Sherehe za Ndoa Katika Kanisa la Mk...

Egypt's Dar Al-Ifta

Sherehe za Ndoa Katika Kanisa la Mke Kisha Kuifunga Ndoa Msikitini

Question

Mimi ni mwanamume Mwislamu. Nataka kumwoa mwanamke Mkatoliki, Je tunaweza kusherehekea ndoa katika kanisa kisha aje pamoja nami katika msikiti? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu ni dini ya usamehevu, na inataka wafuasi wake wawe mfano mzuri kwa kuishi pamoja na kutendeana katika jamii wanaoishi ndani yake, na Kuingia mwislamu kwenye kanisa si haramu, ambapo hapatakuwa na jambo baya, Sheikh Shihabu-Diin A-Ramliy katika Maelezo yake ya Asnal-Matalib anasema: “Haijuzu kwa mwislamu kuingia makanisani bila ya idhini ya kitendo na ya kitamko; kwa sababu wao wanachukia kuingia kwa waislamu ndani yake. Alisema hivi Sheikh Ezzi-Diin.
Suala lake ni kujuzu kwa idhini, kwa kuangalia kutokuwepo picha ndani yake, kama ilivyosemwa na mtungaji wa kitabu cha [Ash-shamil na Al-Bayan kutoka kwa wanachuoni 4/219, Ch. ya Dar Al-kitaab Al-islamiy].
Mkataba wa ndoa ambapo upande mmoja wake ni mume mwislamu katika kanisa si haramu, sharti kuwepo nguzo na masharti ya usahihi wa ndoa, na haya yakipatikana basi ndoa ni sahihi, lakini kupotea nguzo au sharti au yakiwepo matendo yanayopinga dini ya Uislamu, basi ni haramu, na mtendaji wake ni mwenye dhambi.
Kwa mujibu wa hayo: Hakuna ubaya kwenda pamoja na mke wako kanisani kwa ajili ya kuwapendezesha na kuwafurahisha jamaa zake, sharti usishiriki katika matendo yanayopinga imani ya kiislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas