Matukio ya Kuacha Uislamu Ili Kupa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Matukio ya Kuacha Uislamu Ili Kupata Haki za Mali Zilizo Chukuliwa.

Question

Mimi ni Mwislamu - raia wa Kimarekani - kiasi cha miaka kumi, nilikuwa naishi nchini kwangu (Marekani) maisha mazuri na yenye raha kutokana na kazi yangu kama mfanyabiashara - pesa zangu ni kiasi cha milioni 3.4 dola za Kimarekani - na nina miliki nyumba nilikuwa naishi kwenye nyumba hiyo na mchumba wangu wa zamani na ambaye anamiliki nusu yake - inakadiriwa kiasi cha milioni 4.5 dola za Kimarekani - lakini pindi nilipokuwa Mwislamu maisha yangu yamekuwa ni magumu sana nchini kwangu, kwa sababu familia yangu na marafiki yangu wamenishinikiza sana ili niache Uislamu na kurudi kanisani, na pindi waliposhindwa familia na marafiki ambao walikuwa washiriki wangu katika kazi wote wamenitenga, mzazi wangu wa kiume amehamisha pesa zangu kwenye akaunti yangu na kuingiza kwenye akaunti nyengine amelifanya hili kwa sababu ya uwakili niliompa wakati nikiwa katika safari zangu za kazi, lakini hata mchumba wangu wa zamani amekataa kuuza nyumba au kununua hisa zangu kwenye nyumba, hivyo nimeondoka Marekani kiasi cha miaka kumi hivi sasa na kuelekea nchini Kuweit, ili niweze kutekeleza ibada za sala kusoma Qur`ani kwenda msikitini na kufuata Sunna za Mtume S.A.W. kwa sababu ilikuwa ni vigumu sana kutekeleza mwenendo huu nyumbani kwangu, na mimi hivi sasa nimeoa mwanamke wa Kikuweit na nimezaa naye mtoto mwenye umri wa miaka mitatu, na ndani ya kipindi hiki nilikuwa najaribu kufanya kazi zangu za kibiashara, lakini kwa masikitiko makubwa kumekuwa na vikwazo vingi, kwani maafisa wengi husika wanataka mrungura ili kurahisisha na kuniwezesha kupata mikataba ya kibiashara, na kwa kile ninachokijua mimi ni kuwa mrungura ni haramu hivyo si kubaliani nao, ama kwa upande wa Marekani mzazi wangu amekuwa akizungumza na maafisa husika kila ninapotaka kuingia mtakaba wa kazi na wao basi wanarudi nyuma kufanya kazi na mimi, kwa hakika maisha yangu yamekuwa ni magumu sana na hasa nimekuwa na familia ya kuihudumia, madeni yetu yamekuwa ni mengi mno na kwa sababu ya kutowezekana kufanya kazi, uhusiano wangu na mke wangu umekuwa ni wenye kuyumba, na mimi hivi sasa naishi na mke wangu nyumbani kwao mpaka nitakapo pata ufumbuzi wa hali hii ambayo tunaishi nayo.
Nilifanya mawasiliano na mzazi wangu ndani ya masiku kadhaa yaliyopita ili kutaka mali zangu, ili niweze kulipa madeni yetu na kununua nyumba ili kuhifadhi familia yangu na kuzifanyia kazi, lakini amekataa na kusema kuwa yeye alinitahadharisha na Waislamu kuwa ni watu wenye kuuwana wenyewe kwa wenyewe na kuuwa Wamarekani, na kwa upande mwingine pia serikali ya Marekani hivi sasa inawafuatilia kwa ukaribu Waislamu na kuwachunguza msikitini, wananchi wengi nchini Marekani wanachukia kushirikiana na Waislamu, na akasema kuwa ili iwezekane kurudisha pesa zangu ninapaswa kumwacha mke wangu na nimuoneshe talaka kisha nirudi kanisani na kujiunga na kundi la (freemason) ambalo yeye ni mfuasi wake, na kukiri mbele ya watu wote kuwa mimi nilikuwa nimefanya makosa kuhusu kuwa Mwislamu, na kumuoa mchumba wangu wa zamani.
Kwa hakika nimekuwa Mwislamu baada ya kujua maadili ya Uislamu ndani ya Qur`ani tukufu na Sunna, lakini kwa masikitiko makubwa sijaona kwenye nchi za Kiislamu ambazo nimekwenda dalili yeyote juu ya hilo, nimeona uongo, mrungura/rushwa, na unywaji pombe, na kuanza kuamini kuwa maadili haya ya Uislamu yalikuwepo tu enzi za Mtume na Masahaba, na nilisoma kuwa matatizo humzidishia Mwislamu imani lakini pia kwa masikitiko imani yangu inapungua.
Basi je Mwislamu anaweza kujiunga kwa njia ya siri na makundi mfano wa (freemason) juu ya kuwa ndani yake ana Uislamu? Na ifahamike kuwa baba yangu ndugu zake watoto wao na familia ya mchumba wangu ni wafuasi wa kundi hili na wameshikashika nyadhifa za juu.
Na kama nilivyotaja kuwa nina nyumba mchumba wangu wa zamani anakataa kuiuza au kununua hisa zangu, basi je ninaweza ishi ndani ya hii nyumba na nikatumia chumba kilichojitenga na yeye?
Na je kwa uwezo wangu naweza fanya udanganyifu kwa mzazi wangu na nikadai narudi kanisani na kumuoa mchumba wangu wa zamani ili nipate rejeshewa mali zangu kisha nirudi tena nchini Kuweit kwa mke wangu na mtoto wangu? Na ifahamike kuwa ni kujifanya tu bado Uislamu upo moyoni mwangu?
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu umekuja toka kwa Mwenyezi Mungu nao unawabainishia watu njia sahihi ambayo inaridhiwa na Mwenyezi Mungu, watu wapo makundi katika kuupokea Uislamu:
Miongoni mwao wapo walioikataa njia ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu Uislamu ndani yake kuna amri za kutekeleza: Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha na kukataza, na wanadamu wanapenda sana tamaa na matamanio {Watu wametiwa mapenzi ya kupenda wanawake na watoto na mirundiko ya dhahabu na fedha, na farasi wanaotunzwa vizuri, na wanyama na mashamba. Na hayo ni matumizi ya maisha ya dunia, na kwa Mwenyezi Mungu ndiko kwenye marejeo mazuri}[AAL IMRAAN, 14].
Na miongoni mwao wapo walioamini kwa uwazi ima wameamini kwa sababu ya kupata urithi wa baba yao, ima ili kupata maslahi anayoyaona, na hao ndio wanafiki ambao wanaonesha wasiyoyaamini, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Bila shaka wanafiki wako katika daraja ya chini ya Moto, wala hutakuta kwa ajili yao msaidizi yeyote}[AN NISAA, 145].
Na miononi mwao wapo wenye kupenda sana dunia na kusahau siku ya mwisho, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wanajua hali ya dhahiri ya maisha ya dunia, nao ndio wameghafilika na Akhera}[AR ROOM, 7].
Na mwanadamu atahesabiwa juu nafsi yake tu, na anapaswa kuwa ni mwenye kusubiri kwa yale aliyokadiriwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu {Siku ambayo mtu atamkimbia ndugu yake mama yake na baba yake, mke wake na watoto wake, kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali itakayomtosha}[ABASA, 34: 37].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena: {Na kila mwanadamu Tumemfungia matendo yake shingoni mwake; na Tutamtolea siku ya Kiyama daftari atakayoikuta imekunjuliwa. Soma daftari yako. Nafsi yako inakutosha leo kukuhesabia. Anayeongoka, basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake tu, na anayepotea * basi anapotea kwa hasara (ya nafsi) yake. Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine. Nasi si waadhibishao mpaka Tumepeleka Mtume}[AL ISRAA, 13: 15].
Na akasema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kama ukiwatii wengi wa wale waliomo ardhini Watakupoteza katika njia ya Mwenyezi Mungu}[AL AN'AAM, 116].
Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema tena: {Na wengi wa watu, lau ukipenda, hawatakuwa waaminio}[YUSUF, 103].
Mwenyezi Mungu Mtyukufu Amesema: {Basi uyatangaze uliyoamrishwa na ujitenge mbali na washirikina} [AL HIJR, 94].
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na uwaepuke mwepuko wa wema}[AL MUZAMMIL, 10].
Mwenyezi Mungu Mtukufu kasema: {Kwa hiyo na mimi sasa uvumilivu mtukufu ni mzuri kwangu}[YUSUF, 18].
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlioamini! Atakayeiacha miongoni mwenu dini yake, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu Ataleta watu ambao Atawapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa waaminio, wenye nguvu juu ya makafiri. Watajitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawataogopa lawama ya anayelaumu. Hizo ni fadhila za Mwenyezi Mungu. Humpa Amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua} [AL MAAIDAH, 54].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema tena: {Na katika watu yuko anayemwabudu Mwenyezi Mungu akiwa katika ukingo wa imani; hivyo basi iwapo heri itamfikia hutulia kwayo, na kama atakumbwa na majaribio humgeuzia kisogo Mwenyezi Mungu. Anapata hasara humu humu duniani na vile vile huko Akhera. Hiyo ndiyo hasara dhahiri} [AL HAJJ, 11].
Ni juu yake: Hakika ya kusubiri ni jambo la lazima, basi hii ni kodi ya imani, na dalili ya Uislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Je, watu wanadhani wataachwa waseme tumeamini, nao wasijaribiwe? Na bila shaka Tuliwajaribu wale waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu Atawatambulisha wale wasemao kweli na Atawatambulisha wale wasemao uwongo} [AL ANKABOOT, 1: 3].
Masahaba watukufu na wafuasi wa Mitume walipita katika njia yako kama hiyo: Wamekutangulia na wewe umewafuata, na mwisho mwema ni kwa wachamungu {Na Tukawafanya miongoni mwao maimamu wanaoongoza kwa amri Yetu waliposubiri; na walikuwa wakiziyakini Aya Zetu} [AS SAJDAH, 24].
Ama udanganyifu na kughushi ni haramu, hatutaki kuzuia katika dini ya Mwenyezi Mungu na kuwazuia watu katika dini pindi wanapoona tukio lako, kama vile ulivyostushwa na maadili ya Waislamu, isipokuwa tunataka kurejesha mwenendo wa watu wa mwanzo na mifumo ya watu bora.
Umepata mtihani baada ya juhudi zako kubwa, ndugu zako umewaacha mali zako na nchi yako kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu akukamilishie njia, kwani dunia ni subira ya saa moja, na katika yale matatizo uliyonayo kwa hakika ni bishara ya upendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwako, kutoka kwa Saad Ibn Abiy Wiqas R.A. amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni watu gani wenye mitihani sana? Akasema: “Mitume kisha wa mfano wao na mfano wao, mtu anatahiniwa kutokana na imani yake, basi ikiwa imani yake ni yenye nguvu matatizo yanakuwa mazito zaidi, na ikiwa imani yake ni nyepesi hupatwa na mtihani kwa mujibu wa imani yake, basi mitihani haimwachi mtu akitembea kwenye ardhi pasi ya kuyaondoa matatizo”
Na kwa wale waliokuwa pembezoni mwako mke na wakwe wakusaidie na kubeba maumivu ambayo yamekuumiza wewe na wao, kwa hakika walibeba uzito watu wa Madina na Makka na wakawagawia mali zao nyumba zao na wake zao, na familia yako ipo Kuweit hivi sasa ni sawa na hukumu ya watu wa Madina kuongezea pia hao ni wakwe.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas