Kutoa Zaka kwa Ajili ya Kujengea M...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoa Zaka kwa Ajili ya Kujengea Msikiti

Question

Je, ninaweza kutoa Zaka kwa ajili ya kujengea msikiti?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Quraani Tukufu imezianisha njia za kutoa Zaka kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sadaka hupewa (watu hawa): Mafakiri na Masikini na Wanaoitumikia na Wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislamu) na katika Kuwapa Ungwana watumwa na katika Kuwasaidia Wenye deni na katika (Kutengeneza) Mambo aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu na katika (Kupewa) Wasafiri (walioharibikiwa). Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima} [AT TAWBA, 60].
Wengi wa wajuzi wa Fiqhi wa madhehebu manne yenye kufuatwa walielekea katika kutojuzu kutolewa kwa Zaka katika mambo ya kheri na kuiweka sawa hali ya jamii kama vile kujenga vizuizi vya maji, kujenga misikiti, shule, kurekebisha barabara na kukafini maiti n.k.
Walibainisha sababu ya kutojuzu kutoa Zaka katika mambo hayo kwa kutokuwepo hali ya kuyamiliki kama walivyosema wafuasi wa madhehebu ya Hanafia, au kwa kuwa hayo mambo ya kheri hayaingii katika njia nane za kutolea Zaka kama ilivyotajwa katika Aya tukufu kama walivyosema wengine.
Walieleza maana ya kutoa Zaka “katika njia ya Mwenyezi Mungu” kuwa ni mambo mawili; jihadi na vita (ghazwa) pamoja na mambo yanayoambatana navyo, kwani jihadi inaingia katika “njia ya Mwenyezi Mungu” kwa makubaliano ya wote, ama uhalali wa kutoa Zaka kwa wapiganaji tofauti na kuitoa kwa ajili ya masilahi ya jihadi na vifaa vyake ni jambo lenye hitilafu ndani yake.
Kwa hiyo, hajuzu kutoa Zaka ya Mali kwa ajili ya kujenga misikiti, kwani katika hali hii zaka hutolewa kwa binadamu kabla ya kutolewa kwa jengo lolote, na hutolewa kwa mwenye kusujudu kabla ya misikiti.
Ikiwa hakuna njia nyingine ya kujenga msikiti isipokuwa kwa mali ya Zaka, na ikiwa jambo la kutojenga msikiti linaweza kuchelewesha uwepo wa alama za Dini ya Mwenyezi Mungu kama vile Kutokuwapo msikiti au msikiti uliopo hauwatoshi watu wote wenye kusali ndani ya msikiti huo, basi katika hali kama hii inajuzu kutoa mali ya Zaka kwa ajili ya kujengea na kwa kiwango kinacholifanikisha lengo lililokusudiwa; kwa kufuata maoni ya wenye kutofautiana na Jamhuri ya wanazuoni, nayo ni maoni mapana zaidi kwa maana ya njia za kutoa Zaka “katika njia ya Mwenyezi Mungu” ambapo kutokana na maoni hayo “njia ya Mwenyezi Mungu” inajumuisha mambo yote bora ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hali kadhalika, masilahi ya Waislamu wote yanayoinua juu mambo ya Dini na dola, yasiyo ya binafsi, ambayo yanaweza kuingia katika njia ya kutoa Zaka: “katika njia ya Mwenyezi Mungu”.
kadhalika maoni ya kuwa njia ya kutoa zaka “katika njia ya Mwenyezi Mungu” inajumuisha mambo yote bora ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, ni maoni ambayo Imamu Al Fakhr Al Razy aliyadokezea katika tafsiri ya Qraani Tukufu (Mafateeh Al Ghaib, vol. 16, uk. 78, cha. Dar Ihiyaa Al Turath Al Araby, Beirut, 420 BH) ambapo alisema: “Mtambueni kwamba uwazi wa lafudhi katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Katika njia ya Mwenyezi Mungu} haulazimishi kunyima hukumu iambatane na wapiganaji tu”, kisha alitaji aliyoyasema Al Kafal kutoka kwa baadhi ya Mafaqihi: Ya kwamba waliruhusu kutoa sadaka katika mambo yote ya kheri kama vile kukafini maiti, kujenga boma na kujenga misikiti kwani maneno ya Mwenyezi Mungu: (Katika njia ya Mwenyezi Mungu) ni jumuia”.
Hapa inaonekana kwamba Imamu Al Razy hakusema cho chote kuhusu maneno ya Al Kafal, jambo ambalo linabainisha kwamba Imamu Al Razy hakuyakataza.
Miongoni mwa walielekea kauli hii ni Sheikh Sedik Hassan katika Kitabu chake [Al Rawdha Al Nadiya, vol. 1, uk. 206: 207, cha. Dar Al Jeel, Beirut, Lebanon], aidha Sheikh Jamal Al Din Al Qasimiy katika tafsiri yake [Mahasin Al Taawil, vol. 8, uk. 3181, maelezo ya: Muhammad Fuad Abdel Baky, chapa ya kwanza, Dar Ihiyaa Al Kotub Al Arabiya, Issa Al Halaby, 1957] baada ya kutaja maneno ya Imamu Al Fakhr Al Razy.
Walipata dalili ya kisheria katika suala hili kutokana na kuwa (Katika Njia ya Mwenyezi Mungu) ni lafudhi jumuishi, na kwa hiyo haijuzu kuiambatanishi na baadhi ya msamiati wake bila ya kuwepo dalili. Hali ya kuwa hakuna dalili.
Ama yale maoni ya kuwa masilahi ya wote ambayo yanasimamisha mambo ya dini na dola yaweza kuingia katika ile njia ya kutolea zaka “Katika njia ya Mwenyezi Mungu”, basi waliyasema hayo jobo la Maulamaa wa kisasa; maana ni kauli ya Sheikh Muhammad Rashid Redha katika [Tafsiri ya Al Manar vol. 10, uk. 585: 587, chapa ya pili, Dar Al Manar, Cairo, 1947], akafuatiliwa katika jambo hilo na Sheikh Mahmoud Shaltut [Uislamu ni Itikadi na Sheria, uk. 104: 105, Dar Al Shorouk] alipoulizwa kuhusu ruhusa ya kutoa zaka katika kujenga misikiti, akajibu [Al Fatawa, uk. 119, chapa ya Al Azhar] kwa kusema: “Hakika katika hali ya kutaka kujenga au kufanyia marekebisho msikiti, ikiwa katika kijiji hakuna msikiti au msikiti uliopo hautoshi kuwapokea wenye kusali wote, basi inajuzu kisheria kutoa zaka kujenga au kuifanyia marekebisho, na katika hali hii mali inatolewa {katika njia ya Mwenyezi Mungu} iliyotajwa katika Aya ya Sura ya AL Tawba iliyoziainisha njia za kutolea zaka. Kauli hii ilitegemea maana ya {katika njia ya Mwenyezi Mungu} kuwa ni yanaambatana na masilahi wanaonufaika nayo Waislamu wote siye mtu binafsi. Kauli hii ilitegemea maana ya kuwa katika njia ya Mwenyezi Mungu “Yanaambatana na masilahi ya Waislamu wote wanaonufaika nayo siye mtu binafsi”, yakajumuisha misikiti, hospitali, taasisi za kutolea huduma za kielimu, viwanda vya chuma na mengine yanayoweza kuleta manufaa kwa wote … mpaka alisema: Hayo ndiyo niliyoyachagua na kwa hayo nilitoa fatwa, sharti –kama nilivyosema kuhusu misikiti– kuwepo dharura ya kujenga msikiti huu. Kwani ikiwa hakuna dharura, basi mali ya zaka hutolewa katika njia nyingine inayostahiki zaidi”.
Hali kadhalika idara ya fatwa nchini Misri iliwahi kutoa fatwa kadhaa kuhusu suala la kujuzu kutoa mali ya Zaka kwa ajili ya kujengea msikiti na kuukarabati; ya kwanza: Ni ile fatwa iliyotolewa katika zama za Sheikh Abdel Magid Selim – Mwenyezi Mungu Amrehemu – mwezi wa Muharram 1363 BH / January 1944. Ya pili: Ni ile iliyotolewa katika zama za Sheikh Hassan Maamuun –Mwenyezi Mungu Amrehemu– tarehe 7 mwezi wa Muharram 378 BH / August 1958. Ya tatu: Ilitolewa katika zama ya Sheikh Gad Al Hak Aly Gad Al Hak – Mwenyezi Mungu Amrehemu – 1400 BH / 30 Desemba 1979, ambapo fatwa hizo zote zinaruhusu kutoa mali ya Zaka kwa ajili ya kujengea misikiti na kuikarabati, kwa sharti la kutokuwepo msikiti mwingine au uliopo hautoshi kuwapokea watu wote wenye kusali katika msikiti huo.
Kutokana na yaliyotangulia jibu la swali lililoulizwa limepatikana.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

Share this:

Related Fatwas