Mwanamke Mwislamu Kwenda kwa Daktar...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwanamke Mwislamu Kwenda kwa Daktari wa Magonjwa ya Wanawake

Question

Mwanamke Mwislamu anaishi katika nchi isiyo ya Kiislamu na anataka ushauri wa kimatibabu kutoka kwa daktari wa magonjwa ya wanawake, na nchi hiyo haina daktari hata mmoja wa kike wa kiiislamu aliyebobea katika uwanja huu, lakini kuna madaktari wa kike na wakiume ambao sio Waislamu bali ni miongoni mwa watu waliopewa Kitabu.
Je, ni inafaa kwenda kutibiwa na daktari wa kiume Mwislamu ama daktari wa kike hata kama atakuwa ni miongoni mwa waliopewa Kitabu?
 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kutibiwa kunazingatiwa ni miongoni mwa mambo yaliyohalalishwa; kwa Hadithi iliyosimuliwa na Abu-Dawood kutoka Abi-Al-Dardaa R.A. anasema: Mtume S.A.W. anasema “Mwenyezi Mungu Mtukufu ameshuka ugonjwa na dawa, na amejaalia kila ugonjwa kuwa na dawa yake, basi jitibuni), na Hadithi ya Tirmidhy kutoka Usama bin Shuraik R.A. anasema: “Mabedui walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Je, tusaidiane katika kujitibu? Mtume akasema: ndiyo, Enyi waja wa Mwenyezi Mungu saidianeni katika kujitibu, kwani Mwenyezi Mungu haleti ugonjwa ila huleta na dawa yake isipokuwa ugonjwa mmoja tu, wakauliza: Ni upi ugonjwa huo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni ukongwe)
Ibn Al-Qayim alisema katika kitabu cha: [Zad Al-Miaad 4/15, chapa ya Al-Risala]: “Katika Hadithi sahihi kuna amri ya kusaidiana katika kujitibu, na amri hii haipingani na imani ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, kama ambavyo pia haipingani na hali ya kuepusha njaa, kiu, joto na baridi kwa vinyume vyake”.
Na kwa kuwa kusaidiana kimatibabu halali, basi daktari ambaye ndio njia na chombo cha matibabu hayo ni halali vile vile, kwani ruhusa ya kitu ni ruhusa ya yaliyosaidia kupatikana kwa kitu hicho hicho. Lakini mgonjwa angekuwa mwanamke, na kwa kutibibiwa ni lazima kufichua uchi wake au kuugusa, basi wana Fiqhi wameafikiana juu ya kujuzu kwa daktari kuona uchi na kuugusa kwa lengo la matibabu, na kuona kunakuwa ni pahala pa ugonjwa tu kwa kiasi cha dharura; kwani dharura zinatangulizwa kwa kiasi chake, na hafichui mgonjwa ila pahala pa haja, pamoja na kufumba macho yake kadri awezavyo asiangalie pahala pengine, na ni bora kutafuta daktari wa kike hata kama angekuwa miongoni mwa waliopewa Kitabu kwa sharti awe mwaminifu na mjuzi katika kazi yake; kwani hali ya kuonana kwa watu wa jinsia moja ina madhara kidogo zaidi.
Na Ibn Hajar Al-Haytamy Al-Makki anasema katika kitabu cha Tuhfatul Muhtaj (7/202, chapa ya Dar Ihiyaa Al-Turath): “na Al-Balqiny anasema kwamba katika kusaidiana kujitibu anatangulizwa mwanamke Mwislamu, kisha mwanamke asiye Mwislamu, kisha mwanamume Mwislamu, halafu mwanamume asiye Mwislamu, na Al-Azra’i anaafikiana naye hasa katika kumtanguliza mwanamke kafiri juu ya mwanamume Mwislamu, kisha anasema: Atatangulia mwenye ujuzi zaidi juu ya wengine hata kama mtu huyo ni wa jinsia tofauti, au dini kuliko mwingine”.
Kutokana na hayo, na kuhusu swali hilo: Ni bora zaidi kwa mwanamke huyu aanze kutibiwa na daktari wa kike hata akiwa si Mwislamu, akiwa mwaminifu katika kazi yake, basi katika hali ya kushindikana anatangulia daktari wa kiume Mwislamu akiwa ndiye mjuzi zaidi kuliko wa kike.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas