Kutazama Filamu za Ngono kwa Wanandoa.
Question
Mimi nimeolewa tangu miaka kumi na mbili iliyopita na mume wangu ananiomba tutazame pamoja filamu za ngono au atizame pekee yake, kiasi ambacho humpelekea mwishoni kupiga punyeto, na hali hii imesababisha matatizo mengi katika maisha yetu. Na kila mara anakariri kuwa hayupo radhi na mimi, na kwamba mimi siyo kama wanawake wengine, katika baadhi ya nyakati mimi huwa ninadhani kwamba mimi ni sababu ya kupiga kwake punyeto. Nanajisemea moyoni kwamba kama nikikubali kutazama aina hii ya filamu labda atakidhi haja yake pamoja nami kwa njia ya halali. Swali langu ni: Je ni lazima kumtii katika jambo hili au ni lazima niendelee na msimamo wangu wa kukataa kutazama filamu hizi pamoja naye? Ni muhimu kutajwa kuwa yeye anasali, anatoa sadaka nyingi, na pia alifanya Umrah. vile vile, ana tabia njema ingawa ana kasoro hii.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kutazama filamu za ngono ni haramu, na ni lazima kufanya kila unachoweza kwa ajili ya kumzuia kuzitazama hata kama utamdanganya kwamba utazitazama pamoja naye pamoja na kujitahidi kujipamba na kumtosheleza kwa njia zote za kimapenzi, na kimwili, ili asipige punyeto, na mpaka akidhi haja zake pamoja nawe.
Hali hii itakuwa kwa makusudio ya kufanya madhara yaliyo madogo zaidi kwa ajili ya kuondosha madhara yaliyo makubwa zaidi. Ni bora zaidi kama ukijitahidi kwa kutenda mema ili ahisi kuwa hahitaji kuzitazama filamu hizi, na kwamba halali ni nzuri zaidi kuliko haramu.
Kwa njia hii unaweza kumsaidia mume wako ili ajizuie kuzitazama filamu hizi hatua kwa hatua, badala ya kumwacha mateka wa Shetani ambaye anamchezea kama anavyopenda na kukidhi matamanio yake kupitia njia yake hiyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.