Kula Nyama Isiyochinjwa kwa njia ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kula Nyama Isiyochinjwa kwa njia ya Kisheria.

Question

 Mimi ni mwislamu na ninaishi nchini Uitaliano, Je, Naweza kula nyama za wanyama ambao hawakuchinjwa kwa njia ya Kisheria?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kwa kuwa mnyama hajachinjwa kwa njia ya kisheria kama ilivyopokelewa katika swali, basi si halali kuila nyama yake; kwani hakiwi halali chochote katika wanyama wanaoliwa, bila ya kuchinjwa kisheria; kwa tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja} [AL MAIDAH 3].
Basi tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {ila mkimdiriki kumchinja}; Kujitenga na uharamu na wala sio na vilivyoharamishwa, ina maana mmeharamishiwa juu yenu yaliyopita isipokuwa mlivyovichinja kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu hivyo ni halali kwenu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas