Hukumu ya Kuvaa Mavazi Yaliyoenea ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kuvaa Mavazi Yaliyoenea Katika Nchi Zisizokuwa za Waislamu

Question

 Mimi ninakaa nchini Ufaransa .Ni mavazi gani yanayofaa kwa kutokea barabarani, na kadhalika wakati wa swala? Na ni ipi mipaka ya kushabihiana na wasio waislamu katika nchi isiyo yaKiislamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Suala la mavazi katika Uislamu linaachiwa katika mila na desturi za watu zisizopingana na Uislamu; kwa maana kuwa Uharamu huwa unapatikana kwa kwenda kinyume na mwonekano wa kiislamu kama vile mavazi yaliyovaliwa yakawa yanaudhihirisha uchi au yanaonesha kilicho ndani ya mwili na hivyo kudhihirisha uchi na maeneo yanayotakiwa kufunikwa.
Ama mwislamu anapovaa mavazi ya watu wa nchi yake – ni sawasawa wawe watu hao ni waislamu au makafiri – huko sio katika kujifananisha kwa lolote; kwani uislamu hauhangaikii wafuasi wake wawe na sifa ya kipekee kwa kuwa tu na sifa hiyo.Hakika mambo yalivyo ni kuwa Uislamu unawaamrisha wao kuwa na maadili mema ya kipekee na yenye kujumuisha wema na kuchunga utukufu wa binadamu pamoja na utekelezaji wa ahadi na mikataba mbali mbali, na kuchunga mfumo mkuu, na kuheshimu maadili na kuwapenda pamoja na kuwahurumia.
Hakika mambo yalivyo ni kuwa Uislamu unawaamrisha wao kuwa na maadili mema ya kipekee na yenye kujumuisha wema na kuchunga utukufu wa binadamu pamoja na utekelezaji wa ahadi na mikataba mbali mbali, na kuchunga mfumo mkuu, na kuheshimu maadili na kuwapenda pamoja na kuwahurumia.
Na kauli ya Mtume S.A.W. iliyosimuliwa na Abu Dawud katika Sunna zake kutoka kwa Ibn Omar R.A. wote wawili kwamba akasema: Mtume S.A.W. akasema: "Yeyote atakaejifananisha na watu basi yeye ni katika watu hao". Inasemekana kuwa maana yake ni: Inahukumika uharamishaji wa kujifananisha kwa sababu ya kuwa kwake kujifananisha. [Iqtidhaa Aswiratwal Mustaqeem kwa Ibn Taimiah 271/1, Ch. Alam Al Kutub]
Na kwa mujibu wa hayo yaliyotangulia, nguo zitakazokuwa katika mazoea ya watu mila na desturi zao na likatoweka kusudio la kujifananisha nao basi hazikatazwi. Basi Mtume S.A.W. aliswalia akiwa amevaa kanzu ya kishamu kama ilivyopokelewa katika vitabu viwili sahihi toka kwa Hadithi ya Al Mughirah Bin Shubah na Imamu Al Bukhari akafasiria kwa mlango huo kwa kauli yake: Mlango wa Swala katika kanzu ya kishamu; na Al Hafidh Bin Hajar akaielezea katika kitabu cha: [Al Fathu 473/1, Ch. Dar Al Maarifa, Bairut, 1379 H] basi akasema: "Ufasiri huu ni mgumu kwa kujuzisha swala kwa nguo za makafiri iwapo hapatapatikana uhakika wa unajisi wake, bali isipokuwa ameelezea kishamu ni kwa ajili ya kuchunga tamko la Hadithi, na kwa wakati huo, Miji ya Shamu ilikuwa ni ya kikafiri"
Na bwana wetu Omar Bin Al Khatwab R.A. akaigiza waajemi katika kuanzisha madiwani ya serikali na wala hawajaleta wasifu wa kushabihiana na wasiokuwa waislamu. [Rejea: Al Ahkaam Aswultwaniyah kwa Al Mawardiy uk. 249, Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Na hivi sasa, waislamu wanavaa mavazi ambayo asili yake sio ya waislamu kwa jinsi yalivyo, na wala huku hakujawahi kuzingatiwa kuwa ni kujifananisha nao hao wasio waislamu; kwa kuwa asili ya kujifananisha kwa mavazi hayo imekwishasahaulika na wala haizingatiwi kuwa ni alama ya hao wasio kuwa waislamu, na inasemwa kuwa: Ni mazoea yaliyoenea baina ya watu, na asili yake imesahaulika.
Kisha kujifananisha hakuitwi kujifananisha kwa kupatikana mfanano tu, bali hapana budi pawepo kusudio na mwelekeo huo; kwani kujifananisha: Ni kutenda, na mada hii inamaanisha mfungamano wa nia na mwelekeo wa kukusudia kitendo husika na usumbufu wake. Kwa hivyo, kujifananisha kunakokatazwa haipatikani maana yake isipokuwa kwa kutia nia ya kufanya hivyo kwa makusudi.
Na inaashiria kwa hayo pia yaliyopokelewa na Imamu Muslim katika kitabu chake [Sahih Muslim] kutoka kwa Jabir R.A. alisema: "Mtume S.A.W alilaumu tuliswali nyumba yake akiwa amekaa na kisha akatugeukia na kutuona tukiwa tumesimama na akatuashiria tukakaa na alipotoa salamu kisha akasema: Mlikaribia hapo kabla kufanya kama wafanyavyo wafursi na warumi wao husimama mbele ya wafalme wao huku wafalme hao wakiwa wameketi, msifanye hivyo, wafuatisheni maimamu wenu wakiswali wamesimama basi nanyi swalini mkiwa mmesimama, na wakikusalisheni wakiwa wameketi basi nanyi swalini mkiwa mmeketi."
Na inakaribia kumaanisha katika uthibitishaji wake juu ya kutoweka habari yake pamoja na mkaribiano na kutuka kwake, na kitendo cha Wafursi na Warumi kimetokea kweli miongoni mwao lakini Maswahaba kwa yale ambayo hawajayakusudia kuwa ni kujifananisha, basi wasifu wa kufanya hivyo ulitoweka kwao kisheria
Na baadhi ya wasomi walieleza mambo hayo katika vitabu vyao; Ibn Najiim Al Hanafiy anasema katika kitabu cha: [Kanz Adaqaiq 11/2, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy]: "Tambua kuwa kujifananisha na watu wa kitabu haichukizi katika kila kitu, na sisi tunakula na kunywa kama wafanyavyo wao, isipokuwa uharamu unakuja kwa kujifananisha nao kwa yale mabaya na yale ambayo yanakusudiwa kujifananisha nao."
Sheikh Taqiyu Adiin Ibn Taimia hueleza kwamba kwenda kinyume na wasiokuwa waislamu katika mavazi na mila na desturi zao za wazi sio wajibu katika hali ya kuyafikia masilahi ya kidini au kuondosha ufisadi wa kidunia kwa kukubaliwa, bali huwenda ikafikia kutaka kukubaliwa kiwango cha kupendeza na wakati mwingine kuwa wajibu katika nyakati nyingine.
Basi Ibn Taimia akasema katika kitabu chake cha: [Iqtidhaau Aswiratu Al Mustaqeem 471/1]: "Kama mwislamu atakuwa katika nchi inayoupiga vita uislamu, au nchi ya kikafiri isiyoupiga vita uislamu; na wala hakuamrishwa kwenda kinyume nao kwa mwongozo wa wazi kwa madhara yanayoweza kumpata bali inaweza kuwa vizuri kwa mtu au ni wajibu juu yake kushirikiana nao baadhi ya nyakati katika mwenendo wao wa wazi, kama kufanya hivyo kuna masilahi yeyote kwa ajili ya dini; kwa kuwalingania katika dini na kuyachungua kiundani mbambo yao ili kuwaambia waislamu mambo hayo, au kuwaondoshea waislamu madhara yao na mengine yanayofanana na hayo miongoni mwa makusudio mazuri. Ama kwa upande wa kusudio la mfananisho wa wazi bila ya uwepo wa haja yeyote inayozingatiwa hupelekea kutangazwa uelemeaji na ufuasi na kusudio la kutaka umaarufu na kwa ajili hii ni jambo linalosemwa vibaya kisheria."
Na kwa mujibu wa yaliyotangulia jibu la swali linajieleza.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas