Uthabiti wa Misingi ya Fiqhi (Usuu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uthabiti wa Misingi ya Fiqhi (Usuul Al-Fiqh)

Question

Je, Misingi ya Fiqhi ni jambo ambalo ni thabiti au la kidhana ?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Elimu ya Misingi ya Fiqhinimiongoni mwa elimu zinazozisaidia elimu nyingine.Nayo ni chombo kinachopelekea kujua hukumu za kisheria za Kiislamu zinazohusiana na vitendo vya waislam.Pia hupelekea kujua mbinu sahihi ya kushughulikia matini za kisheria na Misingi kwa ajili ya kuchukuliwa faida yakekatikamatawi ya fiqhi.
Al-Baydhawy anaeleza Misingi ya Fiqhiakitaja katika ufafanuzi wake mihimili yakemitatu ambayo inashughulikia misingi ya elimu hii akisema: "Misingi ya Fiqhi ni: kujua dalili za fiqhi nzima, na jinsi ya kuzitumia, na hali ya anayezitumia". [Minhajul Usuuluk 2, Al-Mahmudiya].
Tajuddin Al-Subki anasema katika (Majmuu Al-Jawamii): [Misingi ya Fiqhi ni: Jumla ya dalili za kifiqhi.]
Al-Mahali anasema: [ni kujua dalili za kifiqhi za jumla. Mwandishi wa kwanza amesema kwamba elimu hii ni karibu na maana ya kilugha, kwa sababu Usuulni lugha yadalili. (Sharhul Al-Mahali ala Jamil Jawamii 1/47, Darul Kutub Al-Elmiiya, pamoja na Hashiyatul Sheikh Hassan al-Attar).
Na yaliyosemwana Al-Subki yanaashiria tofauti yawanavyuonikuhusukuainisha maana inayooneshwa kwa «Misingi ya Fiqhi», je, hii ni misingi yote ikiwa yupo mwenye kujua kwake au la, au kuwa Misingi ya Fiqhi na vipengele vyake vya kweli ni elimu na ujuzi wa kinafsi unaohusiana na misingi hii iliyotokana nayo?
Sheikh Al-Attar anaelezea katika kitabu chakeSharhul Mahalli kwamba chanzo cha kutokubaliana ni ushiriki wa majina ya elimu kati ya mambo hayo akisema: "Ujue kwamba majina maalumuya elimu kama vile mantiki yanaitwa kwa maelezo fulani, husemwa, kwa mfano: Mtu mmoja anajua elimu ya sarufi, yaani anajua maelezo maalumu ya sarufi, na mara nyingine maelezo yanaitwa kwa elimu, na hali hii ni wazi, basi kuhusu hali ya kwanza ukweli wa kila elimu ni masuala yake, na kuhusu hali ya piliukweli wake ni kusadiki masuala ya elimu hii.Pia neno la elimu linaitwa katika kumiliki". [Hashiyatul Attar ala Sharhul Mahali ala Jamii Al-Jawamii 1/45].
Kutokubaliana katika kuainisha maana ya istilahi - ambazo miongoni mwake ni Misingi ya Fiqhi- mara nyingi kunasababisha aina ya matatizo na mkanganyiko dhahiri kati ya maoni, na wakati wa kuainishasuala la kutokubaliana ni wazi kuwa suala hili ni la kimatamshi tu, na hali hii ni ile iliyotokea katika Misingi ya Fiqhi.
Ni wazi kwamba dalili ambayo haina shaka lolote ni dalili ya kiyakini amabyoina faida kwa elimu, haiwezekani kurudishwa au kuipinga, na haikubaliwi kutoafikiana kuhusu jambo hili, kwa sababu dalili ambayo haina shaka yeyote hutenganisha kati ya haki na batili.
Ama kuhusu maana ya jambo la kidhahania ni chanzo kilichotengenezwa na dhana, na maana yakekatika lugha ni kama alivyosema Al-Zubaidi: "Ni kusita sita kati ya pande mbili za itikadi isiyo sahihi ...,pia Al-Minyawi anasema: Jambo la kidhahania ni itikadi iliyo sahihi zaidi pamoja na uwezekano wa kuwepo kwa jambo la kinyume ambalohutumika katika hali ya yakini na ya shaka, Al-Raghib akasema: Jambo la kidhahania ni jina la alama ambayo wakati inapokuwa na nguvu inasababisha elimu na wakati inapokuwa na udhaifu haifiki kuwa njozi. [Taji Al-Arus 1/8102].
Kutokana na hivyo ni wazi kwamba dalili ya kidhahania ina uwezekano wa dalili sahihi zaidi ya maana kwa kuishinda dhana moja, lakini pamoja na uwezekano wa makosa katika dalili hii, katika wakati huu ni bora zaidi kuangalia, kujitahidi, na inaruhusiwa kuwepo kwa kutoafikiana bila ya kukanushwa.
Na misingi ya Misingi ya Fiqhi katika vitabu ya wanavyuonimiongoni mwao ni ile iliyo ni thabiti kama vile Quraani na Sunna iliyopokelewa kutoka kwa masahaba zake Mtume mmoja kwa mwengine, na baadhi ya Sunna hii ni ya kidhana wanavyuoni wanawezakujadiliana kama vile kazi ya watu wa Madinah,maslahi ya wazi,kuzuia madhara,sheria ya watu waliotutangulia na dalili nyingine, kutokana na sababu hii hatuwezi kusema kwamba misingiyote ya Misingi ya Fiqhi haina shaka yeyote, lakini inasemekana kuwa baadhi yao ni thabiti na baadhi yao ni ya kidhani, kwa hiyo baadhi ya matawiya kifiqhi ambayo ni thabiti hairuhusiwi kwa wanavyuoni kuijadiliana, na baadhi yao ambayo ni ya kidhanawanavyuoni wanaruhusiwa kujadiliana bila ya kukanusha.
Lakini kama tukiangalia sababu nyingine ilhali tutapata kuwa imepokelewa taarifa kutoka kwa baadhi ya wanavyuonizinazosisitiza kuwa misingi yote ya Misingi ya Fiqhi ni thabiti, hata kama wanavyuoni wameijadili, kwa sababu hali hii itakuwa kutokana na tofauti yao kuhusu kufahamu jambo moja ambalo ni thabiti katika wakati moja, baadhi yao wanalifahamu jambo hilo kutoka njia nguvu, ilhali analisadiki barabara, na baadhi yao wanalifahamu jambo hilo kutoka njia dhaifu ilhali hawafiki ngazi ya dhana.
Na anayekwenda mwendo huu miongoni mwawanavyuoni ana nia ya kwambamisingi ya asili ni thabiti kwa kweli, lakini kuifahamu kunatofautiana kutokana na ukosefu wa utafiti, basi anayeendelea na utafiti wake na atajua kwamba Misingi ya Fiqhi ni thabiti.
Imamu Al-Qarafi anasema katika kitabu cha [Nafais Al-Usuul 1/147, Nizar Mustafa Al-Baz.]: "Misingi ya Misingi ya Fiqhi yote ni thabiti, lakini hali hii haitokei kwa kutoa baadhi ya dalili kutokana na matukio fulani, bali hutokea mara nyingi kwa kufahamu vizuri dalili hizi, na anayeangalia hali za masahaba zake Mtume R.A. na anayefahamu matini za Quraani na Sunna, husadiki.... anayetaka kusadikimisingi ya Misingi ya Fiqhi kama vile makubaliano, kipimo na vpengele vingine basi ni bora zaidi afahamu hali za masahaba zake Mtume R.A. mjadala wao, majibu yao na fatwa zao, na ni bora kwake azidi kuangalia matini za Quraani na Sunna, ili asadiki misingi hiyo, na kutoangalia kwa vitu hivi kunasababisha kusema kuwa: makubaliano ni jambo la kidhana, kwa sababu hakuangalia isipokuwa matini chache katika baadhi ya vitabu tu, kwa hivyo, hakuti ndani ya nafsi yake isipokuwa dhana tu, atasema: mwarabu anayeitwa Hatem ukarimu wake ni jambo la kidhana, ingawa katika wakati huo huo ni jambo la thabiti kwa wengine ambao wanafahamu matini vizuri. Hii ni msingi makini mtukufu lazima ufahamiwe vizuri, nao ni asili kubwa ya Uislamu ambayo ni siri ya kauli ya wanavyoni kuwa: Hakika misingi ya dini ni thabiti, na ukosefu wa elimu yao ni sababu ya upinzani, na mfano wake ni makundi mawili ambayosuala moja lilipokelewa kutoka kwa watu wengi kwa timu moja miongoni mwao lakini halipokelewi kutoka kwa wengi wa kundijingine, basi kila timu miongoni mwao ilitoa fatwa kufuatana na ufahamu wake, na pengine ujumbe wa Mtume Muhammad haukufikia baadhi ya watu, na pengine umefika kupitia mmoja tu, lakini katika wakati huu huu tayari umesadikiwa].
Lakini katika mahali pengine Al-Qarafi anasema kuhusu kauli ya Abu Hussein Al-Basri kwamba anayekosea katika Misingi ya Fiqhi hana udhuru, na kwamba hairuhusiwikumuiga, na kwamba asiyekosea katika misingi hali yake ni kama Misingi ya dini, Al-Qarafi anasema: "Unapaswa kujua kuwa miongoni mwa masuala ya Misingi ya Fiqhi ni masuala ambayo ni dhaifu katika ufahamu kama vile makubaliano ya ukimya (maana yake ni kwamba baadhi ya wanavyuoni wanatoa fatwa moja na wengine wengi hawasemi chochote kuhusu fatwa hii) na makubaliano ya vita na kadhalika, kutoafikiana katika masuala kama hayo kuna nguvu, na mpinzani hakupinga ila kwa dhana tu, kwa hivyo hairuhusiwi kwa mpinzani huyo awe na dhambi kama kwamba katika Misingi ya dini haturuhusiwi kumtuhumu mtu fulani kuwa ana dhambi anayesema kuwa vitu ya papo kwa papo haviishi zama mbili au anayekataa anga na anathibitisha kinyume chakena masuala kama hayo yasiyo na makusudi kutoka Misingi ya asili ya dini, lakini ni majina katika elimu hii tu" [Nafais Al-Usuul 1/161].
Kutokana na hivyo, kuna idadi kubwa ya masuala Misingi ya Fiqhiya kidhana na yanatazamiwa ni dhaifu kufahamiwa, lakini baadhi ya wale wanaosema kuwa Misingi ya Fiqhi ni thabiti hawayazingati masuala haya kutoka ya nzo, bali wameyazingatia kutoka masuala yaliyoambatana na Misingi kwa ajili ya kuonesha hakika yake na cheo chake wakati wa uwezekano wake na kupinga kwake, pia masuala hayo pengine yanalazimisha kutekeleza fatwa kwa anayedhani usahihi wake miongoni mwa wenye jitihada.
Imamu Al-Ghazali anasema: "Na makusudio ya elimu ya Misingi ya Fiqhini kujua dalili zauthabiti uliotokana na hukumu zinazoagizwa. Na habari zilizopokelewa na mtu mmoja vile vile vipimo vilivyogunduliwa kwa njia ya jitihada siyo miongoni mwa ya nzo, bali ni mambo ya kidhana na yanachukuliwa pia kama mambo thabiti, lakini hayakutajwakwa ajili ya kuonesha jambo ambalo ni sahihi na lililooza, jambo ambalo ni muhimu zaidi na lisilo muhimu, na kwa sababu hali hii ni miongoni mwa njia za elimu ya Ya nzo, na hakuna njia kwake isipokuwa kwa kuonesha daraja zake". [Al-Mankhool uk. 4- 5].
Lakini Imam AR-Razi alisema kuwa Misingi ya Fiqhi ni: "Njia zote za Fiqh kwa ujumla, na jinsi ya kuzitoa kama dalili, na hali ya anayezitoa kama dalili". [Al-Mahsool 1/80, Mu’asasatul Risalah].
Maana yake kwa kusema: [Njia za Fiqhi] dalili zote ambazo ni thabiti na zisizo thabiti, zote ni miongoni mwa Misingi ya Fiqhi, Al-Isnawi anasema: "Ujue kwamba kueleza kwa dalilikunavitenga Misingi vingi ya Fiqhi, kama vile hali za jumla, habari zilizopokelewa na mtu mmoja tu, kipimo, Al-Istsahab (kuamua kwa kuthibitishwa kwa hukumu ya kisasa kutegemea kuwepo kwake katika zama zilizopita, ila kama ilikwepo dalili nyingine inabadilisha maana hii) na vinginevyo, ingawa wenye Misingi wamekubaliana kutumia Misingi hivi, lakini kwao Misingi hivi siyo dalili za Fiqhi, bali ni ishara tu, kwa sababu kwao Misingi ambavyo ni thabiti tu ni vinavyoitwa dalili, kwa hivyo imesemekana katika kitabu cha Al-Mahsool ni kwamba: Misingi ya Fiqhi ni jumlaya njia za Fiqhi. Kisha akasema: Na kauli yetu njia za Fiqhiinagusia dalili na ishara pia". [Nihayatul Saul 1/16,Muhammad Ali Subih].
Wanachuoni wa Ussul Al-Fiqh wamekubali mtazamo wa Imamu Ar-Razi kuhusukuvizingatia Misingi ya Fiqhi vinavyoitwa ni thabiti na visivyo thabiti pia, na wameita Misingi hivi vyote dalili, Al-FutohiAl-Hanbali alisema katika kuelezea maana ya dalili kisheria iwapomwenye kitabu cha Al-Kaukab anaielezea kwamba:[Ni jambolinaloweza kufikishia mahitaji yanayotakiwa kupitia mtazamo sahihi]. Al-Futohi anasema: "Na miongoni mwa mahitaji yanayotakiwa ni mambo ambayo ni thabiti na yasiyo thabiti, na madhehebu hii ni madhehebu ya wenzetu na wingi wa wanavyuoni wa Fiqhi. Mtazamo wa pili ni kwamba mambo ambayo ni thabiti tu ni dalili, na yasiyo thabiti ni ishara". [Sharhul Kaukab Al-Muniir uk. 16, Nyumba ya Kuchapicha ya Al-Sunnah Al-Muhammadiyah].
Kutokana na hivyo, dalili za Fiqhiza jumla au za kina ni jambo linaloweza kufikishia kuthibitisha hukumu ya kisheria au kuizingatia ni kidhana kupitia mtazamo sahihi, hali hii inajumuisha dalili ambazo wanavyuoni hawazikubaliani nazo kama kufanya kazi watu wa Madinah, Al-Istishab, na mambo yaliyokubaliwa na wanavyuoni kama Quraani na Sunnah iliyopokelewa na watu wengi.
Pia pengine inakusudiwa kwa uthabiti wa Misingi ya Fiqhi ni thabiti katika kulazimisha hukumu za kisheria wakati mwenye jitihada anapozifika mara nyingi kwa kudhania tu, ikiwa hukumu hizo zimechukua faida kutoka hukumu zilizokubaliwa au zisizokubaliwa, kwa mfano mwenye jitihada aliyetafuta na aliyeangalia mpaka anadhani kwamba jambo fulani ni sahihi zaidi, kisha lilitukia tukio fulani akafikia hukumu ya tukio hili baada ya kufanya bidii, basi anapaswa kuitekeleza hukumu hii na kuitoa fatwa kutokana na dalili alizozitoa, hata kama dalili zake hazikuthibitishwa na wanavyuoni wa Usuul (misingi), kwa hivyo, ImamAl-Baydhawi alisema: "Mwenye jitihada akidhani hukumu fulani analazimishwa kuitekeleza na kuitoa fatwa, kwa sababu kuna dalili thabiti kuhusu kupasa kwa kufuata dhana tu, basi hukumu ni thabiti na ambayo inachukuliwa kwa dhana inakaribiana nayo". [Manahij Al-Usuul uk.2- 3].
Baadhi ya wanavyuoni wameita Misingi ya Fiqhimisingi ya kifiqhi na madhumuni ya sheria na uhalisi wake ambao ni thabiti kutokana na kufahamu matini za Quraani na Sunna iliyopokelewa na wengi kwa maana, itakuwa kwa hivyo ni thabiti kwa sababu asiliyake ni kuifahami vizuri au kutoa hoja ya kiakili kwa njia thabiti [Rejea: Al-Muwafakat fi Usuul Al-Sharia kwa Al-Shatby 1/29 0.30, Dar Al-Fikril Arabi].
Ibn Najim Al-Hanafi anasema mwanzoni mwakitabu chake Al-Ashbaah wal Nadhairakieleza uhalisi wa misingi ya kifiqhi, akisema: [Navyo ni Misingi ya Fiqhi kwa kweli. [Ghamz Uyuun Al-Basai’r fi Sharhi Al-Ashbaah wal Nadhair 1/34, Darul Kutub Al-Ilmiyyah]. Alikusudia kwa hivyo misingi mingi miongoni mwao ni: «Mambo kwa madhumuni yake», na «Ugumu huleta urahisishaji», na «Uharibifu inaondolewa» na kadhalika. Lakini wanavyuoni wengi hawakukubalimisingi hiiyote, kwa sababu misingi hii ni kama matini za sehemu tu japokuwa matini hizi zinafaa kwa kutoa dalili kuhusu hukumuza matawi mengi yasiyo na mwisho, lakini kuthibitisha kwa misingi hii inakosa kwanza kuthibitisha kwa sahihi yaMisingi ya kuifahamu kwake na sahihi ya kupokelewa kwake kutoka kwa watu wingi, na kujua jinsi ya kufaidika maana kutoka matini za Wahi (ufunuo), na mambo mengine ambayo ni lazima yatambuliwe kwanza kabla ya kukubali kwa msingi wa kifiqhi wenyewe, na elimu ambayoinatafuta mambo hayo na kupata uhalisi na hoja na vinginevyo, kwa kweli ni elimu ya Misingi ya Fiqhi, kwa sababu pasipo na kujadili maudhui yake haiwezekanikuthibitishamisingi hii, uhalisi na makusudi yasheria, basi misingi ya FiqhiinakosaMisingi ya Fiqhikama kwamba matawi yake yanavyoya kosa.
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu: Misingi ya Fiqhiina nguzo thabiti zinazokubaliwa na wanavyuoni, pia ina nguzo za kidhanazisizokubaliwa na wanavyuoni.Na hali hii haizuiikuthibitisha hukumu ya matawi ya kifiqhi na kupaswa kuyatumia, ingawa matawi haya yamegawika kwa misingi ya kiasili isiyokubaliwa kama ilivyotajwa hapo juu.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas