Huhumu ya Kuwapongeza Wazazi kwa Kuzaa Mtoto Asiye Halali
Question
Je, inawezekana kuwapongeza wazazi wa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa? Na je, sherehe yeyote kuhusu mnasaba huu inakubalika?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kitendo kinachoenea sana katika nchi za Magharibi ni mtu kuwa na mahusiano na mwanamke nje ya ndoa kisha mwanamke huyo akishika mimba baadaye anaamua kumwoa. Na pengine anaweza kumwoa baada ya kuzaa kwa muda mfupi au mrefu, hali ya kuwa ananasibishwa na watoto.
Suala hili linajulikana katika fiqhi kwa jina la kulea mtoto wa wa uzinifu, na miongoni mwa aina zake mzinzi kumchukua mtoto nje ya ndoa kutoka kwa mwanamke wa mtu mwengine au mwanamke asiye na mume.
Wanazuoni hawajahitilafiana katika hukumu ya jambo hili, nayo ni kutojuzu kwa mzinifu kumfanya mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni wake hata kama atatokana na tendo lake la uzinifu. Lakini kuna kundi la Wanazuoni ingawa ni wachache, walioelekea kuhalalisha suala la kumfanya mtoto ni wake akizaliwa na mwanamke asiye na mume kwa kutokuwepo mgongana katika hali hiyo.
Inajulikana kwamba dalili kuu katika suala hili ni Hadithi inayosema: “Mtoto ni wa kitanda (Mwanake)”, na mzinifu anazuilia”.
Na kauli yake Mtume S.A.W: "Mtoto ni wa kitanda" inamaanisha kwamba mwanamume akiwa na mke au kijakazi na akamwingilia akashika mimba na kuzaa mtoto katika muda wa kukaa naye, basi mtoto ananasibishwa kwake, anakuwa ni mtoto wake mwenye haki ya kumrithi pamoja na haki nyingi nyinginezo zinazohusiana na mtoto na baba yake, akiwa anafanana naye kwa sura au la, kwa sharti mwanamume huyo akae na mama wa mtoto huyo kwa muda wa miezi sita au zaidi.
“Na mzinifu anazuilia"; inamaanisha kwamba mzinifu anapata hasara na hana haki kwa mtoto. Na Waarabu wanaiita hali ya kumnyima mtu: Zuio la kuwa na undugu.
Na waliohalalisha suala la kumlea mtoto wa nje ya ndoa na wa mwanamke asiye na mume, waliitegemea hali ya kugombana kwa mzinifu na mwenye kitanda yaani mwanamke, ilhali mwanamke akiwa hana mume basi katika hali hiyo hapatakuwepo mgongano wowote, basi inajuzu kumchukua mtoto wa nje ya ndoa kutoka kwa mwanamke na kumlea.
Na sisi hatuoni ubaya wowote kufuata madhehebu yanayokwenda kinyume na maoni ya Wanazuoni wengi katika nchi hizi kutokana na kuenea kwa balaa hilo.
Ibn Qudama alisema katika kitabu cha: [Al-Mughniy, 6/345, chapa ya Maktabat Al-Kahira]: "Na mtoto wa uzinifu hanasibishwi na mzinifu kwa mujibu wa maoni ya Maulamaa wengi, naye Al-Hassan na Ibn Sereen walisema: Mtoto wa mzinifu ananasibishwa na babake na anamrithi ikitekelezwa adhabu, na Ibrahim alisema: Ananasibishwa na babake anapopigwa viboko au anapomiliki mwanamke aliyeingiliana naye. Naye Is-hak Alisema: Anamnasibishia. Na ilitajwa kutoka kwa U’rwa na Sulaiman Ibn Yassar rai kama yaliyotangulia. Na ilipokelewa na Ali Ibn A’asim kutoka kwa Abu-Hanifa kwamba: Sioni ubaya wowote anapoingiliana mwanamume na mwanamke nje ya ndoa akashika mimba amwoe akiwa na mimba yake ili kumsitiri, na mtoto katika hali hii ni mtoto wake".
Imamu Ibn Taymiyah katika kitabu cha: [Al-Fatawa Al-Kubra, 5/508, Dar Al-Kutob Al-Elmiya, Bairut] alisema: “Mwanamume anapomnasibisha mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hali ya kuwa mwanamke (mama wa mtoto) hana mume, basi mtoto ananasibishwa kwake na hiyo ni madhehebu ya Al-Hassan na Ibn Sereen na Al-Nakhi’i na Is-hak”.
Hitimisho: Inawezekana kuwapongeza wazazi waliozaa mtoto kabla ya ndoa baba akimfanya mtoto ni wake; maana anazingatiwa kama kwamba anatokana na ndoa au mfano wake (katika shubha) au hata ndoa batili; kwani anakuwa katika hali hiyo ni mtoto wake wa kisheria.
Na anapokuwa mtoto nje ya ndoa kwa mwanamke asiye na mume kama tulivyotaja, basi hakuna ubaya wowote katika hali hiyo kwa kufuata maoni ya waliyohalalisha kumnasibisha mtoto.
Na inajuzu katika hali zote kumpongeza mwanamke baada ya kuzaa kwa salama; kwa lengo la kuonyesha huruma kwa mama mzazi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.