Hukumu ya Nikabu

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Nikabu

Question

 Nikabu ina hukumu gani katikaUislamu? Je, Nikabu inatokana na dini?

Answer

  Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mavazi ya kisheria yanayotakiwa kutoka mwanamke mwislamu ni vazi lolote lisiloonesha wasifu wa maeneo fitinishi ya mwili wala lisiloonesha mwili, na linausitiri mwili isipokuwa uso na viganja viwili. Ama kwa upande wa Nikabu ya mwanamke inayoufunika uso wake pamoja na vitambaa vya kufunika viganja vyake, jamhuri ya wanavyuoni miongoni mwa kihanafiya, kimalikiya na kishafiya, na hiyo ni madhehebu ya Al Awzaa'i na Abi Thaur miongoni mwa masalafu wenye ijitihadi na kauli moja katika madhehebu ya Ahmad wanasema kuwa: Uchi wa mwanamke wa kiislamu aliye huru ni mwili wake wote isipokuwa uso na viganja viwili vya mikono yake ndivyo inajuzu kuonekana.
Imamu Al Mirghinaniy Al Hanafiy akasema katika kitabu cha: [Al Hidayah 258/1, pamoja na Sharhu Al Inayah, Ch. Dar Al Fikr] "Na mwili wote wa mwanamke aliye huru ni uchi isipokuwa uso wake na viganja vya mikono yake".
Na Sheikhi Adarder akasema katika kitabu cha: [Asharhu Al Kabiir, miongoni mwa vitabu vya Al Malikiyah 215/1, pamoja na Sharhu Adusuqiy, Ch. Dar Ihyaa Al Kutub Al Arabiyah]. "Na Uchi wa mwanamke alie huru mbele ya mwanamume mwislamu mgeni ni mwili wake wote isipokuwa uso wake na viganja vya mikono wake"
Na imekuja katika kitabu cha: [Isniy Al Matwalib miongoni mwa vitabu vya kishafiy kwa Sheikh Zakariyah Al Answari 177/1, Ch. Dar Al Kitab Al Islamiy], "Na uchi wa mwanamke aliye huru katika swala (mbele ya wasiokuwa ndugu) au hata nje ya swala ni mwili wake wote isipokuwa uso na viganja viwili"
Na Al Mardawiy Al Hanafiy akasema katika kitabu cha: [Al Inswaf 452/1, Ch. Dar Ihyaa Aturath Al Arabiy] "Yaliyo sahihi katika madhehebu kwamba uso sio uchi, na maswahaba wanaafikiana na hayo, na katika viganja viwili simulizi mbili"
Na miongoni mwa dalili zao ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika}[AN NUUR 31]. Ambapo Jamhuri ya maswahaba na waliokuja baada yao, wameelezea pambo linalodhihirika kuwa ni uso na viganja viwili. Hayo yamenukuliwa kutoka kwa Ibn Abaas, Anas na Aisha R.A wote.
Imamu Atwabariy amesema -na huyo ni miongoni mwa maimamu wakuu wa Tafsiri na mmoja miongoni mwa maimamu wa Ijitihadi katika Fikihi ya Kiislamu- baada ya kunukulu kutoka kwa maswahaba na waliokuja baada ya maswahaba tafsiri nyingi za uzuri wa wazi unaokusudiwa katika aya [Tafsiru Atwabariy Jami'u Al Bayaan 158-189/19, Ch. Mu'asasat Aresalah]: "Na katika kauli zilizo bora kwa usahihi: Kauli ya aliyesema: Alikusudia kwa hayo: Uso na viganja viwili: Huingizwa katika kauli hizo iwapo itakuwa hivyo: kama vile Uwanja, pete, mikufu na hina (vipodozi vya kupakaa).
Hakika mambo yalivyo ni kwamba sisi tumesema hivyo kauli zilizo bora katika jambo hilo katika tafsiri, kwa Ijmaai ya wanavyuoni wote juu ya kwamba kila mtu anayeswali analazimika kusitiri uchi wake katika swala. Kwamba mwanamke anapaswa kufichua uso wake, na kwamba anapaswa kusitiri kisichokuwa hivyo viungo viwili, isipokuwa yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. kwamba yeye amemhalalamikia amfichulie mkono wake kiasi cha nusu yake.
Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo kwa wote wao, basi inaeleweka hivyo kwamba mwanamke ana nafasi ya kudhihirisha mwili wake kwa zile sehemu zisizokuwa uchi kama ilivyo kwa mwanaume. Kwani kisichokuwa uchi sio haramu kukidhihirisha, na iwapo atalazimika kukidhihirisha, inaeleweka kwamba hakika ni katika kile alichokitenga Mwenyezi Mungu Mtukufu, {isipokuwa unao dhihirika} kwani vyote hivyo ni wazi kwake.
Na inaunga mkono hayo pia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao}[AN NUUR 31]; Kwani kilemba ni kitambaa kinachofunika kichwa, na kile kinachositiri kama vile gauni na mfanowe. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Alimwamrisha mwanamke mwislamu kukifunikia kwa shungi yake kichwa na kifua chake. Kama kusitiri uso kungelikuwa wajibu basi Aya tukufu ingeliweka wazi jambo hilo.
Na kutoka Sunna Tukufu: Hadithi ya Aisha R.A.: "kwamba Asmaa Bint Abi Bakr aliingia kwa Mtume S.A.W. Na alikuwa amevaa nguo nyepesi na Mtume S.A.W, akamkwepa, na akasema: "Ewe Asmaa, Hakika mwanamke anapobaleghe na kutokwa hedhi haifai kwake kuonekana sehemu za mwili wake isipokuwa hapa na hapa, akaashiria usoni na katika viganja viwili vya mikono." [Ikatolewa na Abu Dawud], Na zinginezo miongoni mwa dalili za wazi za kutowajibisha kusitiri uso na viganja viwili vya mikono.
Na Al Bukhariy akapokelea katika kitabu chake: [Sahihi ya Al Bukhariy] kutoka kwa Ibn Omar R.A. wote wawili, kwamba Mtume S.A.W. akasema: "Mwanamke aliyehirimia asivae nikabu wala vitambaa vya kufunika viganja". Na hiyo ni dalili ya kuwa uso na viganja viwli vya mwanamke aliye huru si uchi.Je iweje alete picha kuwa viungo hivyo ni uchi pamoja na kukubaliana kuvifichua katika swala na uwajibu wa kuvifichua katika Iharamu?
Inaeleweka kuwa sheria kamwe haiwezi kuja kuruhusu kuufichua uchi katika swala na kuwajibisha kuufichua katika Ihramu. Na vinavyoharamishwa katika Ihramu ni vitu ambavyo kiasili ni halali kama vile kuvaa nguo zilizoshonwa, mafuta uzuri, kuwinda na mfano wa vitu hivyo. Na wala hakuna katika hivyo kitu chochote ambacho kilikuwa wajibu kisha kikawa haramu katika Ihramu.
Na kadhalika yaliyopokelewa na Al Bukhariy na Muslim katika vitabu vyao viwili sahihi, kutoka kwa Ibn Abaas R.A. wote wawili; akasema: "Alfadhlu alikuwa amepanda kipango nyuma ya Mtume S.A.W, akaja mwanamke kutoka Khothom na Alfadhlu akawa anamwangalia. – Na imekuja katika baadhi ya mapokezi: na huyo mwanamke alikuwa mzuri - akimwangalia Alfadhlu na Mtume S.A.W, akawa anauepusha uso wake na kuuelekeza upande mwingine, na akasema huyo mwanamke: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika faradhi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake katika Hijja naishi na Baba yangu akiwa Mtu mzima hawezi kutulizana juu ya mnyama, Je, inajuzu mimi ninahiji badala yake? Mtume S.A.W. akasema: Ndiyo." Kama uso ungelikuwa uchi basi ni lazima usitiriwe na Mtume S.A.W asingelikubali kufunuliwa kwa uso mbele ya watu, na angelimuamrisha aufunike, na kama uso wake ulikuwa umefunikwa basi Ibnu Abas asingeweza kumtambua kama mzuri au mbaya.
Na yaliyopokelewa na Abu Dawud katika sunna zake kutoka kwa Aisha R.A., "Kwamba Asmaa Bint Abi Bakr akaingia kwa Mtume S.A.W. Na alikuwa amevaa nguo nyepesi na Mtume S.A.W, akamkwepa, na akasema: "Ewe Asmaa, Hakika mwanamke anapobaleghe na kutokwa hedhi haifai kwake kuonekana sehemu za mwili wake isipokuwa hapa na hapa, akaashiria usoni na katika viganja viwili vya mikono."
Na kwa kuwa kuna haja inayopelekea kuonesha uso wakati wa kuuza na kununua na kudhihirisha viganja kwa ajili ya kuchukulia na kutoa kitu na kwa ajili hii viungo hivyo havikufanywa kuwa ni uchi.
Kwa hivyo basi kuufunika uso na viganja viwili vya mikono ya mwanamke mwislamu sio faradhi, na mwanamke akiamua kusitiri uso na viganja vyake basi inajuzu, na iwapo atatosheka na hijabu inayotambulika kisheria bila ya kufunika uso na viganja vyake basi atakuwa ameepukana na lawama na ametekeleza wajibu wake.
Na kinachofaa kukitaja ni kukumbusha kuwa Nikabu na nyinginezo ni katika mambo yanayohusu mavazi yanayozidi kiwango cha kusitiri uchi ambako ni wajibu – na huwa ni ufuasi wa mila na desturi walizonazo watu.Na wafuasi wa Madhehebu ya Maliki wameeleza kuwa Nikabu kama sio mazoea ya watu wa nchi maalumu basi kuivaa kunakuwa ni katika ukali na uongezaji katika Dini
Sheikh Eliish amesema katika kitabu cha: [Manhu Ajalili Sharhu Mukhtaswer Khalil 226/1, Ch. Dar Al Fikr]: "Na inachukiza (mwaname kuvaa nikabu) yaani kufunika uso wake hadi katika macho yake katika swala na nje ya swala na mguu ni bora zaidi isipokuwa na desturi ya watu maalum, basi haiwi karaha katika isiyo kuwa swala na pia huchukiza katika hali yeyote kwani ni katika ukali wa Dini. "Na amefananisha katika chukizo akasema ni kama mkono yaani kukusanya na kuinua kitamba mikononi na nywele katika swala, rejea katika kiganja, kwa hiyo vazi la Nikabu kwa vyovyote vile linachukiza."
Pamoja na kuchukiza wametaja kuwa itahofiwa fitna kwa sababu ya mwanamke kufichua uso na viganja vyake basi ni wajibu kuvisitiri. Al Khatwab akasema katika kitabu cha: [Mawaheb Al Jalili 499/1, Ch. Dar Al Fikr], " Jua kuwa iwapo itachelewa kutuka fitna basi ni wajibu kwa mwanamke kuufunika uso na vinganja vyake viwili" Al Kadhi Abdulwahaab akasema hayo na Sheikh Ahmad Zaruuq akainukulia hiyo katika kitabu cha [Sharhu Aresalah] na hiyo ni dhahiri ya maelezo."
Na imebainika kwa hoja hii kuwa asili ya Nikabu kwa Madhehebu ya Maliki inarejea katika mila, na iwapo itakuwa ni katika mila basi ni halali kama sehemu ya maisha ya watu wote, kwa namna ambayo inakuwa nje ya mzunguko wa ibada kwa kuivaa kwake.Kama haikuwa ni kawaida basi huchukiza kwa vyovyote iwavyo, ni sawa sawa kwa ibada au kwa vinginevyo; kwani wakati huo huwa ni kupindukia katika Dini ambako Sheria Samehevu haikuja na hukumu hiyo, na kutumia kwa ibada kitu kinachochukiza kwa upande wa kuwa kwake kinachukiza ni kuchukiza kwenyewe, au kinyume cha sheria, na kwa kile kilichopindukia katika Dini ni uzushi ambao haijuzu kuufanya.
Ama pale hali itakapobadilika kwa namna kuondosha madhara kwa wotu wote au kwa baadhi kunategemea kuvaa Nikabu kwa kuchelea fitna au maudhi basi kwa hali hiyo Nikabu huwa wajibu kuvaliwa. Na kwa njia hii hii, hali zinaweza kubadilika zikalifanya vazi la Nikabu kuwa haramu kwa mfano kama patahofiwa maudhi kwa mwanamke atakaelivaa, kwa hivyo uwajibu na uharamu wake katika hali hizo una hukumu zinazojitkeza na wala hazitokani na vazi lenyewe kwa kitu chochote, bali zinatokana na mazingira yanayolizunguka vazi hilo na matokeo yanayopatikana juu yake.
Na kwa mujibu wa hayo yaliyotangulia, hakika vazi la Nikabu, kama halikuwa mazoea ya watu kulivaa kwake na likageuzwa na kuwa alama inayompelekea mtu katika kuwagawa wanawake wa kiislamu walio wamoja na wenye kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake S.A.W,Kwa namna ambayo, mwenye kuvaa vazi hilo hupewa sifa ya dada mwenye kufuata mafundisho ya dini, na yule asiyelivaa yuko kinyume na hivyo au hajafikia ufuataji wa mafundisho ya dini aliyoyafikia dada yake mwenye kuvaa Nikabu, na pakawepo ufuasi na uadui kwa ajili hiyo, na hili ni jambo linalochukiza kisheria.
Kwa hivyo basi, ufupisho wa maneno haya ni kuwa: Vazi la Nikabu kwa jinsi lilivyo ni halali kwa sharti la kutokufanywa kama alama ya ufuasi wa Dini na kwa ajili ya kufanyia ibada; kwani kufanya hivyo ni kuwagawa waislamu kwa jambo lenye hitilafu ndani yake na linaloendana na mila na desturi za watu. Bali vazi hili linaweza kupelekea kiburi kwa jinsi ambavyo mwenye kulivaa akawa anawadharau wenzake ambao hawalivai au akawa anawaangalia kwa kuwadogesha kicheo mbele ya Mwenyezi Mungu.
Na ikiwa hijabu ilijulikana katika enzi za Mtume S.A.W, - na hajaikataza; basi hii ni dalili ya uhalali wake kwake, ama ikiwa yatajitokeza yale tuliyoyasema ya uduasi na usafi juu yake na kuwagawa watu na kuwa ndugu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wengine wasio wafuasi wa mafunzo ya dini; kwa ajili hiyo, maandiko ya kisheria kwa hivyo, yanahukumika kuzuia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas