Biashara ya vito

Egypt's Dar Al-Ifta

Biashara ya vito

Question

Sisi Waislamu wa eneo la Sheng Yang lililoko Kaskazini Magharibi mwa Uchina, tumekuwa tukiishi katika mji mdogo, wenye hali duni ya kiuchumi, lakini Mwenyezi Mungu ameujaalia Utajiri wa asili wa madini ya vito. Kwa hiyo kuna wakazi wanoofanya biashara hii, na idadi ya wafanya biashara hao miongoni mwao kuna Waislamu wapatao elfu ishirini au zaidi, mbali na wafaidikaji na kazi hii, na twaweza kuwagawanya wote kwa ujumla katika sehemu tatu:
1- Wafanya kazi: Hawa ni wachimbaji wanaotafuta madini kama ni njia ya pili ya ujira wa wenye madini.
2- Mawakala: Hawa hununua madini yanayochimbwa ardhini, kisha huyauza kwa wafanya biashara.
3- Wafanya biashara: Hawa hununua madini kutoka kwa Mawakala, na pengine moja kwa moja kutoka migodini, na wanapopata kiasi kikubwa cha vito, huenda katika miji mingine ya mbali ya Uchina, wakaviuza kwa wasio waislamu miongoni mwa masonara na wanaochonga kiasi cha 70% maumbo ya kimwili kama vile: Masanamu na wanyama, na kiasi cha 30% maumbo mengine kama vile: Bangili na pete.
Kwa kujua bei za vito hivi zinagawanyika sehemu mbili:
1- Vito vya bei ghali, ni vichache sana, na sonara hatengenezi kitu, isipokuwa yeye huwa anavihifadhi kwa ajili ya kujivunia tu.
2- Vito vya bei nafuu, ni vingi sana, ambavyo sonara huwa anavitengeneza kwa maumbo mbali mbali, kama ilivyokwishatajwa.
Tunakuambieni kuwa: Wengi wa wahusika wa kazi hii ni miongoni mwa watawa ambao wanafanya kazi yao ya wema kwa bidii katika kuwasaidia mafakiri. Na wao pia wana imani sahihi.
Inatupasa kuashiria kuwa nguvu za uchumi wa Waislamu ziko mikononi mwa wahusika wa kazi hii, na Waislamu wasipoishughulikia ipasavyo, basi wasio waislamu wataitawala. Kwa hiyo uchumi wa Waislamu utaendelea kuwa dhaifu. Na matokeo yake ni Waislamu kufunga virago vyao na kuiachilia mbali kazi hizi za mema.
Swali:
Nini hukumu ya biasahara hii
? Na zaka huwa inatolewaje? Na ikiwa haramu, basi ni njia gani ya kuondosha mali zilizokwishachumwa? Tunaomba mtueleze jambo hili pamoja na kutupatia fatwa iliyo wazi pamoja na kutaja dalili. Na Mola atawalipa thawabu.
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ikiwa hali hii ndivyo ilivyo na swali lake: Basi hakuna kizuizi chochote cha kisheria katika biashara ya vito hivi, na haidhuru kwa masonara kutengeneza vito hivi kama masanamu na michoro mingine, kwa sababu vitu hivi kama yanavyowezekana kuchongwa masanamu, yanawezekana pia kuchongwa vitu vingine, basi uhalali na uharamu unahusiana na anayevitengeneza. Ama kuhusu mfanyabiashara, yeye hana dhambi yeyote katika hali kama hii. Pia hakuna zaka kwa vito hivyo.
Na namna ilivyoelezwa, jawabu la swali lililoulizwa limefahamika.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote

 

Share this:

Related Fatwas