Kulipa (kukidhi) Swala Zilizompita ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kulipa (kukidhi) Swala Zilizompita Mtu Aliyeziacha Kwa Makusudi

Question

Ipi hukumu ya kulipa Swala kwa mtu aliyeziacha (kupita wakati wake) kwa makusudi?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kauli iliyopo kwa madhehebu yote manne yenye kufuatwa pamoja na wanazuoni waliotangulia na waliopo kuwa Swala haiondoki dhima yake kwa aliyeiacha kwa makusudi. Inamlazimu kuilipa, na ataitanguliza kabla ya kusali Swala ya Sunna, kama alivyosema Mtume –rehma na amani zimshukie - : “Lipeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu ana haki ya kulipwa.”
Imamu Ibn Qudama Al Hanbaliy anasema katika kitabu cha: [Al Mughniy]: "Upambanuzi: Iwapo Swala nyingi zimempita, ni lazima ajishughulishe kwa ajili ya kuzilipa, ilivyokuwa hakupatwa na matatizo ya mwili au mali yake… na Ahmed ameelezea katika Hadithi iliyopokelewa na Saleh inayohusu kijana mwenye kupoteza Swala: Anatakiwa azilipe mpaka asiwe na shaka kama kuna Swala kaiacha. Na atazilipa Swala za Faradhi tu, na wala hataswali Swala za Sunna zozote baina ya Swala za Faradhi, kwani Mtume – rehma na amani zimshukie – alizilipa Swala nne siku ya Khandaq, na akamuamrisha Bilali akakimu Swala kisha akaswali Adhuhuri, kisha akamuamrisha, akakimu Swala akaswali Alasiri, kisha akamuamrisha, akakimu Swala akaswali Magharibi, kisha akamuamrisha, akakimu Swala na akasali Swala ya Isha. Na haikutajwa kuwa aliswali Sunna baina ya kila Swala, kwani Swala ya faradhi ni muhimu sana, na kujishughulisha nayo ni bora, isipokuwa kama zitakuwa Sunna nyepesi nyepesi, hali kama hiyo haitakuwa tatizo kuzilipa Sunna hizo (Kabla ya Swala na baada ya Swala), kwani Mtume – rehma na amani zimshukie – ilimpita Swala ya Asubuhi, na akalipa Sunna yake (Kabla ya Swala)." ] Mwisho.
Na nasaha kuhusu kutekeleza Sunna hizo, ataswali kila Swala na Sunna inayoambatana nayo, kwa mfano Sunna ya Swala ya Asubuhi atasali akiambatanisha na Swala ya Asubuhi, Adhuhuri iambatane na Adhuhuri, Alasiri kwa Alasiri na mfano kama huu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas