Hukumu ya kuchora michoro ya Wanad...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kuchora michoro ya Wanadamu na Wanyama

Question

 Mimi nimesilimu, lakini kabla ya kufanya hivyo nilipata baadhi ya pesa kutokana na kuchora michoro ya wanyama wafugwao. Nina kipaji cha uchoraji, lakini sasa hivi sina uhakika ikiwa jambo hili linaruhusiwa kwangu au la. Nimejaribu kuchora picha za mandhari ya kimaumbile, lakini kipaji changu ni katika kuchora wanyama wafugwao. Je, naweza kuendelea kuchora wanyama?, hiki ni kipaji changu cha pekee kinachonifurahisha.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Malik, na baadhi ya Wanavyuoni waliotangulia wamesema kuwa inaruhusiwa kuchora wanyama. Na Ibn Himdan wa madhehebu ya Ahmad Ibn Hanbal ameafikiana na wanavyuoni wa madhehebu ya Maliki, kwani uharamu ni kwa masanamu ambayo yana urefu upana na kina. Mtazamo huu umepokelewa kutoka kwa Ibn Abi Shaibah katika “Al-Musanaf” kutoka kwa Al-Qasim ambaye ni Mfuasi bora wa watu wa wakati wake kwa mapokezi sahihi kama alivyosema Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha “Fathul Bari”, kutoka kwa Ibn Uwan alisema: Nimeingia nyumbani kwa Al-Qasim naye akiwa upande wa juu ya Makkah nikaona pazia ina picha ya aina ya mnyama na aina moja ya ndege. Al-Nawawi amesema katika sherehe ya Muslim kuwa: “Wanavyuoni waliotangulia walisema kuwa zilizoharimishwa ni picha zile zenye kivuli, lakini picha zisizo na kivuli hazikuharamishwa kabisa, na mtazamo huu ni batili. Ibn Hajar alisema katika kitabu cha “Fathul Bari” Hatuna uhakika kuhusu ubatili wa mtazamo huu”.
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu, wanavyuoni wametofautiana kuhusu suala hilo. Kwa hivyo, hakuna ubaya kama Mwislamu akifuata mtazamo mmoja miongoni mwa mitazamo ya Wanavyuoni katika suala hilo, kwani kama kuna tofauti ya Wanavyuoni ipo nafasi. Kwa hivyo, hakuna ubaya wowote kuwachora wanadamu au hata wanyama wa kufugwa n.k. Ni sawasawa picha hizo zitokee akilini mwako au ni sura za asili au picha za kupiga kwa kamera, na hakuna ubaya kwako kama ukiendelea kukitumia kipaji hiki na kupata pesa, na namwomba Mwenyezi Mungu akusaidie.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote
 

Share this:

Related Fatwas