Mtazamo wa Uislamu kuhusu Demokrasi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtazamo wa Uislamu kuhusu Demokrasia

Question

 Nini hukumu ya Uislamu kuhusu Demokrasia kwa upande wa dhana na utekelezaji wake?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Demokrasia ni istilahi yenye asili ya Kigiriki, imeundwa kutokana na maneno mawili : (Demos), na maana yake ni: Watu, na (Kratos); na maana yake ni utawala, Demokrasia inaainishwa kuwa ni Utawala wa watu kutoka kwa watu na kwa ajili ya watu.
Kwa ufafanuzi wake huo wa kimagharibi Demokrasia inaitukuza hadhi ya utawala wa watu mpaka ikawafanya wawe na mamlaka ya juu, na haki ya kutunga na kuweka sheria. Hakuna mamlaka nyingine inayokuwa sawa na mamlaka hii. Kwa hivyo, inawatawala watu wote, na inawalazimisha watu wote, kutokana na uwezo wa hali ya juu iliyo nao kwa amri na makatazo. Na mambo hayo ndivyo yalivyo katika Mihimili yote Mikuu; Mhimili wa Serikali unatekeleza sheria ya umma au utashi wa watu, Mhimili wa Sheria unagusia mambo yote kwa mujibu wa hukumu na sheria zinazopitishwa na kutolewa na Mhimili wa Bunge.
Kama watu wataafikiana kuhusu jambo lolote, likapitishwa kisheria litatumika hata kama likiwa miongoni mwa makatazo na marufuku katika dini zote.
Demokrasia kwa maana hii haikubaliani na Sheria ya Mwenyezi Mungu isiyoitambua isipokuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu tu; {Hakuna hukumu yeyote isipokuwa ya Mwenyezi Mungu peke yake.} [Al-Anaam: 57]; Mwanazuoni Abu Al-Souud alisema katika tafsiri yake [3/142, Dar Ihyaa Al-Turaath Al-Arabi]: {Yaani: …hakuna hukumu katika kila kitu isipokuwa ya ile ya Mwenyezi Mungu peke yake pasi na kuwapo mchango wowote wa mwengine}.
Mhimili wa Bunge katika Uislamu umefungamana na hali maalumu ya kidini. Yaani wanaowawakilisha watu katika kutunga sheria hawawezi kufanya kitu chochote nje ya mipaka ya sheria. Kila uamuzi unaopinga sheria hauzingatiwi. Hali hii inatofautiana na mfumo wa kidini wa Nchi za Magharibi unaokiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye utawala wa kisiasa wa juu, na kwamba sheria za Mungu ni sheria za kiraia ambazo ni wajibu kutekelezwa, na kwamba wanavyuoni wa kidini ambao ni wataalamu wa sheria hizi za Mungu wanawakilisha mamlaka ya Mwenyezi Mungu na ni lazima kwao kutekeleza sheria hizi za mungu.
Ni wazi kuwa kuna tofauti kubwa kati ya mifumo hii miwili, Mfumo wa Kiislamu na Mfumo wa Kimagharibi, kwa sababu hakuna ukuhani katika Uislamu au mamlaka ya Mungu kwa yeyote.
Lakini Demokrasia ikiwa na maana ya misingi ya kisiasa au ya kijamii kama kushauriana, na msingi wa kutenganisha Mhimili wa Bunge, Mhimili wa Mahakama, Mhimili wa Serikali, kubadilishana maoni, kuhakikisha uadilifu, uhakika wa haki ya kuishi, haki ya kazi, na haki ya uhuru kwa wote. Hakuna shaka kwamba hali hii Uislamu unaikubali na unailingania iwepo. Vile vile inawezekana kufahamu hali hii kutoka katika mfumo wa Kiislamu ikiwa ni kwa njia ya uwazi au kwa njia ya dalili, Mwenyezi Mungu anasema: {Na shauriana nao katika mambo} [AALI IMRAAN: 159]. Pia alisema: {Na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao} [AS SHURA: 38].
Mwisho:
Demokrasia ina aina mbalimbali zinazofaa na kuendana na nchi zinazoifuata. Waislamu katika nchi yeyote wanaruhusiwa kufuata aina za Demokrasia ambazo hazipingani na Mambo thabiti ya Sheria ya Kiislamu na misingi yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya woye

 

Share this:

Related Fatwas