Ushiriki wa Waislamu Katika Uchagu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ushiriki wa Waislamu Katika Uchaguzi wa Bunge Katika Nchi za Wasiokuwa Waislamu

Question

Je, inaruhusiwa kushiriki katika uchaguzi wa ukafiri wenye sheria ambazo ni kinyume na Sheria ya Kiislamu katika nchi isiyo ya Kiislamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Inaeleweka kwamba miongoni mwa matakwa ya Sheria ya Kiislamu ni kuleta maslahi na kuondosha ufisadi; Alghazali anasema katika kitabu chake kiitwacho [Al-Mustasfa, uk. 174, Darul Kutub Al-Ilmiyyah]: “Na maslahi katika asili yake ni kuleta manufaa au kuondosha madhara, lakini hatukukusudia hivyo. Kwa sababu kuleta manufaa au kuondosha madhara ni makusudio ya viumbe na sifa ya wema ya viumbe ni kufanya makusudio yao, lakini tunakusudia kwa maslahi ni kulinda makusudio ya Sheria, nayo ni matano: Kuhifadhi dini yao, nafsi zao, akili zao, kizazi chao, na mali zao. Kila kinachogusia mambo hayo ni maslahi, na kila kisichoyagusia ni ufisadi, na kuuondosha ni maslahi”.
Inajulikana kuwa nchi zisizo za Kiislamu zina sheria zinazotungwa na watu, sheria hizi zinazingatia manufaa ya kidunia tu, nazo zinazokubaliwa na Halmashauri zikiwemo zinazofaa Waislamu, na zikiwemo zisizowafaa. Kwa hivyo, ushiriki katika uchaguzi wa chama fulani kinachoelekezwa kwa ajili ya maslahi ya Waislamu unaweza kuleta manufaa na kuondosha madhara mara nyingi.
Muislamu ambaye ana haki ya Uzalendo katika nchi isiyo ya Kiislamu ana haki ya kushiriki katika uchaguzi wa bunge wa nchi hii kama akidhani kwamba ushiriki wake utaleta manufaa kwa Waislamu. Kama vile: Kutoa picha sahihi ya Uislamu, kutetea masuala ya Waislamu, kupata mapato ya kidini na ya kidunia kwa wachache, kuimarisha mchango wao katika madaraka, kufikisha matakwa ya wazalendo Waislamu kwa wenye madaraka, na hayo yote ni miongoni mwa maslahi yanayotakiwa, kwa sharti ya kuwa mambo hayo hayaleti madhara katika dini yake.
Sheikh Ibn Taymiyah katika kitabu chake kiitwacho [Al-Istiqamah 2/216, Chuo Kikuu cha Mohammad Ibn Saud] anasema: “Kanuni ya jumla kuhusu kupinga kwa maslahi na ufisadi, faida na hasara, inalazimika kupendelea jambo ambalo ni sawa zaidi. Kama amri na katazo likitakiwa kuleta maslahi au kuondosha madhara inatazamiwa kwa kinyume chake, kama maslahi yanayopatwa au ufisadi unaofanywa ni zaidi, hairuhusiwi kama ikiwa na madhara zaidi kuliko maslahi”.
Ushiriki huu unatazamiwa kupitia mtazamo wa uwiano kati ya maslahi na madhara. Na kutoa Fatwa kuhusu suala hili kunatofautiana kwa mujibu wa hali ya watu, wakati na mahali. Kutokana na hivyo, Baraza la Kifiqhi la Kiislamu katika zamu yake ya tisa lililofanyika katika Makao Makuu ya Kiunganishi cha nchi za Kiislamu, Makah, katika kipindi cha 22-27 mfunguo wa pili 1428 H., tarehe 3-8 Novemba 2007, azimio la Baraza hili limetolewa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas