Tofauti Kati ya Kujiambatanisha na ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tofauti Kati ya Kujiambatanisha na Kujinasibisha na Mtoto wa Zinaa kwa Mzinifu.

Question

Je inawezekana vipi kwa mwanamume kujiambatanisha na mtoto ikiwa hakuna dalili au uthibitisho wa uhusiano wake na mtoto huyo? Nimesikia kwamba Abu-Hanifa na Ash-Shafii walizuia mtu kujiambatanisha na mtoto asiyekuwa wa halali; kwani hazingatiwi kuwa ni mtoto wake wa kweli. Je, hayo ni sahihi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Maneno yako ni sahihi mno katika ubatili wa kunasibisha mtoto wa zinaa kwa mzinifu na haijuzu kwa Wanazuoni wote wa Kiislamu wote - sio Imamu Shafii na Abuu Hanifa peke yao, na haijuzu kwa uzinifu kuwa ndio sababu ya kujipatia mtoto, na tulitanabahisha kwamba kuna tofauti kati ya kunasibisha mtoto wa zinaa kwa aliyezalika kutokana na manii yake hali ya uzinzi na mwanaume kudai ubaba wake kwa mtoto, na hakuna hitilafu kati ya Maulama kuhusu Ubaba kama ni uhusiano wa kisheria sio kimaumbile na mwenye manii hatakuwa baba mpaka awe kwenye ndoa sahihi na halali; kwani manii ya uzinifu hubezwa; kwani Mtume S.A.W amesema: "Mtoto huyo ni halali kwa waliooana, na mwanmke mzinzi hana chake", isipokuwa Umama wenye uhusiano wa kimaumbile. Lakini swali lako juu ya aliyetaka kudai mtoto kuwa ni wake, na tulikujibu kwamba ni halali kutokana na kauli za baadhi ya Wanazuoni wa Fiqhi; kwa sharti la mwanamume kutotaja kwamba yeye anataka kujiambatanisha na mtoto kwa sababu ya uzinifu; na hii ni kwa lengo la kuilinda hatima ya watoto na jinsi wanavyoliangalia suala la kutopoteza nasaba, na uhusiano huu unazingatiwa ni kama ni mtu atamwingilia mwanamke huku akiwa na shaka shaka kama mwanamke huyo ni mkewe au la, hali ya kutokuwepo ndoa sahihi.
Na hayo yote ni kwa sharti la kuwa mwanamke huyo hakuwa na pingamizi yeyote dhidi ya madai ya ubaba, na akawa hajaolewa wakati wa ujauzito na mwenye kudai ubini wa mtoto –kwani mtoto huyo atanasibishwa kwa mwenye ndoa kwa Ijmai/ itifaki- na mwenye kujiambatanisha na mtoto akidai kwamba mtoto aliyedaiwa alikuja kutokana na uzinifu, kwani kama atadai kuwa yeye ndiye aliyezini na anataka kuufanya uzinifu kuwa sababu kwa kujiambatanisha na mtoto basi hayakubaliki madai hayo ubaba huo bila ya shaka au hitilafu, na kama anataka kujiambatanisha na mtoto na bila ya kusema kwamba sababu yake ni uzinifu basi hiyo inazingatiwa kama ni mtu aliyemwingilia mwanamke huku akiwa na shaka shaka kama mwanamke huyo ni mkewe au la, hali ya kuwa hakuna ndoa sahihi, kwani sheria haimwangalii mtu asiyeeneza munkari anapokuwa katika hali ya kujisitiri yeye mwenyewe na hatafuatiliwa nyuma yake na wala hataadhibiwa adhabu ya Hadi (maalum kwa mzinifu) bali ataamrishwa kufanya toba ya kweli kati yake na Mwenyezi Mungu, na hii ni kutokana na masuala ya kifiqhi yaliyo madhubuti, ambayo yako katika kanuni ya kutenganisha hukumu; na yanahitaji kufafanuliwa na kuyaweka wazi zaidi, na sisi tumekufupishia kwanza na kisha ulipobabaika tukayaeleza kwa umakini Zaidi na kwa kiasi tulichoweza.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas