Vitu Vyenye Shaka na Aina Zake

Egypt's Dar Al-Ifta

Vitu Vyenye Shaka na Aina Zake

Question

Tunasikia mara nyingi neno "Vitu vyenye shaka", hasa katika mfano usemao, epukeni vitu vyenye shaka, au: Adhabu huondolewa kwa vitu venye shaka, basi ni nini maana ya vitu vyenye shaka? Ni zipi aina zake? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume S.A.W. kwa Dini aliyoikubali iliyo mwisho wa dini zote, na Mtume S.A.W, hakutuacha ila katika njia iliyo wazi baada ya kubainisha halali na haramu, na ametuamuru kuchunguza ili kulijua jambo hili. Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah, R.A, kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, amesema: "Enyi watu, Mwenyezi Mungu ni mwema na hapokei ila vilivyo vizuri tu, lakini Mwenyezi Mungu aliwaamuru waumini kama alivyowaamuru Mitume, alisema: {Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda} [AL MUUMINUN 51], na akasema: {Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni} [AL BAQARAH: 172],
Kisha alitaja mtu anayeongeza muda wa kusafiri Kichwa chake kimetimka nywele, miguu yake imejaa mavumbi akinyoosha mikono yake mbinguni: Ewe Mola wangu Ewe Mola wangu, na vyakula vyake vya haramu, vinywaji vyake vya haramu, na mavazi yake ya haramu, na amelishwa kwa haramu, ni namna gani atajibiwa dua zake?) [Imepokelewa kutoka kwa Muslim].
Hivyo, kujua mambo ya halali na ya haramu ni miongoni mwa mambo yanayotakiwa kisheria ili hali ya mja isahihishwe. Na kujua huku ni rahisi, kwa sababu ni suala la wazi sana, hali ambayo inaashiriwa katika Hadithi ya Al-Nu'man Ibn Bashir, R.A, aliesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akisema kuwa: "Halali iko wazi na haramu iko wazi, baina yake ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawavijui. Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka anajisafisha nafsi yake kwenye Dini na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika Mambo yenye Shaka, huangukia katika haramu, kama mchungaji anayechunga pembezoni mwa mpaka, mara huingia ndani (ya shamba la mtu) [Hadithi hii imekubaliwa na Al-Bukhari na Muslim].
Hadithi hii inadhihirisha halali na haramu kwa dalili zake, lakini tatizo kwa watu wengi ni mamabo ambayo yenye shaka, na hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu imetaka kuwapo mambo yaliyo wazi na Mambo yenye Shaka, na kwamba mambo yaliyo wazi kuwa si wazi kabisa, wala Mambo yenye Shaka ni mengi. Al-Shatibi anasema katika kitabu cha: [Al-Muwafaqat 3/86, Ch. Darul Maarifa]: “Inajulikana kwamba mambo yanayofanana yamejitokeza katika Sheria, lakini kuyaangalia mambo hayo yamejitokeza kiasi gani, ni mara nyingi au mara chache?
Na yaliyothibiti miongoni mwayo ni kwa uchache au kwa wingi”. Neno la Kiarabu “Shubha” linalomaanisha Mambo yenye Shaka, lina maana nyingi. Na miongoni mwazo ni: Mithili, inasemwa: Kitu hiki kinafanana na kitu kile: Na kutokana na maana hii tunakuta aya ya Qur`ni isemayo: {Na wataletewa matunda yaliyofanana} [AL BAQARAH: 25], yaani: Matunda ambayo yanafanana mfanano wa umbo. Neno la “Shubha” lina maana ya Kuchanganyikiwa pia, inasemwa: Mambo yamechanganyika. [Rejea: Lisan Al-Arab 13/503, Kidahizo cha (Shu b ha), Dar Sader, na tajul Aruus 36/411, sehemu ya Shiin kutoka mlango wa Haa, Taa, Baraza la Taifa la Sanaa na Utamaduni na Fasihi, Kuwait, na Al-Misbahul Muniir uk. 303 na kurasa zifuatazo, kidahizo cha (Shu b ha). Al-Maktaba Al-Ilmiyyah, na Tahdhiib Al-Lugha 6/92, Al-Muasasah Al-Misriyah Lil Taliif wal Anbaa wal Nashr, na kitabu cha Al-Huduud Al-Aniqah kwa Sheikh Zakaria Al-Ansari, uk. 77, Darul Fikr, na kitabu cha Kashaaf Islahaat Al-Funuun kwa Tahanui 1/1005, Maktabat Lebanon].
Fafanuzi za wanavyuoni za Mambo yenye Shaka zimetofautiana, lakini fafanuzi zao zote zinarejea katika maana ya kilugha iliyotangulia hapo juu. Miongoni mwa fafanuzi hizo ni: Mambo yasiyo na uhakika kuwa ni haramu au halali. [Anis Al-Fuqhaa kwa Qonoi uk: 281, Darul Wafaa- Jeddah, Al-Huduud Al-Aniqah: 77].
Imesemwa kuwa: Mambo yenye Shaka ni yale ambayo ukweli haujulikani kwa uchambuzi wake na tena ni haramu. [Al-Mawahib Al-Sunniah Sharhu Al-Fraid Al-Bahiyyah kwa Al-Jarhazzi 1/134, Darul Bashair.
Fafanuzi hizi mbili ni katika zile zinazothibitishwa kwa Hadithi ya Al-Nu'man Ibn Bashir itanguliayo: "Halali iko wazi na haramu iko wazi, baina yake ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawavijui...". Katika Hadithi ya Al-Tirmidhi: "Watu wengi hawajui kama mambo hayo ni miongoni mwa mambo ya halali au ya haramu". Kwa hivyo, kila jambo lisilojulikana hukumu yake linakuwa miongoni mwa Mambo yenye Shaka.
Imesemwa pia kuwa hayo ni mambo ambayo hukumu yake ina shaka kutokana na kutoafikiana kwa wanavyuoni. [Al-Hawi kwa Maurdi 13/467].
Vile vile imesemwa kuwa ni uwezekano wa kuwapo uharamu unaotegemea dalili na unapinga asili ya uhalali. [Muftahul Saada kwa tash Kubra Zadah 3/223, Darul Kutub Al-Elmiyah].
Maana hii ya kiistilahi iliyopita inakusanya mambo yote yenye shaka katika kila hali ambayo uhalali umechanganyika na uharamu, na maana hii ni ya ujumla. Pia kuna maana nyingine ya Mambo yenye Shaka, lakini inahusiana na adhabu (Al-Hudud) na mambo ambayo yana maana ya adhabu, kama vile Kafara, ambapo wanafiki wameitolea hukumu maalum kufuatana na kuwepo kwa shaka kama hii katika mlango wa adhabu na kafara, hukumu hizi ni kama kuondolewa kwa adhabu, kama walivyosema wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi kwamba Mambo yenye Shaka ni: “Jina la kile kinachothibitika lakini siyo thabiti” [Badaa'i Al-Sanai 7/36, Darul Kutub Al-Elmiyah, Al-Inayah 5/260, Darul Fikr, na Al-Darul Mukhtar 4/18, Darul Kutub Al-Elmiyyah].
Maana ya hayo ni kwamba sababu ya hukumu inaambatana na jambo linalofanana na jambo ambalo ni thabiti lakini kwa kweli jambo hili siyo thabiti. Basi kwa mfano, kufungwa kwa ndoa baina ya mwanamume na mwanamke ambaye kwa yule ambaye haruhusiwi kuoa, na mwanamume huyu aliyeoa hana adhabu kwa mujibu wa madhehebu ya Abu Hanifa ingawa alijua uharamu huu; kwa sababu kuwepo kwa mkataba wa ndoa kuna maana ya uhalali wa kuoa, lakini hali ya uharamu wa kuoa kwa mwanamke katika suala hili imebatilisha mkataba huo, na kwa hivyo, kama mkataba huu haukuwa sahihi, basi sura yake ambayo inafanana na mikataba ambayo ni sahihi, huondosha na kuepusha adhabu.
Lakini mbali na adhabu mambo ambayo yenye shaka yana maana ile ya ujumla ya kiistilahi, au yana maana ya kilugha tu.
Na Mambo yenye Shaka yana sababu zake, labda kwa sababu ya kutokuwepo dalili au kwa sababu ya kutoifahamu au kuificha dalili hiyo na kadhalika; hivyo hawaijui ila wachache tu, na iliyofahamika kutokana na Hadithi ya Mtume aliyosema: "Watu wengi", kwamba wachache tu wanaofahamu hukumu za Mambo yenye Shaka, wachache hawa ni wenye jitihada kwa utofauti wa vyeo vyao, mambo yasiyo wazi kwa wengine huwa yanakuwa wazi kwa wachache hawa, na sababu ya Mambo yenye Shaka labda kupingwa kwa dalili au kutokuwepo kwa dalili, au kutokukubaliana kwa wanavyuoni kama itakavyotajwa baadaye.
Lakini jambo ambalo tunataka kulithibitisha ni kwamba msingi wa jumla unaohusiana na Mambo yenye Shaka – na ambao asili yake ni Hadithi ya Al-Nu'man Ibn Bashir- ni kwamba inabidi mja aache mambo ambayo hayana shaka kwa ajili ya kuepuka Mambo yenye Shaka, na hali hii ni cheo cha kiucha-Mungu, na maelezo ya hayo ni: “Mambo ambayo ni halali basi ni halali, mambo ambayo si halali basi ni haramu, na mambo ambayo wananvyuoni wametofautiana kuhusu uhalali na uharamu wake kwa mujibu wa sifa na sababu zake, basi inabidi kutazamwa kwa sababu za uhalali na uharamu wake, kama dalili zake zikitofautiana, basi suala ambalo dalili za uharamu wake ni zaidi litakuwa haramu, na suala ambalo dalili za uhalali wake ni zaidi litakuwa halali. Lakini kama dalili zake zikiwa sawa, basi ni jambo lenye shaka, na kuachwa kwake ni minogoni mwa kuachwa kwa Mambo yenye Shaka, kwa sababu suala hili linafanana na lengine ambalo ni halali na lina dalili ya uahalali wake.
Na katika wakati huo huo linafanana na lengine ambalo ni haramu na lina dalili ya uharamu wake, yule anayeepuka vyenye shaka anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake kwa sababu amesafisha na kuiweka dini yake mbali haramu. Na anajisafisha yeye mwenyewe kwa ajili ya heshima yake, kwa sababu atakuwa amejiweka mbali na maneno kama vile: Mtu fulani anakula haramu. Kama dalili zikiwa sawa, basi jambo ambalo dalili zake zilikaribiana na uharamu, litakuwa haramu, na jambo ambalo dalili zake zinakaribiana na uhalali, basi hilo ni halali, na jambo ambalo dalili zake za uharamu na za uhalali zilikaribiana, limeachwa na halikuchaguliwa kufuatana na mtazamo ulio sahihi. [Rejea: Al-Qawaid Al-Kubra kwa Al-Iz Ibn Abdul Salam 2/190, Darul kalam].
Inafahamika kwamba kuwepo kwa Mambo yenye Shaka kulikuwa na fadhila katika kubainisha asili ya baadhi ya misingi kama vile: Msingi wa kujihadharisha, yaani kufanya jambo la haramu kunahitajia kujua jambo hili wakati wa kuwepo kwa Mambo hayo yenye Shaka, kwa hivyo basi, anayechunga pembezoni mwa mpaka, mara huingia ndani (ya shamba la mtu), kwa hiyo tunakuta maoni ya wanazuoni wa Fiqhi kuhusu anayechanganya kati ya halali na haramu au alie na shaka katika jambo ni la halali au la haramu, basi katika hali hii msingi wa kujihadharisha unatekelezwa, na Mambo yenye Shaka hayakuondolewa ila kwa msingi huu tu.
Na mwenye kuangalia katika vitabu vya madhehebu atakuta kwamba wenye vitabu hivi hawakujali wote kwa kiwango kimoja kuyagawanya Mambo yenye Shaka. Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi na Shaafi'i walijali zaidi kuliko madhehebu zote katika kutaja migawanyiko ya Mambo yenye Shaka, ambapo tumeyakuta haya kupitia maneno ya wanazuoni hawa wa Fiqhi, wakati tunaona kwamba wanavyuoni wa madhehebu ya Malik na Hanbal ingawa walitaja mgawanyiko wa Mambo yenye Shaka, hata hivyo, wengi wao wanaashiria tu kuwepo kwa Mambo yenye Shaka, na wamebainisha athari za kuwepo kwao Katika hukumu.
Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi wamegawanya Mambo yenye Shaka katika sehemu tatu:
Ya kwanza: Shaka ya kitendo: Maana yake ni kudhani kuwa hakuna dalili nyingine isipokuwa ile ya kuhalilisha ndio dalili sawa. Aina hii inaitwa shaka katika kitendo, ambayo ni kuoa kwa mfano, ambapo kulikuwa miongoni mwa Mambo yenye Shaka kuhusu uharamu wake, na anayemwoa mwanamke mtalaka aliyeachwa kwa talaka tatu naye bado yuko katika eda kisha akasema: "Nilidhani kuwa ni halali kumwoa, basi haadhibiwi. Na kwa hivyo basi kuna shaka katika suala hili ambapo hakuna dalili inayothibitisha uhalali wake, yaani suala hili lenye shaka haliwezi kujadiliwa, bali mtu huyo alikuwa na shaka katika dalili na akadhani kuwa dalili hiyo ni sawa. Kwa hivyo basi shaka inategemea kudhani, au hakuna shaka katika kudhani kuwa hakuna dalili inayothibitisha shaka hii katika jambo lile lile."
Hivyo, sababu za kuondoa adhabu katika suala hilo ni mbili:
Ya kwanza: Kuwa ni jambo lenye shaka, basi anayemwoa mwanamke mgeni huadhibiwa hata kama akidai kuwa alidhani kuwa mwanamke huyo ni halali kwake.
Ya pili: Kudai kuwa ni kudhani tu, kwa maana kwamba kama yeye akisema: Nilifahamu kwamba tendo hili ni haramu, basi ataadhibiwa, na kama hakudai kudhani ataadhibiwa pia, lakini haadhibiwi kama akidai na kama hakudhani; kwa sababu dhana ni jambo la ndani ambalo jaji halijui isipokuwa kwa dai la mwenye dhana hiyo, na kwa hivyo basi sharti la kuondoa adhabu ni kuwa jaji anafahamu kwamba mtu huyu amedhani kuwa suala hili ni halali, na hali hiyo haikuwa isipokuwa kwa dai lake na kwa kumwambia.
Na shaka hii -katika tendo- inaondosha adhabu kwa mtazamo wa wanavyuoni wengi wa madhehebu wa Hanafi kwa mujibu wa shaka yake, lakini nasaba haithibitishwi katika hali hii; kwa sababu kitendo hicho ni uzinifu kweli, na nasaba haithibitishwi kwa uzinifu, lakini wanavyuoni wametenga hali mbili za kutothibitishwa kwa nasaba,
Ya kwanza: Ni kumwoa mwanamke mtalaka ambaye amepewa talaka mara tatu katika eda.
Na ya pili: Ni kumwoa mwanamke asiyekuwa mkewe akitegemea kauli ya wanawake kuwa ni mke wake. Kwa kusema kwamba hali hii ya shaka ni miongoni mwa shaka katika kitendo siyo katika mahala. [Tabiin Al-Haqaiq 3/175, Darul kitabul Islami, Sharhu Minla Miskin ala Al-Kanz 2/358, Wadul Mihtaar 4/21, Al-Inayah Maa Fathul Qadiir 5/247 na zaidi, Darul Fikr wallubaab 3/190, Al-maktabh Al-Ilmiyyah].
Aina ya pili: Ni shaka katika hali, na maana yake ni kuzuka kwa dalili inayouondosha uharamu. Aina hii haitegemei kudhani na imani ya mtu mwenyewe, lakini inategemea kuwa hali ya kitendo ina uhalilishaji wa kitendo hicho. Aina hii inaitwa shaka ya hali kwa sababu shaka hiyo inatokana na dalili inayolazimisha kuhalilisha suala moja, pia huwa inaitwa shaka ya hukumu; kwani shaka katika hukumu ya kuhalilisha ndio iliyo thibiti, nayo aina hii inaweza kuondoa adhabu pia, hata kama mtu akidai kuwa anajua uharamu wa kitendo alichokitenda. [Radul Muhtaar 4/20].
Wanavyouni wa madhehebu ya Hanafi wameeleza aina hiyo kwa mifano mingi, na miongoni mwayo ni: Mtu kumwoa kijakazi wa mwanae, kumwoa mtalaka aliyepewa talaka mara tatu, kumwoa kijakazi aliyeozwa kabla ya kukabidhiwa, kijakazi aliyepewa mahari kabla ya kukabidhiwa kuwa mkewe, na kijakazi ambaye ni pamoja na mwingine.
Na maana katika shaka hii ni kuthibiti kwa miliki hata kutoka upande mmoja; Kwa mfano, katika suala la kumwoa kijakazi wa mwanawe, mzazi huyo hataadhibiwa kwa sababu kuna dalili ya kummiliki kijakazi huyo, nayo ni kauli ya Mtume S.A.W: "Wewe na mali yako ni miliki za baba yako" [Imepokelewa na Ibn Majah, Al-Buseri akasema: "Mapokezi yake ni Sahihi, na waliopokea Hadithi hii ni Waaminifu kwa sharti ya Al-Bukhari na Muslim]; Hadithi hii inalazimisha uhalali wa suala hili, kwani ndani yake kuna Umiliki wa kijakazi."
Na shaka hii ni kama aina ya shaka ya kitendo kuhusu kuepuka adhabu, lakini nasaba itathibitishwa kama akiidai.
Aina ya tatu ni: Shaka ya mkataba: Nayo ndio iliyotajwa na Abu Hanifa. Baadhi ya wanavyuoni wa madhehebu ya Abu Hanifa wameiambatanisha aina hii na aina zingine mbili zilizotangulia, kwa sababu mifano iliyotolewa kwa aina hii inatokana na aina hizi mbili zilizotangulia, na kwa hiyo Ibn Abdiin alisema: “Ni bora kuambatanisha aina ya tatu na aina hizo mbili zilizotangulia” [Radul Muhtaar 4/19]; yaani aina ya shaka ya mkataba inaambatanishwa na shaka ya kitendo pamoja na shaka ya hali.
Anasema Mwanachuoni Al-Tahtaui katika kitabu chake: [2/396, Bulaq]: “Inaonekana kuwa kugawanywa - kwa aina za shaka - sehemu tatu, ni kauli ya Imamu” – “Kama akitaka kuzigawanya, basi aina za shaka ni mbili kwa wanavyuoni wote, lakini hukumu ya shaka ya mkataba kwa Imamu yule ni hukumu ile ile ya shaka ya hali, na kama akitaka kuzigawanya aina za shaka kwa mujibu wa maana, basi ni aina mbili pia, kwa sababu shaka ya mkataba inaweza kuwa ni ya kitendo na pia inaweza kuwa ya hali kama vile kuoa bila mashahidi”.
Na shaka ya mkataba wa ndoa ni kama ya mtu aliyefunga ndoa pamoja na mwanamke asiyefaa kumwoa kama maharimu, basi haadhibiwi kwa mujibu wa mtazamo wa Abu Hanifa ingawa alijua uharamu wa kutenda kitendo hicho, ndoa hii ingawa ni haramu kwa mujibu wa mtazamo wa wanavyuoni wote, lakini mtindo wa mkataba kwa njia hii unaufanya mkataba huu uwe na shaka inayosababisha kuondoshwa kwa adhabu, vilevile hukumu ya mkataba wa ndoa kwa mwengine, au kwa mtalaka aleyepewa talaka mara tatu, au ndoa ya kijakazi pasipo na idhini ya bwana wake, au kufanya mkataba wa ndoa pamoja na kijakazi ingawa ana mwanamke mwengine asiyekuwa kijakazi, au mwanamke majusi, au ameoa wanawake watano kwa mpigo, au ameoa dada wawili kwa pamoja, katika hali zote hizi kwa mujibu wa maoni ya Abu Hanifa anayefanya hivyo haadhibiwi, kwa sababu ya kuwepo mtindo wa mkataba unaosababisha kuondoshwa adhabu.
Ingawa adhabu inaondolewa katika hali hizi, lakini mtu ataadhibiwa hata kama akiwa hajui uharamu wa kitendo hicho, lakini inapaswa kukadiria adhabu ndogo zaidi kwa asiyejua uharamu wa kitendo hicho.
Al-Sahiban (wanavyuoni wawili) kutoka madhehbu ya Abu Hanifa walisema kuwa: anayefunga ndoa na asiyefaa kwake kumwoa kwa sababu ya nasaba au wamenyonya pamoja, na akamwoa basi ni lazima aadhibiwe. Vile vile kama akioa mwanamke aliyeajiriwa kwa ajili ya uzinifu, basi aadhibiwe kwa sababu mkataba wa ujira hauruhusu kuoa, mtu huyo alikuwa kama aliyekodi mwanamke kwa ajili ya kumpikia na kisha yeye akaamua kuzini naye, kwa mujibu wa maoni ya wanavyuoni wote mtu huyo lazima aadhibiwe. Lakini hali zote zilizobakia Al-Sahiban hawakujadiliana na Abu Hanifa kwa sababu shaka inathibiti katika hali hizi, na kama tukiangalia vizuri tutaona kuwa hakuna majadiliano kati ya Abu Hanifa na marafiki zake wawili kutokana na tofauti ya sababu zao [Al-Tahtaui 2/396].
Athari ya shaka hii katika kuthibitika kwa nasaba, wanavyuoni hawakuafikiana kuhusu jambo hilo, aliyeambatanisha shaka ya mkataba na shaka ya kitendo alisema kuwa nasaba haithibitiki pamoja na shaka hii, na shaka ya hali ni kinyume cha hivyo, lakini iliyokaribu zaidi ni kuambatanishwa kwa shaka ya kitendo; kwa sababu shaka ya hali inahitaji kuwepo kwa uhalali hata kwa upande mmoja, ambapo itategemea kuthibitika kwa miliki katika hali ile kwa upande mmoja kama tulivyosema, kinyume cha shaka ya kitendo ambapo hakuna hata upande mmoja wa uhalali, na katika aina za shaka za mkataba zilizotajwa hakuna hata upande mmoja wa uhalali, kutokana na hivyo nasaba haithibitiki pamoja na kuwapo shaka hii.
Maoni ya wanavyuoni wa madhehebu ya Shaafi yanafanana sana na maoni ya wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi, lakini mfanano huu kati ya wanavyuoni wa madhehebu ya Shaafi na wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi ni katika asili ya msingi, au kuna tofauti kati yao kwa baadhi ya masuala kwa kuzingatia hali hizi iwapo ni miongoni mwa aina za shaka au la.
Wanavyuoni wa madhehebu ya Shaafi wameigawanya shaka kwa aina tatu:
Ya Kwanza ni: Shaka ya mtendaji: Al-Mawardi anaiita aina hii ya shaka ni kitendo, na mfano wake ni yule anayemkuta mwanamke katika kitanda chake kisha akamwingilia akidhani kuwa ni mke wake au kijakazi wake, basi haadhibiwi kama atadai hivyo, nao ni mtazamo wa wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi, kuepusha adhabu kunategemea kudhani uhalali wa kumwingilia mwanamke huyo, lakini wanavyuoni wa madhehebu ya Shaafi walifanya kulazimisha kuwa jambo hilo ni miongoni mwa shaka ya mtendaji, na wakasema kuwa nasaba inafuata kuingiliana pamoja na shaka hii, kinyume cha mtazamo wa wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi [Al-Ashbaah wa Al-Nadhaair kwa Al-Suyuti: 123, Darul Kutub Al-Ilmiyah, na Al-fawaid Al-Janiyah kwa Al-Fadani 2/130, na Rawdhatul Taalibiin 7/311, Alam Al-Kutub, na Mughni Al-Muhtaaj 5/444, Darul Kutub Al-Ilmiyah].
Ya Pili ni: Shaka katika hali: Baadhi ya wanavyuoni wanaiita aina hii shaka kwa mwolewaji. Na wamemfananisha na mtu ambaye alijamiiana na mke wake aliyepata hedhi au aliyefunga saumu au aliyenuia ihraam kwa ajili ya kufanya hija, au aliyeolewa na babayake au kwa mwanawe, na kama akiiba mali ya mwanawe, basi haadhibiwi katika hali hizi zote, na maana ya aina hii ya shaka ni kuthibitika kwa miliki hata kwa upande mmoja.
Ya Tatu ni: Shaka katika madhehebu au upande au njia: Nayo ni kila upande uliosahihishwa na baadhi ya wanavyuoni na dalili zao zenye nguvu, na mfano wake ni kutoadhibiwa kwa anayeoa mtalaka au mjane pasi na walii kwa mujibu wa majadiliano ya Abu Hanifa asemaye kuwepo kwa walii ni sharti ya kuoa, pia kuoa pasi na mashahidi kwa mujibu wa majadiliano ya Imam Maliki, ndoa ya muda kwa mujibu wa majadiliano ya Ibn Abbas, vile vile, kama mtu atakunywa pombe kama dawa. [Al-Ashbaah wal Nadhair kwa Al-Suyuti uk.123, Al-Qawaid Al-Kubra kwa Al-Ezz Ibn Abdul Salam 2/279, 280, na Al-Fawaid Al-Janiah 2/130].
Maana ya hayo maelezo yaliyotangulia ni kwamba kitendo ambacho ni haramu kwa watu ni halali kwa wengine, basi haadhibiwi anayefanya kitendo hicho, yaani majadiliano yenyewe hayasababishi shaka. Al-Ezz Ibn Abdul Salam anasema katika kitabu chake kuwa [2/191]: “Wanafiki walisema kwamba majadiliano ya wanavyuoni ni shaka, lakini kauli hii siyo sahihi kwa ujumla wake, hivyo, majadiliano yenyewe siyo shaka kwa dalili ya kuwa majadiliano ya Ataa kuhusu kuruhusiwa kuoa vijakazi ingawa yapo majadiliano kuhusu suala hili, lakini adabu haiondoki kwa mujibu wa hali hii, bali shaka inayoondosha adhabu inakwepo kwenye ukweli wa majadiliano na dalili zake zinazofanana”. Inawezekana kufananisha aina ya shaka hii kwa masuala yote yanayojadiliwa na wanavyuoni kati ya wanaoruhu na wanaokataza, hata kama masuala hayo mbali na adabu, na misiba inaingia katika hali hiyo, ambapo wanavyuoni wanaweza kutofautiana kutokana na kutokuwepo kwa dalili au kufichwa kwake kama ilivyotajwa hapo juu, lakini sharti katika majadiliano yanasababisha shaka kuwa na nguvu, lakini kama majadiliano ni dhaifu basi hayasababishi shaka ambayo inaondosha adhabu. Imetajwa katika Al-Mawahib Al-Sunniah kwa Al-Jarhazi kuwa [2/141, 142]: “Na katika Qawaid Al-Taji: Kama kuna mtazamo mmoja ni dhaifu unahesabiwa miongoni mwa makosa tu, wala siyo miongoni mwa majadiliano yanayofanyika kwa jitihada za wanazuoni; kwa sababu hawazingatiwi waliosema mtazamo huu lakini mtazamo wenyewe ambao ni nguvu au dhaifu ndio unaozingatiwa, tunakusudia kwa neno "Nguvu" kuwa ni hali inayovuta akili”. Pia majadiliano hayazingatiwi kuwa ni shaka inayoondosha adhabu kama jaji akiamua kuchukua mtazamo mmoja tu; kwa sababu katika hali hii hakuna majadiliano.
Lakini Wanavyuoni wengi wa madhehebu ya Maliki na Hanbali hawakutaja wazi mgawanyo wa shaka kama walivyofanya wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi, na ya Shafi, lakini wamezungumza kuhusu aina ya shaka katika maneno yao kwa mujibu wa suala linalotafutiwa, bali wamefananisha katika baadhi ya masuala hayo kwa mifano ile ile iliyotajwa na wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi, na wamebainisha matokeo ya kuwepo kwake, ama kuhusu mgawanyiko kwa wanavyuoni wa madhehebu ya Maliki, Ibn Shas alitaja katika “’Ekd Al-Jawahir Al-Thaminah”, na Al-Qaraafi amesema hivyo, Ibn Shas anasema katika kitabu cha Al-Zinaa [3/306, Darul Gharb]: “Na kuangalia pande zote mbili:
Ya Kwanza: Kuangalia jambo linalolazimisha, na linalolazimishwa: Ilhali ni kwamba ukiukaji wa maadili kwa kuoa kuna ambayo ni haramu pasi na haki yoyote na hakuna shaka yoyote basi adhabu inaondolewa... na kauli yetu kuwa: Hakuna shaka yoyote, yaani shaka katika hali au shaka kwa mtendaji au shaka katika njia. Kuhusu shaka katika hali tunakusudia kuwa kijakazi, hata kama akiwa haramu kwa sababu ya kunyonya maziwa au kwa sababu ya nasaba, au kushiriki au idda au kuoa basi hakuna adhabu katika kumwoa kwake. Ama kuhusu shaka katika mtendaji yaani kudhani kuwa ni kijakazi wake au mke wake. Ama kuhusu shaka katika njia yaani wanavyuoni wanajadiliana juu ya kuruhusiwa kuoa kama vile katika hali ya kuoa pasipo na walii au bila ya mashahidi, hali hizi zote zinaondosha adhabu”. Mtazamo kama huu umetajwa katika kitabu cha “Al-Furuuq wa Tahdhibuh” lakini umeongezea kuwa shaka hii haiondoshi adhabu tu, bali huondosha kafara pia, lakini sharti yake ni nia ya mtendaji kulingana na sababu inayorahisisha hali hiyo, na mtazamo huu ni ule uliotajwa na wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi kuhusu shaka katika kitendo. Al-Qaraafi anaeleza msimamo wake kwamba hakuna isipokuwa wanafiki tu ndio wanaojua shaka ya sababu zinazoruhusu na kutekelezwa masharti yake na kwa kiasi chake, na kwamba ni vigumu kufikiwa na watu wengi hali hii, na kwa hivyo utata katika jambo hili una udhuru, na jambo ambalo ni maarufu halina udhuru.
Kwa mujibu wa hayo, hali ambayo haikuwa na sharti hilo au ilikuwa mbali na shaka hiyo, basi mtendaji ataadhibiwa na kafara haitaondolewa.
Mifano ya hali ambazo adhabu au kafara huondolewa ni: Kama mtu akijamiiana na mke wake katika mwezi wa Ramadhani akiwa amesahau akadhani kuwa kitendo hicho kinabatilisha saumu yake akafungua kwa makusudi mara nyingine, au mwanamke ambaye alitwaharika katika usiku wa Ramadhani na hakuoga mpaka asubuhi, akidhani kwamba hairuhusiwa kufunga saumu kwa ambaye hakuoga kabla ya alfajiri, akala, au kama baba kwa mfano, anaiba mali ya mwanawe, au kama mtumwa anayeiba mali kutoka kwa bwana wake.
Ama kuhusu mifano ambayo haina udhuru, kama vile, mwanamke mmoja asema: Leo nitapata hedhi, na alikuwa kwenye siku yake hii akifungua saumu mwanzoni mwa siku yake hiyo na kisha akapata hedhi mwishoni mwake, au kama mtu mmoja akinywa pombe, akidhani imegeuka na kuwa siki, au kama mtu mmoja alijamiiana na mwanamke akiwa na wazo la kumwoa, adhabu haiondolewi, kwa ajili ya kutozingatia kwa kulinganisha sababu zinazoruhu hali hizi, vile vile aliyemwoa dada yake kwa njia ya kunyonyesha, nasaba, au mwanamke aliye maharimu kwake na akawaoa kwa makusudi huku akiwa anajua uharamu wa jambo hili. [Al-Furuuq wa Tahdhibuh 4/172, Alam Al-Kutub].
Ama kuhusu wanavyuoni wa madhehebu ya Hanbali, Al-Baali amesema katika kitabu cha “Al-Ikhtiaraat Al-Fiqhiyyah” katika maneno yake juu ya mahari kwamba [uk. 142, Matbaat Kurdistan Al-Ilmiyyah- Kairo]: “Shaka ina aina tatu: Shaka ya mkataba, Shaka ya itikadi, na Shaka ya miliki”. Na aina hizi kwa ujumla zinafanana sana na aina zilizotajwa na wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi pamoja na wa madhehebu ya Shafi.
Kuhusu aina za shaka kwa wanavyuoni wa madhehebu manne, tayari tumeshataja hapo juu kuwa: Kuna mifano mingine inadaiwa kuwa ni miongoni mwa aina za shaka lakini wanazuoni wa Fiqhi hawakuzitaja zikiwa peke yake, bali wamezitaja katika maneno yao, kwa hivyo tunakuta wanazuoni wa Fiqhi wa sasa wanajitahidi kuzihesabu aina hizi na kuzipa majina, labda wanavyuoni hawa watatofautiana kuhusu jambo hili. Lakini aina hizi husemwa vile vile kama zilivyo zingine: Hakuna majadiliano katika istilahi. Ni muhimu kubainisha athari ya shaka juu ya hali itakayokuwapo.
Tukitoa mfano kutoka katika mifano hiyo -ambayo ni mingi-, kwa mfano kama mtu akinunua nguo na akaitia rangi nguo hiyo, kisha akakuta aibu ya zamani ambayo ilikuwapo kabla hajaitia rangi, je? inawezekana kuendelea kuiuza? na je mnunuzi atachukua kwa bei ya aibu hiyo au anaweza kuirudisha nguo hiyo na kuichukua kwa bei ya rangi hii aliyoitia katika nguo?
Baadhi ya wanavyuoni wamesema waliyoyasema tofauti na wengine, lakini kuhusu kuirudisha nguo hiyo na kuchukua gharama ya rangi aliyoitia katika nguo kuna shaka ya kuwapo riba katika muamala huo, yaani ni kama vile mnunuzi anampa muuzaji elfu moja ili achukue elfu moja na mia mbili. Baadhi ya wanavyuoni wamelipa suala hili jina la “Shaka ya riba” na wakalifanya kuwa ni aina moja, na wakajitahidi katika ukusanyaji wa masuala yanayofanana nalo kutoka katika matawi ya Fiqhi.
Kuhusu mifano ya masuala hayo na kufuata matawi ya Fiqhi yanayohusu masuala hayo, labda yatachukua muda mrefu sana, na pengine yakagawanyika sehemu nyingi. Na tayari kuna tafiti zinazohusu masuala hayo yote, lakini kwa ujumla uhusiano uliopo kati ya mifano hii na mengine ni maana ya shaka iliyotajwa hapo juu. Kila suala linalofanana na suala thabiti tunaweza kulizingatia kuwa ni shaka, halafu ikatafutwa athari ya shaka hiyo katika hukumu inayohusiana nalo kwa mujibu wa Nguzo na Masharti, na Mungu Mwenyezi anajua zaidi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.
 

Share this:

Related Fatwas