Shaka Kuhusu Adhabu Maalumu ya Kuua...

Egypt's Dar Al-Ifta

Shaka Kuhusu Adhabu Maalumu ya Kuua kwa Kupiga Mawe Katika Uislamu

Question

Mimi nina rafiki kutoka Marekani huwa anaushambulia Uislamu. Na yeye hudai kwamba kumwua mke ambaye amezini na mtu mwingine asiyekuwa mume wake kwa kumpiga mawe, baada ya mume kuthibitisha hiyana yake hiyo kwa kuwepo mashahidi wanne ni jambo lisilokubalika. Yeye husema: Kwamba kwa njia hiyo basi wanawake wasio na dhambi wanaweza kuuliwa kwa dhuluma pale mume wake anapowaleta mashahidi wanne wa uwongo na akawapa mali ili waongee. Mtu huyo hakufikiria kukubalika kwa mashahidi; kwani huwenda wakawa wanaongea siku fulani kwa ajili ya sababu yoyote. Tafadhalini nakuombeni mnisaidie ili nimweleze jambo hili rafiki yangu huyo. 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu umeweka misingi kadhaa katika mlango wa adhabu maalumu ya zinaa, miongoni mwa misingi hiyo ni kwamba adhabu ya zinaa huepukwa kwa kuwapo shaka, na kwamba mtu aliyefanya zinaa ambayo inawajibisha adhabu maalumu ya kosa hili, na akajisitiri na akatubu na hakumwambia mtu yeyote, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu huikubali toba yake na humsamehe, kwa kauli ya Mtume S.A.W. katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Malik katika kitabu chake: [Al Muatwa'] kutoka kwa Zaid Bin Aslam: "Aliyefanya uchafu huu wa uzinzi basi ajisitiri kwa sitara ya Mwenyezi Mungu, na yule anayetudhihirishia ukurasa wake huo tunatendeana naye kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu". Na maana ya ukurasa wake ni amali yake aliyoificha katika jambo lake hilo.
Na pia miongoni mwa misingi katika mlango wa zinaa ni kwamba zinaa haimthibitikii mtu isipokuwa kwa njia ya ushahidi wa watu au kwa muhusika kukiri au dalili hasa ya kitendo hicho, na masharti ambayo Uislamu umeyaweka ili kukubali ushahidi wa mashahidi, masharti hayo yanasababisha kuwepo ugumu wa kutekeleza adhabu ya zinaa kwa muhusika yeyote ila akilikiri yeye mwenyewe jambo hilo mbele ya watu, na hazingatiwi anayemwona, isipokuwa awe miongoni mwa mashahidi hao, na sifa hizi kwa ujumla; Uislamu, Kubaleghe, Akili, Uhuru, Uadilifu na udhibiti.
Na nyongeza juu ya hayo katika ushahidi wa adhabu ya zinaa kwamba hao mashahidi wawe wanne, walioona, na watoe maelezo yanayolingana; waseme kwa mfano: Tulimwona akiwa ameiingiza tupu yake yote katika uchi wa yule mwanamke; hii ni kwa sababu ya kuondosha shaka ya kilichofanyika kuwa kinachokusudiwa sio kingine bali ni zinaa, na kwa hivyo basi, azingatie kuzitaja sifa zake. Na miongoni mwa kutoa maelezo pia; ni kwamba mashahidi wanaelezea namna ya tukio lilivyotokea, iwe ni kwa kulala, kuketi au kusimama, au fulani alikuwa juu ya fulani au chini yake na kadhalika.
Na anayeyatazama masharti hayo anakuta kwamba adhabu ya zinaa kimsingi hutekelezwa kwa lengo la kuhifadhi nidhamu kuu, na wala siyo tu kwa ajili ya kumwadhibu aliyezini. Kwa hiyo kuthibitika kwa adhabu ya zinaa hufanyika kwa kutolewa ushahidi na hasa ni katika mambo ya nadra kutokea, na hili ndilo haswa lililowafanya wataalamu wa Sheria ya Misri kwa mfano wasitishe matumizi ya Adhabu maalumu, kwani wao walizingatia kwamba zama hizo ni zama za shaka (shubha).
Na kuna tofauti baina ya kuisitisha adhabu maalumu kama alivyofanya bwana wetu Omar Bin Al Khatwab katika ule mwaka mgumu ujulikanao kama "Ramadah" na kuifuta, kwa sababu ya kuvunjwa kwa masharti ya ushahidi na kuenea kwa uharibifu wa dhima. Na hayo yote yanaafikiana na malengo ya sheria ya kwamba adhabu maalumu huepukwa kwa kuwepo shaka.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas