Inayotakiwa kwa Mwenye Uadui kwa Ui...

Egypt's Dar Al-Ifta

Inayotakiwa kwa Mwenye Uadui kwa Uislamu

Question

Kuna Jumuiya nchini Uholanzi inayouelezea Uislamu kuwa ni dini ya kibaraka, na inaona kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Uislamu na tabia ya uhalifu. Je, hali hii inazingatiwa ni uadui wa Uislamu wa moja kwa moja ambao inalipa taifa haki ya kufaradhisha jihadi ya “kimaadili?"  

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ni wajibu juu ya Waislamu kutochangia kwa upinzani wao kuhusu kusisitiza picha ya uongo dhidi ya Uislamu na Waislamu, bali ni juu yao kufafanua utata huu, kuthibitisha kwa watu na wanajamii kwamba Uislamu ndio ni dini ya huruma, upendo na kuishi pamoja. Jihadi ina maana pana katika Uislamu, hali ya kuonesha picha hii ni jihadi kwa njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo, Wanazuoni wanasema kuwa: “Wino wa Wanazuoni ni bora zaidi kuliko damu ya mashahidi” ; kwani Jihadi kwa mdomo, kulingania, kuonesha dhana kunausitisha umwagikaji damu, na kunahifadhi nafsi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas