Miamala ya Benki Katika Ardhi za Wa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Miamala ya Benki Katika Ardhi za Wapalestina Ziliyotekwa.

Question

 Sisi ni wa Palestina, Je inajuzu kuamiliana na benki za Israili, ikiwa ni sharti la kisheria la kufanya kazi na kufungua akaunti ya benki?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Fatwa iliyotolewa kuhusu suala la kuamiliana na benki za maadui katika ardhi zilizotekwa ni kwamba inajuzu kisheria kuzitumia benki hizo kwa mujibu wa maoni ya wafuasi wa Imam Abu Hanifa wanaohalalisha kufunga mkataba batili na asiye Mwislamu katika nchi zilizo na ukafiri, na ardhi zilizotekwa na maadui wa Kizayuni zinasifika kwa sifa hiyo kwa mujibu wa mwelekeo wa Abu Yusuf na Muhammad bin Al-Hassan (Mwenyezi Mungu Awarehermu) unaosema: Nchi za Kiislamu zinaweza kugeuka kuwa ni nchi za ukafiri zikitawaliwa kwa hukumu za kikafiri kitabu cha: [Bada’i Al-Sanai 7/130. Chapa ya Dar Al-Kotub Al-Elmiya].
Dalili za wafuasi wa madhehebu ya Abu Hanifa ni:
1) Iliyopokelewa na Mak-Hul kutoka kwa Mtume S.A.W. anasema kwamba: “Hakuna riba katika kuamiliana baina ya Mwislamu na mtu wa vita katika nyumba ya vita”.
2) Na iliyopokelewa na Ibrahim Al-Nakhi’y akisema: “Hakuna ubaya wowote kwa Waislamu kuamiliana na watu wa vita kwa msingi wa dinari moja kuuzwa kwa dinari mbili katika nyumba ya vita”, na kwa maana hiyo, hiyo ni Hadithi ya Abu Sufian Al-Thauriy. [Al-Tahawiy, Mushkel Al Athaar, 4/245 na I’laa Al Sunan, 13/6257: sanadi yake ni sahihi].
3) Iliyopokelewa na Ibn Abass R.A. kwamba Yazid bin Kinana alishindana na Mtume S.A.W. mara tatu na kila mara mashindano yalikuwa kwa mbuzi na kondoo mia moja naye Mtume S.A.W. alikuwa anamshinda na kumuangusha mgongo wake ardhini, basi katika mara ya tatu huyo Yazid akamwambia Mtume S.A.W.: Ewe Muhammad! Hakuna aliyewahi kuniangusha kwa mgongo wangu ardhini kabla yako na wala sijamchukia mtu zaidi yako lakini nashuhudia kwamba hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake na kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi Mtume S.A.W. akasimama akamwacha na kumrudishia mbuzi na kondoo wake [Al-Sarkhasiy, Al-Mabsout, 14/59].
Kutokana na hilo tunapata dalili kwamba kama lingekuwa limekatazwa, asingelifanya Mtume S.A.W.
4) Hakika mali za watu wa vita ni halali bila ya kuwepo mkataba, basi inakuwaje ukiwepo mkataba huo! Hakuna ubaya wowote bali ni bora zaidi kwa sharti la kutokuwa na hiyana na mali zao zichukuliwe kwa ridhaa ya nafsi.
5) Wafuasi wa madhehebu ya Abu Hanifa walitumia Qiyasi ili kupata dalili juu ya ruhusa ya kuuza watu wa vita, watoto wao na Waislamu kuwanunua katika nyumba ya vita au ya amana ambapo walipata dalili kutokana na kitendo cha Amru bin Al A’as. Na kutoka kwa Abdullah bin Habira Al Sabaiy anasema: Amru bin Al A’as alikubaliana na watu wa Intables - mojawapo ya miji ya Burka iliyoko baina ya Afrika na Misri - juu ya kulipa Kodi au kutoa watoto wao - kuwauza - wakitaka kufanya hivyo badala ya kulipa Kodi. [Bada’i Al-Sanai’, 5/192 pamoja na maelezo ya Ibn Abdiin 5/426].
Ufahamu wa dalili unabainisha kwamba: Kuuza mtoto au kitu kingine miongoni mwa mikataba batili ni sawa katika hukumu (haramu kishera) kama inavyojulikana, na kuruhusu hukumu mojawapo katika nyumba ya vita kunaruhu pia hukumu nyingine.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas