Hukumu ya Spiriti katika manukato n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Spiriti katika manukato na vipodozi.

Question

 Assalaamu alaykum. Je, mfuasi wa madhehebu ya Imamu Shafi anaweza kuvitumia vipodozi kama manukato, losheni na shampuu vilivyo na Spiriti ndani yake?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hukumu Iliyo sahihi na inayotakiwa katika misingi ya Madhehebu ya Imamu Shafi – pia na ya Madhehebu mengine – Ni kwamba Spiriti asili yake sio najisi, na inajuzu kuitumia katika manukato na katika mambo ya usafi, madawa, na vitu vinginevyo katika matumizi nufaishi, na mtu anaposali akiwa ametumia manukato, Sala yake ni sahihi, kwa sababu zifuatazo:
1- Ilivyo katika sheria ni kwamba asili katika vitu ni twahara, na japokuwa kunywa Spiriti ni haramu lakini jambo hilo halilazimishi kuwa kitu kilicho haramu kuwa ni najisi; kwani najisi ni hukumu ya kisheria na inapaswa kuwa na hoja maalumu. Mihadarati na sumu zinazo ua ni haramu ingawa ni twahara; kwani hakuna dalili za unajisi wake, kwa hivyo ilivyo katika misingi ya kifiqhi ni kwamba: Najisi inalazimisha uharamu, na uharamu haulazimishi unajisi; kwa hivyo basi kila kitu najisi ni haramu, na sio kinyume chake.
2- Madhehebu ya Shafi yamelifanya tamko la Pombe "Alkhamr" kwa ujumla ni kila kinacholewesha na kinatokana na Kinywaji cha zabibu, na wameweka masharti, ili kinywaji hicho kiwa najisi ni lazima kiwe na ladha kali inayopoteza akili, na Madhehebu ya Hanafi yameweka sharti la kuondosha povu, kisha wafuasi wa Shafi wameongeza yaliyo katika maana hiyo kutokana na vinavyolewesha ni kinywaji cha zabibu na pia kikiwa na ladha kali inayopoteza akili, na waliifanya hukumu yake kuwa kama pombe iliyotengenezwa kwa zabibu yaani ni haramu na najisi, lakini wafuasi wa Hanafi wanaona kwamba vinavyolewesha na havitokani na zabibu si najisi hata vikiwa ni haramu kwa upande ya kunywa. Basi kutokana na maelezo hayo Spiriti katika asili yake yenyewe si pombe mpaka iwe ni najisi, yaani najisi katika asili yake yenyewe, na hii si katika vinywaji vinavyolewesha na si kama pombe ambayo wamehitalifiana wanachuoni katika unajisi wake au utwahara wake, bali hii ni mada ya sumu kama sumu zingine zote, na kwa hali ilivyo si kinywaji katika hali ya kawaida kwa kusudio la kulewa, na ilivyo ni kuwa Spiriti imeharamishwa kwa matumizi kama ni sumu kwani sumu husabibisha mauti na madhara, na Spiriti asili yake ni twahara kama utwahara wa Hashishi na Afiyuni na kila kinachodhuru.
3- Spiriti si kinywaji na hainyweki, na kuwa kwake ni kimiminika hailazimishi kuwa ni najisi, na iliyozingatiwa katika Madhehebu ya Shafi kwamba kila kinywaji chenye kilevi ni najisi, makusudio ni kila kinywaji cha ulevi: Kilichokuwa na ladha kali inayopoteza akili na hawasemi kila kilicho majimaji: Wanaashiria kwamba kama inakuwa majimaji ya ulevi tu haitoshi kusema ni najisi, bali ni lazima kiwe kinywaji; ili kunywa si kuwa ni katika hali ya majimaji tu, na hayo yamefahamika kutokana na kauli yao kuwa kukamua kwa maana kuyafanya matunda kwa mfano yawe kama kinywaji, na kauli yao (divai) na haya ni maji yaliyowekwa ndani yake yanayokuwa kama kinywaji chenye kilevi.
4- Asili ya kilevi ni haramu katika matini ya kisheria na ni kile kilichojulikana kuwa ni kinywaji, na ama ambacho hakinyweki, kama vile ilivyo Spiriti basi matini hiyo haihusishi mpaka iwepo dalili ya wazi, na hasa kwa kuwa Spiriti haikuwepo wakati wa utungaji wa sheria, lakini inaharamika kuitumia kutokana na madhara yake.
5- Najisi ni hukumu ya kisheria na sio hakika ya kikemikali, maana yake ni kwamba pombe ni najisi na hii najisi ni hukumu ya kisheria, na Spiriti ni sehemu inayosababisha kilevi katika pombe na huu ni uhakika wa kipimo cha kemikali, na si lazima kwa uhakika huu na kwa upweke kuwa ni najisi au haramu inapokuwa peke yake katika umajimaji mwingine usio kuwa pombe; kwani najisi ya mchanganyiko hailazimishwi kwa unajisi wa elementi zake; hakika najisi walizoafikiana watu kuwa ni najisi; ni kama mkojo wa binadamu na kinyesi chake kilichochanganyikana na elimenti za kemikali zinazowezekana kuwa katika vitu vya twahara bali katika chakula na kinywaji; lakini unajisi unakuja kutokana na mchanganiko mahsusi kwa kiasi mahsusi. Na uchachu utakuja inapokuwa maada ya kisukari katika kitu cha asili, na bila ya hayo haiwezekani kutengenezeka uchachu hata ikibakia kwa muda mrefu kama Handhali, na uchachu ni kubadilika kwa mada ya kisukari kwa kuwa Spiriti na asidi ya kaboni na kinywaji itakuwa yenye uchachu na kwa hivyo itakuwa ulevi kwa sababu ya Spiriti hiyo, na Spiriti kwa peke yake hailevi, lakini inadhuru; na inaponywewa kwa upweke, aliyeikunywa atapata kulala fofofo au itapotea akili yake, na inapotaka kubadilishwa ili kufanya ulevi lazime ichanganywe na maji kwa kiasi cha mara tatu zaidi ya kiasi cha Spiriti, kisha itabadilika na itakuwa ulevi; basi kuchanganya na maji itaingia katika sifa ya kilevi, na msingi wa kutofautiana kwa mada zilizofanya kilevi ni kutofautiana kwa kiasi cha sukari iliyopatwa kutoka kiasi cha maji na Spiriti wakati wa kuchanganyika kwa ziada au kasoro, kinywaji cha mtende kilichokuwa na kiasi cha asilimia 40 kutokana na Spiriti na zaidi, na pombe zingine zilikuwa na asilimia10 na Boza ya shairi ilikuwa na kiasi cha asilimia 5 na kadhalika, na Spiriti yenyewe ni mada yenye sumu na haiathiri kwa kutia katika kilevi ila kwa kuchanganyika na maji kwa kiasi maalum.
6- Al-Imam An-Nawawi katika kitabu cha "Al-Minhaj" ameeleza juu ya najisi kwa kauli yake kuwa " Ni kila kinacholevya na kinakuwa na sifa ya majimaji" baadhi ya wafuasi wa Shafi walipinga juu ya kauli yake ya
An-Nawawy kwa kuwa na sifa ya majimaji kwani kuna baadhi ya vinywaji vyenye sifa ya kulevya na majimaji lakini si najisi kama vile Hashishi iliyokuwa kama majimaji, na waliohojiwa kuhusu kauli ya An-Nawawi walifasiri kauli yake ni kuwa na ladha kali inayopoteza akili, na wapinzani na walioafikiana naye wanakubali kuwa sio kila majimaji ya kulevye ni najisi na sharti ya najisi ya majimaji ni kuwa na ladha kali inayopoteza akili. Lakini An-Nawawi katika mlango wa vinywaji katika kitabu hicho" Al-Minhaj" Alieleza kwa kauli yake: " Kila kinywaji kinacholevya kwa wingi wake basi uchache wake ni haramu na aliyekinywa lazima apate adhabu".
7- Kilichothibitika ni kwamba kitu kinachobadilika katika asili na sifa yake na kuwa kitu kingine hukumu yake itabadilika kufuatana na mabadiliko hayo, na najisi kwa mfano haibaki kuwa najisi inapotupwa katika maji mengi sana na rangi yake ikawa haikubadilisha rangi, ladha, au harufu ya maji hayo. na Spiriti inapochanganyika na manukato au dawa au vitu vya usafi, sifa yake ya pombe huondoka. Na mfano huu ni kama pombe iliyobadilika yenyewe na ikawa siki basi siki hilo huwa linakuwa ni twahara katika sheria hata kama wanasayansi wa kikemia wakikuta baadhi ya Spiriti ndani yake, na hayo ni makubaliano ya wanachuoni.
8- Na wafuasi wa Shafi wanaieleza najisi kama ni: Kitu kichafu kinachozuia usahihi wa Swala hali ya kuwa kitu hicho si chenye kuruhusiwa, na Spiriti si kitu kichafu kiasili, bali hutumika kwa shughuli za tiba kama maada ya kusafishia, na huondosha visivyo ondoshwa kwa maji pamoja na sabuni kutokana na uchafu na najisi, na pia inaingia katika kutengeneza baadhi ya manukato na michanganyiko ya dawa, kwani Spiriti ni mada iliyoandaliwa kwa ajili ya kusafishia na kwa ajili ya manukato, na kudai kwamba manukato na harufu yake vinatokana na najisi, ni jambo lenye tofuati na hisia na tabia, na manukato na uturi hayaitwi pombe katika istilahi ya kilugha au katika mila na desturi za jamii au hata katika utumiaji, na utumiaji wake wa kimakosa kwamba hutumika kwa kula na kunywa hakuondoi maana ya kuwa kwake manukato au uturi.
Na Imam Al-Izz Ibn Abdul-Salam Al-shafi katika kitabu chake "Kawa'd Al-Ahkam Fi Masalih Al-Anaam" (Misingi ya hukumu za Manufaa ya Ulimwengu wote) amesema: "Asili ya twahara huambatana na sifa za manukato, na asili ya unajisi huambatana na sifa za uchafu. Kwa hivyo kama kinywaji kingekuwa pombe basi ingekuwa najisi kwa sababu ya kuwa kwake uchafu katika Sheria, na pia kama ingegeuka na kuwa siki basi ingekuwa twahara kwa sababu ya utwahara wa kisheria na kihisia, na pia maziwa ya wanyama wanaoliwa yanapobadilishwa sifa zake kwa kuchanganywa katika manukato yaliyokuwa twahara na pia makohozi, mate, machozi na jasho, na pia mnyama aliyetokana na najisi, na pia matunda yaliyomwagiliwa maji yaliyo najisika ni twahara, na ni halali kutokana na ubadilikaji wake wa sifa za utwahara, na pia mayai ya mnyama anayeliwa na miski. Na maulama wamehitalifiana katika majivu ya najisi; waliuosema utwahara wake walitoa dalili ya ubadilikaji wa sifa zake za kiuchafu na kuwa katika sifa za kimanukato, na kama najisi zinatwaharika kwa ubadilikaji wa sifa zake pia vitu vingine vinavyopata najisi vinatwaharika kwa kuondoka najisi, na ngozi inapowambwa ni lazima kuondosha takataka zake na kubadilisha sifa yake. Na kwa hivyo basi baadhi ya wanazuoni waliitaja rai ya kubadilika tu, na baadhi yao wakaitaja rai ya kutobadilika, na wapo waliozitaja rai zote mbili".
Na Imam Al-Karafi anasema katika kitabu cha: [Az-Zakhira 1/188]:"Kanuni inabainisha yaliyotangulia, kamba Mwenyezi Mungu alipohukumu juu ya unajisi wa miili maalumu, kwa sharti ya kuwa na sifa hasa hasa za uchafu, basi kama hakuna sifa hizo miili yote ni sawa, na hitilafu zake ni kwa sifa za uchafu zilizoletwa, na zinapoondoshwa sifa hizi kwa sura kamili, hukumu ya unajisi wake huisha kwa makubaliano ya wanachuoni.
Kama damu inavyobadilika kuwa manii na baadaye kuwa mwanadamu, na sifa hizo zinazobadilika zinapokuwa katika kitu kichafu zaidi ya kitu cha awali hukumu ya uchafu huthibitisha, kama damu itakuwa usaha, au damu ya hedhi, au damu ya kilichokufa. Na inapobadilika kuwa sifa zinazobadilika kwa tabia ya uchafu lakini ni chache sana kuliko ya mwanzo. Je inasemwa kwamba sura hii ina kasoro kwa amujibu wa makubaliano ya wanachuoni, na kwa hivyo basi hukumu ya asili pia huwa ni dhaifu, au huzingatiwa kuwa asili ya hoja sio ukamilifu wake, na kwa hivyo hukumu yake ikalingana na hukumu ya Ijmaa (Makubaliano ya wanazuoni wote?)
Hapa ni pahala pa kuwaangalia Wanazuoni kwa maelezo yaliyotangulia; kwa hivyo maulama wanatofautisha kati ya ubadilikaji wa pombe na kuwa siki, na hukumu yake ni utwahara, na ubadilikaji wa mifupa iliyokuwa najisi na ikawa jivu kwa sababu ya kuwa na baadhi ya uchafu na kutotumika, kinyume cha hali ya kwanza"
Na kauli ya kwamba Spiriti si najisi na si pombe ni hukumu ya fatwa iliyotolewa na Shekhe, mwanachuoni mkubwa Bukhit Al-Moti'I katika gazeti la Al-Irshad, toleo la kwanza, mwaka wa kwanza, mwezi Shaabani, 1351 H, na fatwa hii iliafikiana na ya Dar Al-Iftaa nchini Misri; na ilitolewa fatwa hiyo katika enzi za Shekhe Mohammad Khatir tarehe 27 mwezi wa Dhul-Kaadah, mwaka wa 1391H, sawa na 13 januari mwaka 1972. Na Shekhe Mohammad Rashid Ridha Alishikamana na rai hii katika "Tafsir Al-Manar", na pia ni kauli ya Wengi wa wanazuoni wa kisasa na baadhi ya Mabaraza ya kitaalamu yaliyothibitishwa kama vile katika kundi la fatwa za kisheria zilizotolewa na Kitengo cha fatwa katika Wizara ya Mambo ya Waqfu nchini Kuwait, na kwa hivyo Spiriti sio pombe, na wala sio katika madhehebu ya Shafi au madhehebu nyingine, na ni halali kuitumia spiriti katika manukato, uturi, mambo ya usafi, na madawa, na hakuna shaka kwa hilo katika Sheria.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas