Hukumu ya kurefusha Nywele za Kichwani kwa Wanaume.
Question
Nimewaona Waislamu wengi wana nywele ndefu sana kichwani. Je, hali hiyo ina hukumu gani katika Sheria?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kuwa na nywele na kuzirefusha, asili yake ni Halali kwa wanaume; kwani hii ni kutokana na mazoea pamoja na maumbile, na imepokelewa na Abu-Dawud katika kitabu chake cha “Sunan” kutoka kwa Abu-Huraira kwamba Mtume S.A.W anasema: “Mtu yeyote mwenye nywele kichwani, na azitunze”, na kutoka kwa Anas R.A : “Nywele za Mtume S.A.W zilikuwa zikifika hadi mabegani mwake” (Bukhari).
Lakini pamoja na hayo, mazoea na hali zinazoambatana na kitendo hiki cha kufuga nywele ndefu zinaweza kubadilika, na hukumu yake pia ikageuka na kubadilika kutoka katika uhalali na kuwa inachukiza au haramu, kama kitendo cha kurefusha nywele kitakuwa ni alama ya uchafu, ukhanithi au ushoga katika wakati au pahala maalumu, bali kitu kikiwa kimependwa kiasili kisha kikawa ni alama ya wenye maovu, basi itakataliwa kukigusa, na kwa hivyo Maulamaa walisema kwamba wenye maovu wakiwa na mavazi maalumu, basi haijuzu kwa wengine kuyavaa, kwa jinsi ilivyotajwa katika Hadithi tukufu kutoka kwa Ibn Umar alisema: Mtume S.A.W alisema: “Anayejifananisha na watu, basi yeye atakuwa ni miongoni mwao" (imepokelewa na Abu-Dawoud).
Na pia Mtu mwenye kujifananisha na wenye maovu basi anajisababishia tuhuma au dhana mbaya dhidi yake. Sheikh Aly Alkary alisema katika kitabu chake "Mirkatul Mafatih katika maelezo ya Mishkatul Masabih" [7/2782, chapa ya Dar Al Fikr]: "Aliyejifananisha na makafiri yeye mwenyewe kwa mfano katika mavazi na mambo mengineyo, au na wenye maovu au wakosevu au watu wasufi au watendao mema, (basi yeye ni miongoni mwao): “Kwa thawabu na adhabu. na Al-Hafidh Al-Manawy alisema katika kitabu chake Faydhu-Al-Kadeer [6/104, chapa ya Al-Maktaba Al-Tijaria Al-Kubra]: “Haijuzi hivi sasa kuvaa kilemba cha rangi ya buluu au njano - kwa maana: Katika zama zake alizokuwa na wala sio kwa sasa - kadhalika alitaja Ibn Raslan na kwa maneno yaliyo wazi zaidi Alkurtuby alisema: Watu wa ufuska na uchafu wanapohusiana na mavazi maalumu, basi mavazi hayo hukatazwa kuvaliwa na wingene; kwani wale wasiowajua wanaweza kudhani kwamba wao ni pamoja na wale wenye ufuska wakapata dhambi wote waliodhani na waliodhaniwa”.
Na kuhusu suala la kurefusha nywele za kichwani kwa mwanamume linapokuwa katika kujifananisha na wajinga, basi anasema Al-Hafidh Al-Faqih Ibn Abdel-Bar katika kitabu cha Al-Tamhid [6/80-chapa ya Wizara ya Fedha, Wakfu na Mambo ya Kiislamu nchini Moroko]: “Watu wa siku hizi wamekuwa hawakati nywele zao isipokuwa askari wetu, watu hao wamefanya nywele zao vishungi na kisogoni mwao wamezifunga, watu wema na wanachuoni wamepinga ada hiyo na ikawa kuwa na vishungi ni sifa na alama za wajinga na ilipokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W kwamba yeye alisema: “ aliyejifananisha na watu basi yeye yupo pamoja nao katika siku ya kufufuliwa.
Na imesimuliwa kwamba aliyejifananisha nao kwa vitendo vyao, na ilisimuliwa kwamba aliyejifananisha nao kwa sura zao, na hayo yote yanatosha, kwani hii ni kutokana na kufuata watu wema na katika hali yeyote wao walikuwa wakirefusha nywele na kukata nywele hakumnufaishi mtu Siku ya Mwisho lakini hesabu yake itakuwa juu ya nia na vitendo, labda mtu aliyekata nywele ni bora zaidi kuliko aliyeirefusha na labda pia mwenye nywele ndefu ni mtu mwema kwa mfano kuvaa pete mkono wa kulia kulikuwa halali na baadhi ya Wanazuoni wa Salafi walivaa pete mkono wa kulia na pia baadhi yao walivaa pete mkono wa kushoto lakini baada ya Raafidhwa (wapingaji) walivaa pete mkononi wa kulia na hawakuivaa pete isipokuwa mkono huu wa kulia, na ada hii ilikuwa na uhusiano na mazingira yao, na kwa hivyo basi Wanazuoni walisema kuwapo chukizo katika kuvaa pete mkono wa kulia, kwani kufanya hivyo ni kujifananisha na wengine na inachukiza kufanya hivyo, lakini sio Haramu kuivaa pete katika mkono huu wa kushoto bali inachukiza tu.
Na Madhehebu ya wafuasi wa Imam Hanbali ni kuwa kurefusha nywele ni Sunna na mtu anaweza kusuka nywele na pamoja na hayo Alama Ibn Moflih alitaja kwamba ni wajibu kuainisha hukumu isiyosababisha kasoro ya murua (mwonekano uliozoeleka), au kumpuuza mwenye kuifanya sunna hiyo kwa kwenda kwake kinyume na desturi ya jamii anayoishi mtu huyo, na alisema katika kitabu cha: [Al-Adabul Al-Shariya 3/329, chapa ya Alam Al Kotub]: “Mlango wa (yanayopendekezwa katika kurefusha nywele na kuchana kwake pamoja na kusuka kwake na kufuga ndevu). Inapendekezwa kuosha nywele zake na kuzichana na kuzisuka na kuzifikisha hadi mabegani mwake, au chini ya masikio yake au mwanzo wa masikio yake, na inapaswa kusema kwamba: ikiwa haisababishi uvumi au kasoro katika mwonekano wake uliozoeleka au kumpuuza mwenye kuifanya ada hii na kadhalika kama walivyosema wanazuoni katika mavazi”. na baadhi ya wafuasi wa Imamu Hanbali waliyataja hayo kwa kuainisha hukumu ya kufuga ndevu kama ilivyonukuliwa na Al-Mirdawy katika kitabu cha: [Al-Insaf 1/122, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby] alisema kwamba:“na mwanaume hufuga ndevu zake. Na Ibn Aj-Juzi katika kitabu cha Al-Madhehab alisema: “mtu hufuga ndevu zake ikiwa urefu wake haushangazi.
Na baadhi ya riwaya zilitajwa kuhusu suala hili kutoka kwa (Salaf) wema waliotangulia, na miongoni mwa riwaya hizo ni ile iliyosimuliwa na Ibn Abyl-Dunia katika kitabu cha: [Al-Tawadhuu na Al-Khumoul, uk.86, chapa ya Dar Al kutub Al-Elmiya]: “Alitusimulia Muhammad bin Salam Al-Jumahy, kutoka kwa Adiy bin Al-Fadl alisema: Ayoub Aliniambia: chukua viatu kama vile viatu vya Mtume S.A.W na nikafanya hivyo na alivivaa baadhi ya siku kisha akaviacha, akasema nilivivaa kwa muda wa siku kadhaa kisha nikaviacha na nikamwambia: sijawaona watu wanavaa viatu kama vile” (Hadithi hii ilipokelewa na Ibn Shaiba katika kitabu cha: [Al-Mosanaf 6/81, chapa ya Dar Al-Fikr]: kutoka kwa Al-Hasiyn alisema kwamba Zubayd Al-Yamany alikuwa akivaa burnoose (vazi refu linalofunika mwili mzima hadi kichwa na aghalabu huwa linatumika baada ya kuoga), alisema: basi akasikia Ibrahim akimlalamikia kuhusu kanzu hiyo, alisema: basi nikamwambia: watu hawavai nguo kama hiyo siku hizi, akasema: ndiyo, lakini watoweka watu waliokuwa wakiivaa, basi mtu yeyote akiivaa kwa sasa hivi atasababisha uvumi na watu watamuashiria kwa vidole".
Kwa hiyo, mambo ya sura na mavazi yanategemea mila na desturi, na yanatawaliwa na kanuni kuu: kama, wajibu wa kusitiri uchi, na uharamu wa kujifananisha na waovu na uovu, na uharamu wa wanaume kujifananisha na wanawake, na wanawake kujifananisha na wanaume, na uharamu wa kiburi na kujikweza pamoja na ubadhirifu, kwa hivyo basi desturi za mila na kanuni kuu zinazoangaliwa hapa ikiwa suala la kurefusha nywele za kichwa kwa mwanamume halipingani na mila ya watu pamoja na kanuni kuu, basi hakuna ubaya wowote.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote