Kuwasadiki Makuhani kwa Yule Ulio ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwasadiki Makuhani kwa Yule Ulio Dhihiri Ukweli wa Ukuhani Wake Mara Nyingi.

Question

Kwa nini haijuzu kwa waislamu baada ya zama za Mtume Muhammad S.A.W kusadiki na kuwaamini Makuhani na utabiri wa watu wenye busara ya kutoa habari za zisizojulikana mara nyingi, kama vile: Nostradamus, Edgar Cayce, Lenorman, Fanga, na Wolf Messing? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Hakika kuijua ghaibu ni jambo linalomuhusu Mwenyezi Mungu mwenyewe, na maana ya hayo ni kuwa: Hakuna mtu yeyote anayeweza kushirikiana na Mwenyezi Mungu katika kuijua ghaibu kikamilifu na kiuwazi, na inaweza kusemwa ni ghaibu ya uwazi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Yeye ndiye Mjuzi wa siri; wala hamdhihirishii yeyote siri yake}. [AL JINN: 26]. Kuhusu mambo ya ghaibu ambayo wanayajua Manabii na baadhi ya watu wema, nayo ni kutokana na wao kuambiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu tu, na Yeye anasema: {wala (hao viumbe) hawalijui lolote katika (yaliyo katika) ilimu Yake (Mwenyezi Mungu) ila kwa alipendalo (Mwenyewe)}. [AL BAQARAH: 255], kuhusu Mitume na Manabii ni jambo la yakini, kinyume cha wengine ambapo ni la dhana; kama vile; hisia za moyo, ndoto, n.k, kwa aliyopokea Bukhariy, kutoka kwa Abi-Huraira R.A, kuwa: Mtume S.A.W, anasema: “Hakika ilikuwa katika hao waliotangulia watu wenye busara, na miongoni mwao katika umma wangu ni Umar Ibn Al-Khattab”.
Al-Manawiy katika At-Taysiir [2/193, Ch. ya Maktabat Al-Imam Ashafiy, Riyadh] anasema: “Mwenye busara yaani; mwenye ilhamu, mwenye mawazo ya kweli, au mwenye usemi wa kweli (kupatia kweli) bila ya kukusudia, au malaika wanamsemesha bila ya kuwa nabii”. [Mwisho].
Na ilhamu ya kweli ilikuwa miongoni mwa sifa kuu za Amiri wa waumini Umar Ibn Al-Khattab R.A, kwa sababu baadhi ya ilhamu zake ziliafikiana na hukumu za Wahyi, na pengine na lafudhi zake pia hata kabla ya kuteremshwa. Na imepokewa na Anas Ibn Malik R.A, akisema kuwa Umar Ibn Al-Khattab R.A, amesema: “Niliwafikishwa na Mola wangu mara tatu: Niliposema Ewe Mtume wa Allah: Tuchukue usimamizi wa Ibrahimu mahali pa kusalia, basi Aya ikateremshwa: {Na mahali alipokuwa akisimama Ibrahimu pafanyeni pawe pa kusalia}. [AL BAQARAH: 125]. Na Aya ya Hijabu, niliposema Ewe Mtume wa Allah waamrishe wake zako kuvaa Hijabu, kwa sababu wanaamiliana na watu, na miongoni mwa watu hawa ni wema, na wengine ni wabaya. Na hapo, Aya ya Hijabu ikateremshwa; na wake za Mtume S.A.W, walikuwa na wivu wenyewe kwa wenyewe kwa mtume, niliwasema: "(Mtume) akikupeni talaka, Mola wake atampa, badala yenu, wake wengine walio bora kuliko nyinyi}, basi Aya hii ikateremshwa". [Imepokelewa na Imamu Bukhariy, na hii ni kauli ya; Muslim kutoka kwa Ibn Umar].
Na At-Tirmidhiy amepokea kutoka kwa Abi-Said Al-Khudriy, akisema: Mtume S.A.W, amesema: “Ogopeni busara ya muumini, kwa sababu yeye anatazama kwa nuru ya Allah, kisha alisema: {Hakika katika (masimulizi) haya yamo mazingatio (makubwa) kwa watu wenye kupima mambo}. [AL HIJR: 75].
Ibn Al-Athiir katika kitabu cha An-Nihaya [3/482, Ch. ya Al-Maktabah Al-Ilmiyah] anasema na kuielezea Hadithi: “Husemwa kwa maana mbili, maana ya kwanza: Ni ile inayoonesha udhahiri wa Hadithi hii, nayo ni jinsi mwenyezi Mungu anavyowafunulia waja wema katika nyoyo zao, ambapo wanaweza kujua baadhi ya hali za baadhi ya watu, na hii ni aina ya Karama, dhana ya kweli, na utabiri; Maana ya pili: Aina ya kujifunza kutokana na dalili, majaribio, uumbaji, na tabia, ambapo hali za watu zinaweza kujulikana, na maudhui hii yenye tasnifu nyingi za zamani na za kisasa”. [Mwisho].
Matini tukufu hizi zinaonesha kuwa ndoto na ilhamu za kweli ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Yeye anawajulisha waja wake wema mambo ya ghaibu yanayowapendeza, lakini hawawezi kuyachukua kama hoja au kutoa hukumu ya Sheria kutokana na mambo haya peke yake bila ya dalili au misingi ya kisheria; kwa sababu ya kujiepusha na makosa au wasiwasi wa shetani siyo ya yakini kwa watu wa kawaida, isipokuwa Manabii. Kwa hiyo, kufaidika kwa ilhamu na ndoto ni kwa njia ya matumaini mema, matamanio mema, na mapenzi ya mwenyezi Mungu Mtukufu, ya kumuongoza muumini kwa ilhamu na ndoto yake njema, ambapo hayapingani na Wahyi Maa’suum, na bila ya kuyanasibisha haya kama ni yakini kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Mambo kama hayoyanaweza kuwa na njia sahihi ya kidini, na pengine kuwa na njia ya Shetani, ambapo watu wahalifu na wasio waumini wajue baadhi ya mambo ya ghaibu kwa njia ya uaguzi na ukuhani.
Imesemwa kuwa: Uaguzi na ukuhani zina maana moja, na imesemwa kuwa uaguzi ni kutoa habari ya ghaibu ya zamani, lakini ukuhani ni kutoa habari ya ghaibu ya wakati ujao [Al-misbah Al-Muniir, na Al-Fayumiy, Uk. 404, Ch. ya Al-maktabah Al-Ilmiyah].
Katika ufafanuzi wa kinabii kwa hakika ya ukuhani na kubainisha sababu ya ulinganisho wa maneno ya makuhani kwa yatakayotokea siku zijazo, imetajwa katika Hadithi Sharifu iliyopokelewa na Aisha R.A, akisema: “Watu waliuliza Mtume S.A.W, juu ya makuhani, akasema: Si kitu, wakasema: Ewe Mtume, pengine walituambia kitu kisha kikawa cha kweli, na Mtume S.A.W, akasema: Neno hili ni kutokana na haki, na Jini analinyakua, kisha analitupa katika sikio la mwenzake, basi wanazidisha maneno mia ya uongo”. [Muttafaq].
Katika mapokezi ya Muslim: “Lile neno la haki, na Jini analinyakua, akalitupa katika sikio la mwenzake na kuzidisha maneno mia ya uongo”.
Al-hafidh Ibn hajar katika [fathul-Bariy: 10/217, Ch. ya Dar Al-maa’rifah] anasema: “Al-Khattabiy anasema: Makuhani ni watu wenye akili kali, nafsi mbaya, na tabia za moto, kwa hiyo Mashetani waliwapenda kutokana na sifa zao za pamoja juu ya mambo haya na kusaidiana kutokana na uwezo wao, na ukuhani ulikuwapo kwa wingi wakati wa Ujahili hasa kati ya waarabu, kwa sababu ya kutokuwepo Unabii. Na ukuhani una aina nyingi, miongoni mwake: Ulivyofunuliwa kwao na majini; ambapo majini walikuwa wakipanda upande wa mbingu wenyewe kwa wenyewe, hapo aliye juu kabisa anaweza kusikia maneno, kisha akawasilisha kwa aliye chini yake mpaka kufikia aliyemuwasilisha katika sikio la kuhani, na huyu anaongeza ndani yake, na Uislamu ulipokuja na Qur`ani kuteremshwa, mbingu imelindwa dhidi ya Mashetani, na vimondo hupigwa dhidi yao, kwa hiyo yaliyobaki ni aliyoisikia aliye juu na kumtupia aliye chini kabla ya kupigwa na kimondo, na hii ni ishara ya kauli ya Mwenyezi Mungu: {Isipokuwa anayenyakuwa kitu kidogo hivi (katika maneno yanayosemwa huko); mara kikamfuata kimondo (kijinga cha moto) king’aracho (kikamuangamizia mbali)}. [AS SWAFFAAT: 10].
Utoaji habari ya kweli kwa upande wa makuhani ulikuwa mkubwa sana kabla ya Uislamu… lakini baada ya Uislamu ni nadra sana, mpaka kukaribia kuwa si kitu, na shukrani zote za Mwenyezi Mungu. [Mwisho].
Hakika ya neno hili linalonyakuliwa na Jini au Shetani ni namna anavyopata kwa njia ya kusikiliza kwa siri au kuvizia kauli za Malaika na mazungumzo yao kwa alivyowajulisha Mwenyezi Mungu kuhusu yanayojiri na matokeo ya mambo, na Mwenyezi Mungu amesema akitaja baadhi ya mazungumzo haya yanayojiri kati ya Malaika: {Wala hautafaa uombezi mbele Yake (Mwenyezi Mungu) ila kwa yule aliyempa idhini. Hata inapoondolewa hofu nyoyoni mwao, husema: “Mola wenu amesema nini?, (Na wao) huwaambia; (amesema maneno ya) Haki, naye ndiye Aliye juu, Mkubwa”}. [SABA: 23]. Na Mwenyezi Mungu alitaja kuwa Viumbe watukufu Malaika huwa wanaenda kushindana na kujadiliana katika mazungumzo yao, akasema S.W: {Sema: “Haya (ninayokwambieni) ni habari kubwa kabisa”. Mnajiepusha nayo (Mnayapuuza). Sikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe watukufu (Malaika) walipokuwa wakishindana, (ila amenijulisha Mwenyezi Mungu)}.[Sad: 67-69].
Na baada ya Utume wa Mtume S.A.W, Majini hawajaweza bado kusikiliza kwa siri kama walivyokuwa wakifanya kabla ya hapo, kwani Mwenyezi Mungu amewapelekea walinzi na vimondo vya mbinguni ambavyo huwakataza kufanya hivi, isipokuwa alivyowakadiria Mwenyezi Mungu kunyakuliwa na baadhi ya maneno, ambapo wanaongezea maneno ya uongo yawe ya habari inayotolewa kwa watu, Mwenyezi Mungu alisema: {Bila shaka sisi tumeipamba mbingu ya karibu (hii) kwa pambo la nyota.Na kulinda na kila shetani asi. Wasiweze kusikiliza (yanayosemwa na hao) viumbe watukufu (Malaika); na wanafukuzwa huko kila upande. Kwa hizaya; na wanayo adhabu (inayowazuia kufika huko) inayodumu kwao. Isipokuwa anayenyakuwa kitu kidogo hivi (katika maneno anayosemwa huko); mara kikamfuata kimondo (kijinga cha moto) king’aracho (kikamuangamizilia mbali)}. [AS SWAFFAAT: 6-10].
Na Mwenyezi Mungu anasema akieleza usemaji wa majini na kukosa kwao kusikiliza habari zinazojiri heri au shari, baada ya ukali wa ulizi wa mbingu: {Nasi tulizigusa mbingu (tulikwenda mbinguni) tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na nyota (zing’arazo). Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini anayetaka kusikiliza sasa atakuwa kimondo (kijinga cha moto) kinamvizia. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa katika ardhi au Mola wao anawatakia uongofu (kheri)}. [AJ JIN: 8-10].
Bukhariy amepokea katika kitabu chake, kutoka kwa Aisha R.A, mke wa Mtume S.A.W, kuwa yeye amesikia Mtume S.A.W, akisema: “Hakika Malaika hushuka katika mawingu, wakataja jambo lililokadiriwa katika mbingu, na Mashetani walisikiliza jambo hili, wakawafunulia makuhani, na hao wanasema maneno mia ya uongo kwa wenyewe”.
Maaguzi ya makuhani ni upotevu unaochanganywa na uongo, kwa hiyo hayafai yawe hata dhana, mbali na ngazi ya elimu na yakini, na upotevu huu uongo wake hushinda ukweli wake, na kuyasadiki na kuyapa uaminifu ni dhulma; kwa sababu ni kuweka kitu mahali pasipo pake, na hii kwa upande wa hukumu ya akili, ama kwa upande wa matini ya sheria, tunakuta maonyo na vitisho vinavyokataza kumsadiki kuhani au mwaguzi, kwa hiyo haijuzu kwa mwislamu kumuuliza kuhani au mwaguzi au anayedai kuwa ana uwezo wa kuagua ghaibu, na watu kama hao wanaoomba msaada wa Mashetani na wanaungana nao, haijuzu kwa mwislamu kuwaamini na kuwasadiki wanvyodai, hata maaguzi yao yangali kweli mara nyingi, kwa alivyopokea Muslim katika kitabu chake, kutoka kwa Mua’awiyah Ibn Al-Hakam As-Salamiy, amesema: “Nilisema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tulikuwa tukifanya mambo wakati wa ujahili, tulikuwa tunawaendea makuhani, akasema: Msiendee makuhani, nikasema: Tulikuwa tumekorofika, akasema: Hili ni jambo linalojiri nafsini mwa watu, basi msilifuate”.
Vile vile, ilivyopokelewa na Muslim katika kitabu chake, kutoka kwa baadhi ya wake wa Mtume S.A.W, alisema: “Aliyefika kwa mtabiri na kumuuliza kitu, sala yake haitakubaliwa siku arobaini”.Pia kauli yake: “Aliyefika kwa kuhani, akamsadiki anavyosema, basi yeye amekufuru kwa aliyoteremshiwa Muhammad”. [Ameipoke Ahmad katika kitabu chake, na Al-Hakim katika kitabu chake.
Kwa muhtasari, kuna tofauti kubwa kati ya Unabii na kujua baadhi ya mambo yasiyojuliwa. Unabii ni kutokana na Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na unaambatana na miujiza yenye changamoto, na watu hawawezi kufanya mfano wake, ama kujua baadhi ya mambo ya ghaibu na kutoa habari zake, inaweza kutokea kwa mikononi mwa baadhi ya watu, na hii haioneshi kuwa mhusika huyu ni Nabii maasumu, walii, mtawa, kwa sababu Mwenyezi Mungu ni muweza kumpa anayemtaka miongoni mwa waja wake idhini kwa kujua siri yeyote ya ulimwengu kwa njia yeyote ya kujulisha, lakini hii haimaanishi kuwa mhusika huyu ni Nabii au Mutume anayefunuliwa, na anastahiki kusadikiwa na kufuatwa; kwani hakuna Nabii baada ya Mtume wetu Muhammad S.A.W, na usahihi wa kudai Unabii ni kwa kuitangaza kwanza, kisha kufuatiliwa na miujiza ya kihisia ambayo watu wa kawaida hawawezi kuiga, na ufungamano wa miujiza hii na changamoto mbele ya watu wafanye mfano wake, pamoja na kutokuweza kuifanya kivitendo.
Na hao waliotajwa katika swali, mmoja miongani mwao hajapata Unabii wala miujiza, kwa sababu wao si Manabii wala watawa wanaofuata Sunna za Manabii, bali ni walii wa Mashetani, ambapo watu wanalazimika kujiepusha, na Mwenyezi Mungu amesema: {Bila shaka sisi tumewajaalia mashetani kuwa marafiki wa wale wasioamini}. [AL ARAAF: 27]. Na pia alisema: {Anayeyafanyia upofu maneno ya Mwingi wa rehema tunamwekea Shetani kuwa rafiki yake, (kuwa mwenziwe)}. [AZ ZUKHRUF: 36].
Kwa mujibu wa hayo: Haijuzu kwa njia yeyote ile, kuomba msaada kwa makuhani na wanaodai kujua ghaibu, wala kuwasadiki vitu wanavyovisema, zadi ya hayo maneno mengi ya watu hawa yanafuata njia ya alama na ishara, na si kwa uwazi kuagua tukio maalum, bali ni maneno ya ajabu, yenye sura nyingi, na yasiyo na maana maalumu, kama vile TAbiri za Nostradamus.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas