Hukumu ya Vitendo vya Kuua na Vurug...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Vitendo vya Kuua na Vurugu

Question

Nina swali kuhusu vitendo vya ugaidi vilivyotolewa na baadhi ya Waislamu. Nataka kuuliza kuhusu kumwua mtu yeyote kunaruhusiwa wakati gani? Je, vitendo vya Al-Qaida ni sahihi, na kujua kwamba wapo Waislamu pia wanauwawa kutokana na vitendo vyao hivi?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ni lazima kupambanua kati ya dhana mbili nazo ni: “Al-Jihad” na “Al-Irjaf”.
Istilahi ya “Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu” Ni istilahi tukufu ya Kiislamu, nayo ina maana pana katika Uislamu; istilahi hii huainishwa kama ni kupambana na nafsi, matamanio, na Shetani, pia huainishwa kama ni kupambana na maadui kwa lengo la kuondosha uadui na kuzuia udhalimu.
Aina ya Jihadi hii ina masharti yake na pasipo na masharti haya haiwezi kuwa sahihi. Masharti haya ni kama vile: Kuwepo kwa Mwislamu ambaye ni Imamu na anawahamasisha Waislamu kufanya Jihadi, kuwepo kwa bendera ambayo ni ya wazi, kuwepo kwa nguvu kwa Waislamu, kuwepo kwa dharura inayopelekea Jihadi kwa ajili ya kuzuia uadui au kuondosha udhalimu.
Azimio la Jihadi lifikiriwe matokeo yake vizuri, usomwe vizuri uuwiano kati ya maslahi na madhara, na wala usiangaliwe juujuu. Majukumu haya ni ya watawala wanaotawala nchi na watu, nao ni wenye uwezo wa kujua matokeo ya maazimio haya zaidi kuliko wengine, watachukua malipo ya Jitihadi zao. Kama wakipata watalipwa mara mbili, na kama wakikosea watalipwa mara moja, kama wakiwa na mapungufu watapata dhambi.
Hakuna yeyote ana la kufanya isipokuwa kushauri na kutoa nasaha kama akiwa miongoni mwa wenye ushauri. Kama si miongoni mwa wenye ushauri, basi asizungumze, wala kuanzisha Jihadi mwenyewe, na akifanya hivyo, atakuwa kamkiuka mtawala, na pengine hali hii itakuwa na madhara mengi zaidi kuliko manufaa yake, kwa hivyo atapata dhambi kutokana na madhara haya.
Ama kuhusu istilahi ya “Al-Irjaf” ni istilahi ya Quraani ambayo imetajwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: {Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika mji wa Madina hawataacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu * Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa * Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu} [AL-AH'ZAB : 60-62].
Istilahi hii ina dhana yake mbaya inayomaanisha kuchochea fitna, machafuko, na migogoro kwa kuhalalisha umwagaji damu, na kuiba mali kati ya watu wa jamii moja, kwa madai tofauti, miongoni mwao: Ukafiri wa mtawala au kwa dola au kwa makundi ya watu. Na miongoni mwao madai ya kuamrisha wema na kukataza maovu, kuhalalisha umwagaji damu za wasio Waislamu walioingia nchi za Kiislamu kwa kudai kwamba nchi zao zinapigania Uislamu… na madai mengine ya kuchochea fitna ambayo Shetani anayapamba kwa watu wenye kuchochea fitna, ambayo baadhi yao walikuwa ndio sababu ya kuzuka kwa Khawarij katika zama za Maswahaba na waliokuja baada yao, na kwa kufananisha wanashikamana na kuhalalisha kutoka kwao kwa watawala wa Kiislamu wa zamani na wa kisasa
Hapo hukumu inatofautiana kwa mujibu wa tofauti ya dhana yenyewe; kama ikikusudiwa vitendo vya ufisadi vinavyotendwa na makundi ya wale wanaojiita Makundi ya Kiisalmu katika nchi za Waislamu, kama vile kutoka kwenye utawala wa Waislamu baada ya kudai kuwa ni makafiri na polisi na majeshi pia, au kuchukua silahi kwa kudai kuwa kufanya hivyo ni kuamrisha wema na kukataza maovu, na vitendo vengine vya ufisadi vinavyojitokeza kutokana na mbinu za kuchochea fitna, mambo haya yote ni haramu, nayo ni aina ya udhalimu ambao Sheria ilikuja kwa ajili ya kuuzuia na kuuondosha, bali kuwaua wenye kufanya hivyo kama hawakuacha kuwadhuru Waislamu na wasio Waisalmu miongoni mwa wazalendo na wenye mikataba ya amani (dhimiy). Kuiita hali hii jihadi ni udanganyifu na uongo kwa ajili ya kuupamba ufisadi wao kwa wenye akili dhaifu wanaodanganywa kwa ubatili wao. Nao ni madhalimu wanaopigwa vita kama watakuwa na nguvu, mpaka waache udhalimu pamoja na uchochezi wao wa fitna.
Lakini kama ikikusudiwa yaliyotokea katika baadhi ya nchi zisizo za Kiislamu miongoni mwa kuzuia mauaji ya kikabila kwa wachache au wengi wa Waislamu, na kuzuia kwa kushambulia nafsi, au mali, au heshima zao, hizo zote ni jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na kuchukua azimio kuhusu jihadi ni jukumu la mtawala wa kiislamu au wenye madaraka wanaotawala mambo ya Waislamu na maslahi yao, wakifanya uwiano kati ya maslahi na madhara na wanawahamasisha Waislamu wanaowatawala kwa wafanye hivyo. Lakini hawana nguvu za kuwahamasisha Waislamu wasiowatawala, kwa sababu hawana taarifa ya ukweli wao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas