Hukumu ya Kupiga Makofi kwa Ajili y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kupiga Makofi kwa Ajili ya Kufurahi

Question

Barani Ulaya, upigaji makofi una maana ya kukubali na kuridhika, kama ilivyo popote pale ulimwengu. Lakini baadhi ya watu waliichukua Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari isemayo: “Kumsabihi Mwenyezi Mungu ni kwa wanaume, na kupiga makofi ni kwa wanawake”, kama dalili ya uharamu wa kupiga makofi, ambapo Hadithi hii inahusiana na jinsi ya kujibu mtu unapokuwa unaswali. Ni yepi Maoni ya Wanazuoni wa madhehebu manne (hasa Imam Shafi) kuhusu jambo hili? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hadithi hii Tukufu imepokelewa ikiwa inamuhusu Mwislamu anayekuwa katika Swala, na kwamba haifai kufahamika kwa Hadithi hii kwa kukusudia hali yeyote nyingine. Wanavyuoni wa Fiqhi walipoizungumzia hukumu ya kupiga makofi nje ya Swala, walizungumza hivyo kwa kuzingatia sababu yake na hali inayoambatana nayo katika mazingira yanayomuepusha Mwislamu na mambo yanayokiuka adabu; kama vile wale wanaofanya hivyo kwa ajili ya kuwasumbua watu misikitini, au wale wanaofanya hivyo kama ibada wakiepuka unyenyekevu, na wana kuwa katika hukumu hiyo kati ya uharamu, chuki na uhalali; kufuatana na yaliyotokana na usumbufu huo. Wanasema pia kwamba hali hii kama ikiwa kwa ajili ya manufaa basi ni halali.
Ibn Hajar Al-Haitami Ash-Shafiy alitaja kuwa baadhi ya Wanavyuoni walichukua Hadithi hii kama dalili ya uharamu wa kufanya hivyo. Kisha walijibiwa kuwa Hadithi hii inahusiana na Sala, na kwamba kupiga makofi huko siyo kwa wanawake katika hali yeyote, na kwa hivyo basi hakuna kufanana nayo. Ibn Hajar Al-Haitami Ash-Shafi alisema katika kitabu chake “Kaf Ar-Riaa” kilichochapishwa sambamba na kitabu cha: [Az-Zawajir, 2/296, Al-Halabi] kuwa: “Baadhi ya Wanavyuoni waliharimisha kupiga makofi kwa mujibu wa Hadithi isemayo: (Kupiga makofi ni kwa wanawake), ingawa inafahamika kuwa Hadithi hii inahusiana na Sala, na kwamba hairuhusiwi kuwaiga wanawake, na hali hii siyo kama ile a mwanzo”.
Ama kuhusu aya isemayo: {Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga miruzi na makofi.} [AL-ANFAAL: 35] aya hii ni dalili isiyo sahihi, kwa sababu aya hii imeteremshwa kwa Wale ambao walikuwa wakizuia Njia ya Mwenyezi Mungu kwa kitendo chao hicho. Kwa hivyo, kukana hapa ni kwa ajili ya kuizuia Njia ya Mwenyezi Mungu, na kwamba wao walikuwa wanafanya hivyo kwenye Al-Kaaba, siyo kwa ajili ya kupiga miruzi na makofi tu.
Al-Hafidh Al-Iraqi alisema katika kitabu chake kinachoitwa [Tarhul Tathriib, 2/244, Daru Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiah] kuwa: “Baba yangu Mwenyezi Mungu amrehemu alisema kuwa: Katika aya hii isemayo: {Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga miunzi na makofi.} hakuna sababu ya kuzuia wanawake kufanya hivyo katika Sala au katika hali nyingine yeyote. Lakini zaidi ya mmoja wa Wanavyuoni wa tafsiri wamesema kwamba makafiri walikuwa wakimfanyia fujo Mtume S.A.W, kwa kitendo hicho alipokuwa katika Sala na katika kutufu ili kumsumbua, kwa hivyo aya hii imeteremshiwa Makkah. Kisha Mtume S.A.W, aliwaamuru Wanawake wapige makofi ili kuyaelezea yaliyowapata. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi”.
Wanavyuoni wa Kamati ya insaiklopidia ya Fiqhi nchini Kuwait walisema kuhusu suala hili kuwa: “Inafahamika kuwa kuna matatizo katika maoni haya, kwani maana ya kwamba suala la kupiga makofi ni miongoni mwa mambo ya pambo lisilo na Kazi, maana yake ni kwamba hakuna thawabu ndani yake. Na siyo kila kisicho na thawabu ni haramu. Na kwani kuiga ibada ya watu wa Jahiliya hapa hakupo. Dharau hali ya kupiga makofi ni kwa sababu kwenye hii Nyumba (Al-Kaaba) na kwani waliitumia hali hii katika Sala zao. Na kuiga Wanawake katika hali ya kupiga makofi hutumika kama mwanamume mmoja akipiga makofi katika Sala yake kwa ajili ya kusahau kwa Imam badala ya Kumsabbih Mwenyezi Mungu hali ambayo ameruhusiwa” Wanavyuoni wa Kamati walisema hivyo.
Rai iliyochaguliwa katika Madhehebu ya Imam Ash-Shafi ni kwamba kama hali ya kupiga makofi haimuepushi Mwislamu na adabu za kijamii, basi ni halali na siyo haramu hata ikiwa ni kwa kucheza, nayo ni halali ikielezea furaha.
Ibn Hajar Al-Haitami alisema katika kitabu chake “Sharhul Irshaad” kama alivyotaja katika kitabu cha “Kaf Ar-Riaa” kwamba yeye mwenyewe alisema: “Kutokana na hayo, inaruhusiwa kupiga makofi kwa nia ya kucheza, hata kama ikiwa ni aina ya tarabu. Kisha Al-Mawardi, Asha-Shi, na wenye kitabu cha (Al-Istisqaa) na (Al-Kafi) walisema hivyo hivyo, na huwenda wanavyoni wakawa wanatofautiana kuhusu suala hili, na rai niliyoichagua ni uhalali wake”. Na kila jambo linalohitaji kupigwa makofi, linafuta hukumu hiyo; kama alivyosema Asha-Bramlsi katika kitabu chake: [Nihaiatul Muhtaaj, 2/47, Mostafa Al-Halabi]. Kwa hivyo kuna watu wanaopiga makofi kwa ajili ya kufurahia sana maalum; kama vile kuimba n.k. Vile vile kuna wanawake wanaopiga makofi kwa ajili ya kuwachezea watoto wao.
Ikiwa mila na desturi zinauzingatia upigaji makofi kuwa ni kielezi cha furaha na kuthamini jambo, basi maneno ya Wanavyuoni hayahusiki na hali hii, na haifai kutoa hukumu ya kuzuia kupiga makofi au kuharimisha kama ilivyoenezwa baina ya watu siku hizi, wawe Waislamu watu hao au si Waislamu, kwa hivyo haifai kuharamisha jambo hili lililogeuzwa maana yake, kwani Wanavyuoni walikubaliana kwamba kama mila na desturi zimegeuzwa, basi hukumu zinazohusika nazo pia huwa zinageuzwa, na kinyume cha hivyo ni ujinga wa Dini tu, kama alivyosema Imam Al-Qarafi Al-Maliki katika kitabu chake cha [Al-Ihkaam fii Tamiizul Fatawa anil Ahkaam uk. 218, Maktabatul Matbuaat Al-Islamiyah- ya Aleppo].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

 

Share this:

Related Fatwas