Maana ya Kutawala Juu ya Kiti cha E...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya Kutawala Juu ya Kiti cha Enzi

Question

Nini maoni ya Al Azhar katika mwelekeo uitwao Wasalafi unaoona kwamba Mwenyezi Mungu “Ametawala juu ya Kiti cha Enzi”, bila ya kuwepo katika mahali maalumu. Wanasema kwamba: Mwenyezi Mungu amekaa juu ya Kiti cha Enzi, lakini hatujui namna ya ukaaji huu ulivyo? Hakika watu wengi waligawanyika katika suala hili, basi je, maoni ya Masalafi yanalingana na Uislamu jinsi unavyotaka au yanahitilafiana? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Miongoni mwa mambo thabiti ya Imani (itikadi) ya Waislamu ni kwamba Mwenyezi Mungu hana pahala maalumu pa kumzunguka wala hana mipaka ya wakati; kwani pahala na wakati ni miongoni mwa viumbe vyake, naye Mwenyezi Mungu Ametukuka na hali ya kumzungukwa na kitu chochote Alichokiumba, bali Yeye ni Muumbaji wa kila kitu, Naye Anavizunguka vitu vyote. Hii ndiyo itikadi ambayo Waislamu wote waliafikiana juu yake, na hakuna yeyote anayeikanusha isipokuwa mwenye kukanusha haki. Watu wa elimu walisema: “Mwenyezi Mungu Alikuwepo wakati wa kuwa hakuna pahala, Naye Anaendelea kama Alivyo kabla ya kuumba pahala, hajabadilika ...”, na miongoni mwa maneno ya waja wema waliotutangulia katika suala hili:
Maoni ya Imamu Jafar Al Sadik ya kwamba: “Yeyote anayedai kuwa Mwenyezi Mungu anazungukwa na kitu au ametokana na kitu basi amemshirikisha Mwenyezi Mungu; kwani akiwa anazungukwa na kitu, basi anakuwa ananyimwa Pahala maalumu, na akiwa juu ya kitu basi anakuwa anabebwa, na akiwa ametokana na kitu basi anakuwa ameumbwa”.
Iliulizwa kwa Yahya bin Muaz Al Razy amzungumzie Mwenyezi Mugu, basi alisema: Ni Mmoja tu peke yake, akaulizwa: Vipi anakuwa Yeye, alijibu: Mwenye kumiliki Mwenye Uwezo. Ikaulizwa: Yuko wapi: Akajibu: Yuko kwenye mavizio Anawavizia. Basi mwenye swali akasema: Si kukuuliza hivyo! Akasema: Iliyo kinyume na hiyo ni sifa ya viumbe ama sifa Yake Mwenyezi Mungu, basi nilikwisha kubainishia.
Dhu Al Noon Al Misry R.A. aliulizwa ni nini maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Arrahman, Mwingi wa Rehema, aliyetawala juu ya Kiti cha Enzi}[TWAHA, 5], akajibu: “Alithibitisha dhati Yake na akakanusha pahala pake; maana anakuwepo kwa dhati Yake na vitu kwa hehima Yake kama anavyotaka”.
Ama yaliyotajwa katika matini za Qur`ani Tukufu na Sunna iliyotakaswa yaliyobainisha kwamba Mwenyezi Mungu yuko juu ya viumbe vyake, basi yanamaanisha kuwa Mwenyezi Mungu Anajitukuza kwa cheo Chake na uwezo Wake; hakuna yeyote katika viumbe Vyake anayekuwa na mfano Wake. Sifa zao haziwezi katu kufananishwa na sifa Zake Mwenyezi Mungu, Naye hana sifa iliyoweza kuambatanishwa na sifa za viumbe viliyo na kasoro. Bali Yeye Ana sifa za ukamilifu na majina mazuri mazuri, na kila unayoyawaza hayawezi kuyaafikiana na ya Mwenyezi Mungu. Na ukosefu wa kutambua utambuzi ni utambuzi, na kutafiti katika dhati ya Mola ni ushirikina.
Itikadi (Akida) ya Al Azhar ni Al Asha’riya nayo ni Itikadi ya watu wa Sunna na Jamaa, na Ashai’ra R.A. ni wengi wa Maulamaa kati ya watu wa Umma, nao ndio waliojibu shaka kwa wasio na mungu na wengineo. Nao ndio walioshikamana na Qur`ani Tukufu na Sunna ya Mtume wetu S.A.W. katika zama zote, na yeyote anayewakufirisha au anayewatuhumu kwa ufasiki au anayewakashifu katika Itikadi yao, basi anakuwa ameruka mipaka. Al Hafez bin A’saker – Mwenyezi Mungu Amrehemu – amesema katika kitabu chake: "Kudhihirisha uwongo wa …": “Ujue – Mwenyezi Mungu Anipe na wewe tawifi ya kupata radhi zake na Atujaalie kuwa ni miongoni mwa waliomcha kwa hali iliyotakiwa – ya kwamba nyama ya Maulamaa ina sumu, na ada ya Mwenyezi Mungu wa waliokashifu kasoro yao ni maalum, na yeyote anayewapunguzia haki zao Mwenyezi Mungu Atafisha moyo wake kabla ya kufa”.
Al Azhar ni chimbuko la elimu na dini katika zama za historia ya Kiislamu, na taasisi hii ilijenga Jopo kuu la kielimu iliyo maarufu sana katika Umma baada ya karne zilizo bora za mwanzo, na Mwenyezi Mungu Ameihifadhi dini yake kwa taasisi hii ya Azhar dhidi ya kile mwenye ukaidi na mwenye kutia shaka; na yeyote anajaribu kukashifu Itikadi yake atakuwa katika hatari kubwa tena inaogopeka awe miongoni mwa wale Khawarij na Murjifiin ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewasema: {Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu}[AL AHZAAB, 60].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

 

 

Share this:

Related Fatwas