Urafiki Pamoja na Wasio Waislamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Urafiki Pamoja na Wasio Waislamu

Question

Tangu miaka mingi iliyopita nina rafiki yangu mpenzi, naye ni mkiristo. Niliposilimu na kuwa mwislamu, rafiki yangu aliendelea kuwa msamehevu kwangu kutokana na jambo hilo, na wala hakubadilisha mtangamano wake wa upendo nami. Kwa hivyo basi, nataka mnijulishe kama ikiwa inajuzu kuendelea urafiki pamoja naye au hapana?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kwa hakika, asili ya hukumu katika uhusiano baina ya waislamu na wasio waislamu ni Kuishi pamoja na wala sio mgongano na uadui, na jambo hili linakusanya aina zote za mahusiano ya kibinadamu, kama vile kuleana na kusaidiana kiujenzi ngazi ya mtu mmoja mmoja na ngazi ya watu wote.
Ama kwa upande wa ukaribu uliozuiliwa na Mwenyezi Mungu kwa wasiokuwa waislamu ni ule ambao unakusanya mapenzi ya dini ya asiyekuwa mwislamu. Ama kwa upande wa mtangano mzuri, wema na ukarimu pamoja na tabia njema, hivi vitu ni katika mambo ambayo mwislamu ameamrishwa kujipamba nayo na kuwatendea walimwengu wote.
Na kwa hivyo basi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Quraanitakatifu: {Na semeni na watu kwa wema} [AL BAQARAH 83], Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema pia: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.(8). Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.(9)} [AL MUMTAHINAH 8,9]
Basi ewe ndugu yangu, endeleza urafiki wako na rafiki yako mkiristo, na uzifanye tabia zako za kiislamu kuwa ndizo unazozitumia pale unapouzungumzia kwake Uislamu kama walivyokuwa wakifanya wale wema waliotutangulia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas