Kumwingilia Mke Wakati wa Hedhi.
Question
Je, yafaa kwa mume kumwingilia mke wake wakati akiwa na hedhi?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kumwingilia mke wakati wa hedhi ni haramu kwa kauli za wanachuoni wote, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na wanakuuliza wewe Mohammad kuhusiana na hedhi sema yenyewe ni udhia basi jitengeni na wanawake katika hedhi, na wala musiwaingilie mpaka wawe wametakasika, na pindi watakakapo takasika basi waendeeni katika pale alipowaamuru Mwenyezi Mungu} [Al-Baqara, 222].
Ama kustarehe nae kinyume na kumuingilia katika starehe zingine, zitakapokuwa nje ya eneo la kati ya kitovu na magoti inafaa kwa makubaliano ya wanachuoni wote, ama kustarehe nae sehemu ya kati ya kitovu na magoti pasi ya kumwingilia kwenye tupu wanachuoni wengi wamesema inafaa.
Na dalili yao ni Hadithi iliyopokelewa na Abu Dawud kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A. kuwa Wayahudi walikuwa pindi mwanamke anapokuwa na hedhi wanamtoa kwenye nyumba, hawampi chakula maji wala kumwingilia ndani ya nyumba, basi akaulizwa Mtume S.A.W. kuhusu jambo hilo, ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu Akateremsha kauli yake: {Na wanakuuliza wewe Mohammad kuhusiana na hedhi sema yenyewe ni udhia basi jitengeni na wanawake katika hedhi} mpaka mwisho wa Aya, basi Mtume S.A.W. akasema: “waingilieni majumbani, na wafanyieni kila kitu isipokuwa tendo la ndoa”
Na Imam Al-Nawawiy amesema kuhusu madhehebu haya: “Ni yenye nguvu zaidi kwa upande wa dalili”
Mwanaume ni halali kustarehe na mke wake kinyume na kumwingilia kwenye tupu hata ikifikia kuteremsha manii, na ni juu yake mwanaume kujihifadhi na kutochafuka na damu, hasa damu ya kwanza ya hedhi ambapo inakuwa ni nzito, na mwanamke anatakiwa asitiri tupu yake vile wanavyo fahamu wenyewe wanawake na hivyo kuzuia uchafuzi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.