Kutafsiri Maana na Uwakilishi Kati...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutafsiri Maana na Uwakilishi Katika Sifa za Mwenyezi Mungu

Question

 Nini njia sahihi kuhusu sifa za Mwenyezi Mungu: Je ni kuwakilisha namna au kuwakilisha maana? Kisha inajuzu kufasiri maana za sifa za Mwenyezi Mungu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Waliotangulia na waliowafuatia wamekubaliana katika kukanusha shani zenye shaka kwa viungo au matukio katika haki ya Mwenyezi Mungu, kisha waliotangulia waliwakilisha maana zilizotakiwa wala hawakuziainisha. Ama waliowafuata wamejitahidi katika kuziainisha maana hizo, ingawa wote waliafikiana juu ya kwamba maana zilizo dhahiri ni tofauti na zilizo ndani, na ya kwamba haijuzu kuainisha namna maalumu kwa sifa hizi pamoja na kuwepo hali ya kutozitambua, basi hapa unakusudiwa uwakilishi wa maana baada ya kukanusha shani zenye shaka kwa matukio, sio uwakilishi wa namna; kwani namna zote ziliumbwa na Mwenyezi Mungu, hayo ndiyo yaliyopokolewa na watu wema waliotangulia miongoni mwa Masahaba na waliowafuata na Maulamaa Waislamu; hakika Maimamu wa waliotangulia na waliowafuata R.A. wote waliafikiana juu ya kutakasika Mwenyezi Mungu na matukio, na ya kwamba hakuna mipaka ya wakati wala pahala inayoweza kumzunguka yeye, na ya kwamba haijuzu kuyachukua maandiko haya yaliyotaja sifa Zake kidhahiri kwa hali yeyote. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Bakr R.A. alisema: “Kushindwa kuufikia utambuzi ni utambuzi, na kutafiti katika dhati ya Mwenyezi ni ushirikina”, kadhalika alisema: “Ametakasika yule ambaye hajawawekea viumbe vyake njia ya kumjua yeye ila kwa njia ya kushindwa kumjua”, aidha imesimuliwa na Sayidna Ali R.A. ya kwamba alisema: “Haiulizwi wapi? Kwa nani wa wapi? Tena haiulizwi ni kwa jinsi gani? Vipi na kwa nani”, Imamu Malik R.A. alisema: “Mwenye Rehema Alitawala juu ya Kiti cha Enzi kama Alivyojisifu, haiulizwi: Ni kwa jinsi gani? Na vipi haijuzu katika haki yake” … n.k. miongoni mwa matini zilizotajwa kutoka kwa watu wema (masalafu) waliotangulia katika kumtakasika Mwenyezi Mungu.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas