Kuhusu Madhehebu ya Ibn Omar Katika...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhusu Madhehebu ya Ibn Omar Katika Kupunguza Sala

Question

Kuna Hadhithi kutoka kwa Ibn Omar inayofahamika kwamba, mtu huzingatiwa kuwa ni msafiri iwapo masafa ya nyumba yake yanafika maili moja, na mimi nimesoma fatwa zenu nyingi kuwa inafaa kwa mtu pamoja na kuwa kuna tafauti za rai kuwa kumfuata aliyesema kuwa inafaa kupunguza, je, inafaa kwangu kuifuata ruhusa hii kwa kuzingatia masafa machache yanayozingatiwa kuwa ni ya msafiri na kupata ruhusa ya kukusanya sala ukizingatia ilipo nyumba yangu na eneo ninalofanya kazi ni karibu kilomita 15?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kauli (maneno) ambayo ameitaja Ibn Omar –radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie – hakuna katika kauli hiyo kinachothibitisha kuwa masahaba walikuwa wakikusanya au wakipunguza (sala) walipokuwa wako mbali na nyumba zao kwa kiasi cha maili moja, isipokuwa hii ni kauli amejinasibisha nayo Abdallah Bin Omar – radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie - aliposema: Lau kama nitatoka masafa ya meli moja basi hupunguza sala. kisha hayo ni mapokezi mamoja kati ya mapokezi tafauti ambayo ameyapokea – radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie- na kwa njia tafauti.
Na kauli iliyo sahihi na yenye kutegemewa kimapokeo ni iliyopokelewa kutoka kwake ni ile iliyoelezewa na Imamu Bukhari, kwa kuwa kaifanyia sehemu maalumu katika kitabu chake kwa anuani ya (Sura, ni kiasi gani cha masafa cha kupunguza sala.) amesema: Mtume – rehma na amani zimshukie- ameita mchana na usiku safari. Na Ibn Omar na Ibn Abbas –radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie– walikuwa wakifuturu (hawafungi swaumu) kwa (masafa ya) maili nne. Mwisho. [Na kauli hii imemfikia Ibn Mundhir na Al bayhaqiy kwa njia sahihi].
Na kwa kuwepo mapokezi mengi na kauli nyingi kutoka kwa ibn Omar –radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie- Al hafidh Ibn As qalaniy anasema katika [Fat-hu l bari]:
Na wametofautiana na Ibn Umar katika kuweka mipaka ya masafa hayo, kwa hitilafu ambayo haikutajwa:
Abdul Razak amepokea kutoka kwa Ibn Jurayh: "NafiI amenieleza kuwa Ibn Omar alikuwa kiwango cha chini alichokuwa akipunguza sala –alipokuwa- akienda Khaibar." Na kutoka Madina mapaka Khaibar ni maili tisini na sita.
Na Waki`i amepokea kwa mapokezi mengine kutoka kwa Ibn Omar kuwa amesema: "Anapunguza kutoka Madina mpaka Asuweida." na baina yake ni masafa ya maili sabini na mbili.
Na Abdul Razak amepokea kutoka kwa Malik Kutoka kwa Ibn Shihab kutoka kwa Salim kutoka kwa baba yake kuwa "Alisafiri kwenda Riym na akapunguza sala." Abdul Razal amesema: Nayo –Riym- ni masafa ya maili thalathini kutoka Madina.
Na Ibn Abi Shaibah amepokea kutoka kwa Waki`i kutoka kwa Musa`r kutoka kwa Muharib amesema: Nimemsikia Ibn Omar akisema: "Mimi husafiri kwa saa wakati wa mchana na hupunguza." Athauri akasema: Nimemsikia Jalabah Bin Suhaim kutoka kwa Omar akisema: "Lau kama nitatoka masafa ya maili moja basi hupunguza sala." Na mapokezi yote ni sahihi.
Na mapokezi hayo yametafautiana sana. Mwisho.
Na kusema kuwa masafa machache ya kupunguza ni maili ni maneno ambayo pia ameyasema Ibn Hazim Adha hiriy, amepokea imamu An nawawi kutoka kwa Adh dhahiri kuwa wao wameweka makadirio ya maili tatu.
Isipokuwa haya yote ewe ndugu imewekewa shuruti ya kuwepo maana ya safari, sawa iwe ni kwa Ibn Omar au Sahaba mwingine – radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie- au kwa Ibn hazim au kwa Adhahiriya. Na Ibn Omar na wengine hawakusema kuwa kusafiri kutoka katika mji wake au kijiji chake kwa masafa ya maili au zaidi au chini ya hapo, -kwa namna yeyote usafiri- safari ya kuruhusika kupunguza sala na kufuturu kwa aliyefunga huzingatiwa bali wanazuoni wameafikiana kuwa sharti la kuwepo safari ni kuzidi masafa ya makazi anayoishi.
Na kwa maana hii ndio ikawekwa ruhusa ya kupunguza sala na kuweka mipaka katika kuondoka (kusafiri) kwa namna yeyote au hali yeyote; inawezekana safari ikawa kuondoka Nchini au Mji wake au bandari yake au anga yake au mahema yake au viwanja vyake au maeneo yaliyoshikamana na Nchi.
Na wala haikupokewa kwa yeyote katika waliotangulia na wala waliopo ya kuwa, kwa kufanya safari ya kwenda Mjini au Kijijini kwa masafa ya aina yeyote –kwa urefu wowote – itaitwa kuwa ni safari, lakini hakuna budi kuhakikisha kile kinacholazimu kuitwa safari, nacho ni kuondoka na kwenda Mjini au sehemu yeyote, na hii ndio alichokusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema: {Na mnaposafiri katika Nchi si vibaya kwenu mkifupisha sala} [AN NISAA: 101].
Maneno ya waliotangulia na wanazuoni na kutofautiana kwao kwa jitihada zao hizi zote zimejengeka kwa kuangalia maana ya safari na katika aya hii kwa kuzingatia tofauti za zama zao na matatizo yao na mazingira yao. Hakuna tofauti ya undani, na wala haisihi kusema kuwa mwanazuoni yeyote anaruhusu kupunguza sala iwapo mtu anaondoka na kwenda sehemu nyingine katika Mji mmoja (Mji huo huo). Isipokuwa watakuwa wameifasiri aya kinyume, kwa ajili hiyo Ibn Mundhir amesema kama alivyonukuu kutoka kwa Ash Shaukani katika [Nail Al autwar 3/235] "Wamekubaliana kuwa, mwenye kutaka kusafiri akitoka na kuacha nyumba zote katika Kijiji, na wametofautina iwapo kabla ya kutoka nyumbani (na tafauti hii yote, ni kutaka safari (safari ya uhakika) ambayo ni kuondoka."
Wanazuoni wakaeleza kuwa ni lazima uziache nyumba zote, na baadhi ya wanazuoni wa Kuffi, wanaona kuwa akitaka kusafiri atasali rakaa mbili hata kama ni nyumbani kwake, na wapo waliosema: Akiwa katika kipando akitaka atapunguza. Na kutilia mkazo Ibn Al mundhir Al awal, kuwa wao wamekubaliana kuwa ataanza kupunguza pindi akiwa keshayapita (yupo nje ya Mji) majumba na wakatofautiana kabla ya kuyapita majumba.
Itamlazimu itimize (kusali kama kawaida bila ya kupunguza) mpaka ithibiti kuwa inamlazimu kupunguza. Akasema: sielewi kwamba Mtume –rehma na amani zimshukie- alipunguza alipokuwa katika safari miongoni mwa safari zake isipokuwa alipotoka na kwenda Madina.
Hivyo, tafauti za mapokezi kutoka kwa Ibn Omar na wengine katika Masahaba –radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie – zitafahamika –kama alivyoelezea Ibn Taimiyya na wengine– hizo hazitokuwa zimepingana isipokuwa ni tofauti za hali – namna - ya safari (yenyewe) kwa kulingana na maeneo na Miji ambayo huanza safari kwa upande na kwa upande mwengine kwa kuangalia ukubwa wa Mji na maeneo ya safari yake na kwa kuangalia –pia- ukubwa wa majengo yake kwa upande wa tatu.
Kwa hivyo, ukubwa wa Mji kwa hivi sasa na kukua maeneo yake na majengo yake kwa kuwa na masafa makubwa hali huwa ni tafauti sana, na hupelekea kuendana na mapokezi yaliyopokewa kutoka kwa Ibn Umar –radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie– ndani ya Miji ya kisasa iliyokuwa kimaeneo kuwa haiwezekani hata kidogo. Na ikibidi basi huwa ni kutoichukua ruhusa iliyokuja katika aya tukufu. Na haisihi ruhusa kwa safari ya mwendo wa magari ndani ya Mji kwa masafa ya maili au chini yake au zaidi yake.
Lakini masafa ya safari ambayo wanazuoni wameyakisia ni yale yenye kuanza mwisho wa majengo, hii ni kwa upande wa Mji ambao mtu huanzia safari yake, na si kwa upande mwingine wowote, kwa mfano tukijaalia Mji ni mkubwa na eneo lake ni kubwa kiasi cha kufikia masafa ya safari kwa mtazamo wa wanazuoni , basi kukata masafa hayo haitokuwa (haitojulikana) kama ni safari kisheria yenye kuhalalishiwa kupewa ruhusa ya kupunguza.
Nasi tunaposema: Inafaa kwa mtu kumfuata yule aliyeruhusu, tulikuwa tunakusudia;
kwanza: Maneno ya wenye kujitahidi walio huru ambao wamethibiti kutoka kwa wenzake mapokezi yake na hadithi zake, ikiwa na maana maneno yake yako sahihi kwa upande wa uthibitisho na kwa upande wa uelewa (kufahamika).
Pili: Kutekelezwa kwa masharti ambayo yanaambatana na tukio.
Tatu: Kumfuata anayetoa –anayejibu– maswala (anayefutu maswala) katika jambo hilo inakuwa kwa maneno ya waliotoa majibu (katika waliotangulia) wenye ujuzi na fani yao kwa kufahamu mazingira yaliyotangulia. Kwani kuna tofauti kati ya kusoma maneno kutoka huku na huko na kati ya kufahamu kisha kutoa fatwa ambayo inakwenda sambamba na maelezo yake na tukio lake pamoja na usambamba wa wakati halisi na uhalisi wa jambo lenyewe. Na wala haifai kwa mtu aliyekalifishwa na sheria kufanya haraka katika kutekeleza kauli yeyote ambayo anaisikia au kuisoma bila ya kuichunguza kwa umakini, kwani kuichunguza kwa umakini ndio asili ya fatwa.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas