} na hakusema: kwa wenye deni" [234/3, Ch. Dar Ihiyaa Aturaath Al Arabiy]
Na Al Bahutiy anasema katika kitabu cha [Kashaafu Al Qena'i 269/2, Ch, Dar Al Kutub Al Elmiyah]: "Hailipiwi mali hiyo deni la maiti alilojitia kwa masilahi yake binafsi au ya mtu mwingine) imesimuliwa na Abuu Ubaida na Bin Abdulbar kwa pamoja, kutokana na kutokuwa kwake na sifa, kwa maana ya maiti ya kuipokea mali hiyo ya Zaka. Na Ibnu Qudaama anaweka sababu ya jambo hili kwamba Mdaiwa ni Maiti na hawezi kulipa deni yeye mwenyewe, na iwapo atampa mali hiyo mdai wake malipo yatakuwa kwa mdai na wala sio kwa mdaiwa." [Tazama kitabu cha Al Mughniy 498/2, Ch. Maktabat Al Qahirah]
Rai ya pili: Inajuzu kulilipa deni la maiti ambaye hajaacha cha kulipa, iwapo masharti ya mdaiwa yatatimia. Na hiyo ni rai ya wanazuoni wa Malikiyah na kauli ya wanazuoni wa kishafiyah, na simulizi moja kwa wanazuoni wa kihanbaliyah.
Na ilitajwa katika kitabu cha [Asharhu Al Kabeer Ala Mukhtaswar ya Khalil] alipowazungumzia watu wanaostahiki Zaka: "Na iwapo mdaiwa atakufa basi deni lake litalipwa. Anasema Dusuqiy katika Hashiya yake: (na lau mtu alikufa) ametoa jibu kwa kutumia (neno Lau) kwa yule anaesema kuwa deni la maiti halilipwi kwa Zaka; kwa kuwa kwake wajibu kulipwa na Baitil Mali (tamko lake: deni lake litalipwa kutokana na mali ya Baitul Mali) bali baadhi yao wamesema kwamba: deni la maiti lina haki zaidi kuliko la mtu aliye hai kulipwa kwa Zaka; kwani hapatarajiwi kulipwa kwake kinyume na deni la mtu aliye hai." [496/1, Ch. Dar Al Fikr]
Na utoaji wa sababu za wanachuoni wa kauli ya kwanza ni kuwa fungu la wadaiwa lenye sharti la kumiliki hutiwa kasoro na kujuzu kulipia deni la mdaiwa kutoka katika Zaka na kumlipa mdai hata bila ya idhini ya mdaiwa, na hapo milki haijapatikana pia, na hilo ndilo walilolijuzisha wafuasi wa madhehebu ya Hanbali." Basi katika kitabu cha [Al Inswaf 234/3]: "Na iwapo mmiliki atamlipia mdaiwa bila ya idhini ya fakiri, kwani usahihi katika Madhehebu haya ni kwama inasihi. Na hata kama mdaiwa atatoa idhini kwa mtoaji Zaka kuwa amlipie deni umiliki pia hautapatikana; kwa sababu upokeaji wa mali ni sharti la kumiliki."
Kwa ajili hiyo, kulilipa deni la Maiti ambaye hakuachamali ya kulipia deni lake, ni malipo na mali ikakatwa kutoka katika fungu la Zaka, kutoka katika fungu la wadaiwa, inajuzu. Na deni hilo linafutika kwa maiti. Na dhima ya mlipaji wa zaka inaondoka.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas