Kupachiza na Uhandisi wa Maumbile

Egypt's Dar Al-Ifta

Kupachiza na Uhandisi wa Maumbile

Question

Ni nini hukumu ya kutumia uhandisi wa maumbile kwa ujumla na kutumia kupachiza na hasa katika nyanja za kibinadamu, mimea, na wanyama? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Katika Uislamu hakuna kikwazo chochote kwa utafiti wa kisayansi, lakini kikwazo kiko katika kugeuka kutoka utafiti wa kinadharia wa kisayansi kwa kuwa matumizi ya kweli. Miongoni mwa vikwazo hivi ni vinavyohusiana na maadili, maadili ya kazi, makubaliano na maafikiano, nia, lengo na hatima, mtazamo uliotawala, mfumo wa kisheria, na halali na haramu katika sheria ya Kiislamu.
Kusoma kupachiza kwa mujibu wa vikwazo hivi, Wanazuoni Waislamu wa siku hizi wameona kuwa kupachiza kwa wanadamu ni haramu, lakini kupachiza kwa wanyama na mimea kunaruhusiwa kama kukiwa na manufaa kama kuboresha kwa uzazi, kwa sharti ikiwa hakuna madhara kwa wanyama au mimea, au kama ikiwa hali hii haileti dosari yeyote katika uwiano wa mazingira hata baada ya muda mrefu.
Katika kongamano la Baraza la Fiqhi la Kiislamu lililofanyika katika mji wa Jadah, Saudi Arabia, mfunguo tano (Safar), mwaka 1418 B. H, tarehe 28 Juni, 1997 B. K, kwa mujibu wa mazungumzo yaliyohudhuriwa na madakatari na wanazuoni wa Fiqhi, Baraza la Fiqhi la Kiislamu lilitoa baadhi ya maamuzi kama ifutavyo:
Maamuzi namba 94 (2/10) kuhusu kupachiza wanadamu:
- Kwanza: Hairuhusiwi kupachiza wanadamu kwa nija yeyote inayopelekea uzalishaji wa binadamu.
- Pili: Kama hukumu hii ya kwanza haikutekelezwa, athari za hali hizi zinaonesha hukumu za Sheria.
- Tatu: Ni haramu kwa hali zote ambazo upande wa tatu unaingizwa kwa uhusiano wa kindoa, kama ikiwa tumbo la uzazi au yai au mbegu za kiume au seli ya mwili kwa ajili ya kupachiza.
- Nne: Inaruhusiwa kwa mujibu wa Sheria kuchukua mbinu za kupachiza na uhandisi wa maumbile katika nyanja za bakteria, vidudu wote, mimea, na wanyama katika mipaka ya Sheria kufuatana na yanayofikia manufaa na kuepusha maovu.
- Tano: Kukata rufaa nchi za Kiislamu kwa kutoa sheria na mifumo itakiwayo kwa ajili ya kufunga mlango wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja mbele ya pande za ndani au za mgeni, taasisi za utafiti, na wataalamu wageni ili kuzui kuchuku nchi za Kiislamu mifano ya kujaribia kupachiza wanadamu na ukuzaje wake.
- Sita: Kufuatilia kwa pamoja kutoka Baraza la Fiqhi la Kiislamu, na Shirika la Kiislamu Sayansi ya Utabibu kuhusu suala la kupachiza, maendeleo yake ya kisayansi, kudhibiti istilahi zake, kufanya makongamano yatakiwayo kwa ajili ya kuonesha hukumu za Sherea zianzohusiana na suala hili.
- Saba: Kutoa wito kwa kuunda kamati maalum zinakusanya wataalamu na wanazuoni wa Sheria kwa ajili ya kuweka udhabiti wa kimaadili katika nyanja ya tafiti za biolojia ili ipitiwe katika nchi za Kiislamu.
- Nane: Kutoa wito kwa kuanzisha na kukuza Chuo na taasisi za kisayansi zinazofanya tafiti katika nyanja ya Biolojia.
- Tisa: Kuweka misingi maalumu kwa maendeleo ya kisayansi kutoka mtazamo wa Kiislamu, na kuviita vyombo vya habari kwa ajili ya kupitia mtazamo wa kiimani pamoja na suala hili na kuepusha kulitumia kinyume cha Uislamu kwa ajili ya kuongeza uelewa wa Umma ili kuthibitisha kabla ya kuchukua uaamuzi wowote.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

 

Share this:

Related Fatwas