Uwalii wa Mwanamke Juu ya Nafsi Yak...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uwalii wa Mwanamke Juu ya Nafsi Yake Katika Ndoa

Question

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka thelathini, nakaa na kufanya kazi Ulaya, kijana mwenye tabia njema na dini anataka kuniposa, baba yangu amekufa, na mama yangu aliwaambia baba zangu wakubwa wakutane na kijana huyo kwa ajili ya kuchunguza ombi lake, lakini baba zangu wakubwa wanakataa kukutana naye, pia wanapinga suala la mimi kuolewa naye kwa vyovyote iwavyo. Je inajuzu kwangu niolewe bila ya kukubali baba zangu wakubwa, na katika hali hii nani ni walii wangu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mwanamke mwenye akili na mwenye kuvunja ungo ana haki ya kujiozesha akiwa ni bikira au asiye bikira, na inakuwa ndoa yake ni sahihi kisheria, na hii ni kutokana na kauli zenye nguvu zaidi za madhehebu ya Imam Abi-Hanifa; ambapo inaamuliwa kuwa kuwepo walii si sharti la usahihi wa kufunga ndoa, na kuwa mwanamke akifunga ndoa yeye binafsi inasihi kufanya hivi; na mtazamo wa wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy kuwa: mwanamke ameitumia haki yake halisi, wakati akiwa mwenye madaraka, kwa sababu yeye ni mwenye akili na mtambuzi, na kwa ajili hii ana haki ya kuitumia mali yake, vile vile ana haki ya kuchagua mume wake kwa makubaliano ya wanachuoni, na kila tendo la aina hii linajuzu.[Taz.: Al-Inayah na Al-babertiy 3/257, Ch. Ya Dar Al-Fikr].
Katika kitabu cha [Multaqal-Abhur] na Sherehe yake [Majmaul-Anhur] na mwanachuoni Damad, ni miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy [1/332, Ch. Ya Dar Ihyaa’ Atturath Al-Arabiy] amesema: “(Imetekelezwa) yaani: Inasihi (ndoa ya mwanamke huru …mzima) aikiwa bikira au asiye bikira (bila walii) yaani: Ikiwa ndoa ni bila ya idhini ya walii na kuwepo kwake, kutokana na rai ya mashekhi wawili - yaani: Abi-Hanifa na Abi-Yusuf katika pokezi lililo wazi – kwa sababu mwanamke alitekeleza katika haki yake halisi na yeye ni mwenye madaraka, ambapo yeye ni mwenye akili na mwenye kuvunja ungo, kwa ajili hii ana haki ya kuitumia mali yake, na la msingi hapa ni: Kila mwenye haki ya kuitumia mali kwa madaraka yake mwenyewe, inajuzu kwake kujiozesha, na kila asiye na haki hii haijuzu. [mwisho].
Wanachuoni walieleza Hadithi iliyopokelewa na Abi-Dawuud na wengineo: “Hakuna ndoa bila ya walii na mashahidi wawili waaminifu” kuwa: Kukanusha ni kwa njia ya ukamilifu na si kwa njia ya usahihi, na uwalii katika Hadithi hii unafasiriwa kwa upendeleo na si kwa uwajibikaji, na rai hii ndiyo inayotumiwa na sheria ya mambo ya kifamilia ya Misri.
Pamoja na kwamba inajuzu kwa mwanamke ajiozeshe yeye mwenyewe, isipokuwa inapendeza ampe jukumu jamaa yake yeyote atakayekuwa walii wa kufungisha ndoa yake, kama haiwezekani anaweza kumpa jukumu yeyote amtakaye miongoni mwa waislamu, na huu ndio ni uwalii kwa niaba.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas