Msongamano wa Makaburi
Question
Jumuiya moja ya Kiislamu ina makaburi katika eneo la kuzikia la Sayyida Nafisa R.A, na hivi sasa eneo hilo limejaa kwa wafu waliozikwa, wapo waliozikwa hivi karibuni na wapo waliozikwa zamani, wao wanapindukia miaka miwili. Pamoja na kujua kuwa maumbile ya ardhi katika eneo hilo ni unyevunyevuu nao chelewesha miili kutoweka, na tulipoielezea Jumuiya hiyo kuhusu jambo hili tukakuta kuna ugumu. Ambapo wengi wao wanakariri kusema kwamba aliyefariki ni katika wafuasi wao na yawezekana akausia azikwe katika maeneo ya Sayyida Nafisa. Pamoja na kujua kwamba Jumuiya inamiliki maeneo mengine ya kuzikia katika Mji wa 6 Oktoba, na katika Mkoa wa Fayuum pia, na kuna sehemu zakutosha. Je, Ni ipi Hukumu yake juu ya Wasia unaotajwa na wanachama wa Jumuiya hiyo kwa maiti zao?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Na iwapo wafu watakuwa wameusia wazikwe katika makaburi ya Sayyida Nafisa R.A, utekelezaji wa wasia wa aina hii sio lazima kwa kuwa kuna sehemu nyingine ya Jumuiya hiyo hiyo katika Mikoa mingine miwili iliyotajwa ambayo inafaa kuzikia bila ya kuwepo kizuizi cha kisheria.
Ama ikiwa itawezekana kutekeleza nyasia hizo pamoja kuchunga tahadhari za kisheria: Kama vile kukiuka heshima ya maiti na mfanowe, kama vile kuyajengea makaburi juu ya mengine, au kuyafunika juu ya makaburi mapya kwa udongo au kwa mawe bila kugusa miili yao kisha kuweka juu ya makaburi yao mchanga na kuwazika wengine wapya juu yake, jambo hili lina pendeza na wala halikatazwi kisheria.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.