Kutoa Dalili kwa Hadithi Dhaifu Ka...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoa Dalili kwa Hadithi Dhaifu Katika Hukumu za Sheria.

Question

 Je! Inaruhusiwa kutoa dalili kwa Hadithi dhaifu katika hukumu za Sheria?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kuna Hadithi dhaifu zinafaa sana katika suala la kifiqhi, lakini mapokezi yake ni dhaifu. Tunakuta baadhi ya wanavyuoni wametoa dalili kwa Hadithi hizi, na hapa swali linaulizwa: Namna gani mwanachuoni anaitoa dalili kwa Hadithi dhaifu? Je, inaruhusiwa kufuatwa njia hii na mwanachuoni na Mufti kutoa dalili kwa Hadithi dhaifu kwa siku hizi?
Suala hili linahusiana na Hadithi kwani ni chanzo cha pili cha sheria ya Kiislamu, lakini chanzo hiki hasa kinathibitika kwa dhana kwani Hadithi za Ahaad (Hadithi isiyokuwa Mutawatir) ni nyingi zaidi kuliko Hadithi Mutawatir (Hadithi waliyoipokea Maswahaba wengi).
Wataalamu wa Hadithi waliweka misingi ya elimu ya Hadithi, wakabainisha usahihi na udhaifu wake, pia wakaonesha kuwa udhaifu umegawanyika daraja tofauti. Hadithi haikuhukumiwa kuwa na udhaifu kwa sababu ya uongo wa baadhi ya wapokezi.
Tumetoa fatwa kuhusu kutumika kwa Hadithi iliyo dhaifu katika kuhimiza matendo mema, lakini tumeyaondosha matumizi ya Hadithi iliyo dhaifu katika kupitisha hukumu za kisheria, na kwa hivyo basi kinachofahamika sana kwa watu ni kutozifuata kabisa aina hizi za Hadithi, lakini wakati tunaporejea maneno ya wanavyuoni tunaona kwamba wameeleza jambo hili kinaganaga.
Kabla ya kuingia katika suala hili tutataja dhana ya Hadithi; ili kumthibitishia mwulizaji na watu wengine kile tunachokizungumzia kwa uwazi. Miongoni mwa dhana za Hadithi Marfuugh kwa mujibu wa wataalamu wa Hadithi ni ile iliyosemwa na Al-Qassimi [Qawaid Al-Hadith uk. 60, Dar Al-Kutub Al-Alamiyah]: “Ni kila kinachonasibishwa kwa Mtume S.A.W. katika maneno yake au vitendo vyake au kuthibitisha jambo au sifa katika tabia zake”
Miongoni mwa dhana za Hadithi kwa mujibu wa wanavyuoni wa kifiqhi ni ile iliyosemwa na Al-Zarkashiy [Al-Bahrul Muhiit, 6/6, Dar Al-Kutub]: “yale yiyotokana na Mtume S.A.W. miongoni mwa maneno, vitendo, kuthibitisha jambo na kutaka kufanya kitu. Na hili jambo la mwisho halikutajwa na wataalamu, lakini Imamu Shafi alilitumia kama dalili”.
Tunapaswa kujua ni nini maana ya Hadithi dhaifu, na hasa kwa kuwa wanavyuoni walizoea kubainisha maana ya Hadithi Sahihi na Hassan kisha kubainisha maana ya Hadithi dhaifu: kwamba ni Hadithi isiyo na sifa za Hadithi Sahihi na Hassan. Itakuwa vizuri kubainisha aina hizi.
Hadithi Sahihi: Ni Hadithi aliyoipokea mtu muadilifu mwenye kukamilika kudhibiti kwa mapokezi yenye Ambatanisho (sanad yenye kushikana) na ikasalimika na riwaya za wapokezi wengine na pia ikasalimika na Ila (Kasoro)”.
Hadithi Hassan: Ni aina mbili: Ya kwanza: Ni Hadithi dhaifu zikiwa nyingi njia zake, yaani riwaya zake kwa njia ambayo huunga baadhi ya riwaya baadhi ya nyingine na asipatikane hapo mpokezi mwongo wala mwenye kutuhumiwa kwa uongo. Aina ya pili: Ni Hadithi aliyoipokea mtu muadilifu ambaye ni dhaifu wa kudhibiti kwa mapokezi yenye Ambatanisho na ikasalimika kukhitilafiana na riwaya za wapokezi wengine na ikasalimika na Ila (Kasoro).
Hadithi dhaifu: ni Hadithi isiyo na sifa za Hadithi Sahihi na Hassan zilizotajwa hapo juu. [Kutoka Talkhiis Ibn Kathiir limuqadimati Ibn Swalah].
Kuhusu kuifuata Hadithi dhaifu, basi asili yake ni kutoruhusiwa kuifuata, kwa sababu Hadithi hii siyo Mutawatir ili kutoa elimu wala ni Hadithi Aahad Sahihi ili kutoa dhana, lakini katika hali maalum mtu anaweza kuifuata Hadithi dhaifu katika hukumu za kisheria, miongoni mwao ni:
1) Wakati kuna Hadithi dhaifu, na hakuna Hadithi nyingine inayoipinga:
Ibn Al-Najjar Al-Hanbali [Sharhul Kawkab Al-Muniir, 2/573, Maktabatul Obeikan]: “Katika “Jamii Al-Qaadhi”: kwamba Hadithi dhaifu haijatumiwa katika dhambi. Al-Khallal alisema: Madhehebu yake - anamaanisha: Imam Ahmad - kwamba Hadithi dhaifu ikiwa haikuwa na upinzani ilitumika. Alisema katika suala la kafara ya kufanya jimai na mwanamke mwenye hedhi: madhehebu yake katika Hadithi, kama zilikuwa na wasiwasi na hazikuwa na upinzani basi zinatumika.Imamu Ahmad alisema katika Hadithi ya Abdullah kuwa: mbinu yangu ni kuitumia Hadithi dhaifu kama ikiwa hakuna yeyote inayoipinga.
Ibn Al-Salah [Muqadimat Ibn Al-Salah, uk.36, Darul Fikr]: “Abu Abdullah BinManda amesema kuwa: “Na pia Abu Dawood Al-Sijistani anatumia mtazamo wake, na hatumii mapokezi dhaifu kama huna Hadithi nyingine, kwani Hadithi kwake ina nguvu zaidi kuliko mitazamo ya wataalamu”.
Ali Ibn Hazm [Al-Muhala, 3/61, Darul Fikr]: “Athari hii ya Duaa Al-Qunut (Kuomba dua katika raka ya pili ya Salah ya Al-Fajiri), ambayo ingawa hakuna aliyoipinga katika aina, hatukuweza kupata Hadithi nyingine iliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allah (S.W.A). Imamu Ahmed BinHanbal alisema: ninapenda sana Hadithi dhaifu zaidi kuliko mtazamo wenyewe. Ali alisema hivyo . Na hivyo tunavyosema”.
2) Umma umepokea kwa kukubalika:
Al-Sakhawiy alisema: [Fatihul Mughiiyth bisharhi Alfiyatul Hadith, 1/350, Maktabatul Sunnah nchini Misri]: “Kama watu wakiitumia Hadithi dhaifu inaruhusiwa kuitumia kwa mujibu wa mtazamo sahihi, na kwamba ni sawa sawa na Hadihi Mutawaatir kuhusu kufuta Hadithi nyingine ambayo ni Maktuu (imekatika mapokezi yake), kwa hivyo Imamu Shafi alisema katika Hadithi isemayo: Hakuna urithi kwa Mrithi”: Wataalamu wa Hadithi hawakuthibitisha aina hii ya Hadithi, lakini watu waliikubali wakaitumia, mpaka ikiwa kuifuta aya za usia].
3) Akiba:
Al-Sakhaawi alisema [Fathul Mughaith Bisharh Alfitaul Hadith, 1/350]: «Au ilikuwa katika nafasi kama akiba kama ikipokelewa Hadithi dhaifu kuhusu chuki ya baadhi ya suala la mauzo au la ndoa, ni Mustahab (yapendekezwa) -kama alivyosema An Nawawi- kuwa inaruhusiwa kuiachwa, lakini hailazimiki. Ibn Al-Arabi Imamu Maliki hakuruhusu kabisa kuitumia Hadithi dhaifu. Lakini An-Nawawiy alisema katika vitabu vyake vingi makubaliano ya wataalamu wa Hadithi na wengine kuhusu kuitumia Hadithi dhaifu katika fadhila na kama hivyo”.
Imamu Suyuti alisema [Tadriib Ar-Rawi, 1/351, Dar Taibah]: “Pia inaruhusiwa kuitumia Hadithi dhaifu katika hukumu, kama ilikuwa akiba”.
4) Kupendekezwa katika fadhila:
Ibn Hammam alisema katika kitabu cha [Fathul Qadeer / 2, 133, Darul Fikr]: “Mwenye kuosha wafu afanye ghusl, na anayembeba atie udhu” Al-Tirmidhi alisema Hadithi hii ni Hasan, wengine wengi walisema ni dhaifu. Hakuna Hadithi Sahihi katika mapokezi ya Ali lakini Hadithi zake ni nyingi.
Uthibitisho wa haya yote:
Kuihukumu Hadithi kwa usahihi au udhaifu kunaonekana katika dhahiri tu, Wataalamu waliweka dhana kwa kila aina ya Hadithi, wakati wa kutumika kwa maana ya Hadithi ilichukua hukumu yake katika uwazi wake.
Ibn Al-Salah alisema katika [Muqadimatu Ibn Al-Salah uk.13.] kuwa: “Na wanaposema kuwa: Hadithi hii ni Sahihi ina maana: kwamba mapokezi yake yaliwasili na maelezo mengine yaliyotajwa, si hali yake kuthibitishwa katika kitu hali ile ile. Miongoni mwao wanaona kuwa ni iliyopokelewa kutoka kwa mwadilifu mmoja, na sio miongoni mwa habari zilizokubaliwa na Umma. Pia kama akisema katika Hadithi: Si Sahihi, basi siyo maana ya hivyo kwamba Hadithi ni uongo katika hali ile ile, kama inaweza kuwa na ukweli katika hali ile ile, lakini maana yake ni kwamba hakuruhusiwa kuipokea kufuatana na sharti lililotajwa, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi ».
Wakati ambapo hali ni ya uwezekano, na hakuna Hadithi nyingine kinyume na Hadithi dhaifu, inatumika Hadithi hii dhaifu na kuna uwezekano wa usahihi, licha ya kwamba baadhi ya wataalamu wanaitumia. Hii inaonesha usahihi wa maana kwa mujibu wa mwenye mtazamo huo. Kwa maana kwamba baadhi ya wataalamu wangeutaja mtazamo huu wa kifiqhi, kama haukuja udhaifu huo.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, inadhihirika kuwa hukumu ya Hadithi dhaifu ni kutoruhusiwa kuitumia katika utoaji wa hukumu za kisheria, hata hivyo, kunaweza kuwa na hali ambayo inaruhusiwa kuitumia Hadithi dhaifu katika utoaji wa hukumu za kisheria kufuatana na udhibiti wa hali zilizotajwa hapo juu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas