Kuvua Hijabu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuvua Hijabu

Question

Mimi ni mwanamke mwislamu, nilieolewa na mwanamume mwislamu kutoka Marekani, na tunaishi pamoja katika nchi hiyo ya Marekani.
Naye hanipi fedha zozote za matumizi isipokuwa huwa ananinunulia chakula tu, pamoja na kuwa yeye daima hunitendea ubaya na kunitishia kuwa atanipa talaka, na hunitia kasoro kuwa mimi ni mgumba.
Na mimi hivi sasa nimekuwa katika hali mbaya ya kinafsi na nimekuwa nikienda kwa Mganga wa Magonjwa ya Nafsi mara kwa mara, na wala siwezi kuendelea na Swala zote, kwani matibabu yananisababishia usingizi, na mimi ninataka hivi sasa niivue hijabu yangu.
Je jambo hili ni katika madhambi makubwa?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu Mtukufu hailazimishi nafsi kufanya jambo isiloliweza, na wala Mwenyezi Mungu Mtukufu hajatuleta hapa Duniani ili tuje kuwa wanyonge. Kwa hiyo, kuwa na dhana nzuri kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na iwapo hutaweza kuendelea na ndoa hiyo basi inajuzu kwako kisheria kuomba talaka. Na wala hulazimiki kuishi maisha ya huzuni kama vile uko kifungoni.
Na inawezekana mume huyo akawa mtu mwema moyoni mwake lakini Sheria haiamrishi kuendelea kuwa nae hata kama hali hii itafikia kuwa ni maradhi ya nafsi na kutoka katika mafunzo ya kiislamu. Bali kwa kuwa na nguvu, ondoka katika hali ya unyonge na kusalimu amri, hali ambayo umekuwa ukiishi na uufungue moyo wako kwa ajili ya maisha, na utafute furaha vizuri na kwa nguvu bila ya kuzembea au kukata tamaa, na umchague Mola wako Mtukufu katika kuiendeleza ndoa yako na iwapo utaiona furaha yako kwa kuwa na mume wako huyo basi endelea kuwa naye. Na kama sio hivyo, basi omba talaka na utafute maisha mengine utakaiyokuta furaha yako ndani yake pamoja na mapenzi yako ya elimu yenye mafunzo ya Kiislamu.
Na kwa upande wa Swala hapana ubaya wowote kuiacha ukiwa katika hali ya kupitiwa na usingizi lakini unapozinduka utazilipa swala zote zilizokupita.
Ama kwa upande wa Hijabu, hiyo ni Faradhi kwa Mwanamke wa kiislamu, na unaweza ukatumia kile kinachositiri nywele zako na kifua chako bila ya kupindukia, na Madhambi Makubwa ya kweli ni wewe mwanamke kujiachia katika hali kama hii ya kinafsi iliyo mbaya ambayo inaweza kukuangamiza. Na usinyongee katika kupambana na maisha kwa nguvu, kwa hivyo mwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na umtegemee yeye pamoja na kumdhania kheri, kwani yeye ndiye Mola Mkarimu asiyetutakia isipokuwa furaha hapa Duniani na kesho Akhera.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas