Kuwateka Wanawake Katika Vita

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwateka Wanawake Katika Vita

Question

 Nimeulizwa na mtu mmoja asiye Mwislamu: Je, Uislamu unaruhusu wanaume Waislamu kuwaoa wanawake ambao wameolewa na mateka wa kivita? Na je, Hadithi ambayo Mtume S.A.W. aliwaruhusu Waislamu kuwabaka wake wa Makafiri mbele ya waume zao, ni sahihi?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu kamwe hauruhusu kuwabaka wanawake, wala hauruhusu kuzini pasipo na kubaka hata kwa idhini ya pande mbili.
Lakini kuhusu kuoa vijakazi (waliomilikiwa na mikono ya kulia) siyo miongoni mwa kubaka, bali ni njia inayoruhusiwa kisheria ambayo Mwenyezi Mungu ameiruhusu, ameijengea mfumo maalum na hukumu zake, pia ameruhusu kuoana na wanawake kwa mujibu wa mfumo na hukumu maalumu, na hizi zote ni hukumu za Mwenyezi Mungu ambaye hakuna wa kuzipinga hukumu zake. Uislamu umeruhusu kuwaingiza watu utumwani kwa wapiganaji, wanawake na watoto ambao wapo katika vita pia. Lakini wasio wapiganaji hairuhusiwi kuwaingiza wao utumwani kamwe. Utumwa wa wapiganaji ni bora zaidi kuliko kuwaua. Utumwa ukitokea, ni jambo la lazima kufuata adabu zilizolazimishwa kwa watumwa hawa; kama vile Kutendeana vizuri na upole, kutoruhusiwa kuwaudhi na uharamu wa kuwashambulia. Hadithi ile ilikuwa katika kipindi ambacho kuteka na kuwaingiza watu utumwani ilikuwa ni hali ya kawaida kwa watu wote ulimwengu kwa wakati huo. Wasio Waislamu walikuwa wakiwateka wake wa Waislamu kama wangeweza, mpaka ilipokuja kubadilishwa hali hii na kuwapo jela kwa mateka, na vitendo vingine vinavyoainishwa katika mikataba ya kimataifa, na ambavyo Waislamu wanawajibika kutekeleza pamoja na nchi nyinigne zote. Lakini kuhusu anayedai kuwa kuna Hadithi moja ambayo Mtume S.A.W. aliwaruhusu Waislamu kuwabaka wake wa Makafiri mbele ya waume zao, Hadithi hii kamwe siyo sahihi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas