Kuvua Hijabu Kuogopa Juu ya Maisha ya Baba
Question
Nilisilimu na nikakata nia kuvaa hijabu tangu miezi mitatu, na familia yangu haikuwa ikijua jambo hili mpaka sasa, kwani familia yangu ina kasumba kwa kiasi kikubwa mno na inauchukia Uislamu, na familia yangu ikanialika kuhudhuria sherehe ya krismasi na baba yangu akakazia hayo. Na madaktari wametuonya kuwa mzazi wangu asipatwe na jambo lolote la kumsababishia hali tete au hata shinikizo, ambapo aliwahi kupatwa na tatizo kubwa la moyo wiki mbili zilizopita, na mimi natambua kuwa hali ya mzazi wangu haitaweza kuhimili kuniona mimi nimevaa hijabu, Na kwa wakati huo huo, haitawezekana kwangu kuwadhihirishia ndugu zangu wageni wasio na hijabu. Je nifanye nini? Kwani mimi hivi sasa niko baina ya ung'ang'anizi wangu wa kuvaa hijabu na hatari ya kuzoroteka kwa afya ya mzazi wangu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hijabu ni vazi lenye hukumu ya Faradhi kwa mwanamke wa kiislamu aliyebaleghe, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao,na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri waoisipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao} [AN NUUR 31].
Na Abu Dawud, Al Baihaqiy na Atwabaraniy wakatolea kutoka kwa Aisha R.A., kwamba Asmaa Bint Abi Bakr R.A. akaingia Mtume S.A.W., Na alikuwa amevaa nguo nyepesi na Mtume S.A.W, akamkwepa, na akasema: "Ewe Asmaa, Hakika mwanamke anapobaleghe na kutokwa hedhi haifai kwake kuonekana sehemu za mwili wake isipokuwa hapa na hapa, akaashiria usoni na katika viganja viwili vya mikono.
Na jambo likiwa kama hilo: Haijuzu kuivua na kufichua kile kinachositiriwa katika mwili mbele ya watu wasio kuwa ndugu isipokuwa katika hali ya dharura tu au haja ambayo inaingia katika nafasi ya dharura kama vile matibabu au utoaji wa ushahidi; kwani mambo ya dharura huhalalisha vilivyokatazwa. Na haja huwa inakuwa katika nafasi ya dharura kwa ujumla au kwa taifa maalumu/na wamesema: Hakika huu ni uchungaji katika kila dini. [Al Ashbaah Na Anadhair kwa Asyutwe K. 85-88, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Ashatwebiy akasema katika kitabu cha:[Al Mwafaqaat 10/2, Ch. Dar Al Maarifah]: " Na mjumuiko wa dharura ni katika hali tano; kuhifadhi Dini, roho, kizazi, mali, na akili. Na wamesema kwamba yanaangaliwa katika kila mila. Ama kwa upande wa mahitaji mbali mbali: Maana yake kuwa yeye anayahitaji kwa mapana zaidi, na kuondosha uzito ambao mara nyingi hupelekea ugumu na matatizo hapo baadae kwa kukosa kinachohitajika, na kama kipato hakitaangaliwa".
Ama kuhusu hali inayouliziwa: Na ikiwezekana kwako kujiepusha na hasira za mzazi wako ambazo zitakuathiri kiafya kwa kuzizungumzia na kutosheka au kujizuia na kwenda katika sherehe inayotazamiwa kufanyika kwa udhuru wowote unaoweza kuwa kuutoa au hata kinyume na hayo, basi utalazimika kufanya hivyo. Na kama sio hivyo, na kama haiwezekani kwako, kwa hali yeyote iwayo; kwa namna ambayo inasababisha kujizuia kwako na machafu yanayoongeza uovu wa uvuaji wa hijabu, basi utalazimika kuivua ndani ya usiku huu tu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mjuzi zaidi ya wote.