Kosa la Kueleza Katika Ufungaji wa Ndoa
Question
Tarehe 24/6/1997 nilifunga ndoa kwa mujibu wa Sheria ya kiislamu, katika makao makuu ya Jumuiya ya Al-Ghadiir ya kiislamu, Paris, Ufaransa.
Tarehe 30/1/2001 mimetalikiwa talaka kubwa kwa kuacha haki za kimali, talaka iliyofuata Sheria ya kiislamu kwenye Jumuiya hiyo hiyo.
Tarehe 20/4/2004 nimeolewa kwa mujibu wa hati rasmi ya ndoa kwa njia ya Mfungishaji wa ndoa, Kairo, Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, lakini tukio la ndoa yangu ya Paris halikuwekwa katika hati rasmi ya ndoa yangu ya Kairo, bila ya mimi kujua.
Swali: Nataka mnipe fatwa ya kisheria kuhusu ndoa yangu rasmi ya Kairo, tarehe 20/4/2004 ni sahihi na haina makatazo ya kisheria kutokuwekwa ndoa ya Paris?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kwa mujibu wa swali: Ndoa ya pili iliyofungwa kwa njia ya hati rasmi, tarehe 20/4/2004, iliyoambatanishwa na ombi, ni ndoa sahihi, na kutotajwa katika ndoa hiyo ya kwanza ya mke hakudhuru, kwa sababu kueleza ubikira au usiokuwa ubikira ni jambo lililo mbali na hakika ya ufungaji wa ndoa, kwa hiyo tukio hili si miongoni mwa nguzo za ndoa wala masharti yake, lakini mke akiwa anajua (Tukio la ndoa ya kwanza na hakusema) basi ni uwongo ulioharamishwa, na haiathiri katika usahihi wa ndoa, na akiwa hajui basi kakuna kitu kwa upande wake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.